Sunday, November 15, 2020

WATANZANIA TUMUUNGE MKONO JPM KULINDA HIFADHI ZA TAIFA: KIKWETE

Rais Mstaafu wa Tanzania awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ametoa wito kwa Watanzania kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli katika ulinzi wa hifadhi za Taifa ni pamoja na kutoruhusu mifugo kuchungiwa kwenye hifadhi ili hifadhi hizo endelevu kwa manufaa ya Taifa na vizazi vijavyo. 

Dkt. Kikwete ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa mikoa ya Simiyu,  Mara pamoja na washiriki wa Mbio za Serengeti Safari Marathon kutoka mikoa mbalimbali nchini na wengine kutoka nje ya nchi na nje ya bara la Afrika zilizofanyika katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia lango la Ndabaka.

“Mikoa miwili ya  Simiyu na Mara tu ina ng’ombe zaidi ya milioni tano, tukisema turuhusu mifugo ichungiwe kwenye hifadhi hakuna mnyama atakayebaki na hapo hakutakuwa na hifadhi tena hili siyo suala la kisiasa; sisi viongozi wa kisiasa tukilipigia siasa jambo hili hiyo sifa tunayoisema ya Serengeti kuwa  Hifadhi ya kwanza Duniani haitakuwepo baada ya kuruhusu ng’ombe kuingia kwenye hifadhi,” alisema Dkt. Kikwete.

Aidha, Dkt. Kikwete amewapongeza waandaaji wa Serengeti Safari Marathon kwa namna kwa kuanzisha mbio hizo ambazo zao jipya la utalii ambayo ikitangazwa vizuri itatangaza utalii nchini na kuweza kulifikia lengo la serikali la kufikisha watalii 5,000,000 ifikapo 2025 kutoka 1,300,000 wa sasa, huku akitoa wito kwa wadau wa utalii kujenga hoteli kwa ajili ya kuwapokea wageni/watalii.

Baadhi ya washiriki wa mbio za Serengeti Safari Marathon wakiwa katika eneo la kumalizia mbio hizo ambazo zimefanyika Novemba 14, 2020 kupitia lango la Ndabaka katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Baadhi ya washiriki wa mbio za Serengeti Safari Marathon wakiwa katika eneo la kumalizia mbio hizo ambazo zimefanyika Novemba 14, 2020 katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia lango la Ndabaka.
Baadhi ya viongozi wa mikoa ya Simiyu na Mara pamoja na baadhi ya washiriki wakiwa katika mbio fupi za kilomita tano katika mashindano ya Serengeti Safari Marathon Novemba 14, 2020 katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia lango la Ndabaka.
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Adam Malima akimweleza jambo Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (wa pili kulia) wakati akitembea kuelekea lango la Ndabaka katika Hifadhi ya Tifa ya Serengeti  Novemba 14, 2020 kwa lengo la kufungua mashindano ya mbio za Serengeti Safari Marathon
Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi zawadi mmoja wa washindi wa Serengeti Safari Marathon, Bibi. Josien Vergroesien kutoka nchini Netherland, ambazo zimefanyika Novemba 14, 2020 katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia lango la Ndabaka.

Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na mmoja wa wanafunzi wa shule ya sekondari Anthony Mtaka wilayani Busega aliyeshiriki  mashindano ya mbio za Serengeti Safari Marathon katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia lango la Ndabaka.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kulia) akifurahia jambo na Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Novemba 14, 2020  mara baada ya kumpokea katika Hoteli ya Serenity On the Lake wilayani Busega kwa ajili ya kwenda kufungua mashindano ya mbio za Serengeti Safari Marathon.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(katikati) akimweleza jambo Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ( kulia) wakati akitembea kuelekea lango la Ndabaka katika Hifadhi ya Tifa ya Serengeti Novemba 14, 2020 kwa lengo la kufungua mashindano ya mbio za Serengeti Safari Marathon.

Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo mara baada ya kuwasili katika Hoteli ya Serenity On the Lake wilayani Busega kwa ajili ya kwenda kufungua mashindano ya mbio za Serengeti Safari Marathon.
Kikundi cha ngoma kikitoa burudani wakati wa mashindano ya mbio za Serengeti Safari Marathon yaliyofanyika katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia lango la Ndabaka.
Baadhi ya washiriki wa Mbio za Serengeti Safari Marathon wakiwa katika eneo la kumalizia mbio hizo ambazo  katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia lango la Ndabaka.
Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (wa nane kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na watumishi wa mkoa wa Simiyu mara baada ya kufunga mashindano ya mbio za Serengeti Safari Marathon yaliyofanyika katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia lango la Ndabaka.

Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Simiyu mara baada ya kuwasili katika Hoteli ya Serenity On the Lake wilayani Busega kwa ajili ya kwenda kufungua mashindano ya mbio za Serengeti Safari Marathon.

Baadhi ya wananchi wakifuatilia hotuba ya Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa kufunga mashindano ya Mbio za Serengeti Safari Marathon ambazo  zimefanyika katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia lango la Ndabaka.
Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi zawadi mmoja wa washindi wa Serengeti Safari Marathon ambazo zimefanyika Novemba 14, 2020 katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia lango la Ndabaka.
Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimvisha medali mmoja wa washindi wa Serengeti Safari Marathon ambazo zimefanyika Novemba 14, 2020 katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia lango la Ndabaka.
Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimvisha medali mmoja wa washindi wa Serengeti Safari Marathon ambazo zimefanyika Novemba 14, 2020 katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia lango la Ndabaka.
Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya siasa ya mkoa wa Simiyu (CCM) mara baada ya kuwasili katika Hoteli ya Serenity On the Lake wilayani Busega, Novemba 14, 2020  kwa ajili ya kwenda kufungua mashindano ya mbio za Serengeti Safari Marathon.
Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa mkoa wa Simiyu, Mkoa wa Mara, UNDP na waandaaji wa Serengeti Safari Marathon baada ya kufunga  mbio hizo Novemba 14, 2020 katika hifadhi ya Serengeti lango la Ndabaka.
Mmoja wa Wakurugenzi wa Serengeti Safari Marathon Henri Kimambo akiwasilisha taarifa ya mbio za Serengeti Safari  Marathon zilizofanyika Novemba 14, 2020 katika hifadhi ya Serengeti lango la Ndabaka.
Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa mkoa wa Simiyu, Mkoa wa Mara, UNDP na waandaaji waSerengeti Safari Marathon baada ya kufunga  mbio hizo Novemba 14, 2020 katika hifadhi ya Serengeti lango la Ndabaka.
Baadhi ya viongozi wa mikoa ya Simiyu na Mara pamoja na baadhi ya washiriki wakiwa katika mbio fupi za kilomita tano katika mashindano ya Serengeti Safari Marathon Novemba 14, 2020 katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia lango la Ndabaka.
Mjasiriamali kutoka Busega Mkoani Simiyu akimkabidhi zawadi Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete baada ya kufunga mashindano ya mbio hizo ambazo  zimefanyika katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia lango la Ndabaka.
Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi zawadi mmoja wa washindi wa Serengeti Safari Marathon ambazo zimefanyika Novemba 14, 2020 katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia lango la Ndabaka.
Kutoka kushoto Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Adam Malima, Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakifuatilia matukio mbalimbali katika ufungaji wa mbio za Serengeti Safari Marathon ambazo  zimefanyika Novemba 14, 2020 katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia lango la Ndabaka.
Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na baadhi ya wananchi wa mikoa ya Simiyu na Mara, washiriki wa mbio za Serengeti Safari Marathon ambazo  zimefanyika Novemba 14, 2020 katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia lango la Ndabaka.







Thursday, November 12, 2020

RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE MGENI RASMI SERENGETI SAFARI MARATHON

 Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mashindano ya Serengeti Safari Marathoni yanayotarajiwa kufanyika tarehe 14 Novemba 2020 kuanzia lango la Ndabaka wilayani Busega mkoani Simiyu 

Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 12, 2020 ofisini kwake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema mbio hizo zitahusisha mikoa miwili ya Simiyu na Mara  na akatoa wito kwa wananchi wa mikoa ya hiyo kujitokeza kwa kushiriki katika mbio hizi ambazo zinalenga kutangaza hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambayo asilimia 70 ipo mkoa wa Mara na asilimia 30 ipo mkoa wa Simiyu.

“Mhe. Rais Mstaafu Jakaya Kikwete atakuwepo hapa tarehe 13/11/2020, tarehe 14/11/2020 ataanzisha rasmi mbio hizo na atashiriki mbio za kilomita tano na baadaye ataongoza uvalishaji wa medali kwa wachezaji na washiriki watakaokuwepo kwenye mbio ndefu,” alisema Mtaka.

