Friday, November 23, 2018

WAFANYABIASHARA WA UTURUKI WAONESHA NIA YA KUWEKEZA KATIKA KIWANDA CHA NGUO SIMIYU

Wafanyabiashara kutoka nchini Uturuki wameonesha nia na dhamira ya kuwekeza katika ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza nguo mkoani Simiyu ambacho kitakuwa na uwezo wa kuajiri watu zaidi ya 4000.


Hayo yamebainishwa katika kikao kati ya Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo ambaye aliambatana na Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na mwakilishi wa Wafanyabiashara wa Uturuki kutoka makampuni saba ya nchi hiyo, katika kikao maalum na viongozi wa Mkoa wa Simiyu, Wakuu wa Taasisi mbalimbali na jumuiya ya wafanyabiashara ya mkoa wa Simiyu, kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi.

Balozi Kiondo amesema Wafanyabiashara hao wanayo azma ya kuwekeza katika kiwanda cha kutengeneza nguo katika mnyororo mzima wa utengenezaji kutoka bidhaa ya awali ya pamba mpaka bidhaa ya mwisho kabisa, ambayo ni nguo kwa ubia(partineship) na Watanzania.

Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS amesema  mpaka sasa ni makampuni sita kutoka nchini humo yameonesha nia ya kuwekeza katika kiwanda cha nguo mkoani Simiyu na akaahidi kwenda kuwashawishi wafanyabiashara wenzake hivyo watakaporudi kwa mara nyingine  makapuni mengi yatakuja kuwekeza katika viwanda vya nguo.

“Nikirudi nyumbani kama kiongozi wa wafanyabiashara nitawashawishi wengine pia waje wawekeze katika viwanda vya nguo,ombi langu kwenu ni kwamba ninahitaji Mfanyabiashara Mtanzania ambaye tutashirikiana naye katika uwekezaji huu(partinership), lakini niwahakikishie tu kuwa katika kiwanda tutakachojenga mashine na vifaa vyote vipo tayari kule Uturuki” alisema  Cengiz.

Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka amewahakikishia wafanyabiashara hao upatikanaji wa soko la uhakika la nguo zitakazotengenezwa, pamoja na upatikanaji wa malighafi kwa kuwa Simiyu ndiyo mkoa unaozalisha zaidi ya asilimia 55 ya pamba yote nchini, ambapo kwa  mwaka 2018 Simiyu imezalisha takribani kilo milioni 131.

Ameongeza kuwa pamoja na uhakika wa soko na malighafi  Simiyu ina viwanda vingi  vya kuchambua pamba, ardhi itatolewa bure, miundombinu muhimu yote ipo, utashi wa kisiasa kwa viongozi wa wilaya upo, hivyo akawatoa hofu wawekezaji hao na kuwaeleza kuwa mkoa utashirikiana nao, huku akiomba waone uwezekano wa kuwekeza katika uongezaji thamani wa mazao ya mifugo kama ngozi na nyama

Mkurugenzi wa Kiwanda cha kuchambua Pamba cha Alliance Ginnery, Bw. Boaz Ogola amesema wako tayari kushirikiana na mwekezaji huyo, huku akibainisha kuwa kuanzishwa kwa kiwanda hicho kitawasaidia wanaochambua pamba na wakulima kupata faida ikilinganishwa na sasa ambapo zaidi ya asilimia 75 ya pamba inasafirishwa nje ya nchi.

Naye Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Mkoa wa Simiyu, Mhe. Najlu Silanga ameahidi ushirikiano kwa wawekezaji aho kutoka Uturuki na kuiomba Wizara ya Viwanda, Baiashara na Uwekezaji kuzitambu na kusughuliakia changamoto mbalimbali za wafanyabiashara hapa nchini .

Wakati huo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda  (TIRDO) Prof. Mkumbukwa Mtambo amepongeza Mkoa wa Simiyu kwa kuzingatia Utafiti na maendeleo katika Viwanda, huku akisisitiza kuwa ili viwanda vinavyoanzishwa viweze kuwa endelevu ipo haja ya kufanya utafiti na maendeleo na akaahidi kuwa Taasisi hiyo itaendelea kushirikiana na Simiyu katika tafiti mbalimbali  za  maendeleo ya viwanda.

MWISHO




Kutoka kulia Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Edwin Mhede wakiteta jambo mara baada ya kumalizika kwa kikao kati ya viongozi na watendaji wa Serikali na ujumbe wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza katika kikao cha viongozi wa Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo na Mwenyekiti na mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS,  kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi.

