Sunday, January 6, 2019

DKT BASHIRU ASHAURI WAKUU WA MIKOA KUJIFUNZA SIMIYU

Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally amewashauri Wakuu wa Mikoa hapa nchini kwenda(kuja) kujifunza namna ya kufanya kazi kwa umoja na mshikamano kati ya Chama na Serikali sambamba na ubunifu na uchapakazi wa viongozi wa mkoa huo.


Dkt. Bashiru ameyasema hayo Januari 05, 2019 wakati akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM pamoja na Viongozi na watendaji wa Serikali, Mjini Bariadi wakati akiwa katika ziara yake mkoani Simiyu.

Dkt. Bashiru amewapongeza Viongozi wa Serikali wakingozwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kwa namna wanavyoshirikiana na viongozi wa Chama kwa namna wanavyosimamia shughuli za maendeleo.

“Niwapongeze  kwa namna mnavyosimamia shughuli za maendeleo, nilikuwa hapa mwaka 2005 kama msimamizi wa uchaguzi nilizunguka maeneo mengi mengine yalikuwa hayapitiki, leo nimekuja nikazungushwa maeneo machache tu, nimeona mambo mengi sana ya tofauti kwa hiyo uongozi wa mkoa huu kwa Chama na Serikali umefanya kazi kubwa na bado mna nafasi kubwa ya kufanya mambo makubwa zaidi” alisema

Aidha, amesema ili uchumi uwe imara, wa kisasa na wenye manufaa ni lazima uwe jumuishi na uwalenge watu walio wengi ambao ni wazalishaji wadogo hususani katika  katika sekta ya kilimo na viwanda huku akisisitiza umakini zaidi ili uwepo wa viwanda na maendeleo ya kilimo viwanufaishe wengi.

Ameongeza kuwa wakati Mkoa wa Simiyu unapanga mipango mbalimbali ya maendeleo ya kiuchumi ni vema kukawa na mpango wa matumizi bora ya ardhi, ili kuondoa migogoro kwa watumiaji ambayo inakuwa chanzo cha chuki na watu kuishi kwa wasiwasi.

Katika hatua nyingine Dkt. Bashiru amesema CCM imejipanga kuhakikisha kuwa itasimamia na kuimarisha ushirika ambao utasimamiwa na wataalam wenye taaluma na maadili ili uweze kuwanufaisha wanaushirika na kutatua changamoto zao.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema kuwa Viongozi na watendaji wa Serikali Mkoani humo watahakikisha wanasimamia utekelezaji wa Ilani ya CCM huku akisisitiza kuwa fedha zote zinazoletwa katika mkoa wa Simiyu zitasimamiwa vizuri na zitafanya kazi iliyokusudiwa.

Aidha, Mtaka amesema Mkoa wa Simiyu unafanya utafiti kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) ili kubaini fursa za kiuchumi zilizopo katika katika kila kijiji kwa Vijiji vyote 470, ambapo utekelezaji wa Falsafa ya Kijiji Kimoja Bidhaa Moja(OVOP) unatarajiwa kuzinduliwa rasmi mwezi Februari.

Ameongeza kuwa viwanda vikubwa vitatu vyenye uwezo wa kuajiri takribani wafanyakazi 2000 kikiwepo kiwanda cha chaki na kiwanda cha vifungashio (Maswa) kiwanda cha bidhaa 18 za afya  zitokanazo na pamba(Bariadi)  vitajengwa mwaka huu  2019 Simiyu.

“Ndugu Katibu Mkuu mwaka jana wakati Mhe. Rais anapokea ndege ya Air Bus alicheza muziki na  ukiangalia ilikuwa ni kitu kinachotoka moyoni kuonesha furaha yake, ninaamini mwaka 2019 Mhe. Rais ataucheza muziki huo hapa Simiyu” alisema Mtaka.

Naye Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Kheri James ambaye ni Mlezi wa CCM Mkoa wa Simiyu amesisitiza viongozi na wanachama kuimarisha uhusiano mzuri, kusaidiana na kupendana katika maisha ya siasa huku akiwasihi viongozi kulinda na kuheshimu dhamana walizopewa kwa kutimiza wajibu wao.

