Monday, September 9, 2019

KUELEKEA MTIHANI WA TAIFA 2019, RC MTAKA AWAFUNDA DARASA LA SABA SIMIYU


Kuelekea katika Mtihani wa Taifa wa Kuhitimu elimu ya Msingi Darasa la saba Septemba 11-12, 2019 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amewaonya wanafunzi wa darasa la saba mkoani hapa kujiepusha na udanganyifu katika mtihani huo badala yake wazingatie yale waliyofundishwa na kufanya mtihani huo kwa utulivu na kujiamini.

Mtaka ameyasema hayo Septemba 09, 2019 wakati akizungumza na wanafunzi wa darasa la saba kutoka katika Kata ya Lamadi wilayani Busega Septemba 09, 2019 katika Shule ya Msingi Mwabasabi, kwa niaba ya wenzao wa Mkoa wa Simiyu, kwa lengo la kuwatakia heri katika  mtihani wa Taifa wanaotarajia kuufanya kuanzia Septemba 11-12, 2019.
Mtaka amesema anaamini walimu wamefanya kazi yao vizuri ya kuwafundisha na kuwaandaa wanafunzi  hao hivyo ni vema wakafanya mtihani huo wakiwa na ujasiri huku wakipuuza taarifa zozote za kuwepo kwa majibu ya mitihani mahali popote.
“Ninawatakia kila la heri kwenye mtihani wenu, nashukuru kwa kazi nzuri iliyofanywa na walimu katika kuwafundisha na kuwaandaa kwa kutoa majaribio ya mara kwa mara, kambi kambi za kitaaluma; niwaombe mkaufanye mtihani huu kwa utulivu na ujasiri; asiwadanganye mtu kuwa kuna majibu ya mtihani au mtihani umevuja sehemu fuulani, mkazingatie mlichofundishwa” alisema Mtaka.
Katika hatua nyingine Mtaka amewashukuru walimu kwa namna wanavyojituma katika kuwafundisha wanafunzi na kutoa wito kwa walimu hao kuanzisha madarasa ya maandalizi ya kidato cha kwanza (pre- form one)  kwa wanafunzi hao wanaohitimu ili wasaidie kuwaandaa wanafunzi hao na  masomo ya kidato cha kwanza na waweze kupata kipato cha ziada kupitia malipo yatakayotolewa na wazazi watakaokuwa tayari kugharamia masomo hayo.
Kwa upande wake Afisa Taaluma Mkoa wa Simiyu , Mwl. Onesmo Simime amesema Mkoa wa Simiyu uliweka mikakati mbalimbali ya maandalizi ya wanafunzi wa darasa la saba ikiwemo walimu kumaliza mada zote mwezi Juni 2019 na kuwepo kwa kambi za kitaaluma kwa kila shule,  hivyo wanafunzi wameandaliwa vizuri na kwa mikakati hiyo matarajio ya mkoa ni ufaulu kuongezeka zaidi ya mwaka jana 2018.
Akizungumza kwa niaba ya walimu, Mwalimu Beatrice Ernest kutoka Shule ya Msingi Mwabasabi amesema wana uhakika na maandalizi waliyofanya kwa wanafunzi wao hivyo  ufaulu utaongezeka, huku akimshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuwaruhusu kuanzisha vituo vya ‘pre-form one’ na kuahidi kuwa walimu watajiunga kuanzisha madarasa hayo ili kuboresha taaluma ya wanafunzi wao na kuboresha vipato vyao.

Nao baadhi ya wanafunzi wakizungumza kwa niaba ya wenzao wamesema wamejiandaa vizuri na wamejipanga  kufanya vizuri ili waweze kutimiza malengo yao ikiwa ni pamoja na  kujiunga na elimu ya sekondari na hatimaye kuendelea na elimu juu ili waweze kufikia ndoto zao.

“Mimi na wenzangu wote tumejiandaa vizuri nina uhakika tutafanya vizuri na wote tutaenda sekondari, ushauri tuliopewa na Mkuu wa Mkoa tutauzingatia naamini tutashinda tu” Eric Malimi kutoka Shule ya Msingi Lamadi.

“Sisi tumejiandaa vizuri na tunaweza kuendelea mbali kimasomo, tunamshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kutupa mawaidha na tutayatekeleza ili tuweze kufaulu mtihani wa Taifa na tufikie tunapotaka” alisema  Glorymary Samwel kutoka Shule ya Msingi Itongo.

Mkoa wa Simiyu una jumla ya wanafunzi 29,248  wa darasa la saba wanaotarajia kufanya mtihani wa Taifa Septemba 11-12, mwaka huu, ambao kati yao  wavulana ni  13, 594 na wasichana 15.654.
MWISHO


Baadhi ya wanafunzi wa darasa la saba katika kata ya Lamadi wilayani Busega Mkoani Simiyu wakiwa wamenyoosha mikono yao kama ishara ya kuwa tayari kujibu swali waliloulizwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(hayupo pichani) wakati akizungumza nao Septemba 09, 2019 katika Shule ya Msingi Mwabasabi kwa niaba ya wenzao wa Mkoa wa Simiyu, kwa lengo la kuwatakia heri katika  mtihani wa Taifa wanaotarajia kufanya kuanzia Septemba 11-12, 2019.



Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wanafunzi wa darasa la saba kutoka katika Kata ya Lamadi wilayani Busega Septemba 09, 2019 katika Shule ya Msingi Mwabasabi kwa niaba ya wenzao wa Mkoa wa Simiyu, kwa lengo la kuwatakia heri katika  mtihani wa Taifa wanaotarajia kufanya kuanzia Septemba 11-12, 2019.

Baadhi ya wanafunzi wa darasa la saba katika kata ya Lamadi wilayani Busega Mkoani Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(hayupo pichani) wakati akizungumza nao Septemba 09, 2019 katika Shule ya Msingi Mwabasabi kwa niaba ya wenzao wa Mkoa wa Simiyu, kwa lengo la kuwatakia heri katika  mtihani wa Taifa wanaotarajia kufanya kuanzia Septemba 11-12, 2019.
Baadhi ya walimu kutoka katika shule ya msingi Lamadi, Mwabasabi na Itongo katika Kata ya Lamadi wilayani Busega wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(hayupo pichani) wakati akizungumza na wanafunzi kutoka katika shule hizo kw naiaba ya wenzao wa mkoa wa Simiyu, kwa lengo la kuwatakia heri katika  mtihani wa Taifa wanaotarajia kufanya kuanzia Septemba 11-12, 2019.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Bw. Anderson Njiginya akitoa taarifa ya Ufaulu ya wanafunzi wa darasa la saba katika Halmashauri wakati Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka  akizungumza na wanafunzi wa darasa la saba kata ya Lamadi  Septemba 09, 2019 katika Shule ya Msingi Mwabasabi kwa niaba ya wenzao wa Mkoa wa Simiyu, kwa lengo la kuwatakia heri katika  mtihani wa Taifa wanaotarajia kufanya kuanzia Septemba 11-12, 2019.
Baadhi ya walimu kutoka katika shule ya msingi Lamadi, Mwabasabi na Itongo katika Kata ya Lamadi wilayani Busega wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(hayupo pichani) wakati akizungumza na wanafunzi kutoka katika shule hizo kw naiaba ya wenzao wa mkoa wa Simiyu, kwa lengo la kuwatakia heri katika  mtihani wa Taifa wanaotarajia kufanya kuanzia Septemba 11-12, 2019
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wanafunzi wa darasa la saba kutoka katika Kata ya Lamadi wilayani Busega Septemba 09, 2019 katika Shule ya Msingi Mwabasabi kwa niaba ya wenzao wa Mkoa wa Simiyu, kwa lengo la kuwatakia heri katika  mtihani wa Taifa wanaotarajia kufanya kuanzia Septemba 11-12, 2019.
Baadhi ya wanafunzi wa darasa la saba katika kata ya Lamadi wilayani Busega Mkoani Simiyu wakiwa wamenyoosha mikono yao kama ishara ya kuwa tayari kujibu swali waliloulizwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(hayupo pichani) wakati akizungumza nao Septemba 09, 2019 katika Shule ya Msingi Mwabasabi kwa niaba ya wenzao wa Mkoa wa Simiyu, kwa lengo la kuwatakia heri katika  mtihani wa Taifa wanaotarajia kufanya kuanzia Septemba 11-12, 2019
Baadhi ya viongozi katika Halmashauri ya Wilaya ya Busega wakiwa katika mkutano wa mkuu wa mkoa na wanafunzi wa darasa la saba kata ya Lamadi wilayani humo, kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri, Bw. Anderson Njiginya

Sunday, September 8, 2019

RC MTAKA AWAHAKIKISHIA WAKULIMA SIMIYU PAMBA YAO KUNUNULIWA NA KULIPWA FEDHA ZAO

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amewakikishia wakulima wa pamba mkoani Simiyu kuwa Serikali itahakikisha mwezi huu pamba yote inanunuliwa kwa bei elekezi ya shilingi 1200 kwa kilo na wakulima kulipwa fedha zao, ambapo amesema hadi sasa zaidi ya kilo milioni 54 zenye thamani ya shilingi bilioni 65.1 zimenunuliwa na wakulima wamelipwa fedha zao.


Mtaka ameyasema hayo wakati wa ziara ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu katika vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS) na Kiwanda cha Kuchambua pamba cha Alliance Ginneries Limited  wilayani Bariadi, iliyofanyika Septemba 08, 2019 kwa lengo la kujionea mwenendo wa ununuzi wa pamba, ambapo amewataka wanunuzi kutumia fedha walizopewa dhamana na Serikali kwa ajili ya kununua pamba zitumike kuwalipa wananchi badala ya kuzielekeza mahali pengine au kufanya tofauti na makubaliano.


Amesema makisio ya mkoa ya mavuno yalikuwa ni kuvuna kilo milioni 180 ambapo hadi sasa pamba iliyokusanywa ni kilo milioni 132 ambayo thamani yake ni shilingi bilioni 159.3 na kati ya hizo kilo milioni 54 zenye thamani ya shilingi bilioni 65.1 zimelipiwa na  ambazo bado hazijalipiwa ni kilo milioni 78.5 ambayo thamani yake ni zaidi ya shilingi milioni 94.2
.
Ameongeza kuwa kuelekea katika kipindi cha mvua za vuli Mtaka ni vema wakulima kutoa pamba majumbani na kupeleka pamba kwenye vyama vya ushirika ili itunzwe katika mazingira salama na iweze kununuliwa, huku akitoa wito pia kwa wanunuzi kujielekeza kwenye maeneo ambayo ni magumu kufikika kipindi cha mvua na maeneo ambayo maghala yake si salama sana.

