Wanafunzi
wa darasa la saba katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu
wamemuahidi Mkuu wa mkoa Anthony Mtaka hawatamuangusha katika mtihani wa Taifa
Septemba 11-12, kwa kuwa wamejiandaa vizuri na wanaimani watafanya vizuri.
Wanafunzi
hao wa shule ya msingi Somanda A na B wametoa ahadi hiyo kwa niaba ya
wanafunzi wote wa darasa la saba wa mkoa wa Simiyu, mbele ya Mkuu wa Mkoa
wa Simiyu, Mhe. Anthoy Mtaka wakati akizungumza nao na kuwatakia heri katika
Mtihani huo.
Wamesema wana
imani ya kufanya vizuri kwa sababu hata Mtihani wa Mkoa Utilimilifu(Mock)
walifanya vizuri, wameandaliwa vizuri kwa kupewa mazoezi na mitihani ya mara
kwa mara na wamepata mbinu na maarifa mapya ya kujibu maswali ya mitihani kupitia
kambi za kitaaluma zilizofanyika katika
kila shule.
“Sisi
tumejiandaa vizuri sana na nina uhakika tutafanya vizuri katika Mtihani wa
Taifa kama tulivyofanya vizuri kwenye Mock, walimu wametuandaa vizuri tulikuwa
na kambi ya kitaaluma ambayo imetusaidia kukutana na walimu tofauti
waliotufundisha vizuri zaidi, tunamuahidi Mkuu wa Mkoa kuwa hatutamuangusha”
alisema Luhinda Nalisha kutoka S/M Somanda A.
“Tumejiandaa vizuri
na tumejipanga kufanya vizuri, pia tunamshukuru Mkuu wa Mkoa kuja kututembelea na
kutupa mawaidha tutayafanyia kazi, shule ipo vizuri kitaaluma na nidhamu hivyo tuna uhakika wa kufaulu mtihani wa Taifa”
alisema Bugumba Nindwa mwanafunzi wa Shule ya Msingi Somanda B
Akizungumza
na wanafunzi hao, Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amewatakia mtihani
mwema na kuwataka watumie mbinu walizopewa na walimu kufanya vizuri, huku akiwaonya
kutojihusisha na vitendo vya udanganyifu
wa aina yoyote.
Katika hatua
nyingine Mtaka ametoa wito kwa wahitimu wa vyuo vikuu kufundisha masomo ya maandalizi ya Kidato cha
kwanza(Pre-form one) kwa wanafunzi watakaohitimu darasa la saba kwa ajili ya kuwaandaa wanafunzi na masomo ya
elimu ya sekondari.
Naye Afisa
elimu Msingi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mwl. Christopher Ligonda akishukuru
kwa niaba ya walimu amesema wanafunzi wameandaliwa vizuri na wamefundishwa
vizuri na wako tayari kwa ajili ya mtihani na matarajio yao ni kupata ufaulu
mzuri kama walivyoahidi wenyewe.
Mkoa wa Simiyu una jumla ya wanafunzi 29, 248 wa darasa la saba wanaotarajia kufanya mtihani wa Taifa mwaka huu, ambao kati yao wavulana ni 13, 594 na wasichana 15, 654.
MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka akizungumza na wanafunzi wa darasa la Saba katika Shule ya Msingi
Somanda A na B Mjini Bariadi wakiwa katika maandalizi ya Mtihani wa Taifa
utakaofanyika Septamba 11-12, 2019, wakati akiwatakia heri katika mtihani huo
kwa niaba ya wenzao wote wa mkoa wa Simiyu Septemba 10, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka akifurahia jambo na
wanafunzi wa darasa la Saba katika Shule ya Msingi Somanda A na B Mjini
Bariadi wakiwa katika maandalizi ya Mtihani wa Taifa utakaofanyika Septamba
11-12, 2019, wakati akiwatakia heri katika mtihani huo kwa niaba ya wenzao wote
wa mkoa wa Simiyu Septemba 10, 2019.
Baadhi ya wanafunzi wa darasa la
saba katika Shule ya Msingi Somanda A na B Mjini Bariadi wakimshika mkono Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kama ishara ya kupokea mkono wake wa heri
kwao katika Mtihani wa Taifa utakaofanyika Septemba 11-12, 2019
Baadhi ya wanafunzi wa darasa la
saba katika Shule ya Msingi Somanda A na B Mjini Bariadi wakimshika mkono Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kama ishara ya kupokea mkono wake wa heri
kwao katika Mtihani wa Taifa utakaofanyika Septemba 11-12, 2019
Baadhi ya wanafunzi wa darasa la
saba katika Shule ya Msingi Somanda A na B Mjini Bariadi wakishangilia mara
baada ya kupokea salamu za heri ya Mtihani wa Taifa utakaoanza Septemba 11-12,
2019 kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo
pichani) wakati alipowatembelea Septemba 10, 2019 shuleni hapo kwa lengo la
kuwatakia heri katika mtihani huo.
Afisa Elimu Msingi Halamashauri ya Mji wa Bariadi, Mwl.
Christopher Legonda akitoa neno la shukrani mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kuzungumza na wanafunzi wa darasa la Saba katika
Shule ya Msingi Somanda A na B Mjini Bariadi wakiwa katika maandalizi ya Mtihani
wa Taifa utakaofanyika Septemba 11-12, 2019, kwa lengo la kuwatakia heri katika
mtihani huo kwa niaba ya wenzao wote wa mkoa wa Simiyu Septemba 10, 2019.
Baadhi ya wanafunzi wa darasa la
saba katika Shule ya Msingi Somanda A na B Mjini Bariadi wakiimba wimbo wa
Tanzania Tanzania na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu =, Mhe. Anthony Mtaka wakati
alipowatembelea Septemba 10, 2019 shuleni hapo kwa lengo la kuwatakia heri
katika mtihani wa Taifa utakaofanyika Septemba 11-12, 2019.
0 comments:
Post a Comment