Kwa upande wake  Mkurungenzi wa Serengeti Safari Marathon Bw.Timothy Mdinka amesema lengo kubwa la Serengeti Safari Marathon ni kukuza utalii wa ndani na nje ya nchi ambapo amebainisha kuwa Mbio hizi zimeanza tarehe 12/11/20  na Kilele chake ni 14/11/2020. 

Kutakuwa na aina nne za mbio; ambazo ni kilomita  42 (Half Marathon),  Kilomita 21 (Half Marathon), Kilometa 10 (Executive Run)  na kilomita tano (Fun Run);  kwa washindi zinategemeana na aina ya Mbio, Zawadi zitaanzia Tsh. 100,000/= hadi Tsh.600,000/=, ,” alisema Mdinka. 

Mdinka ameongeza kuwa wanatarajia kuwa na washiriki takribani  800, kutoka mikoa yote nchini, ,Afrika Mashariki na Ulaya ya Mashariki ambapo pia amebainisha kuwa kutakuwa na mbio za watoto, lengo likiwa kuwahamasisha  watoto wawe wakimbiaji wazuri wa baadaye.

MWISHO

 

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) ofisini kwake Mjini Bariadi juu ya mbio za Serengeti Marathon zinazotarajiwa kufunguliwa rasmi na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Novemba 14, 2020 kuanzia lango la Ndabaka wilayani Busega.

Mkurungenzi wa Serengeti Safari Marathon Bw.Timothy Mdinka(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu mjini Bariadi juu ya maandalizi ya mbio za Serengeti Marathon zinazotarajiwa kufunguliwa rasmi na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Novemba 14, 2020 kuanzia lango la Ndabaka wilayani Busega.

 


UPUNGUFU WA DAMU KWA WANAWAKE WENYE UMRI WA KUZAA WAPUNGUA SIMIYU

Changamoto ya upungufu wa damu kwa wanawake wenye umri wa kuzaa mkoani Simiyu imepungua kutoka asilimia 57 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 34 mwaka 2019 kutokana na juhudi mbalimbali zilizofanywa na viongozi, watendaji na wananchi, ikiwa ni pamoja na kulipa kipaumbele suala la lishe. 

Hayo yamebainishwa na Afisa Lishe wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Chacha Magige wakati akiwasilisha taarifa katika kikao cha kamati ya lishe ya mkoa kilichofanyika jana Novemba 11, 2020 mjini Bariadi.

Magige amesema Elimu ya kujirudiarudia imewafanya wananchi wapate uelewa wa kutosha juu ya ulaji sahihi ambapo amesisitiza kuwa pamoja na elimu mkoa uliweka mkakati kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kuongeza nguvu katika katika utoaji wa vidonge vya kuongeza damu kwa wasichana.

“Suala la lishe limepewa kipaumbele katika mkoa wetu na elimu inaendelea kutolewa katika vituo vya kutolea huduma za afya, ngazi ya jamii ambapo wanawake wanafundishwa kuandaa chakula kwa usahihi katika makundi yote matano ya vyakula,” alisema Dkt. Magige.

Katika hatua nyingine Magige amesema katika kukabiliana na udumavu mkoani Simiyu, Mkoa umejiwekea mikakati kadhaa ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya namna ya kuandaa vyakula vya kuwalisha watoto walio vituo vya kutolea huduma za afya na ngazi ya jamii, elimu ya unyonyeshaji sahih,  elimu ya mabadiliko ya ulaji na kuhimiza wananchi kwenda kuapata matibabu katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Akizungumza na wajumbe wa kamati ya lishe ya mkoa, Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu Bibi. Miriam Mmbaga ametoa rai kwa viongozi na watendaji kuendelea kutimiza wajibu wao na kila mmoja kutambua kuwa suala la lishe ni la muhimu huku akisisitiza ushirikiano ili kuwaokoa wananchi wa mkoa wa Simiyu kuondokana na athari zitokanazo na lishe duni.

Kwa upande wake Afisa Lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Bi. Happiness Kubona amesema Maafisa Lishe wataendelea kuwajengea uwezo wahudumu wa afyangazi ya jamii, ngazi ya vituo kuwatambua watoto wenye utapiamlo na kuwaingiza katika matibabu .