Mwenyekiti na mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS, 

akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo katika kikao kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi  
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Mkoa wa Simiyu ambaye pia ni Mbunge wa Itilima, Mhe. Njalu Silanga akichangia hoja katika viongozi wa Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo na Mwenyekiti na mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS,  kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili uwekezaji katika viwanda vya nguo mkoani humo.
Mkurugenzi wa Kiwanda cha kuchambua Pamba cha Alliance Ginnery, Bw. Boaz Ogola akichangia hoja katika viongozi wa Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo na Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS,  kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili uwekezaji katika viwanda vya nguo mkoani humo.
Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo akizungumza viongozi wa Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali katika kikao kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili uwekezaji katika viwanda vya nguo unaotarajiwa kufanywa na Wafanyabiashara kutoka nchini Uturuki katika mkoa wa Simiyu.




Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa tatu kushoto)  akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo(wa pili kushoto), na Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na  mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS( wa tatu kulia),  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Edwin Mhede( wa pili kulia) na viongozi wa Serikali pamoja na wafanyabiashara wa mkoa huo, mara baada ya kuhitimisha kikao mjini Bariadi kilichofanyika kujadili uwekezaji katika viwanda vya nguo.

Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera akichangia hoja katika kikao cha viongozi wa Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo na Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS,  kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili uwekezaji katika viwanda vya nguo mkoani humo.

Bw. Gungu Silanga mmoja wa wafanyabiashara mkoani Simiyu, akichangia hoja katika kikao cha viongozi wa Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo na Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS,  kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili uwekezaji katika viwanda vya nguo mkoani humo.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akichangia hoja katika kikao cha  viongozi wa Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo na Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS,  kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili uwekezaji katika viwanda vya nguo mkoani humo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda(TIRDO), Prof. Mkumbukwa Mtambo, akichangia hoja katika kikao cha viongozi wa Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo na Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS,  kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili uwekezaji katika viwanda vya nguo mkoani humo.
Diwani wa Kata ya Zanzui Wilayani Maswa, Mhe. Jeremia Shigala akichangia hoja katika kikao cha viongozi wa Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo na Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS,  kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili uwekezaji katika viwanda vya nguo mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza katika kikao cha viongozi wa Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo na Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS,  kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo  (SIDO) Prof. Sylvester Mpanduji, akichangia hoja katika kikao cha viongozi wa Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo na Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS  kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili uwekezaji katika viwanda vya nguo mkoani humo.
Kutoka kushoto Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Edwin Mhede, Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo na Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini wakionesha nakala za Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Simiyu, baada ya viongozi hao kukabidhiwa mwongozo huo Novemba 22, 2018.
Afisa Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Kija Kayenze akiwasilisha taarifa ya fursa za uwekezaji katika kikao cha viongozi wa Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo na Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili uwekezaji katika viwanda vya nguo mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akitoa taarifa ya mkoa wakati wa ugeni wa Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo aliyembatana na, Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki Bw. Cengiz ERTAS, Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi.
Bw. John Sabo mmoja wa wafanyabiashara mkoani Simiyu, akichangia hoja katika kikao cha viongozi wa Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo na Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS,  kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili uwekezaji katika viwanda vya nguo mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa tatu kushoto)  akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo(wa pili kushoto), Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS (wa nne  kulia),  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Edwin Mhede( wa tatu kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo  (SIDO) Prof. Sylvester Mpanduji(kulia) na viongozi wengine wa Serikali wa mkoa huo, mara baada ya kuhitimisha kikao mjini Bariadi kilichofanyika kujadili uwekezaji katika viwanda vya nguo.




Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akichangia hoja katika kikao cha viongozi wa Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo na Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS,  kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili uwekezaji katika viwanda vya nguo mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza katika kikao cha viongozi wa Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo na Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS,  kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi.
Kushoto Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka, ( kulia) Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Edwin Mhede wakiteta jambo, mara baada ya kuhitimisha kikao mjini Bariadi kilichofanyika kujadili uwekezaji katika viwanda vya nguo.

WAZIRI KAIRUKI AAGIZA SUMA JKT KUKAMILISHA UJENZI KITUO CHA UMAHIRI JANUARI 2019

Waziri wa Madini Angela Kairuki amemwaagiza Mkandarasi anayejenga Kituo cha umahiri cha Madini mkoani SIMIYU, Shirika  la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT) kukamilisha ujenzi ifikapo Januari 2019, ili kiweze kuwasaidia wachimbaji Katika masuala mbalimbali ikiwa ni kupata mafunzo ya uchimbaji wenye tija.


