Wednesday, September 25, 2019

UONGOZI WA MKOA SIMIYU WABAINI UBADHILIFU WA SHILINGI MILIONI 55 BUSEGA

Uongozi wa Mkoa wa Simiyu umebaini Ubadhilifu wa kiasi cha shilingi  55,580,000/= ambazo ni sehemu ya mkopo uliotolewa na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Urasimishaji wa makazi Viwanja 3700 katika kata nne za Halmashauri ya Wilaya ya Busega uliofanywa na Watumishi wanne wa Halmashauri hiyo.

Hayo yamebainishwa na Katibu Tawala wa Mkoa, Bw. Jumanne Sagini wakati akiwasilisha taarifa ya uchunguzi wa matumizi ya  fedha za mradi huo katika kikao cha  Baraza  Maalum la madiwani kilichofanyika Septemba 24, 2019 Busega Septemba 06,2019 Nyashimo Busega.

Sagini amewataja watumishi waliohusika katika ubadhilifu huo kuwa ni Mkurugenzi wa Halmashauri, Anderson Njiginya, Mkuu wa Idara ya Ardhi, Magesa Magesa, msimamizi wa mradi Raymond Mahendeka na mhasibu wa mradi,Augustina Kitau na kuwataka kurejesha fedha hizo mara moja na kushauri mamlaka zao za nidhamu kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria

Sagini ameongeza kuwa timu ya uchunguzi imebaini mapungufu mbalimbali katika matumizi ya fedha hizo ikiwa ni pamoja na ukikwaji wa sheria, kanuni na taratibu za fedha, ukiukwaji wa masharti ya mkataba, ukiukwaji wa sheria kanuni na taratibu za manunuzi ya Umma, udanganyifu na uzembe na usimamizi dhaifu wa Mradi.

“Kutokana na mapungufu yaliyobainishwa katika uchunguzi huu Uongozi wa mkoa unaelekeza watumishi waliohusika warejeshe fedha hizo haraka ili mradi utekelezwe kama ilivyokusudiwa na tunashauri mamlaka za nidhamu zichukue hatua stahiki kwa watumishi hao kwa mujibu wa sheria na taratibu za Utumishi wa Umma,” alisema Sagini.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Mhe. Vumi Magoti amewashukuru viongozi wa Mkoa kutuma wataalam wa Mkoa kufanya uchunguzi wa matumizi ya fedha za mradi na kumuagiza Mkurugenzi kuanzisha utaratibu wa kuwachukulia hatua watumishi waliohusika walio chini  ya mamlaka yake kama  viongozi wa mkoa walivyoelekeza.

Diwani wa Kata ya Mkula, Mhe, Goodluck Nkalango amesema madiwani wa Halmashauri ya Busega wakiwemo wajumbe wa kamati inayoshughulikia masuala ya ardhi hawakushirikishwa katika utekelelezaji wa mradi wa urasimishaji, makazi jambo ambalo lilipelekea wananchi kutokuwa na taarifa sahihi za mradi ikiwemo utaratibu wa kuchangia gharama za upimaji.

Kwa upande wake Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Simiyu, Bw. Alex Mpemba amesema TAKUKURU imepokea taarifa ya Kamati ya Uchunguzi na itaanza kuifanyia kazi mara moja kwa lengo la kuthibitisha makosa ya jinai kwa waliohusika.

“Tumeipokea taarifa ya uchunguzi kupitia kikao cha baraza la dharura na kwa sababu wenzetu wa ukaguzi wamemaliza kazi yao na sisi tutaanzia pale walipoishia kwa lengo la kuthibitisha makosa ya jinai,” alisema Mpemba.

Halmashauri ya Wilaya ya Busega ilipokea mkopo wa shilingi 100,000,000/=kutoka Wizara ya Ardhi kutekeleza Mradi wa urasimishaji wa makazi viwanja 3700 katika kata za Mwamanyili, Mkula, Kiloleli na Lamadi; kwa mujibu wa taarifa ya Uchunguzi hadi kufikia Septemba  06, 2019 utekelezaji wa mradi ulikuwa umefikia asilimi 8.5 na fedha zilizokuwa zimetumika ni  asilimia 98.

MWISHO


Katibu Tawala wa Mkoa wa Simyu, Bw. Jumanne Sagini akizungumza na watumishi na madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega katika kikao cha Baraza Maalum la madiwani, Septemba 24, 2019 kwa lengo la kupokea taarifa ya uchunguzi wa matumizi ya fedha za mkopo shilingi 100,000,000/= kutoka wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Mhe. Vumi Magoti akifungua kikao cha Baraza  Maalum la madiwani kilichofanyika Septemba 24, 2019 kwa lengo la kupokea taarifa ya uchunguzi wa matumizi ya fedha za mkopo shilingi 100,000,000/= kutoka wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Bw. Anderson Njiginya akizungumza kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Mhe. Vumi Magoti kufungua kikao cha Baraza  Maalum la madiwani kilichofanyika Septemba 24, 2019 kwa lengo la kupokea taarifa ya uchunguzi wa matumizi ya fedha za mkopo shilingi 100,000,000/= kutoka wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega wakifuatilia kikao cha Baraza  Maalum la madiwani kilichofanyika Septemba 24, 2019 kwa lengo la kupokea taarifa ya uchunguzi wa matumizi ya fedha za mkopo shilingi 100,000,000/= kutoka wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega wakifuatilia kikao cha Baraza  Maalum la madiwani kilichofanyika Septemba 24, 2019 kwa lengo la kupokea taarifa ya uchunguzi wa matumizi ya fedha za mkopo shilingi 100,000,000/= kutoka wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Mhe. Vumi Magoti akiteta jambo na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simyu, Bw. Jumanne Sagini katika kikao cha Baraza  Maalum la madiwani kilichofanyika Septemba 24, 2019 kwa lengo la kupokea taarifa ya uchunguzi wa matumizi ya fedha za mkopo shilingi 100,000,000/= kutoka wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Baadhi ya viongozi wakifuatilia kikao cha Baraza  Maalum la madiwani kilichofanyika Septemba 24, 2019 kwa lengo la kupokea taarifa ya uchunguzi wa matumizi ya fedha za mkopo shilingi 100,000,000/= kutoka wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Diwani wa Kata ya Mkula, Mhe.akichangia hoja katika kikao cha Baraza  Maalum la madiwani kilichofanyika Septemba 24, 2019 kwa lengo la kupokea taarifa ya uchunguzi wa matumizi ya fedha za mkopo shilingi 100,000,000/= kutoka wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Diwani wa Kata ya Mkula, Mhe.akichangia hoja katika kikao cha Baraza  Maalum la madiwani kilichofanyika Septemba 24, 2019 kwa lengo la kupokea taarifa ya uchunguzi wa matumizi ya fedha za mkopo shilingi 100,000,000/= kutoka wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Mmoja wa madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega akichangia hoja katika kikao cha Baraza  Maalum la madiwani kilichofanyika Septemba 24, 2019 kwa lengo la kupokea taarifa ya uchunguzi wa matumizi ya fedha za mkopo shilingi 100,000,000/= kutoka wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!