Ameongeza kuwa hamasa ya kujiunga na Mfuko Afya ya Jamii ulioboreshwa(ICHF) kwa wananchi itaendelea kutolewa ili waweze kupata huduma za matibabu na  hususani wanawake waweze kupata huduam ya vidonge vya kuongeza damu ili wasipungukiwa damu wakati wa ujauzito.

MWISHO

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga akifungua kikao cha kamati ya lishe mkoa kilichofanyika jana Novemba 11, 2020 mjini Bariadi

Mdauwa Lishe kutoka shirika lisilo la kiserikali la CUAMM akiwasilisha taarifa katika kikao cha kamati ya lishe kilichofanyika jana Novemba 11, 2020 mjini Bariadi, kushoto ni Afisa Lishe wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Chacha Magige 

Afisa Lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa akichangia hoja katika kikao cha kamati ya lishe mkoa kilichofanyika jana Novemba 11, 2020 mjini Bariadi.

Mratibu wa Huduma za mama na mtoto mkoa wa Simiyu, Bibi. Mary Makunja akichangia hoja katika kikao cha kamati ya lishe mkoa kilichofanyika jana Novemba 11, 2020 mjini Bariadi.
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya lishe wakifuatilia kikao cha kamati hiyo kilichofanyika jana Novemba 11, 2020 mjini Bariadi.

Baadhi ya wajumbe wa kamati ya lishe wakifuatilia kikao cha kamati hiyo kilichofanyika jana Novemba 11, 2020 mjini Bariadi.

Baadhi ya wajumbe wa kamati ya lishe wakifuatilia kikao cha kamati hiyo kilichofanyika jana Novemba 11, 2020 mjini Bariadi.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga(katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya lishe ya mkoa  mara baada ya kufunga kikao cha kamati hiyo kilichofanyika jana Novemba 11, 2020 mjini Bariadi. 

Baadhi ya wajumbe wa kamati ya lishe wakifuatilia kikao cha kamati hiyo kilichofanyika jana Novemba 11, 2020 mjini Bariadi.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga na baadhi ya wajumbe wa kamati ya lishe wakifuatilia kikao cha kamati hiyo kilichofanyika jana Novemba 11, 2020 mjini Bariadi.




MTAFITI TPRI AAINISHA SABABU ZA VIUATILIFU KUSHINDWA KUUA WADUDU KWENYE PAMBA

Matumizi ya viuatilifu chini ya kiwango kilichoelekezwa, matumizi yasiyo sahihi ya viuatilifu,unyunyiziaji na utunzaji wa viuatilifu usio sahihi na uwezo mdogo wa wakulima kutambua visumbufu vya mazao,vimetajwa kuwa ni miongoni mwa sababu za viuatilifu kushindwa kuua wadudu katika zao la pamba. 

Hayo yamebainishwa na Mtafiti wa kudhibiti visumbufu vya mazao/mimea kutoka Taasisi ya Utafiti wa viuatilifu nchini(TPRI), Bw. Ramadhan Kilewa wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya taaluma maalum kwa watoa huduma ya unyunyiziaji wa viuatilifu kwa zao la pamba mkoani Simiyu jana Novemba 11, 2020 mjini Bariadi.

“TPRI imeamua kabla ya msimu kuanza tuwajee uwezo wadau wetu ili wakafanye kazi nzuri itakayoleta tija katika uzalishaji wa pamba; tumeanza na wadau wanaofanya kazi mashambani ili tuwawezeshe kuwa na mbinu sahihi za kuchagua viuatilifu vilivyyo sahihi, utunzaji sahihi wa viuatilifu na utupaji wa viwekeo tupu kwa kufuata taratibu ili wasilete madhara kwa binadamu, wanyama na mazingira,” alisema Bw. Kilewa.

Ameongeza kuwa mafunzo hayo yanalenga kutimiza takwa la kisheria la Sheria Namba 4 ya Afya ya Mimea ya mwaka 2020 sehemu ya 37 inayosisitiza mafunzo ya usimamizi na udhibiti wa viuatilifu ili kuhakikisha mazao yatokanayo na kilimo na mifugo yanayoweza kutumika na wadau nchini yawe safi na yasiwe na mabaki yenye madhara kwa afya binadamu.

Akifungua mafunzo hayo Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi, Miriam Mmbaga ametoa wito kwa watoa huduma ya unyunyiziaji wa viuatilifu kwa zao la pamba kutekeleza jukumu hilo kwa kuwasaidia wakulima kwa mujibu wa sheria na maelekezo waliyopewa huku akiwaasa kutowapotosha na kuwaibia wakulima.