Kairuki ametoa agizo hilo alipotembelea na kuona hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa Kituo hicho unaoendelea katika eneo la Nyaumata makao makuu ya mkoa wa SIMIYU Mjini Bariadi, Novemba 22, 2018.
.
Kairuki amesisitiza usimamizi uimarishwe zaidi na fedha ziweze kutolewa kwa wakati ili jengo hilo liishe katika muda uliopangwa, huku akiupongeza uongozi wa mkoa wa SIMIYU kwa kukubali kutenga eneo la ujenzi wa kituo hicho.

Katika hatua nyingine Waziri Kairuki amesema Wizara ya madini itahakikisha inawasadia wachimbaji wa chumvi mkoani Simiyu ili chumvi inayozalishwa iweze kuwa bora na yenye uwezo wa  kushindana katika soko, huku akiwakumbusha wenye  leseni za Madini kuzitumia.

“ Kama Wizara tutashirikina na mkoa wa Simiyu katika kuhakikisha wachimbaji wanachimba kwa tija lakini pia kuleta migodi ya mifano na namna za nyingine  ya uchenjuaji, pia  ikiwemo na hiyo chumvi, ambayo tutahitaji izalishwe  katika ubora, ushindani na kuwekwa katika vifungashio bora”

“Tuendelee kuhamasisha wachimbaji wengi zaidi kuendelea kuchimba wasishikilie tu leseni,tunataka kuona ule msamaha uliotolewa na Mhe. Rais kutoka tozo 16 hadi kufikia tozo 09 kwenye chumvi uwe na faida kwao” alisema Waziri Kairuki.
.
Kwa upande wake Mkurugenzi mwendeshaji kutoka SUMA JKT, Mhandisi Morgan Nyonyi amesema watatekeleza maelekezo ya Mhe.Waziri na kubainisha kuwa hadi sasa ujenzi wa jengo hilo umefikia asilimia 35, kufikia Januari 22, 2019 litakuwa limekamilika na mpaka kukamilika kwa litagharimu takribani shilingi bilioni 1.3.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka uwepo wa kituo cha Umahiri Mkoani hapa utasaidia kutoa mafunzo kwa wachimbaji wadogo na wakubwa wa chumvi katika Wilaya ya Meatu, pamoja na wazalishaji wengine kwa ujumla ambao watajikita katika utengenezaji wa chumvi hali itakayosaidia wananchi Simiyu na maeneo mengine nchini kutumia chumvi itakayozalishwa Meatu badala ya kuagiza kutoka nje ya nchi.

Ameongeza kuwa upembuzi yakinifu juu ya uanzishwaji wa kiwanda cha kutengeneza chumvi wilayani Meatu umeshafanyiwa upembuzi yakinifu na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kijamii na Kiuchumi (ESRF) na unatarajiwa kuwa mradi mwingine mkubwa wa Wilaya hiyo baada ya mradi wa kiwanda cha kusindika maziwa.

Aidha, amesema kukamilika kwa kituo hicho kutachangia kutoa mwanya na fursa kwa wananchi wa Simiyu kuwa na uwekezaji mwingine(madini) zaidi ya kilimo na mifugo, huku akibainisha kuwa kitachangia pia kukaribisha wawekezaji wengi kutokana na kuwepo kwa uhakika wa mahali pa kupata mafunzo na kupima sampuli mbalimba za madini .
MWISHO


Waziri wa Madini, Mhe. Angela Kairuki akizungumzana viongozi wa Mkoa wa Simiyu na Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa(SUMA JKT) mara baada ya kutembelea eneo la Ujenzi wa Kituo cha Umahiri cha mkoa wa Simiyu kuona hatua  iliyofikiwa katika Ujenzi wa Kituo hicho Mjini Bariadi, Novemba 22, 2018.
Kushoto ni Mtaalam kutoka Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa(SUMA JKT)   akitoa maelezo kwa Waziri wa Madini, Mhe. Angela Kairuki juu ya hatua  iliyofikiwa katika Ujenzi wa Kituo cha Umahiri cha mkoa wa Simiyu, wakati alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa Kituo hicho Mjini Bariadi Novemba 22, 2018.
 Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) akimweleza jambo Waziri wa Madini, Mhe. Angela Kairuki wakati alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa Kituo cha Umahiri Mjini Bariadi Novemba 22, 2018. 
Waziri wa Madini, Mhe. Angela Kairuki akiwa na viongozi wengine wakati alipotembelea eneo la Ujenzi wa Kituo cha Umahiri cha mkoa wa Simiyu kuona hatua  iliyofikiwa katika Ujenzi wa Kituo hicho Mjini Bariadi, Novemba 22, 2018.
 Waziri wa Madini, Mhe. Angela Kairuki akiwa na viongozi wengine wakielekea katika  eneo la Ujenzi wa Kituo cha Umahiri cha mkoa wa Simiyu kuona hatua  iliyofikiwa katika Ujenzi wa Kituo hicho Mjini Bariadi, Novemba 22, 2018. 



Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka( wa pili kushoto) akimweleza jambo Waziri wa Madini, Mhe. Angela Kairuki wakati alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa Kituo cha Umahiri Mjini Bariadi Novemba 22, 2018.



Waziri wa Madini, Mhe. Angela Kairuki(wa tano kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu, SUMA JKT na Wizara ya Madini mara baada ya kutembelea eneo la Ujenzi wa Kituo cha Umahiri cha mkoa wa Simiyu kuona hatua  iliyofikiwa katika Ujenzi wa Kituo hicho Mjini Bariadi, Novemba 22, 2018.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) akizungumza na  Waziri wa Madini, Mhe. Angela Kairuki wakati alipofika ofisini kwake kabla ya kuanza  ziara ya kukagua ujenzi wa Kituo cha Umahiri cha Mkoa wa Simiyu Mjini Bariadi Novemba 22, 2018.
 Waziri wa Madini, Mhe. Angela Kairuki(kushoto) akiwaonesha kitu Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(katikati) na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Simiyu, Bw. Adili Elinipenda, mara baada ya kutembelea eneo la Ujenzi wa Kituo cha Umahiri cha mkoa wa Simiyu kuona hatua  iliyofikiwa katika Ujenzi wa Kituo hicho Mjini Bariadi, Novemba 22, 2018. 


Tuesday, November 13, 2018

WAKURUGENZI WATAKIWA KUZINGATIA AFUA ZA LISHE KATIKA BAJETI ZA HALMASHAURI KUKABILIANA NA UDUMAVU KWA WATOTO



Kuelekea katika kipindi cha maandalizi ya bajeti ya mwaka 2019/2020 wito umetolewa kwa  Wakurugenzi wa Halmashauri mkoani Simiyu na maeneo mengine kote nchini kuyapa kipaumbele masuala ya Lishe katika mipango na bajeti za Halmashauri zao, ili kukabiliana na tatizo la udumavu kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Msaidizi Sera, kutoka Ofisi ya Raisi TAMISEMI, Bw.Eleuter Kihwele wakati mafunzo maalum yaliyotolewa kwa baadhi ya viongozi na maafisa Lishe, katika kikao cha Maandalizi ya Mipango ya Bajeti ya Afua za Lishe Mkoani Simiyu kwa mwaka 2019/2020 kilichofanyika Mjini Bariadi, Novemba 12, 2018.

Kihwele amesema takribani asilimia 34 ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano nchi nzima wana udumavu, hivyo ipo haja ya kutilia mkazo suala la lishe ili kutoathiri maendeleo ya ukuaji wa watoto, uwezo wao wa kufikiri na maendeleo yao kitaaluma(shuleni).

“Asilimia 34 ya watoto wa  nchi nzima wenye umri chini ya miaka mitano wana utapiamlo, suala hili linaathiri sana watoto, mfano matokeo yao shuleni na uwezo wa kufikiri, ndio maana serikali imeweka lishe kama kipaumbele na Ofisi ya Rais TAMISEMI kama wasimamizi tunapita kwenye Halmashauri nchi nzima kuhamasisha uzingatiaji wa masuala ya lishe katika bajeti ya mwaka 2019/2020” alisema.

Ameongeza kuwa katika mafunzo yanayotolewa na Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa Viongozi pia yamelenga  kuwakumbusha juu ya utekelezaji wa vipengele vya mikataba ya afua za lishe iliyosainiwa katia ya  Wakuu wa Mikoa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI na kutenga shilingi 1000 kwa kila mtoto mwenye umri chini ya miaka mitano katika bajeti zao.

Naye Afisa Lishe kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Bi. Mariam Nakuwa ametoa wito  kwa Halmashauri kutenga  fedha kwa ajili ya masuala ya lishe kwa kuzingatia miongozo na kuhakikisha fedha zinazotengwa zinatumika katika shughuli zilizopangwa ili kuondokana na tatizo la utapiamlo.

Aidha, Bi. Mariam amesema pamoja na kukabiliana na tatizo la utapiamlo fedha hizo zielekezwe katika huduma za utoaji wa virutubisho vya nyongeza kama vile virutubisho vya Vitamini A na vidonge vya kuongeza wekundu wa damu kwa akina mama wajawazito.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa, Bw. Jumanne Sagini aliwasisitiza Wakurugenzi wa Halmashauri mkoani Simiyu kuyachukulia masuala ya lishe kama kipaumbele, huku akiwataka kuhakikisha wanafanya vikao vya kamati za lishe za wilaya kila baada ya miezi mitatu kama ilivyoanishwa  katika miongozo.

