Wednesday, May 29, 2019

MWENGE WA UHURU WAHITIMISHA MBIO ZAKE MKOANI SIMIYU ASILIMIA 97 YA MIRADI YAKUBALIWA

Mwenge wa Uhuru umemaliza mbio zake leo Mkoani Simiyu na kukabidhiwa katika Mkoa wa Mara, ambapo miradi 33 kati 34 sawa na asilimia 97 ya miradi iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri zote sita imekubaliwa na kuzinduliwa, kukaguliwa, kuonwa na kuwekewa mawe ya msingi.
Akitoa taarifa kabla ya kukabidhi Mwenge wa Uhuru mkoani Mara, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka amesema ni mradi mmoja tu wa maji ambao umeonekana kuwa na kasoro ambapo amebainisha kuwa kasoro hizo zitafanyiwa kazi na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2019 atapata taarifa mapema iwezekanavyo ya namna zilivyofanyiwa kazi.

Naye Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali amewapongeza viongozi na wananchi Mkoani Simiyu, huku akibainisha kuwa  tangu mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019 zizinduliwe rasmi Mkoani Songwe, Simiyu ni mkoa wa Tisa lakini umeonekana kuwa mkoa nambari moja kwa namna ulivyolitekeleza jukumu hili.


Aidha, amesema yeye pamoja na wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa wengine katika kipindi cha siku sita walizokaa Simiyu wamebaini kuwepo kwa umoja, ushirikiano na kuheshimiana miongoni mwa wananchi, watumishi na viongozi mambo ambayo ni ya msingi katika maendeleo.


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Adam Malima, Mei 28, 2019.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali akiongea na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu kabla ya kukabidhiwa rasmi mkoani Mara, Mei 28, 2019
 Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali akiagana na Katibu Tawala wa mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini kabla ya kukabidhiwa rasmi mkoani Mara, Mei 28, 2019 
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(mwenye karatasi mkononi) akiwasilisha taarifa yam bio za Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu, kabla ya kukabidhi Mwenge wa Uhuru Mkoani Mara, Mei 27, 2019.


0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!