Aidha, Mmbaga amezitaka Halmashauri zote mkoani Simiyu kuhakikisha zinaandaa maafisa Kilimo watakaowasimamia watao huduma hao na kusisitiza watoa huduma hao kutambulishwa kwa maafisa kilimo wa kata  na kwa wakulima wa pamba katika vijiji ili waeze kutambulika na kufikiwa kwa urahisi wanapohitajika kutoa huduma ya unyunyiziaji.

Kaimu Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Uchumi na Uzalishaji Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Bibi, Kija Kayenze amesema, mara baada ya mafunzo haya matarajio mkoa ni kuongeza tija ya uzalishaji wa pamba mwaka huu kutoka wastani wa kilo 175 mpaka kilo 450 kwa ekari; ambapo amebainisha kuwa tija ndogo ilichangiwa na kukosa elimu ya matumizi sahihi ya viuatilifu.

Jumla ya vijana 600 mkoani Simiyu wanatarajiwa kunufaika na mafunzo ya taaluma maalum ya huduma ya unyunyiziaji wa viuatilifu kwa zao la pamba.

MWISHO

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga akifungua mafunzo ya taaluma maalum kwa watoa huduma ya unyunyiziaji wa viuatilifu kwa zao la pamba Tanzania jana Novemba 11, 2020 yanayofanyika kwa muda wa siku tatu mjini Bariadi hadi kufikia 13 Novemba 2020 TPRI, Gatsby Africa kwa kushirikiana na Mkoa wa Simiyu, ambayo yameandaliwa na TPRI, Gatsby Africa kwa kushirikiana na Mkoa wa Simiyu.

Mtafiti wa kudhibiti visumbufu vya mazao/mimea kutoka Taasisi ya Utafiti wa viuatilifu nchini(TPRI), Bw. Ramadhan Kilewa  akitoa maelezo ya awali katika mafunzo ya taaluma maalum kwa watoa huduma ya unyunyiziaji wa viuatilifu kwa zao la pamba Tanzania jana Novemba 11, 2020 yanayofanyika kwa muda wa siku tatu mjini Bariadi hadi kufikia 13 Novemba 2020 ambayo yameandaliwa na TPRI, Gatsby Africa kwa kushirikiana na Mkoa wa Simiyu. 

Baadhi ya watoa huduma ya unyunyiziaji wa viuatilifu kwa zao la pamba Tanzania wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga (hayupo pichani) wakati akifungua mafunzo wa watoa huduma hiyo Mjini Bariadi jana Novemba 11, 2020 ambayo yameandaliwa na  TPRI, Gatsby Africa kwa kushirikiana na Mkoa wa Simiyu.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga akifungua mafunzo ya taaluma maalum kwa watoa huduma ya unyunyiziaji wa viuatilifu kwa zao la pamba Tanzania jana Novemba 11, 2020 yanayofanyika kwa muda wa siku tatu mjini Bariadi hadi kufikia 13 Novemba 2020 TPRI, Gatsby Africa kwa kushirikiana na Mkoa wa Simiyu, ambayo yameandaliwa na TPRI, Gatsby Africa kwa kushirikiana na Mkoa wa Simiyu.


Saturday, November 7, 2020

TIGO SIMIYU YATOA MSAADA WA KARATASI KWA KIDATO CHA NNE

Kampuni ya Simu za Mkononi ya TIGO Mkoa wa Simiyu imetoa msaada wa karatasi kwa ajili ya maandalizi ya mtihani wa Taifa wa Kidato cha nne mkoani hapa, unaotarajia kufanyika kuanzia tarehe 23 Novemba, 2020. 

Akikabidhi msaada huo jana kwa niaba ya Meneja wa TIGO Mkoa wa Simiyu, msimamizi wa Duka la TIGO Bariadi Mjini Bi. Anna Kazimoto amesema msaada huo ni mwendelezo wa ushirikiano uliopo kati ya kampuni hiyo na Mkoa wa Simiyu huku akitoa rai kwa wanafunzi kusoma kwa bidii ili waweze kufikia malengo yao. 

“Tumetoa msaada huu ili ninyi ndugu zetu msome msiwe na uhaba wa karatasi kwa ajili ya kuchapisha mitihani na majaribio kwa ajili ya kujiandaa na mtihani wa Taifa wa Kidato cha nne, tumetoa rimu 45 zenye thamani ya shilingi 450,000/=” alisema Bi. Anna Kazimoto. 