Diwani wa Kata ya Dutwa  Mhe.Mapolu Mkingwa akizungumza kwa niaba ya  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Mhe.Richard Buyamba amesema maelekezo na mafunzo waliyoyapata watayapelekea katika Mabaraza ya madiwani na kuhakikisha mipango na bajeti zinazopitishwa zinazingatia umuhimu wa afua za lishe.

Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe amesisitiza viongozi na watendaji wakiwemo wajumbe wa kamati za lishe kubadilika na kuachana na mazoea katika kufanya ufuatiliaji na kutekeleza mipango ya masuala ya lishe badala yake wafanye kazi kulingana na miongozo ili kuwa na matokeo mazuri katika masuala ya lishe.

Timu ya Wataalam kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI ipo katika ziara ya kuhamasisha Viongozi katika Halmshauri na Mikoa kuzingatia vipaumbele kwenye maeneo ya lishe na kupanga mipango ya bajeti inayojibu changamoto za lishe, ili kufikia malengo ya  mikataba ambayo Wakuu wa Mikoa walisaini na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI kwenye usimamizi wa afua za lishe katika maeneo yao.
MWISHO



Mkurugenzi Msaidizi Sera, kutoka Ofisi ya Raisi TAMISEMI, Bw.Eleuter Kihwele  akizungumza na baadhi ya viongozi  na Wataalam Lishe wa mkoa wa Simiyu, katika kikao cha Maandalizi ya Mipango ya Bajeti ya Afua za Lishe Mkoani Simiyu kwa mwaka 2019/2020 kilichofanyika Mjini Bariadi, Novemba 12, 2018.


Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akisisitiza jambo katika kikao cha Maandalizi ya Mipango ya Bajeti ya Afua za Lishe Mkoani Simiyu kwa mwaka 2019/2020 kilichofanyika Mjini Bariadi, Novemba 12, 2018.

Afisa Lishe kutoka Ofisi ya Raisi TAMISEMI, Bi. Mariam Nakuwa   akiwasilisha mada kuhusu mipango na bajeti ya masuala ya lishe Mkoani Simiyu kwa baadhi ya viongozi  na Wataalam Lishe wa mkoa wa Simiyu, katika kikao cha Maandalizi ya Mipango ya Bajeti ya Afua za Lishe kwa mwaka 2019/2020 kilichofanyika Mjini Bariadi, Novemba 12, 2018.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Bw. Kai.B. Mbaruk akizungumza na baadhi ya viongozi  na Wataalam Lishe wa mkoa wa Simiyu, katika kikao cha Maandalizi ya Mipango ya Bajeti ya Afua za Lishe Mkoani Simiyu kwa mwaka 2019/2020 kilichofanyika Mjini Bariadi, Novemba 12, 2018 wakati akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Simiyu.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mhe. Martin Singibala akichangia hoja katika kikao cha Maandalizi ya Mipango ya Bajeti ya Afua za Lishe Mkoani Simiyu kwa mwaka 2019/2020 kilichofanyika Mjini Bariadi, Novemba 12, 2018 wakati akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Simiyu.
Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mhe. Dkt. Joseph Chilongani akichangia hoja katika kikao cha Maandalizi ya Mipango ya Bajeti ya Afua za Lishe Mkoani Simiyu kwa mwaka 2019/2020 kilichofanyika Mjini Bariadi, Novemba 12, 2018 wakati akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Simiyu.
Diwani wa Kata ya Dutwa  Mhe.Mapolu Nunde Mkingwa akichangia hoja katika kikao cha Maandalizi ya Mipango ya Bajeti ya Afua za Lishe Mkoani Simiyu kwa mwaka 2019/2020 kilichofanyika Mjini Bariadi, Novemba 12, 2018, ambapo alimwakilisha Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Mhe.Richard Buyamba.
Baadhi ya viongozi na wataalam kutoka Mkoa wa Simiyu na Ofisi ya Rais TAMISEMI wakifuatilia hoja mbalimbali katika kikao cha Maandalizi ya Mipango ya Bajeti ya Afua za Lishe Mkoani Simiyu kwa mwaka 2019/2020 kilichofanyika Mjini Bariadi, Novemba 12, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt.Seif Shekalaghe akichangia hoja katika kikao cha Maandalizi ya Mipango ya Bajeti ya Afua za Lishe kwa mwaka 2019/2020 Mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi, Novemba 12, 2018.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mhe. Martin Singibala akichangia hoja katika kikao cha Maandalizi ya Mipango ya Bajeti ya Afua za Lishe kwa mwaka 2019/2020 Mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi, Novemba 12, 2018.

