Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila
amewahakikishia wachimbaji wadogo katika mgodi wa dhahabu wa Bulumbaka uliopo
katika kijijj cha Gasuma wilayani Bariadi mkoani hapa kuwa watapata leseni za
uchimbaji na kusisitiza kuwa kamwe hawataondolewa katika mgodi huo.
Prof. Msanjila ameyasema hayo jana Novemba 23, 2020 wakati
akizungumza katika kikao chake na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Bariadi, Mkoa
wa Simiyu, baadhi ya wamiliki wa mashamba katika eneo la mgodi na baadhi ya
wachimbaji wadogo, katika Kijiji cha Gasuma wilayani Bariadi.
"Muombe leseni mtapewa, leseni haiwezi kutolewa kwa mtu
kutoka huko aliko halafu hawa vijana ambao wanachimba sasa hivi wakaondolewa
hapana; najua kuna maombi nayaonaona kwenye mitandao lakini msiwe na wasiwasi
hayawezi kutoka," alisema Prof. Msanjila.
Aidha, Prof. Msanjila ameeleza utaratibu wa fidia kwa wenye
mashamba "tusiichukulie kwamba kwa kuwa na shamba unakuwa na haki ya
kuchimba, hapana; ila ni kwamba wale wanaochimba hawana fedha ya kukufidia,
sasa tumeweka utaratibu kwamba fidia
yako uipate taratibu kwenye mgao na naamini huwa ni nyingi kuliko fidia nyingine.”
Katika hatua nyingine Prof. Msanjila amemtaka Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga kuanzisha upya mchakato wa kumpata msimamizi wa
mgodi wa Bulambaka ambaye atahakikisha ulinzi unaimarishwa, mazingira
yanaboreshwa ikiwa ni pamoja na uchimbaji wa vyoo pamoja na kuimarisha uhusiano
mzuri miongoni mwa wachimbaji.
Awali baadhi ya wachimbaji wadogo na wamiliki wa mashamba walisilisha
changamoto mbalimbali zinazowakabili katika mgodi huo ikiwa ni pamoja na kuomba
uboreshaji wa miundombinu na upatikanaji wa huduma muhimu, ambapo Msanjila
amebainisha kwamba Serikali inazifanyia kazi na baadhi zitatatuliwa na
msimamizi wa mgodi huo baada ya kukamilika kwa mchakato wa kumpata ambao
utaanzishwa Mkuu wa Wilaya.
“Wachimbaji tumewekeza gharama kubwa sana, tunaomba serikali
isaidie kuimarisha ulinzi na usimamizi wa mali tunazochimba na kuendelea
kuboresha miundombinu ili tuweze kusafirisha mali tunazochimba hapa kwa urahisi,”
alisema mchimbaji mdogo Wibelo Kihalata.
“Wenye Maeneo tuliomba leseni ili na sisi tuweze kufanya kazi na
Watanzania wenzetu, tunashukuru kwa kuwa mmetueleza kuwa hata sisi tukijiunga
tunaweza kupata leseni tukachimba na siyo wenye hela peke yao tu,” alisema
Masuke Sahani Mwenyekiti wa Kikundi cha Umoja Bulumbaka Bariadi.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga
amesema atahakikisha mchakato wa kumpata
msimamizi wa mgodi linafanyika kwa uwazi na kusimamia uendeshaji wa mgodi huo
kwa kufuata sheria, kanuni, taratibu na miongozo kutoka wizara ya Madini.
Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga
amesema Serikali ya mkoa wakati wowote itahakikisha inasimamia Serikali ya
wilaya katika kuhakikisha shughuli zote zinazofanyika zinafuata sheria, kanuni
na taratibu.
MWISHO
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila
akizungumza baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Bariadi, Mkoa wa Simiyu, baadhi ya baadhi
ya wachimbaji wadogo, wamiliki wa mashamba katika eneo la mgodi wa
Bulumbaka Novemba 23, 2020 katika Kijiji
cha Gasuma wilayani Bariadi.
Baadhi ya wananchi wakimsikilza Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini,
Prof. Simon Msanjila katika kikao chake na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya
Bariadi, Mkoa wa Simiyu, baadhi ya baadhi ya wachimbaji wadogo, wamiliki wa
mashamba katika eneo la mgodi wa Bulumbaka
Novemba 23, 2020 katika Kijiji cha Gasuma wilayani Bariadi.
