Uongozi wa Mkoa wa Simiyu kupitia kwa
Katibu Tawala wa Mkoa, Bw. Jumanne Sagini umesitisha uamuzi wa Mkuu wa Wilaya
ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga, uliotolewa jana Agosti 14, 2019 ambapo watumishi
wote 137 wa Hospitali ya Mji wa Bariadi walitakiwa kukatwa mishahara yao kwa
ajili ya kuchangia fedha ya kununua mashine ya ULTRASOUND, iliyoibiwa katika
wodi ya wazazi hospitalini hapo badala yake ameagiza vyombo vya dola
vifanye uchunguzi kubaini aliyeiba mashine hiyo na hatua stahiki zichukuliwe.
Sagini
ameyasema hayo leo Agosti 15, 2019 wakati akizungumza na watumishi wa Hospitali
ya Halmashauri ya Mji wa Bariadi katika Ukumbi wa Hospitali hiyo Mjini Bariadi.
Amesema
uongozi wa Mkoa umetafakari na kuona kuwa si watumishi wote wa hospitali hiyo
wamehusika katika upotevu wa mashine hiyo kwa kuwa wanafanya kazi katika idara
tofauti na baadhi yao siku ya tukio hawakuwepo, hivyo ni vema vyombo vya dola
vikafanya uchunguzi kubaini waliohusika.
"
Uongozi wa Mkoa tunarekebisha baadhi ya hatua zilichukuliwa na Mhe. DC jana,
hili jambo haliwezi kuwa la watumishi wote 137, kama Serikali tunavyo vyombo
vya dola ambavyo kuna watu wanalipwa mishahara kwa kazi hizo za kiuchunguzi,
tunataka kifaa hicho kirejeshwe, vyombo hivi vifanye uchunguzi, vichukue hatua
kwa watakaobainika ikiwemo kupelekwa mahakamani" amesema.
Katika
hatua nyingine Sagini amewataka watumishi wa Hospitali ya Mji wa Bariadi
kuimarisha mfumo wa makabidhiano ya kazi na vifaa vya kazi ili kuwepo na
taarifa sahihi za wagonjwa na vifaa tiba kama utaratibu unavyotaka.
Kwa
upande wao watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi wamewashukuru viongozi wa
Mkoa wa Simiyu kwa kusitisha uamuzi wa awali ambao ungewaathiri kiuchumi
na kupunguza ari ya kufanya kazi hususani wale ambao hawajahusika na upotevu wa
mashine hiyo.
"
Tunamshukuru sana kiongozi wetu kwa msamaha aliotutolea kwa sababu tangu
jana tumelala kwa presha baada ya kuambiwa kuwa kila mtu alip, mimi uwezo wangu
mdogo na mshahara wangu ni mdogo nilikuwa sioni pesa ya kulipa hicho
kifaa;namshukuru Mungu kwa uamuzi wa viongozi wa mkoa yaani naongea kwa uchungu
mpaka nasikia kulia kwa furaha niliyonayo" amesema Frola
Katoyo Mtumishi katika idara ya dawa.
"Nimepokea
vizuri uamuzi uliofanywa na viongozi wetu wa mkoa kwa sababu maanuzi
yaliyotolewa jana kiuhalisia si kila mtumishi alipaswa kuhusishwa kwenye hili,
maana wengine walikuwa likizo, wengine hawakuwepo kazini, hivyo ni sahihi
kabisa kuviachia vyombo vya dola; nina uhakikia kuanzia leo watu watafanya kazi
maana jana utendaji kazi ulipungua baada ya kupata tu taarifa kuwa wanapaswa
kuchangia" alisema Simon Chisomeko Afisa Afya.
Kwa
upande wake Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE)
Mkoa wa Simiyu, Bi. Catherine Nyingi amesema Chama hicho kinaushukuru uongozi
wa mkoa kwa kutambua sheria, kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma na
wameiomba Serikali iendelee kuwa macho katika kusimamia sheria, kanuni na
taratibu.
Mashine
ya kupima magonjwa ya ndani ya mwili wa Binadamu (ULTRASOUND MACHINE)
iliripotiwa kuibiwa katika Wodi ya wazazi katika Hospitali ya Mji wa
Bariadi Agosti 05, 2019 na jana Agosti 14, 2019 Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akaagiza watumishi wote 137 wa Hospitali hiyo
wakatwe fedha kwenye mishahara yao ili mashine hiyo iliyoibiwa inunuliwe.
MWISHO
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne
Sagini akizungumza na watumishi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Bariadi,
leo Agosti 15, 2019 mjini Bariadi, kwa lengo la kutoa ufafanuzi juu ya
kusitisha uamuzi wa watumishi hao kuchangia mashine ya ULTRASOUND iliyoibiwa
Agosti 05, 2019 ambao ulitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo
Kiswaga hapo jana .
Watumishi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa
Bariadi, wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini leo
Agosti 15, 2019 mjini Bariadi, kwa lengo la kutoa ufafanuzi juu ya kusitisha
uamuzi wa watumishi hao kuchangia mashine ya ULTRASOUND iliyoibiwa Agosti 05,
2019 ambao ulitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga hapo jana.
Watumishi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa
Bariadi, wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini leo
Agosti 15, 2019 mjini Bariadi, kwa lengo la kutoa ufafanuzi juu ya kusitisha
uamuzi wa watumishi hao kuchangia mashine ya ULTRASOUND iliyoibiwa Agosti 05,
2019 ambao ulitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga hapo
jana.
Baadhi ya Viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama
Mkoani Simiyu wakiwa katika kikao na Watumishi wa Hospitali ya Halmashauri ya
Mji wa Bariadi, leo Agosti 15, 2019 mjini Bariadi, kwa lengo la kutoa
ufafanuzi juu ya kusitisha uamuzi wa watumishi hao kuchangia mashine ya
ULTRASOUND iliyoibiwa Agosti 05, 2019, ambao ulitolewa na Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga hapo jana.
Watumishi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa
Bariadi, wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini leo
Agosti 15, 2019 mjini Bariadi, kwa lengo la kutoa ufafanuzi juu ya kusitisha
uamuzi wa watumishi hao kuchangia mashine ya ULTRASOUND iliyoibiwa Agosti 05,
2019 ambao ulitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga hapo
jana.
Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na
Afya (TUGHE) Mkoa wa Simiyu, Bi. Catherine Nyingi akizungumza na waandishi wa
habari hawapo pichani mara baada ya kikao cha uongozi wa Mkoa wa Simiyu na
Watumishi wa Watumishi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Bariadi, leo
Agosti 15, 2019 mjini Bariadi.
Mtumishi Frola Katoyo akizungumza na waandishi wa
habari hawapo pichani mara baada ya kikao cha uongozi wa Mkoa wa Simiyu na Watumishi
wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Bariadi, leo Agosti 15, 2019 mjini
Bariadi.
0 comments:
Post a Comment