RAS SIMIYU: USHIRIKI WA MICHEZO KWA WATUMISHI UNAONGEZA ARI YA UTENDAJI KAZI

Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amesema ushiriki katika michezo kwa watumishi ni moja ya njia za kuongeza ari ya utendaji kazi katika maeneo yao.

Sagini ameyasema hayo mwishoni mwa wiki Novemba 10, 2018 jioni wakati akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Simiyu na Walimu wa Manispaa ya Musoma mkoani Mara mara baada ya kumalizika kwa mechi ya kirafiki kati ya watumishi hao iliyochezwa katika Uwanja wa Posta Mjini Musoma, ambapo wenyeji Timu ya Walimu walikubali kichapo cha goli nne kwa tatu kutoka kwa Timu ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.\

“Mtu aliye na mwili wenye afya, akili yenye afya, aliye na uwezo wa kuruka na kuwepa ngwala kama nilivyokuwa nawaona hapa ni lazima hata katika kazi zake atafanya vizuri” alisema Sagini.

Aidha, Sagini ametoa wito kwa Maafisa Masuuli katika Ofisi za Wakuu wa Mikoa na Halmashauri kuwaunga mkono watumishi wao katika masuala ya michezo kwa kuwezesha wanapohitaji msaada kwao hususani katika suala la kuwawezesha kifedha, ili waweze kushiriki michezo mbambali ambayo pia inawasaidia kuimarisha afya zao na kuwaepusha na magonjwa yasiyoambukiza.

Akitoa shukrani kwa Timu ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Timu ya Walimu Manispaa ya Musoma kucheza mchezo huo  kwa nidhamu ya hali juu, Afisa Michezo wa Mkoa wa Mara, Bw. Evance Sangawe amesema nidhamu iliyooneshwa ni ishara kwamba watumishi hao wa Umma wanaweza kufanya kazi kwa kujituma bila kusimamiwa.

Kwa upande wake Kocha Msaidizi wa Timu ya Walimu wa Manispaa ya Musoma, Mwl. Yisambi Mwazembe amesema mechi za kirafiki zina umuhimu mkubwa kwa watumishi wa umma kwani zina nafasi kubwa ya kuwakutanisha watumishi ambao walioachana muda mrefu shuleni, vyuoni na hata katika maeneo mengine ya kazi zao.

Naye Nahodha wa Timu ya Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Elias Sebastian amesema mechi hiyo ya kirafiki imewakutanisha na  watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Simiyu na watumishi wa Manispaa ya Musoma ambao hawajawahi kuonana hapo awali, hivyo imechangia watumishi hao  kufahamiana na wenzao.
MWISHO

Baadhi ya wachezaji wa Timu ya Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu(wenye jezi za bluu na nyeupe) na Timu ya Walimu wa Manispaa ya Musoma (wenye jezi nyekundu) wakiwa katika mnyukano mkali wakati wa mechi ya kirafiki iliyochezwa mwisho mwa wiki katika Uwanja wa Posta Mjini Musoma, ambapo Timu ya Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu iliibuka kidedea kwa goli nne kwa tatu dhidi ya wapinzani wao.
Kikosi cha Timu ya Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu wakiwa katika picha ya pamoja na Kocha wao Bw. Justine Mnyandwa (kulia) kabla ya kuanza kwa mechi ya kirafiki na Timu ya Walimu wa Manispaa ya Musoma ,iliyochezwa mwisho mwa wiki katika Uwanja wa Posta Mjini Musoma, ambapo Timu hiyo iliibuka kidedea kwakuichapa timu pinzani  goli nne kwa tatu.
Kikosi cha Timu ya Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu(wenye jezi za bluu na nyeupe) na Timu ya Walimu wa Manispaa ya Musoma (wenye jezi nyekundu) wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mechi ya kirafiki,iliyochezwa mwisho mwa wiki katika Uwanja wa Posta Mjini Musoma, ambapo Timu ya Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu iliibuka kidedea kwa kuichapa timu pinzani  goli nne kwa tatu.