Akitoa salamu kwa niaba ya Wabunge wa Mkoa wa Simiyu, Mbunge wa Bariadi,Mhe. Andrew Chenge ametoa wito kwa viongozi na wanachama wa CCM mkoani Simiyu kudumisha upendo, umoja na mshikamano hususani katika kipindi cha kueleka uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally yuko Mkoani Simiyu kuanzia Januari 05,2019 kwa ziara ya kikazi ya siku mbili yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM mkoani humo.
MWISHO


Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally akizungumza na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali  mkoani Simiyu, katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi Januari 05,2019 wakati wa ziara yake mkoani hapa.




Kutoka kushoto Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Mhe. Kheri James na  Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally wakifurahia jambo katika kikao cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na viongozi na watendaji wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali  mkoani Simiyu,  kilichofanyika Mjini Bariadi Januari 05,2019 wakati wa ziara yake mkoani hapa.



Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, mhe. Anthony Mtaka akiwasilisha taarifa ya Serikali katika kikao cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na viongozi na watendaji wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali  mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi Januari 05,2019 wakati wa ziara yake mkoani hapa.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally(wa pili kulia)akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mhe. Benson Kilangi mara baada ya kuwasili wilayani humo kuweka jiwe la msingi la Ofisi ya CCM ya Wilaya, wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM mkoani Simiyu  Januari 05, 2019 .
Baadhi ya viongozi wa CCM wa Mkoa wa Simiyu wakicheza nyimbo za Chama wakati wakijiandaa kumpokea Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally(hayupo pichani) katika Mji mdogo wa Lamadi wilayani Busega, kwa ajili ya kuanza ziara ya siku mbili mkoani hapa Januari 05 na Januari 06 , 2019.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Itilima, Mahamoud Mabula(kushoto) akitoa maelezo ya jengo la Ofisi ya CCM wilaya kwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally(katikati) wakati alipokuwa akikagua jengo hilo kabla ya kuliwekea jiwe la msingi, wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM mkoani Simiyu  Januari 05, 2019 
Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally(kulia) akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo mara baada ya kuwasili Mkoani Simiyu kwa ajili ya ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM mkoani hapa Januari 05, 2019.
 Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally(mwenye skafu) akipokelewa na wanachama wa CCM mara baada ya kuwasili Mjini Bariadi kwa ajili ya ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM mkoani Simiyu Januari 05, 2019.


Viongozi wa Wilaya ya Itilima wakimkabidhi zawadi Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika Ofisi ya CCM Wilaya wakati wa  ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM mkoani Simiyu Januari 05, 2019.
Kutoka kushoto Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Mhe. Kheri James na  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo  wakifurahia jambo katika kikao cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na viongozi na watendaji wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali  mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi Januari 05,2019 wakati wa ziara yake mkoani hapa.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally(wa tatu kulia) akifurahia jambo na baadhi ya viongozi wa CCM wilaya ya Itilima na Mkoa wa Simiyu wakati wa  ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM mkoani Simiyu Januari 05, 2019.
Mbunge wa Bariadi, Mhe. Andrew Chenge akizungumza na wananchi wa wilaya ya Itilima wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally  ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM mkoani Simiyu Januari 05, 2019.




Mwenyekiti wa UVCCM na Mlezi wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Kheri James akizungumza katika kikao cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali  mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi Januari 05, 2019
Baadhi ya viongozi wa CCM mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally(hayupo pichani)  katika kikao chake na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali  mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi Januari 05, 2019
Baadhi ya watendaji, viongozi wa dini na viongozi wa CCM wa Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally(hayupo pichani)  katika kikao chake na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali  mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi Januari 05, 2019.
Baadhi ya watendaji, viongozi wa dini na viongozi wa CCM wa Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally(hayupo pichani)  katika kikao chake na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali  mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi Januari 05, 2019.
Vijana wa Chipukizi Wilaya ya Busega wakimvisha skafu Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally mara baada ya kuwasili Mkoani Simiyu kwa ajili ya ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM mkoani hapa Januari 05, 2019
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akichangia hoja katika kikao cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na viongozi na watendaji wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali  mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi Januari 05,2019 wakati wa ziara yake mkoani hapa.



Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Itilima, Mhe. Mahamoud Mabula(kushoto) akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally (wa tano kulia) kabla ya kumkabidhi zawadi aliyoandaliwa na viongozi wa wilaya hiyo,  mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ofisi ya CCM wilaya wakati akiwa katika ziara yake mkoani Simiyu, Januari 05, 2019.