Aidha, Mtaka amewakata viongozi wa vyama vya ushirika kuwa waadilifu badala ya kushirikiana na machinga kuwanyonya wakulima kwa kuuza pamba chini ya bei elekezi ya shilingi 1200 na kuwataka wanunuzi kununua pamba kwa mujibu wa utaratibu kwa kuwa watakaobainika wananunua kama machinga watachukuliwa hatua na pamba hiyo itapigwa mnada.

“Ujumbe huu uwafikie wanunuzi wote wa pamba wanaokuja kununua pamba Simiyu , pamba itanunuliwa kwenye vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS)kwa bei elekezi ya shilingi 1200 kwa kilo, pamba haitanunuliwa kienyeji kwenye nyumba za watu usiku kwa bei ndogo, atakayekamatwa asije akalaumu vyombo vya sheria”alisema Mtaka.

Naye Mwenyekiti wa CCM, Mhe. Enock Yakobo amewataka wanunuzi wa pamba mkoani Simiyu kuhakikisha kuwa wanawalipa wakulima fedha zao kwa wakati ili waweze kujikimu namahitaji yao na kujiandaa na msimu ujao wa kilimo.

Katibu wa Chama cha Wanunuzi wa Pamba nchini, Bw. Boaz Ogola amesema Serikali imewahakikishia wanunuzi wote kuwa itakuwa tayari kufidia hasara itakayopatikana endapo watapata hasara wakinunua pamba kwa shilingi 1200, hivyo mwenendo wa ununuzi wa pamba nchini ni mzuri  ambapo hadi tarehe 01/09/2019 kilo milioni 210 zimeshanunuliwa nchi nzima.

Kwa upande wao Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga na Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shelakaghe  wamesema pamba inaendelea kununuliwa katika maeneo yao huku wakisema wataendelea kusimamia na kuhakikisha pamba inanunuliwa kwa kufuata utaratibu uliowekwa na wananchi wanapata fedha zao.

Awali  wakulima wamesema kuwa baadhi ya makampuni ya ununuzi pamba hayajawalipa fedha zao hivyo wakaomba  Serikali kuwasaidia kuongea na wanunuzi wa zao hilo ili fedha zao zipatikane kwa wakati waweze kununua chakula na mahitaji mengine na kujiandaa na msimu ujao.

"Sisi tunaitegemea pamba na hapa kuna makampuni tunawadai hela zetu tunaiomba serikali itusaidie tupate fedha zetu tuna mambo mengi ya kufanya,tunataka tununue chakula kabla bei haijapanda sasa hivi kila mara bei ya mahindi inapanda"alisema Charles Ng'andwe kutoka Kijiji cha Ibulyu Bariadi.
MWISHO


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza jambo katika Kiwanda cha kuchambua pamba cha Alliance Ginneries Limited kilichopo Bariadi Mkoani Simiyu, wakati wa ziara ya viongozi wa mkoa huo ya kukagua mwenendo wa ununuzi wa pamba, iliyofanyika leo Septemba 08, 2019.
Katibu wa Chama cha Wanunuzi wa Pamba nchini , Bw. Boaz Ogola ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kiwanda cha kuchambua pamba cha Alliance Ginneries Limited kilichopo Bariadi Mkoani Simiyu, akimweleza jambo viongozi wa Mkoa huo walipotembeelea kiwandani hapo kwa lengo la kujionea namna kiwanda hicho kinavyonunua pamba kutoka kwa wakulima katika ziara iliyofanyika Septemba 08, 2019.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wakulima wa Kijiji cha UIbulyu wilayani Bariadi wakati wa ziara ya viongozi wa mkoa huo ya kukagua mwenendo wa ununuzi wa pamba, iliyofanyika leo Septemba 08, 2019.
Mkulima wa pamba Bw. Charles Ng’wande kutoka katika Chama cha Ushirika cha Msingi (AMCOS) cha Ibulyu wilayani Bariadi akitoa hoja yake wakati wa ziara ya viongozi wa mkoa wa Simiyu,  wakiongozwa na Mkuu wa mkoa Mhe. Anthony Mtaka  ya kukagua mwenendo wa ununuzi wa pamba, iliyofanyika leo Septemba 08, 2019.
Mkulima wa Pamba Bw. Musa Makelemo kutoka katika Chama cha Ushirika cha Msingi (AMCOS) cha Mbiti wilayani Bariadi akitoa hoja yake wakati wa ziara ya viongozi wa mkoa wa Simiyu,  wakiongozwa na Mkuu wa mkoa Mhe. Anthony Mtaka  ya kukagua mwenendo wa ununuzi wa pamba, iliyofanyika leo Septemba 08, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wakulima wa Kijiji cha Mbiti wilayani Bariadi wakati wa ziara ya viongozi wa mkoa huo ya kukagua mwenendo wa ununuzi wa pamba, iliyofanyika leo Septemba 08, 2019.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akiangalia pamba iliyochambuliwa na kufungwa kwenye robota katika kiwanda cha kuchambua pamba cha Alliance Ginneries Ltd, wakati wa ziara ya viongozi wa mkoa huo ya kukagua mwenendo wa ununuzi wa pamba, iliyofanyika leo Septemba 08, 2019.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo akizungumza na wakulima wa pamba katika Kijiji cha Mbiti wilayani Bariadi, wakati wa ziara ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu ya kukagua mwenendo wa ununuzi wa pamba, iliyofanyika leo Septemba 08, 2019.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akizungumza na baadhi ya wakulima wa pamba wa Kijiji cha Ibulyu wilayani humo, wakati wa ziara ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu ya kukagua mwenendo wa ununuzi wa pamba, iliyofanyika leo Septemba 08, 2019.
Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Mkoa wa Simiyu(SIMCU), Bw. Cahrles Madata akizungumza na baadhi ya wakulima wa pamba katika Chama cha Ushirika cha Msingi (AMCOS) cha Kasoli wilayani Bariadi, wakati wa ziara ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu ya kukagua mwenendo wa ununuzi wa pamba, iliyofanyika leo Septemba 08, 2019.
Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe(mwenye miwani katikati) akizungumza na baadhi ya wakulima wa pamba kijiji cha Ibulyu katika ziara ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu ya kukagua mwenendo wa ununuzi wa pamba, iliyofanyika leo Septemba 08, 2019.
Kushoto ni Kiongozi wa Chama cha Ushirika cha msingi(AMCOS)  cha Kasoli akimweleza jambo Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa tatu kushoto) katika ziara ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu ya kukagua mwenendo wa ununuzi wa pamba, iliyofanyika leo Septemba 08, 2019.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akizungumzia hali ya ununuzi wa pamba ilivyo katika wilaya hiyo wakati wa kikao kilichofanyika mara baada ya ziara ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu ya kukagua mwenendo wa ununuzi wa pamba, iliyofanyika leo Septemba 08, 2019.