Katibu Tawala wa mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (mwenye trakisuti ya bluu aliyeinua mkono wa kulia juu) akiwa katika picha ya pamoja na Timu ya Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na mashabiki wa timu hiyo mara baada ya mechi ya kirafiki kati ya timu hiyo na Timu ya Walimu wa Manispaa ya Musoma,  iliyochezwa mwisho mwa wiki katika Uwanja wa Posta Mjini Musoma, ambapo Timu ya Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu iliibuka kidedea kwa goli nne kwa tatu dhidi ya wapinzani wao.
Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Mara(kushoto) na Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini wakifurahia jambo, mara baada ya mechi ya kirafiki kati ya Timu ya Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na Timu ya Walimu wa Manispaa ya Musoma,  iliyochezwa mwisho mwa wiki katika Uwanja wa Posta Mjini Musoma kumalizika , ambapo Timu ya Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu iliibuka kidedea kwa goli nne kwa tatu dhidi ya wapinzani wao.
Afisa Michezo wa Mkoa wa Mara, Bw.  Evance Sangawe akizungumza na wachezaji wa timu ya Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na Timu ya Walimu wa Manispaa ya Musoma, mara baada ya mechi ya kirafiki iliyochezwa Musoma kati ya timu hizo mwisho mwa wiki katika Uwanja wa Posta Mjini kumalizika.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akizungumza na wachezaji wa Timu ya Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu mjini Bariadi  kabla ya safari ya kuelekea Musoma kwa ajili ya kucheza mechi ya kirafiki na Timu ya Walimu wa Manispaa ya Musoma,  iliyochezwa mwishoni mwa wiki katika Uwanja wa Posta Mjini  Musoma.
 Baadhi ya Mashabiki na Watumishi wa Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Simiyu wakiishangilia ushindi wa goli nne kwa tatu ambao Timu ya Watumishi wa Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Simiyu iliupata dhidi ya wapinzani wao Timu  ya Walimu Manispaa ya Musoma katika Mechi ya kirafiki ilichezwa katika Uwanja wa Posta Mjini  Musoma mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya Mashabiki na Watumishi wa Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Simiyu wakiishangilia ushindi wa goli nne kwa tatu ambao Timu ya Watumishi wa Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Simiyu iliupata dhidi ya wapinzani wao Timu  ya Walimu Manispaa ya Musoma katika Mechi ya kirafiki ilichezwa katika Uwanja wa Posta Mjini  Musoma mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya Mashabiki na Watumishi wa Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Simiyu wakiishangilia ushindi wa goli nne kwa tatu ambao Timu ya Watumishi wa Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Simiyu iliupata dhidi ya wapinzani wao Timu  ya Walimu Manispaa ya Musoma katika Mechi ya kirafiki ilichezwa katika Uwanja wa Posta Mjini  Musoma mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wachezaji wa Timu ya Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu(wenye jezi za bluu na nyeupe) na Timu ya Walimu wa Manispaa ya Musoma (wenye jezi nyekundu) wakiwa katika mnyukano mkali wakati wa mechi ya kirafiki iliyochezwa mwisho mwa wiki katika Uwanja wa Posta Mjini Musoma, ambapo Timu ya Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu iliibuka kidedea kwa goli nne kwa tatu dhidi ya wapinzani wao.


Tuesday, November 6, 2018

SIMIYU YAZINDUA MFUMO WA MSHITIRI MMOJA KATIKA DAWA NA VIFAA TIBA (JAZIA)

Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini  amezindua rasmi mfumo wa ununuzi wa dawa na vifaa tiba kupitia kwa mshitiri mmoja wa mkoa ujulikanao kama JAZIA, uliobuniwa kuboresha upatikanaji wa dawa, vifaa tiba, vifaa vya maabara na uchunguzi katika vituo vya kutolea huduma za afya vya Serikali ngazi ya Mkoa na Halmashauri.


Akizindua mfumo huo Novemba 05, 2018 Mjini Bariadi Sagini amesema mfumo wa JAZIA si mbadala wa Bohari ya Dawa (MSD) bali unalenga kuziba upungufu wa dawa, vifaa tiba, vifaa vya maabara na uchunguzi katika Bohari ya Dawa (MSD).

“JAZIA ni mfumo uliobuniwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na wataalam washauri ili kuweza kuboresha upatikanaji wa dawa, vifaa tiba, vifaa vya maabara na uchunguzi katika vituo vya kutolea huduma za afya vya Serikali ngazi ya Mkoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa, JAZIA si mbadala wa MSD bali ni msaidizi wa MSD inapokuwa haina bidhaa husika.” alisema.

Aidha, Sagini alibainisha kuwa mfumo huu utasaidia kupunguza gharama na bei ya upatikanaji wa dawa kwani bei za dawa na vifaa tiba zitalingana na bei ya soko na sio matakwa binafsi ya wazabuni.

Aliongeza kuwa mfumo huo utapunguza urasimu uliokuwepo wa namna ya kununua dawa nje ya MSD na hivyo kusaidia dawa kupatikana kwa muda mfupi huku akiwataka Waganga wafawidhi wa vituo vyote vya kutolea huduma za afya kuagiza dawa na vifaa tiba mapema wanapoona vinapungua kabla ya kusubiri vifaa hivyo na dawa kuisha kabisa.

