Wednesday, October 3, 2018

MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AKUTANA NA VIONGOZI SIMIYU KUJADILI NAMNA YA KUTANGAZA SHUGHULI ZA SERIKALI


Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt Hassan Abbas  amekutana na viongozi wa Mkoa wa Simiyu Mjini Bariadi,Oktoba 02, 2018 kwa lengo la kujadiliana namna ya kutangaza utekelezaji wa shughuli za Serikali.

Mkutano huo ulihusisha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi, Wakuu wa Taasisi na Wakuu wa Idara wa Halmashauri na Mkoa.

Katika mkutano huo, Dkt. Abbas aliwasisitiza viongozi hao umuhimu wa kutekeleza, kutangaza na kutetea shughuli na miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali..Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt Hassan Abbas  akizungumza na Viongozi wa Mkoa wa Simiyu katika mkutano uliofanyika Mjini Bariadi, Oktoba 02, 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka  akifungua mkutano kati ya Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt Hassan Abbas  na viongozi wa Mkoa wa huo, ambao ulifanyika Mjini Bariadi, Oktoba 02, 2018.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt Hassan Abbas(kulia)   akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Oktoba Mosi, 2018 wakati alipofika ofisi hapo (Mjini Bariadi) kuzungumza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (katikati) na Katibu Tawala Mkoa, Bw. Jumanne Sagini.
Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt Hassan Abbas(katikati)   akizungumza jambo na  Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga Oktoba Mosi, 2018 wakati alipofika ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mjini Bariadi kwa ajili ya maandalizi ya Mkutano wake na Viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakiongozwa na  Mhe. Anthony Mtaka (katikati) ambao ulifanyika Oktoba 02, 2018.
Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt Hassan Abbas(kushoto)   akizungumza jambo na  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (katikati) na Katibu Tawala Mkoa, Bw. Jumanne Sagini mara baada ya Mkutano wake na Viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakiongozwa na  Mhe. Anthony Mtaka (katikati) am Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt Hassan Abbas ambao ulifanyika Oktoba 02, 2018.
Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt Hassan Abbas(wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya Mkutano wake na Viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakiongozwa na  Mhe. Anthony Mtaka (wa nne kushoto) ambao ulifanyika Oktoba 02, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mhe. Dkt. Joseph Chilongani akichangia hoja katika mkutano wa Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt Hassan Abbas na Viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakiongozwa na  Mhe. Anthony Mtaka ambao ulifanyika Oktoba 02, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga(kulia) akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mhe. Robert Lweyo , wakati wa Mkutano wa Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt Hassan Abbas na Viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakiongozwa na  Mhe. Anthony Mtaka ambao ulifanyika Oktoba 02, 2018.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mhe. Robert Lweyo , akichangia hoja katika mkutano wa Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt Hassan Abbas na Viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakiongozwa na  Mhe. Anthony Mtaka ambao ulifanyika Oktoba 02, 2018.0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!