Monday, August 5, 2019

BALOZI WA INDONESIA, WAZIRI KIGWANGALLA WATEMBELEA MAONESHO YA NANENANE KITAIFA MKOANI SIMIYU


Balozi wa Indonesia nchini Tanzania, Mhe.  Prof. Dkt..Ratlan Pardede na  Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Dkt.Hamisi Kigwangalla Agosti 04, 2019 wametembelea Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki,  viwanja vya Nanenane Nyakabindi Simiyu.

Akizungumza mara baada ya kuwapokea wageni hao Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka  amesema asilimia 80 ya uchumi wa nchi unategemea kilimo, hivyo kwa kuwa Mhe.Kigwangalla ni Waziri mwenye Dira kwa kutembelea maonesho haya atatoa mchango,mawazo na hamasa kubwa kuhusiana na sekta ya kilimo.

 Aidha, amesema Prof.Dkt.Ratlan Pardede amekuja kwa mara ya pili sasa Mkoani Simiyu, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali ya Indonesia na Mkoa wa Simiyu (Tanzania.)

Naye Waziri wa Maliasili na Utalii Mh Dkt.Hamisi Kigwangalla amepongeza waandaji wa maonesho haya ya Nanenane Kitaifa (Kanda ya Ziwa Mashariki) kwa maandalizi mazuri ya pia amewapongeza Wakulima na Wafanyabiashara kwani kwa kushiriki maonesho haya wanapata fursa ya kujifunza na kuuza mazao yao.

Amesema sekta ya kilimo ni sekta muhimu kwani ndiyo sekta inayoajiri wananchi wengi ikifuatiwa na sekta ya utalii na inategemewa na Uchumi wa Viwanda kutoa malighafi za viwanda, huku akibainisha kuwa Utalii unachangia pato la Taifa kwa asilimia 17.6 , pia unachangia kwa zaidi ya 25% ya upatikanaji wa fedha za kigeni.
.
Mhe. Kigwangalla ameongeza kuwa mwaka 2015 kulikuwa na ongezeko la Watalii kutoka Milioni 1 hadi milioni 1.1, .Mwaka 2018 Watalii waliongezeka hadi kufikia  Milioni 1.6 na lengo likawa ni kufikia mwaka 2020 idadi iongezeke zaidi na kufikia watalii milioni mbili.

Naye Balozi wa Indonesia Prof.Dr.Ratlan Pardede amesema amefurahi kufika Mkoani Simiyu kwa mara ya pili sasa na Indonesia inashiriki Maonesho ya Nanenane ili kuimarisha uhusiano wake na Tanzania hususani katika kilimo.

“Nimefura sana kufika kwa mara ya pili sasa mkoani Simiyu tunashiriki  Nanenane kwa sababu tunataka kuimarisha uhusiano wetu na Mkoa wa Simiyu hususani katika kilimo, kusudi likiwa ni kuona kwa jinsi gani tunaweza kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa katika siku za usoni kwa manufaa ya nchi zote mbili yaani Tanzania na Indonesia” alisisitiza.
MWISHO