Kwa upande wake Mratibu wa Mfumo wa JAZIA Mkoa wa Simiyu, Mfamasia Oscar Tenganamba amesema mfumo huu ulifanyiwa majaribio katika mikoa ya Dodoma, Shinyanga na Morogoro na kuonesha mafanikio makubwa na sasa hivi unatumika katika mikoa yote Tanzania Bara.

Naye mmoja wa wazabuni walioungana na kuwa mshitiri mmoja wa Mkoa katika dawa na Vifaa Tiba (JAZIA) ambaye ni Mkurugenzi wa Operesheni kutoka Kampuni ya Total Health Lab ya jijini Dar es salaam ,  Crispin Mtete amesema kampuni yake na Kampuni ya Mufuruki Traders Company Ltd ya jijini Mwanza zitatoa huduma bora kwa kuzingatia bei elekezi kama mkataba unavyoelekeza.

Mfumo wa JAZIA utatumia mzabuni mmoja aliyechaguliwa kwa ushindani kujazia dawa na vifaa tiba vinavyokosekana katika Bohari ya Dawa (MSD).

MWISHO

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (katikati) akisaini mkataba wa mshitiri mmoja wa Mkoa katika dawa na Vifaa Tiba(JAZIA), Novemba 05, 2018  katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu Mjini Bariadi, waliosimama kushuhudia ni Baadhi ya Wenyeviti wa Halmashauri za Mkoa wa Simiyu.
Mkurugenzi wa Operesheni kutoka Kampuni ya Total Health Lab ya jijini Dar es salaam ,  Crispin Mtete(kulia)  na Mkurugenzi wa Mufuruki Traders Company Ltd ya jijini Mwanza, Khalifa Mufuruki wakisaini mkataba Novemba 05, 2018 kama wazabuni walioungana kama mshitiri mmoja wa mkoa wa Simiyu katika kutoa huduma za dawa na vifaa tiba , katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu Mjini Bariadi.
Mkurugenzi wa Mufuruki Traders Company Ltd ya jijini Mwanza, Khalifa Mufuruki akizungumza jambo katika uzinduzi rasmi wa mshitiri mmoja wa mkoa katika dawa na vifaa  tiba “ JAZIA” uliofanyika Novemba 05, 2018  katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu Mjini Bariadi.



Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, ASF. James John akichangia hoja katika uzinduzi  wa mshitiri mmoja wa mkoa katika dawa na vifaa  tiba “ JAZIA” uliofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu Mjini Bariadi.


Viongozi mbalimbali wa Halmashauri za Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi rasmi wa mshitiri mmoja wa mkoa katika dawa na vifaa  tiba “ JAZIA” uliofanyika Novemba 05, 2018 katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu Mjini Bariadi.

Kutoka kulia, Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Anderson Kabuko, Mkurugenzi wa Halmashauri  ya Wilaya ya Bariadi, ASF. James John, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, Mariano Mwanyigu, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Bariadi, Melkizedeck Humbe na Katibu Tawala wa Mkoa, Jumanne Sagini  wakisaini mkataba wa mshitiri mmoja wa mkoa katika dawa na vifaa  tiba “ JAZIA”, Novemba 05, 2018 mjini Bariadi.

Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Dkt. Mike Mabimbi akichangia hoja katika uzinduzi rasmi wa mshitiri mmoja wa mkoa katika dawa na vifaa  tiba “ JAZIA” uliofanyika Novemba 05, 2018  katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu Mjini Bariadi.
Mratibu wa Mfumo wa mshitiri mmoja wa mkoa katika dawa na vifaa  tiba “ JAZIA”, Oscar Tenganamba (kulia) akiteta jambo na Katibu Tawala wa Mkoa, Bw. Jumanne Sagini katika uzinduzi rasmi wa mshitiri mmoja wa mkoa katika dawa na vifaa  tiba “ JAZIA” uliofanyika Novemba 05, 2018 katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu Mjini Bariadi.
Mratibu wa Mfumo wa mshitiri mmoja wa mkoa katika dawa na vifaa  tiba “ JAZIA”, Oscar Tenganamba (wa tatu kushoto) akimuonesha kitu Katibu Tawala wa Mkoa, Bw. Jumanne Sagini katika mkataba wa mshitiri mmoja wa mkoa katika dawa na vifaa  tiba “ JAZIA” katika uzinduzi rasmi wa mfumo huo uliofanyika Novemba 05, 2018  katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu Mjini Bariadi.

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!