Friday, September 6, 2019

RC MTAKA APEWA TUZO YA KIONGOZI BORA ALIYELETA MAPINDUZI KATIKA ELIMU


Mkuu wa Mkoa wa Simiu, Mhe. Anthony Mtaka amepewa tuzo ya elimu ya Tanzania Elimu Awards na Taasisi ya Elimu Solutions, ikiwa ni kutambua mchango wake kama kiongozi aliyefanya vizuri na mwenye mchango mkubwa katika mapinduzi ya elimu Mkoani Simiyu.

Tuzo hiyo imekabidhiwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu Solutions, Neithan Swed, Septemba 05, 2019 Mjini Bariadi wakati wa uzinduzi wa Kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne waliopata ufaulu hafifu(daraja sifuri) katika mtihani wa Mock kwa lengo la kuwasaidia kuongeza ufaulu wao katika Mtihani wa Taifa utakaofanyika mwezi Novemba 2019.

Swed amesema Taasisi hiyo imefuatilia na kuona juhudi zinazofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu katika mapinduzi ya elimu ikiwemo ubunifu wa kuanzisha kambi za kitaaluma ambazo zimeonekana kuwa na mchango mkubwa katika kuongeza ufaulu wa mkoa wa Simiyu kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo kutoka mwaka 2016 hadi mwaka 2018.

“Anayoyafanya Mhe. Mtaka hayaishii Simiyu peke yake Tanzania inayaona, tulifuatilia habari za kambi za kitaaluma na tukaangalia nafasi ya mkoa katika matokeo na namna mlivyofanya vizuri, mmeweka alama kwenye Taifa na tunatamani Mhe. Mtaka aziendeleze juhudi hizi zaidi ili mtoke kwenye kumi bora mwende tatu bora na mwakani tupate mwanafunzi bora kutoka Simiyu atakayepata tuzo hii” alisema Neithan Swed.

Katika hatua nyingine Swed amesema Taasisi ya Elimu Solutions itatoa ufadhili kwa mwanafunzi wa kidato cha nne mwaka 2019 atakayefanya vizuri katika mtihani wa Taifa na kumpeleka nchini China kuendelea na masomo.

Akipokea tuzo hiyo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ameishukuru Taasisi ya Elimu Solutions kwa kutambua juhudi zinazofanywa na mkoa wa Simiyu na kutoa tuzo huku akibainisha kuwa mkoa wa Simiyu unaithamini sana tuzo hiyo.

Aidha, Mtaka ameipongeza Taasisi ya Elimu Solutions namna wanavyohamasisha maendeleo ya Elimu ya Watanzania ikiwa ni pamoja na kutoa ufadhili kwa wanafunzi wanaofanya vizuri kwenda kusoma nje ya nchi.

