Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally ametoa
salamu za rambirambi na kuwaombea majeruhi na waliofariki katika ajali ya moto
Mkoani Morogoro, huku akitoa wito kwa wananchi kuwa zinapotokea ajali wawe
wepesi wa kuokoa watu na mali za waliopata ajali badala ya kukimbilia kuchukua
vitu ili kuepusha madhara.
Dkt. Bashiru ametoa salamu hizo wakati akizungumza
na viongozi wa CCM wilayani Meatu katika kikao cha Ndani kilichofanyika Ukumbi
wa CCM Mjini Mwanhuzi Agosti 11, 2019 ambapo amewaombea marehemu wote wapumzike
kwa amani na majeruhi wapate afya njema ili waendelee na shughuli za ujenzi wa
Taifa.
“Natoa pole kufuatia vifo vya wenzetu waliofariki
katika ajali ya moto kule Mkoani Morogoro tuendelee kuwaombea
waliotangulia mbele ya haki wapumzike
kwa amani na wale majeruhi waweze kupata afya na kurejea katika shughuli za
kujenga Taifa”
“Kama Mwenyekiti wetu na Rais wetu alivyosema, ni
vizuri tunapopata majanga kama haya ya ajali wote tuwe wepesi wa kuokoa
waliopata ajali na mali badala ya kukimbilia kuchukua vitu kuepusha madhara
makubwa” alisema Dkt. Bashiru.
Akizungumza na Viongozi wa CCM wilayani Meatu, Dkt.
Bashiru amewataka viongozi hao kutoa taarifa za watu wanao nunua pamba kwa njia
ya Umachinga, pasipo kutumia utaratibu
unaotakiwa wa kupitia vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS) kwa bei elekezi ya
shilingi 1200/= ili waweze kuchukuliwa hatua.
Kwa upande wake
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ameishukuru Serikali kwa
kuendelea kutoa fedha za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika
sekta mbalimbali ikiwemo afya, elimu, maji na ujenzi huku akiwashukuru wabunge
wa wilaya ya Meatu(Jimbo la Kisesa na Jimbo la Meatu) kwa namna wanavyojitoa
binafsi na kupitia mifuko ya majimbo kuunga mkono juhudi za Serikali katika
maendeleo.
Naye Mbunge wa Jimbo la Meatu, Mhe. Salum Khamis
amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Dkt. John Magufuli
kukubali kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Draja la Sibiti ambalo ujenzi wake
umerahisisha mawasiliano na utachangia katika kukua kwa uchumi wa wilaya ya
Meatu, mkoa wa Simiyu na mikoa jirani.
Mara baada ya kuhitimisha kikao cha ndani na viongozi
wa CCM Wilaya ya Meatu, Katibu Mkuu wa
CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally alipata fursa ya kutembelea na kuona ujenzi wa
Daraja la Sibiti ikiwa ni ukaguzi wa utekelezaji wa Ilani ya CCM ambapo alipongeza
Serikali kwa ujenzi wa daraja hilo ambalo linaiunganisha mikoa ya Simiyu na
Singida.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Bw.
Fabian Manoza amesema kutokana na ujenzi wa Daraja la Mto Sibiti Halmashauri ina mpango wa kupanua
stendi ya Mjini Mwanhuzi kwa kuwa magari mengi yameanza kupita Meatu kupitia daraja
hilo.
MWISHO
Katibu
Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. BashIru Ally akizungumza na viongozi wa CCM na wananchi
katika kikao cha ndani kilichofanyika Katika Ukumbi wa CCM Mjini Mwanhuzi Wilayani Meatu, Agosti 11,
2019.
