Wednesday, October 3, 2018

RC MTAKA APONGEZA TCRA KWA KUAGIZA VISIMBUZI KUONESHA CHANELI ZA TANZANIA BURE



Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka amewapongeza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kwa kuagiza ving’amuzi vyote vyenye leseni ya kutoa Huduma za Utangazaji kwa kwa Maudhui yanayotazamwa bila kulipia  kuonyesha chaneli za ndani bure.

Pongezi hizo amezitoa  wakati akifungua mkutano wa viongozi wa mkoa wa Simiyu. na baadhi ya viongozi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) uliofanyika kwa lengo la kujadili  Huduma za Utangazaji kwa Maudhui yanayotazamwa Bila Kulipia – FTA, kilichofanyika Oktoba 02, 2018 Mjini Bariadi..

“Niwapongeze sana TCRA kwa kuhakikisha kwamba, watu wanakuwa na uhuru wa kulipia kwenye chaneli wanazozihitaji lakini zile Televisheni zetu za ndani za kuangalia mambo yetu kama Watanzania wanazipata bure”  alisema Mtaka.

Amesema anaridhishwa na utendaji wa kazi wa TCRA kwa kuleta mabadiliko makubwa na kutoa wito kwa TCRA kuangalia gharama ya kulipia ving'amuzi kwa bei  nafuu ili kuwafikia wananchi wengi.

“Ukitaka kushindana kwenye dunia wekeza kwenye teknolojia, TCRA mtusaidie namna vyombo hivi vinavyofanya mawasiliano kwa Umma ambayo ndio chakula chetu cha kila siku wananchi wapate kwa urahisi, tusiwanyime watu fursa,  kama tunawapelekea umeme kwa elfu 27, mtu awe na uwezo wa kuuza kuku wake mmoja na akalipia king’amuzi”alisema.

 Naye Mhandisi. Francis Mihayo TCRA amesema Serikali kupitia TCRA amesema watu wamekuwa wakijuliza kwa nini chaneli ambazo zinatakiwa kuonekana bure zilizokuwa zinabebwa kwenye kisimbuzi cha kulipia, zimeamriwa zirudishwe kwenye visimbuzi vya watoa huduma wanaoruhusiwa kuzibeba chaneli hizo, pasipo malipo ndiyo maana wamelazimika kufanya mkutano huo. 

Amesema Baada ya watoa huduma wenye visimbuzi vya kulipia kuamriwa kutoa chaneli za ndani ambazo si za kulipia TCRA iliwatangazia wananchi  watoe taarifa zao binafsi na kuziwasilisha TCRA, ambazo ni jina , eneo analoishi, aina ya kisimbuzi ,namba ya kisimbuzi, namba ya kadi ya kisimbuzi, muda aliotumia kisimbuzi hicho na kiasi cha fedha ambacho amekuwa akilipia kila mwezi na kutuma kwenye barua pepe ya Mkurugezi Mkuu ambayo ni dg@tcra.go.tz.

Ameongeza kuwa hadi sasa Serikali kupitia TCRA inaendelea kukusanya taarifa ili wale waliokuwa wakitumia visimbuzi vyenye leseni ya kulipisha na vilikuwa vikibeba chaneli ambazo si za kulipisha baadaye itatoa maamuzi.

Amesisitiza kuwa TCRA ilitoa muda mpaka kufikia Septemba 05 2018 chaneli zote ambazo zilipaswa kuonekana bila kulipia zilitakiwa ziwe zinaoneshwa kwenye visimbuzi visivyolipisha lakini kulitokea changamoto ya tatizo la kiufundi ambalo lilipelekea chaneli hizo kuanza kurejeshwa taratibu.


Pamoja na kujibu maswali na kutolea ufafanuzi changamoto mbalimbali zilizowasilishwa na wajumbe wa Mkutano huo, Mhandisi Mihayo alitaja baadhi chaneli ambazo hazipaswi kulipiwa  kuwa ni (kwa mkoa wa Simiyu ) ni pamoja na TBC 1, ITV, Star TV, Channel Ten, EATV, Clouds, UHAI  na Bunge TV.

Akizungumza mara baada ya mkutano huo, Mkuu wa Kitengo cha Sheria katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Mwanahamisi Kawega aliishukuru TCRA kwa kutoa elimu jambo ambalo na namna ya kupata haki yao ya kupata taarifa.
MWISHO



Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akifungua  mkutano wa Viongozi wa Mkoa huo na baadhi ya viongozi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuhusu Huduma za Utangazaji kwa Maudhui yanayotazamwa Bila Kulipia – FTA, uliofanyika Oktoba 02, 2018 Mjini Bariadi. 



Mhandisi. Francis Mihayo kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) akiwasilisha mada kuhusu Huduma za Utangazaji kwa Maudhui yanayotazamwa Bila Kulipia – FTA, kwa Viongozi wa Mkoa wa Simiyu katika mkutano uliofanyika Oktoba 02, 2018 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi katika mkutano wa Viongozi wa Mkoa huo na baadhi ya viongozi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) uliofanyika kujadili Huduma za Utangazaji kwa Maudhui yanayotazamwa Bila Kulipia – FTA,  Oktoba 02, 2018 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mhe. Dkt. Joseph Chilongani  akichangia hoja katika   mkutano wa  Viongozi wa Mkoa wa Mkoa wa Simiyu na baadhi ya viongozi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) uliofanyika kujadili Huduma za Utangazaji kwa Maudhui yanayotazamwa Bila Kulipia – FTA,  Oktoba 02, 2018 Mjini Bariadi.
Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Simiyu, SSF. Crispin Rabiuzima akichangia hoja katika   mkutano wa Viongozi wa Mkoa wa Mkoa wa Simiyu na baadhi ya viongozi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) uliofanyika kujadili Huduma za Utangazaji kwa Maudhui yanayotazamwa Bila Kulipia – FTA,  Oktoba 02, 2018 Mjini Bariadi.


Baadhi ya viongozi wakifuatilia mjadala katika Mkutano wa Viongozi wa Mkoa wa Mkoa wa Simiyu na baadhi ya viongozi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) uliofanyika kujadili Huduma za Utangazaji kwa Maudhui yanayotazamwa Bila Kulipia – FTA,  Oktoba 02, 2018. 


Mkku wa Wilaya ya Meatu, Mhe. Dkt. Joseph Chilongani  akichangia hoja katika   Mkutano wa Viongozi wa Mkoa wa Mkoa wa Simiyu na baadhi ya viongozi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) uliofanyika kujadili Huduma za Utangazaji kwa Maudhui yanayotazamwa Bila Kulipia – FTA,Oktoba 02, 2018 Mjini Bariadi.

  

Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Dkt. Mabimbi akichangia hoja katika   Mkutano wa Viongozi wa Mkoa wa Mkoa wa Simiyu na baadhi ya viongozi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) uliofanyika kujadili Huduma za Utangazaji kwa Maudhui yanayotazamwa Bila Kulipia – FTA,  Oktoba 02, 2018 Mjini Bariadi.
 

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!