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akiwatambulisha Balozi wa Indonesia nchini Tanzania, Mhe.  Prof.Dkt..Ratlan Pardede na  Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Dkt.Hamisi Kigwangalla Agosti 04, 2019 kwa waandishi wa habari walipotembelea Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki,  viwanja vya Nanenane Nyakabindi Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akiwatambulisha Balozi wa Indonesia nchini Tanzania, Mhe.  Prof.Dkt..Ratlan Pardede na  Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Dkt.Hamisi Kigwangalla Agosti 04, 2019 kwa waandishi wa habari walipotembelea Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki,  viwanja vya Nanenane Nyakabindi Simiyu.
Balozi wa Indonesia nchini Tanzania, Mhe.  Prof.Dkt..Ratlan Pardede(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) mara baada ya kuwasili Bariadi, Agosti 04, 2019 ambapo amekuja kushiriki Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki,  viwanja vya Nanenane Nyakabindi Simiyu.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Dkt.Hamisi Kigwangalla akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) mara baada ya kuwasili Bariadi Agosti 04, 2019 ambapo amekuja kutembelea Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki,  viwanja vya Nanenane Nyakabindi Simiyu.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Dkt.Hamisi Kigwangalla (mwenye suti) akikagua vipando vya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) mara baada ya kuwasili Bariadi Agosti 04, 2019 kutembelea Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki,  viwanja vya Nanenane Nyakabindi Simiyu.
Balozi wa Indonesia nchini Tanzania, Mhe.  Prof.Dkt..Ratlan Pardede(wa tatu kulia) akiangalia viatu vilivyotengenezwa na Jeshi la Magereza mara baada ya kutembelea banda la la maonesho, wakati wa ziara yake ya kutembelea Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki,  viwanja vya Nanenane Nyakabindi Simiyu.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini(kushoto) akimuongoza Balozi wa Indonesia nchini Tanzania, Mhe.  Prof.Dkt..Ratlan Pardede(wa pili kulia) kutembelea vipando vya mazao ya Halmashauri za mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga wakati wa ziara yake ya kutembelea Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki,  viwanja vya Nanenane Nyakabindi Simiyu.
Balozi wa Indonesia nchini Tanzania, Mhe.  Prof.Dkt..Ratlan Pardede(wa pili kulia) akiangalia viatu vilivyotengenezwa na Jeshi la Magereza mara baada ya kutembelea banda la la maonesho, wakati wa ziara yake ya kutembelea Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki,  viwanja vya Nanenane Nyakabindi Simiyu.Baadhi ya wananchi wakiangalia huduma na bidhaa mbalimbli zinzotolewa na waoneshoaji katika mabanda ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki,  viwanja vya Nanenane Nyakabindi Simiyu.

 Baadhi ya wananchi wakiangalia huduma na bidhaa mbalimbli zinzotolewa na waoneshoaji katika mabanda ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki,  viwanja vya Nanenane Nyakabindi Simiyu.


Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Dkt.Hamisi Kigwangalla (mwenye suti) akipokea maelezo ya mradi wa ufugaji samaki kwa kutumia matanki na kilimo cha mboga mboga wakati akikagua vipando vya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) mara baada ya kuwasili Bariadi Agosti 04, 2019 kutembelea Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki,  viwanja vya Nanenane Nyakabindi Simiyu
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Dkt.Hamisi Kigwangalla (mwenye suti) akikagua vipando vya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) mara baada ya kuwasili Bariadi Agosti 04, 2019 kutembelea Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki,  viwanja vya Nanenane Nyakabindi Simiyu

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Dkt.Hamisi Kigwangalla (kulia) akipokea maelezo ya mradi wa kilimo kupitia kitalu nyumba(green house)  wakati akikagua vipando vya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Agosti 04, 2019 wakati wa ziara yake ya kutembelea Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki,  viwanja vya Nanenane Nyakabindi Simiyu.


Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Dkt.Hamisi Kigwangalla (mwenye suti) akipokea maelezo ya mradi wa ufugaji samaki kwa kutumia mabwawa  wakati alipotembelea vipando vya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Agosti 04, 2019 kutembelea Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki,  viwanja vya Nanenane Nyakabindi Simiyu.

Baadhi ya wananchi wakipata huduma kutoka kwa waoneshaji


Baadhi ya wananchi wakipata huduma kutoka kwa waoneshaji ambao ni Halmashauri ya Wilaya ya Itilima.
Kitalu nyumba kilichopo katika vipando ya  Jeshi la Magereza

Baadhi ya wananchi wakipata huduma kutoka kwa waoneshaji ambao ni Halmashauri ya Wilaya ya Itilima.
Kitalu nyumba kilichopo katika vipando ya  Jeshi la Magereza
Baadhi ya wananchi wakipata huduma na kununua bidhaa kutoka kwa waoneshaji ambao ni Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi.
Baadhi ya wananchi wakipata huduma na kununua bidhaa kutoka kwa waoneshaji ambao ni Halmashauri ya Mji wa  Bariadi.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!