Baadhi
ya viongozi wa CCM wilayani Meatu wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. BashIru
Ally katika kikao cha ndani kilichofanyika Katika Ukumbi wa CCM Mjini Mwanhuzi Wilayani Meatu, Agosti 11,
2019
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe, Anthony Mtaka akiwasilisha taarifa ya Serikali katika kikao cha ndani cha
Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. BashIru Ally na viongozi wa CCM ngazi ya tawi
hadi Mkoa, kilichofanyika Katika Ukumbi wa
CCM Mjini Mwanhuzi Wilayani Meatu, Agosti 11, 2019.
Mkuu wa Wilaya ya
Meatu, Dkt.Joseph Chilongani akiwasilisha taarifa ya Serikali katika kikao cha
ndani cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na viongozi wa CCM ngazi
ya tawi hadi Mkoa, kilichofanyika Katika Ukumbi wa CCM Mjini Mwanhuzi Wilayani Meatu, Agosti 11,
2019.
Mbunge wa Jimbo la
Kisesa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina akitoa salamu kwa niaba
ya wananchi wa jimbo la Kisesa katika
kikao cha ndani cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na viongozi wa
CCM ngazi ya tawi hadi Mkoa, kilichofanyika Katika Ukumbi wa CCM Mjini Mwanhuzi Wilayani Meatu, Agosti 11,
2019.
Mbunge wa Jimbo la
Meatu, Mhe. Salum Khamis akitoa salamu kwa niaba ya wananchi, katika kikao cha ndani cha Katibu Mkuu wa CCM
Taifa, Dkt. BashIru Ally na viongozi wa CCM ngazi ya tawi hadi Mkoa,
kilichofanyika Katika Ukumbi wa CCM
Mjini Mwanhuzi Wilayani Meatu, Agosti 11, 2019.
Baadhi ya Viongozi wa
Chama na Serikali wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally
katika kikao cha ndani kilichofanyika Katika Ukumbi wa CCM Mjini Mwanhuzi Wilayani Meatu, Agosti 11,
2019.
Mwenyekiti wa CCM
Wilaya ya Meatu, Mhe. Juma Mwiburi akitoa neon la shukrani mara kabla ya
kuhitimisha kikao cha ndani kati ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. BashIru Ally
na viongozi wa CCM ngazi ya tawi hadi Mkoa, kilichofanyika Katika Ukumbi
wa CCM Mjini Mwanhuzi Wilayani Meatu,
Agosti 11, 2019
.Katibu Mkuu wa CCM
Taifa, Dkt. Bashiru Ally aakipokea zawadi ya Batiki iliyotengenezwa na kikundi
cha Umoja wa Vijana wa CCM wialaya ya Meatu mara baada ya kuhitisha kkao chake
na viongozi wa CCM kilichofanyika Katika Ukumbi wa CCM Mjini Mwanhuzi Wilayani Meatu, Agosti 11,
2019.
Baadhi ya Viongozi wa
Chama na Serikali wa Mkoa wa Simiyu na wilaya ya Meatu wakiimba mara baada
ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru
Ally kuhitimisha kikao chake cha ndani na viongozi hao kilichofanyika Katika
Ukumbi wa CCM Mjini Mwanhuzi Wilayani
Meatu, Agosti 11, 2019.
Kutoka Kulia Katibu
Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe, Anthony
Mtaka na Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt.Joseph Chilongani wakiwa katika Daraja la
mto Sibiti.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally, akizungumza na baadhi ya viongozi wa Chama na Serikali mara baada ya kukagua daraja la Sibiti wakatri akihitimisha ziara yake mkoani Simiyu, Agosti 11, 2019.
Sehemu ya Daraja la Mto
Sibiti linalounganisha mikoa ya Simiyu na Singida.
Katibu Mkuu wa CCM
Taifa, Dkt. Bashiru Ally, akipewa maelezo na viongozi wa Chama na Serikali
wilayani Meatu na Mkoani Simiyu wakati alipotembelea daraja la Sibiti mara
baada ya kuhitimisha ziara yake Mkoani Simiyu, Agosti 11, 2019.
0 comments:
Post a Comment