Tuzo za Elimu Tanzania Elimu Awards zimetolewa na Taasisi ya Elimu Solutions kwa wadau mbalimbali wa elimu waliochangia  na kusaidia kuleta mabadiliko kwa ubunifu na juhudi zao binafsi, taasisi zinazoihudumia sekta ya elimu; pia hutolewa kwa viongozi, walimu, wanafunzi waliofanya vizuri kwenye elimu
MWISHO

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Solutions, Neithan Swed akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka tuzo ya elimu iliyotolewa na  Taasisi hiyo kwake ikiwa ni kutambua mchango wake kama kiongozi aliyefanya vizuri na mwenye mchango mkubwa katika mapinduzi ya elimu Mkoani Simiyu

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka akionesha tuzo ya elimu aliyopewa na  Taasisi ya Elimu Solutions kwake ikiwa ni kutambua mchango wake kama kiongozi aliyefanya vizuri na mwenye mchango mkubwa katika mapinduzi ya elimu Mkoani Simiyu

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Komredi Enock Yakobo akionesha tuzo ya elimu iliyotolewa na  Taasisi ya Elimu Solutions kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka  ikiwa ni kutambua mchango wake kama kiongozi aliyefanya vizuri na mwenye mchango mkubwa katika mapinduzi ya elimu Mkoani Simiyu.



Afisa Elimu Mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju akisoma maneno yaliyoandikwa kwenye tuzo ya elimu iliyotolewa na  Taasisi ya Elimu Solutions kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka  ikiwa ni kutambua mchango wake kama kiongozi aliyefanya vizuri na mwenye mchango mkubwa katika mapinduzi ya elimu Mkoani Simiyu.



Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Taasisi ya Elimu Solutions, Nice Alex akimkabidhi zawadi ya fulana Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka mara baada ya kumkabidhi tuzo ya elimu ikiwa ni kutambua mchango wake kama kiongozi aliyefanya vizuri na mwenye mchango mkubwa katika mapinduzi ya elimu Mkoani Simiyu.



Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kulia) akimkabidhi mmoja wa walimu walio katika kambi maalum ya wanafunzi wa kidato cha nne alizokabidhiwa na Taasisi ya Elimu Solutions.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kulia) akimkabidhi mmoja wa walimu walio katika kambi maalum ya wanafunzi wa kidato cha nne alizokabidhiwa na Taasisi ya Elimu Solutions.





KAMBI YA KITAALUMA KWA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE WENYE UFAULU HAFIFU YAZINDULIWA SIMIYU


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amezindua rasmi kambi ya kitaaluma ya siku 60 kwa wanafunzi wa kidato cha nne waliopata ufaulu hafifu (daraja sifuri) katika mtihani wa ‘Mock’, lengo likiwa ni kuwasaidia waweze kuongeza ufaulu wao katika mtihani wa Taifa utakaofanyika mwezi Novemba 2019.

Akizindua kambi hiyo Septemba 05, 2019 Mtaka amesema wanafunzi hao watafundishwa masomo manne tu ambayo ni Kiswahili, Kiingereza ,Uraia(Civics) na Historia, hivyo akatoa wito kwa walimu mahiri waliochaguliwa kuwafundisha wanafunzi hao kwa moyo na upendo ili wanafunzi hao waweze kupata alama D na kuendelea katika mtihani wa Taifa.

“Hawa watoto wafundisheni masomo manne, Kiswahili, Kiingereza, Historia na Civics; wafundisheni kwa moyo, wapeni mazoezi ya mara kwa mara katika siku hizi 60 watakazokuwa kambini, muwasaidie watoke kwenye F wapate angalau D nao wapate vyeti, kwa sababu hata ajira siku hizi kigezo ni angalau mtu awe na cheti cha kidato cha nne” alisema Mtaka.

Katika hatua nyingine Mtaka ametoa wito kwa jamii ya Simiyu kuendelea kuwekeza kwenye elimu ili kuuwezesha mkoa kushindana kiuchumi kwa kuwa maendeleo ya kiuchumi yanategemea maendeleo ya elimu katika eneo husika.

Afisa Elimu mkoa wa Simiyu, Mwl.Ernest Hinju amesema kati ya Wanafunzi 9956 waliofanya mtihani wa  Utimilifu (Mock), 1300 hawakupata alama D hata moja, hivyo waliopata matokeo hafifu (daraja sifuri) wamewekwa pamoja wafundishwe masomo manne ili waweze kuongeza ufaulu katika mtihani wa Taifa, huku waliopata daraja la kwanza hadi la nne wakiendelea na kambi kufundishwa masomo yote.

Aidha, Hinju ameongeza kuwa  kambi za kitaaluma zimechangia kuongeza ufaulu kwenye Mtihani ya Taifa wa darasa la saba, kidato cha nne na kidato cha sita, ambapo katika matokeo ya kidato cha nne mwaka 2016 ufaulu ulikuwa asilimia 74 mkoa ukiwa nafasi ya 14 kati ya mikoa 26, mwaka  2017 ufaulu asilimia 79.8 nafasi ya 11 na mwaka 2018 ufaulu asilimia 82.5  ukashika nafasi ya 9 kati ya mikoa 26.

Kwa upande wao wanafunzi wa kidato cha nne waliopo kambini  wameshukuru kuwekewa kambi hiyo na wakaeleza imani yao juu ya uwepo wa kambi hiyo ambapo wameomba kambi za kitaaluma Simiyu ziwe endelevu ili ziwasaidie kujifunza na kujiandaa vema na mitihani ya Taifa hatimaye mkoa uweze kufanya vizuri.