Mkuu wa Wilay ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akizungumza katika
kikao cha Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila na baadhi ya
viongozi wa Wilaya ya Bariadi, Mkoa wa Simiyu, baadhi ya wachimbaji wadogo,
wamiliki wa mashamba katika eneo la mgodi wa Bulumbaka Novemba 23, 2020 katika Kijiji cha Gasuma
wilayani Bariadi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga akizungumza
katika kikao cha Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila na baadhi
ya viongozi wa Wilaya ya Bariadi, Mkoa wa Simiyu, baadhi ya baadhi ya
wachimbaji wadogo, wamiliki wa mashamba katika eneo la mgodi wa Bulumbaka Novemba 23, 2020 katika Kijiji cha Gasuma

Bw. Samwel Chegeni mmoja wa wamili wa mashamba akichangia hoja
katika kikao cha Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Dkt. Simon Msanjila na baadhi
ya viongozi wa Wilaya ya Bariadi, Mkoa wa Simiyu, baadhi ya wachimbaji wadogo,
wamiliki wa mashamba katika eneo la mgodi wa Bulumbaka Novemba 23, 2020 katika Kijiji cha Gasuma
wilayani Bariadi.
Mchimbaji mdogo, Bw. Wibelo Kihalata akichangia hoja katika kikao
cha Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Dkt. Simon Msanjila na baadhi ya viongozi
wa Wilaya ya Bariadi, Mkoa wa Simiyu, baadhi ya wachimbaji wadogo, wamiliki wa
mashamba katika eneo la mgodi wa Bulumbaka
Novemba 23, 2020 katika Kijiji cha Gasuma wilayani Bariadi.

Baadhi ya wananchi wakimsikilza Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini,
Prof. Simon Msanjila katika kikao chake na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya
Bariadi, Mkoa wa Simiyu, baadhi ya wachimbaji wadogo, wamiliki wa mashamba
katika eneo la mgodi wa Bulumbaka
Novemba 23, 2020 katika Kijiji cha Gasuma wilayani Bariadi.
Afisa Madini Mkazi wa mkoa wa Simiyu, akiwasilisha taarifa
katika kikao cha ndani cha Katibu Mkuu
wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya
Bariadi, Mkoa wa Simiyu, kwa lengo la kujadili uendeshaji wa machimbo madogo ya
Bulumbaka Novemba 23, 2020 katika Kijiji cha Gasuma
wilayani Bariadi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga akiagana na baadhi
ya wananchi baada ya kikao cha Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Dkt. Simon
Msanjila na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Bariadi, Mkoa wa Simiyu, baadhi ya
wachimbaji wadogo, wamiliki wa mashamba katika eneo la mgodi wa Bulumbaka Novemba 23, 2020 katika Kijiji cha Gasuma
wilayani BariadiBaadhi ya wananchi wakimsikilza Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini,
Prof. Simon Msanjila katika kikao chake na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya
Bariadi, Mkoa wa Simiyu, baadhi ya wachimbaji wadogo, wamiliki wa mashamba
katika eneo la mgodi wa Bulumbaka
Novemba 23, 2020 katika Kijiji cha Gasuma wilayani Bariadi.
Afisa Madini Mkazi wa mkoa wa Simiyu, akiwasilisha taarifa
katika kikao cha ndani cha Katibu Mkuu
wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya
Bariadi, Mkoa wa Simiyu, kwa lengo la kujadili uendeshaji wa machimbo madogo ya
Bulumbaka Novemba 23, 2020 katika Kijiji cha Gasuma
wilayani Bariadi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga akiagana na
baadhi ya wananchi baada ya kikao cha Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Dkt.
Simon Msanjila na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Bariadi, Mkoa wa Simiyu, baadhi
ya wachimbaji wadogo, wamiliki wa mashamba katika eneo la mgodi wa
Bulumbaka Novemba 23, 2020 katika Kijiji
cha Gasuma wilayani Bariadi.
Baadhi ya wananchi wakimsikilza Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini,
Prof. Simon Msanjila katika kikao chake na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya
Bariadi, Mkoa wa Simiyu, baadhi ya wachimbaji wadogo, wamiliki wa mashamba
katika eneo la mgodi wa Bulumbaka
Novemba 23, 2020 katika Kijiji cha Gasuma wilayani Bariadi.
Baadhi ya viongozi wakifuatilia kikao cha Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Dkt.
Simon Msanjila na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Bariadi, Mkoa wa Simiyu, baadhi
ya wachimbaji wadogo, wamiliki wa mashamba katika eneo la mgodi wa
Bulumbaka Novemba 23, 2020 katika Kijiji
cha Gasuma wilayani Bariadi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila
akizungumza na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Bariadi, Mkoa wa Simiyu katika
kikao cha ndani kwa lengo la kujadili uendeshaji wa machimbo madogo ya Bulumbaka
Novemba 23, 2020 katika Kijiji cha Gasuma wilayani Bariadi.