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Afisa Elimu Taaluma Mkoa wa Simiyu, Mwl. Onesmo Simime ameishukuru kampuni ya simu ya Tigo na kuahidi kutumia msaada huo kwa matumizi yaliyokusudiwa. 

Nao wanafunzi wa Shule ya Sekondari Simiyu wameishukuru Tigo kwa msaada huo na kuahidi kuwa msaada huo utawasaidia kufikia malengo yao ikiwa ni pamoja na kujiandaa vema na mtihani waTaifa kwa kuwawezesha kupata karatasi kwa ajili ya kujibia majaribiao ya mara kwa mara kuelekea Mtihani wa Taifa wa kidato cha nne. 

“Mitihani inahitaji maandalizi msaada huu utawasaidia sana kidato cha nne kuondokana na uhaba wa karatasi kwa ajili ya kufanya mitihani na majaribio, tunawashukuru sana Tigo na tunaamini dada zetu na kaka zetu watafanya vizuri na hiyo itakuwa ni sehemu ya shukrani kwa Tigo,” alisema Kuyala Lameck kutoka Shule ya sekondari Simiyu. 

Kwa upande wake Mwalimu Kulwa Mtanzania ameishukuru Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo kwa msaada huo na kutoa wito kwa kampuni hiyo kuendelea kuwa mdau muhimu wa elimu wa mkoa wa Simiyu.

MWISHO

Mwakilishi wa Meneja wa Kampuni ya Simu za mkononi mkoa wa Simiyu, Bi. Anna Kazimoto akikabidhi msaada wa karatasi kwa mmoja wa wanafunzi wa shule ya Sekondari Simiyu Mjini Bariadi Novemba 06, 2020 waliopokea msaada huo kwa niaba ya wenzao, ambao umetolewa kwa ajili ya kusaidia katika maandalizi ya mtihani wa kidato cha nne.
Mwakilishi wa Meneja wa Kampuni ya Simu za mkononi mkoa wa Simiyu, Bi. Anna Kazimoto akikabidhi msaada wa karatasi kwa mmoja wa wanafunzi wa shule ya Sekondari Simiyu Mjini Bariadi Novemba 06, 2020 waliopokea msaada huo kwa niaba ya wenzao, ambao umetolewa kwa ajili ya kusaidia katika maandalizi ya mtihani wa kidato cha nne.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya sekondari Simiyu wakifuatilia mapokezi ya msaada wa karatasi ulitolewa na Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo kwa wanafunzi wa Kidato cha nne mkoani Simiyu Novemba 06, 2020 kwa ajili ya maandalizi ya mtihani wa Taifa unaotarajiwa kuanza Novemba 23, 2020
Afisa Elimu Taaluma mkoa wa Simiyu, Mwl. Onesmo Simime akimshukuru mmoja wa wawakilishi wa Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo baada ya makabidhiano ya msaada wa karatasi uliotolewa na kampuni hiyo kwa wanafunzi wa Kidato cha nne mkoani Simiyu Novemba 06, 2020 kwa ajili ya maandalizi ya mtihani wa Taifa unaotarajiwa kuanza Novemba 23, 2020.
Baadhi ya karatasi ziliotolewa na Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo kwa wanafunzi wa Kidato cha nne mkoani Simiyu Novemba 06, 2020 kwa ajili ya maandalizi ya mtihani wa Taifa unaotarajiwa kuanza Novemba 23, 2020
Afisa Elimu Taaluma mkoa wa Simiyu, Mwl. Onesmo Simime akiteta jambo na wawakilishi wa Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo baada ya makabidhiano ya msaada wa karatasi uliotolewa na kampuni hiyo kwa wanafunzi wa Kidato cha nne mkoani Simiyu Novemba 06, 2020 kwa ajili ya maandalizi ya mtihani wa Taifa unaotarajiwa kuanza Novemba 23, 2020.
Afisa Elimu Taaluma mkoa wa Simiyu, Mwl. Onesmo Simime akizungumza na wanafunzi wa Shule ya sekondari Simiyu (hawapo pichani) Novemba 06, 2020 wakati wa makabidhiano  ya msaada wa karatasi uliotolewa na Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo kwa ajili ya maandalizi ya mtihani wa Taifa wa Kidato cha nne  unaotarajiwa kuanza Novemba 23, 2020
 

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!