“Tunawashukuru viongozi wetu na wazazi wetu kwa kukubali kutuwekea kambi ya kitaaluma, ninashauri kambi hizi zisiishie kwetu ziendelee na kwa wadogo zetu ili mkoa wetu uweze kuongeza ufaulu” alisema Esther Nashoni mwanafunzi shule ya sekondari Bariadi(Bariadi)

Mkuu wa Shule ya Sekondari Simiyu, Mwl.Paul Susu amesema walimu wamejiandaa vema katika kuwafundisha wanafunzi na kuwapa mitihani ya mara kwa mara ili waweze kufanya vizuri, huku akitoa wito kwa wadau mbalimbali wa elimu kujitolea katika ujenzi wa miundombinu ya elimu ili kuwe na miundombinu ya kutosha itakayoongeza nafasi kwa kambi za kitaaluma kufanyika  vizuri.

Kambi ya kitaaluma kwa wanafunzi wa Kidato cha nne iliyozinduliwa Septemba 05, 2019 ilianza rasmi Septemba Mosi na inatarajiwa kufanyika ndani ya siku 60 kabla ya kufanya Mtihani wa Taifa mwezi Novemba.
MWISHO

Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne, walimu na wadau wa elimu mkoani Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati akizindua kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne, waliopata ufaulu hafifu katika Mtihani wa ‘Mock’ ili waweze kuongeza ufaulu katika mtihani wa Taifa utakaofanyika Novemba 2019, uzinduzi huu umefanyika Septemba 05, 2019 Mjini Bariadi



Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizindua kambi ya Kitaaluma ya wanafunzi wa kidato cha nne, waliopata ufaulu hafifu katika Mtihani wa ‘Mock’ ili waweze kuongeza ufaulu katika mtihani wa Taifa utakaofanyika Novemba 2019, uzinduzi huu umefanyika Septemba 05, 2019 Mjini Bariadi.
Afisa elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju akitoa taarifa ya kambi maalum ya kitaaluma kwa wanafunzi waliopata ufaulu hafifu katika Mtihani wa ‘Mock’ wakati wa ufunguzi wa kambi hiyo inayofanyika ili kuwasaidia wanafunzi hao waweze kuongeza ufaulu katika mtihani wa Taifa utakaofanyika Novemba 2019, uzinduzi huu umefanyika Septemba 05, 2019 Mjini Bariadi.
Afisa elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju akitoa taarifa ya kambi maalum ya kitaaluma kwa wanafunzi waliopata ufaulu hafifu katika Mtihani wa ‘Mock’ wakati wa ufunguzi wa kambi hiyo inayofanyika ili kuwasaidia wanafunzi hao waweze kuongeza ufaulu katika mtihani wa Taifa utakaofanyika Novemba 2019, uzinduzi huu umefanyika Septemba 05, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne, mkoani Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati akifungua kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne, waliopata ufaulu hafifu katika Mtihani wa ‘Mock’ ili waweze kuongeza ufaulu katika mtihani wa Taifa utakaofanyika Novemba 2019 uzinduzi huu umefanyika Septemba 05, 2019 Mjini Bariadi.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Komredi Enock Yakobo akizungumza na wanafunzi wa kidato cha nne waliopata ufaulu hafifu katika Mtihani wa ‘Mock’ wakati wa ufunguzi wa kambi hiyo inayofanyika ili kuwasaidia wanafunzi hao waweze kuongeza ufaulu katika mtihani wa Taifa utakaofanyika Novemba 2019, uzinduzi huu umefanyika Septemba 05, 2019 Mjini Bariadi.




Baadhi ya walimu mahiri na wadau wengine wa elimu mkoani Simiyu wakati wa ufunguzi wa kambi hiyo inayofanyika ili kuwasaidia wanafunzi hao waweze kuongeza ufaulu katika mtihani wa Taifa utakaofanyika Novemba 2019, uzinduzi huu umefanyika Septemba 05, 2019 Mjini Bariadi.


Mkuu wa Shule ya Sekondari Simiyu ya Mjini Bariadi, Mwl. Paul Susu  akieleza umuhimu wa kambi za kitaaluma wakati wa uzinduzi wa kambi ya kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne waliopata ufaulu hafifu katika Mtihani wa ‘Mock’ inayofanyika ili kuwasaidia wanafunzi hao waweze kuongeza ufaulu katika mtihani wa Taifa utakaofanyika Novemba 2019, uzinduzi huu umefanyika Septemba 05, 2019 Mjini Bariadi.

Baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu  na wadau wengine wa elimu akiwepo mwandishi mashuhuru wa vitabu Richard Mabala(wa tatu kushoto) wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati akifungua kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne Septemba 05, 2019 Mjini Bariadi , waliopata ufaulu hafifu katika Mtihani wa ‘Mock’ ili waweze kuongeza ufaulu katika mtihani wa Taifa utakaofanyika Novemba 2019.
Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Tanzania Mkoa wa Simiyu, akieleza umuhimu wa kambi za kitaaluma wakati wa uzinduzi wa kambi ya kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne waliopata ufaulu hafifu katika Mtihani wa ‘Mock’ inayofanyika ili kuwasaidia wanafunzi hao waweze kuongeza ufaulu katika mtihani wa Taifa utakaofanyika Novemba 2019, uzinduzi huu umefanyika Septemba 05, 2019 Mjini Bariadi.
Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa, Dkt. Mugune Maeka akieleza namna idara ya afya itakavyowahudUmia wanafunzi wa kidato cha nne walio katika kambi ya kitaaluma,  kwa wanafunzi wa kidato cha nne waliopata ufaulu hafifu katika Mtihani wa ‘Mock’ inayofanyika ili kuwasaidia wanafunzi hao waweze kuongeza ufaulu katika mtihani wa Taifa utakaofanyika Novemba 2019, uzinduzi huu umefanyika Septemba 05, 2019 Mjini Bariadi.

