Rais Mstaafu wa Tanzania awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ametoa wito kwa Watanzania kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli katika ulinzi wa hifadhi za Taifa ni pamoja na kutoruhusu mifugo kuchungiwa kwenye hifadhi ili hifadhi hizo endelevu kwa manufaa ya Taifa na vizazi vijavyo.
Dkt.
Kikwete ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa mikoa ya Simiyu, Mara pamoja na washiriki wa Mbio za Serengeti Safari
Marathon kutoka mikoa mbalimbali nchini na wengine kutoka nje ya nchi na nje ya
bara la Afrika zilizofanyika katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia lango
la Ndabaka.
“Mikoa
miwili ya Simiyu na Mara tu ina ng’ombe
zaidi ya milioni tano, tukisema turuhusu mifugo ichungiwe kwenye hifadhi hakuna
mnyama atakayebaki na hapo hakutakuwa na hifadhi tena hili siyo suala la
kisiasa; sisi viongozi wa kisiasa tukilipigia siasa jambo hili hiyo sifa
tunayoisema ya Serengeti kuwa Hifadhi ya
kwanza Duniani haitakuwepo baada ya kuruhusu ng’ombe kuingia kwenye hifadhi,”
alisema Dkt. Kikwete.
Aidha,
Dkt. Kikwete amewapongeza waandaaji wa Serengeti Safari Marathon kwa namna kwa
kuanzisha mbio hizo ambazo zao jipya la utalii ambayo ikitangazwa vizuri
itatangaza utalii nchini na kuweza kulifikia lengo la serikali la kufikisha
watalii 5,000,000 ifikapo 2025 kutoka 1,300,000 wa sasa, huku akitoa wito kwa
wadau wa utalii kujenga hoteli kwa ajili ya kuwapokea wageni/watalii.
Baadhi ya washiriki wa mbio za Serengeti Safari
Marathon wakiwa katika eneo la kumalizia mbio hizo ambazo zimefanyika Novemba
14, 2020 katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia lango la Ndabaka.Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Adam Malima akimweleza jambo Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (wa pili kulia) wakati akitembea kuelekea lango la Ndabaka katika Hifadhi ya Tifa ya Serengeti Novemba 14, 2020 kwa lengo la kufungua mashindano ya mbio za Serengeti Safari Marathon
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(katikati) akimweleza jambo Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete ( kulia) wakati akitembea kuelekea lango la Ndabaka
katika Hifadhi ya Tifa ya Serengeti Novemba 14, 2020 kwa lengo la kufungua
mashindano ya mbio za Serengeti Safari Marathon.
Baadhi ya washiriki wa Mbio za Serengeti Safari
Marathon wakiwa katika eneo la kumalizia mbio hizo ambazo katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia
lango la Ndabaka.Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe.
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na
wajumbe wa Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Simiyu mara baada ya kuwasili
katika Hoteli ya Serenity On the Lake wilayani Busega kwa ajili ya kwenda kufungua
mashindano ya mbio za Serengeti Safari Marathon.



