Thursday, August 1, 2019

MAKAMU WA RAIS AZINDUA MKAKATI WA KUDHIBITI UPOTEVU WA MAZAO


Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo Agosti Mosi, 2019 amezindua mkakati wa udhibiti wa upotevu wa mazao wenye lengo la kumsaidia mkulima namna ya utunzaji Bora wa mazao baada ya mavuno.

Mama Samia amezindua mkakati huo katika ufunguzi rasmi wa Maonesho ya Nane Name Kitaifa, uliofanyika Kanda ya Ziwa Mashariki  katika Viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.

Amesema upotevu wa mazao ni moja ya changamoto zinazowakabili wakulima na kupelekea kuwa na tija ndogo huku akizitaja changamoto nyingine kuwa ni matumizi hafifu ya mbolea,  kutopata mbegu na viuatilifu kwa wakati na vilivyo bora na kutotumia kanuni bora za kilimo.

 Aidha, Mhe. Makamu wa Rais ametoa wito kwa Taasisi za Umma, binafsi, vyama vya ushirika na Taasisi za kiraia zinzojishughulisha na Maendeleo ya Kilimo kuhakikisha wanarekebisha kosoro zilizopo na kutoa elimu bora na kutosha inayojibu changamoto hizo.

Katika hatua nyingine Mhe. Makamu wa Rais ametoa rai kwa watafiti wote nchini kutoa matokeo ya tafiti zao kwa maafisa ugani na wadau wengine ili wakulima wanufaike na matokeo hayo.

Akizungumzia mkakati wa kudhibiti upotevu wa mazao miaka 10, Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga amesema lengo la serikali ni kuhakikisha inapunguza upotevu wa mazao kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2025.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema dhamira ya mikoa inayounda Kanda ya Nanenane ya Ziwa Mashariki ni kuvifanya viwanja vya maonesho ya Nanenane Nyakabindi kuwa ni mahali patakapojibu kwa vitendo sera za wizara ya kilimo na pawe mfano kwa wananchi kujifunza Kilimo Biashara.

Pia ametoa wito kwa wanunuzi wa pamba kuendelea kununua pamba kwa bei elekezi ya shilingi 1200 na taasisi za fedha kutoa fedha kwa wanunuzi pamba ya wakulima inunuliwe, huku akiiomba Serikali kuridhia sehemu ya fedha ikakatwa fedha hiyo iweze kuwekeza kwenye ujenzi wa kiwanda cha nguo kwa kushirikiana na wadau wengine ili kuwa na soko la uhakika la pamba.

Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yanafanyika kwa mara ya pili mfululizo sasa katika Kanda ya Ziwa Mashariki inayoundwa na Mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga, yakiwa na Kauli Mbiu isemayo Kilimo, Mfugo na Uvuvi kwa Ukuaji wa Uchumi wa Nchi”.
MWISHO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akionesha Nakala ya Mkakati wa Udhibiti wa Upotevu wa mazao uliozinduliwa kwenye  ufunguzi wa Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 leo Agosti Mosi, 2019 , yanayofanyika Kanda ya Ziwa Mashariki Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka  Nakala ya Mkakati wa Udhibiti wa Upotevu wa mazao kwa  niaba ya wakuu wa mikoa yote nchini,  uliozinduliwa kwenye  ufunguzi wa Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 leo Agosti Mosi, 2019 yanayofanyika Kanda ya Ziwa Mashariki Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka  Nakala ya Mkakati wa Udhibiti wa Upotevu wa mazao kwa  niaba ya wakuu wa mikoa yote nchini,  uliozinduliwa kwenye  ufunguzi wa Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 leo Agosti Mosi, 2019 yanayofanyika Kanda ya Ziwa Mashariki Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.
Kutoka kushoto Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ,  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan na Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga wakifurahia jambo katika ufunguzi wa Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 leo Agosti Mosi, 2019 , yanayofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.
Baadhi ya Wakuu wa Mikoa  walioshiriki katika ufunguzi wa Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 leo Agosti Mosi  2019 , yanayofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.
Kikundi cha Kwaya ya ICT Bariadi  kikitoa burudani katika ufunguzi wa Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 leo Agosti Mosi 2019 , yanayofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.
Baadhi ya mabanda ya Maonesho  Nanenane Kitaifa 2019 yanayoendelea katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu, Kanda ya Ziwa Mashariki.

Baadhi ya mabanda ya Maonesho  Nanenane Kitaifa 2019 yanayoendelea katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu, Kanda ya Ziwa Mashariki.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe. Benson Kilangi mara baada ya kufungua Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019

Baadhi ya viongozi wa Kitaifa na mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga wakiimba wimbo wa Taifa, wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 leo Agosti Mosi, 2019 , yanayofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.



Baadhi ya mabanda ya Maonesho  Nanenane Kitaifa 2019 yanayoendelea katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu, Kanda ya Ziwa Mashariki.
Kikundi cha Ngoma cha BASEKI mjini Bariadi kikitoa burudani katika ufunguzi wa Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 leo Agosti Mosi 2019 , yanayofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.
Baadhi ya mabanda ya Maonesho  Nanenane Kitaifa 2019 yanayoendelea katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu, Kanda ya Ziwa Mashariki.
Baadhi ya viongozi wa Kitaifa na mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga wakiagana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan , mara baada ya  ufunguzi wa Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 leo Agosti Mosi, 2019 , yanayofanyika  Kanda ya Ziwa Mashariki Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga  Nakala ya Mkakati wa Udhibiti wa Upotevu wa mazao kwa  niaba ya Mawaziri wengine,  uliozinduliwa kwenye  ufunguzi wa Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 leo Agosti Mosi, 2019  yanayofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.
Kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa kilimo, Mhe.Omary Mgumba, Waziri wa Kkilimo Mhe. Japhet Hasunga wakiteta jambo,  mara baada ya ufunguzi  wa Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 leo Agosti Mosi, 2019 , yanayofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe akimsikilza Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainabu Telack mara baada ya ufunguzi  wa Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 leo Agosti Mosi, 2019 , yanayofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Simiyu, Bw. Adili Elinipenda mara baada ya kufungua Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack akitoa salamu za mkoa wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 leo Agosti Mosi, 2019 , yanayofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Adam Malima akitoa salamu za mkoa wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 leo Agosti Mosi, 2019 , yanayofanyika Kanda ya Ziwa Mashariki katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Adam Malima akitoa salamu za mkoa wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 leo Agosti Mosi, 2019 , yanayofanyika Kanda ya Ziwa Mashariki katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.
Kikundi cha Eliza band kutoka Bariadi Simiyu wakitoa burudani  katika ufunguzi wa Maonesho ya Nanenane Kitaifa 2019 yanayofanyika katika Kanda ya Ziwa Mashariki Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.


0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!