Baadhi ya viongozi na wadau wa elimu mkoani Simiyu, wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati akifungua kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne waliopata ufaulu hafifu katika Mtihani wa ‘Mock’ ili waweze kuongeza ufaulu katika mtihani wa Taifa utakaofanyika Novemba 2019 uzinduzi huu umefanyika Septemba 05, 2019
 Meneja wa TANESCO Mkoa wa Simiyu,  Mhandisi. Rehema Mashinji akiwaasa wanafunzi wa kidato cha nne walio katika kambi ya Kitaaluma kwenye ufunguzi wa kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne waliopata ufaulu hafifu katika Mtihani wa ‘Mock’ ili waweze kuongeza ufaulu katika mtihani wa Taifa utakaofanyika Novemba 2019 uzinduzi huu umefanyika Septemba 05, 2019 

Wednesday, September 4, 2019

TAASISI YA AMANI GIRLS HOME YATOA VITENDEA KAZI KWA WAHUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII SIMIYU


Shirika lisilo la Kiserikali la Amani Girls Home limetoa msaada wa vitendea kazi kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii kwa  lengo la kuwasaidia kutekeleza majukumu yao ya kutoa elimu kwa jamii juu mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria kupitia mradi wa “BADILISHA TABIA TOKOMEZA MALARIA,” Mkoani Simiyu.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya vitendea kazi hivyo Meneja Miradi wa Amani Girls Home, Bw. Revocatus Sono, amevitaja vifaa hivyo kuwa ni baiskeli 46, makoti  ya mvua 46,  mabuti ya mvua 46, fulana na vitini vya kutolea elimu kwa jamii vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni tisa, ambavyo vimetolewa kwa wahudumu  wa afya ngazi ya jamii wapatao 46  kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Busega na Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Nao wahudumu wa afya ngazi ya jamii  wameishukuru Taasisi  ya Amani Girls Home kwa kutoa msaada wa vitendea kazi ambavyo wamesema vitawarahisihsia kazi na kuwawezesha kuwafikia wananchi wengi na kutoa elimu iliyokusudiwa kwa jamii ili kufikia lengo la kutokomeza kabisa ugonjwa wa Malaria mkoani Simiyu.

“Tunaishukuru Amani Girls Home kwa kutoa vitendea kazi hivi, awali tulianza kazi tukiwa hatuna vifaa ilikuwa ni changamoto kubwa kwa kuwa tuna mitaa mikubwa na hatukuweza kuwafikia walengwa wote, leo tumekabidhiwa vifaa zikiwemo baiskeli naamini vitatusaidia kufanya kazi yetu kwa wepesi katika kuifikia jamii” alisema Abadi James Mhudumu wa afya ngazi ya Jamii Kata ya Malambo Bariadi Mjini.

Mratibu wa Mpango wa Kudhibiti Malaria Mkoa wa Simiyu, Dkt. Mugune Maeka amewataka wahudumu wa afya ngazi ya jamii kuhakikisha wagonjwa wa malaria watakaowaibua katika jamii wanafikishwa katika vituo vya kutolea huduma, ili wapate matibabu sahihi na kwa wakati lengo likiwa ni kupunguza maambukizi ya malaria kutoka asilimia sita ya sasa na hatimaye  kufuta kabisa ugonjwa wa malaria.

Awali akizungumza na wahudumu hao, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Bw. Melkizedeck Humbe amewataka kutumia vitendea kazi  walivyopewa kwa malengo yaliyokusudiwa, huku akiahidi kuwa Serikali itaweka utaratibu wa kuendeleza juhudi za wadau wa afya katika mapambano dhidi ya malaria ili ugonjwa wa malaria ubaki kuwa historia katika mkoa wa Simiyu.

Katika hatua nyingine Humbe amewataka wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii kutoa elimu kwa jamii kutumia vituo vya kutolea huduma za  Afya kupata matibabu kila wanapoona dalili za ugonjwa badala ya kwenda kwa waganga wa jadi ili waweze kupata tiba sahihi kwa wakati sahihi.

Amesema Serikali imejenga vituo vya kutolea huduma za afya katika maeneo mbalimbali ikiwemo zahanati, vituo vya afya, hospitali za wilaya na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa zinaendelea kujengwa, hivyo ni vema jamii ikaelimishwa umuhimu wa kutumia vituo hivyo kupata huduma za tiba ya magonjwa mbalimbali ikiwemo  Malaria  badala ya kwenda kwa waganga wa jadi.

“Hospitali za wilaya zinajengwa, vituo vya afya vimejengwa, zahanati zimejengwa kawaelimisheni watu watumie vituo vya kutolea huduma za afya ajili ya kwenda kupima afya na kupata matibabu sahihi kwa wakati wanapokuwa wagonjwa, badala ya kwenda kwa waganga wa jadi ili tutokomeze kabisa malaria kwenye mkoa wetu” alisema Humbe.
MWISHO

Mkurugenzi wa Halmashauri Mji wa Bariadi, Bw. Melkizedeck Humbe akiwakabidhi wahudumu wa afya ngazi ya jamii baiskeli kwa niaba ya wenzao ambao wote wamepewa baiskeli na vitendea kazi vingine na Shirika lisilo la Kiserikali la Amani Girls Home ambavyo vimekabidhiwa kwao  Septemba 04, Mjini Bariadi.

Mkurugenzi wa Halmashauri Mji wa Bariadi, Bw. Melkizedeck Humbe akizungumza na wahudumu wa afya ngazi ya jamii kutoka Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi na Busega wakati wa hafla ya makabidhiano ya vitendea kazi zikiwemo baiskeli vilivyotolewa na Shirika lisilo la Kiserikali la Amani Girls Home na kukabidhiwa Septemba 04, Mjini Bariadi.


 Baadhi ya  wahudumu wa afya ngazi ya jamii kutoka Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi na Busega wakimsikiliza Mkurugenzi wa Halmashauri Mji wa Bariadi, Bw. Melkizedeck Humbe(hayupo pichani)  wakati wa hafla ya makabidhiano ya vitendea kazi zikiwemo baiskeli vilivyotolewa na Shirika lisilo la Kiserikali la Amani Girls Home kwa ajili ya kutoa elimu juu ya vita dhidi ya malaria na kukabidhiwa kwa wahudumu hao Septemba 04, Mjini Bariadi.

Mkurugenzi wa Halmashauri Mji wa Bariadi, Bw. Melkizedeck Humbe akimkabidhi mmoja wa wahudumu wa afya ngazi ya jamii fulana kwa niaba ya wenzake 45 ambao wote wamepewa baiskeli na vitendea kazi vingine na Shirika lisilo la Kiserikali la Amani Girls Home kwa ajili ya kutoa elimu juu ya vita dhidi ya malaria na kukabidhiwa wahudumu hao Septemba 04, Mjini Bariadi.

Mkurugenzi wa Halmashauri Mji wa Bariadi, Bw. Melkizedeck Humbe akimkabidhi mmoja wa wahudumu wa afya ngazi ya jamii kitini cha kutolea elimu kwa jamii kwa niaba ya wenzake 45 ambao wote wamepewa baiskeli na vitendea kazi vingine na Shirika lisilo la Kiserikali la Amani Girls Home kwa ajili ya kutoa elimu juu ya vita dhidi ya malaria na kukabidhiwa wahudumu hao Septemba 04, Mjini Bariadi.

Mkurugenzi wa Halmashauri Mji wa Bariadi, Bw. Melkizedeck Humbe akimkabidhi mmoja wa wahudumu wa afya ngazi ya jamii kitini cha kutolea elimu kwa jamii kwa niaba ya wenzake 45 ambao wote wamepewa baiskeli na vitendea kazi vingine na Shirika lisilo la Kiserikali la Amani Girls Home kwa ajili ya kutoa elimu juu ya vita dhidi ya malaria na kukabidhiwa wahudumu hao Septemba 04, Mjini Bariadi.
Mratibu wa Mpango wa Kudhibiti Malaria Mkoa wa Simiyu, Dkt. Mugune Maeka akitoa taarifa ya hali ya malaria mkoani Simiyu, wakati wa makabidhiano ya vitendea kazi vya wahudumu wa afya ngazi ya jamii  zikiwemo baiskeli na makoti ya mvua, yaliyofanyika Septemba 04, Mjini Bariadi.

Baadhi ya baiskeli zilizotolewa na Shirika lisilo la Kiserikali la Amani Girls Home Wahudumu wa Afya ngazi ya jamii kutoka  Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Busega na Halmashauri ya Mji wa Bariadi na Shirika lisilo la Kiserikali la Amani Girls Home,  Septemba 04, Mjini Bariadi
Baadhi ya baiskeli zilizotolewa na Shirika lisilo la Kiserikali la Amani Girls Home Wahudumu wa Afya ngazi ya jamii kutoka  Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Busega na Halmashauri ya Mji wa Bariadi na Shirika lisilo la Kiserikali la Amani Girls Home,  Septemba 04, Mjini Bariadi.



Baadhi ya vitendea kazi vilivyotolewa pamoja na baiskeli na Shirika lisilo la Kiserikali la Amani Girls Home kwa Wahudumu wa Afya ngazi ya jamii kutoka  Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Busega na Halmashauri ya Mji wa Bariadi na Shirika lisilo la Kiserikali la Amani Girls Home,  Septemba 04, Mjini Bariadi kwa ajili ya kutoa elimu juu ya vita dhidi ya malaria .
Baadhi ya  wahudumu wa afya ngazi ya jamii kutoka Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi na Busega wakimsikiliza Mkurugenzi wa Halmashauri Mji wa Bariadi, Bw. Melkizedeck Humbe(hayupo pichani)  wakati wa hafla ya makabidhiano ya vitendea kazi zikiwemo baiskeli vilivyotolewa na Shirika lisilo la Kiserikali la Amani Girls Home kwa ajili ya kutoa elimu juu ya vita dhidi ya malaria na kukabidhiwa kwa wahudumu hao Septemba 04, Mjini Bariadi

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!