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo (kushoto) akizungumza mara baada ya kumpokea Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally(mwenye skafu)  kutoka mkoani Mara, kwa ajili ya kuanza ziara mkoani Simiyu Januari 05,2019
 Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally( mwenye skafu) akikaribishwa naviongozi wa mara baada ya kuwasili mji mdogo wa Lamadi kwa ajili ya ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM mkoani hapa Januari 05, 2019


Baadhi ya viongozi wa CCM mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally(hayupo pichani)  katika kikao chake na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali  mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi Januari 05, 2019.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Mhe. Lydia Bupilipili wakifurahia jambo katika Mji Mdogo wa Lamadi wakati wamapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally(hayupo pichani)  ametokea mkoani Mara kwenda Simiyu kwa ziara ya kikazi ya siku mbili Januari 05-06, 2019.


Baadhi ya viongozi wa UWT mkoani Simiyu wakimkabidhi Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally(wa pili kulia) zawadi, wakati akiwa katika ziara yake mkoani Simiyu Januari 05, 2019. 
Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally(wa tano kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi na viongozi wa Serikali wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya k kikao chake na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali  mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi Januari 05, 2019.
Baadhi ya viongozi wa CCM wa Mkoa wa Simiyu wakicheza nyimbo za Chama wakati wakijiandaa kumpokea Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally(hayupo pichani) katika Mji mdogo wa Lamadi wilayani Busega, kwa ajili ya kuanza ziara ya siku mbili mkoani hapa Januari 05 na Januari 06 , 2019.


DKT BASHIRU AWAONYA VIONGOZI WALIOANZA KUTAFUTA UBUNGE KABLA YA WAKATI


Katibu Mkuu wa Chama cha Mpinduzi (CCM) Taifa Dkt. Bashiru Ally amewaonya baadhi ya Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, na Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma, ambao wameanza kukaa vikao kwa ajili ya kutafuta majimbo kabla ya wakati wa Chama hicho kutangaza mchakato wa kutafuta wagombea wapya wa ubunge na udiwani.

Dkt. Bashiru ameyasema hayo Januari 05, 2019 wakati akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM pamoja na Viongozi na watendaji wa Serikali katika wilaya ya Bariadi na Itilima wakati akiwa katika ziara yake mkoani Simiyu.

Dk Bashiru amesema ikiwa viongozi hao wataendelea kufanya hivyo atawataja hadharani na akasisitiza kuwa ni vema wakaridhika na nafasi walizopewa na Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwani kushindwa kufanya hivyo ni kumdharau aliyewateua.
“Wapo wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, Makatibu tawala wa mikoa, wakurugenzi wa halmashauri, na wakuu wa taasisi na mashirika ya umma, wameanza kukaa vikao kwa ajili ya kutafuta majimbo, CCM hatujatangaza mchakato wa kutafuta wabunge au madiwani wapya, uko wakati nitawatangaza hadharani, mridhike na nafasi zenu mlizopewa na Mhe. Rais” alisema
Katika hatua nyingine Dkt. Bashiru amesema kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika mwaka huu 2019 Viongozi wa CCM wajipange katika kuhakikisha viongozi wa Vijiji na Mitaa wanachaguliwa katika misingi ya demokrasia kwa kuzingatia sifa zao na si fedha zao(rushwa).
“ Katika mwaka huu wa kumuenzi Mwalimu Nyerere baada ya miaka 20 tunataka kufanya mchakato wa kusimamia uchaguzi uwe tofauti, wakati wa kuteua tuzingatie sifa na tuwapime viongozi kwa maisha yao na vitendo vyao......” alisema Dkt. Bashiru.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe. Benson Kilangi ameishukuru Serikali ya awamu ya tano  kwa kutoa zaidi ya shilingi bilioni 26 katika kipindi cha miaka mitatu, kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya  maendeleo.
 Naye Mbunge wa Jimbo la Itilima Mhe.Njalu Silanga, ameishukuru Serikali kwa kuboresha miundombinu ya barabara ambapo amebainisha kuwa kupitia Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) barabara katika jimbo hilo zimetengenezwa zinapitika na zipo ambazo zinaendelea kufanyiwa matengenezo.
Naye Katibu wa CCM Mkoa, Bw. Donald Magesa  akitoa taarifa ya Chama, utekelezaji wa Ilani ya CCM mkoani humo umefanyika vizuri huku akisisitiza kuwa Viongozi wa Chama na Serikali wamejipanga kwa kushirikiana na wananchi kukamilisha maboma yaliyojengwa ili kila mwanafunzi aliyefaulu darasa la saba mwaka 2018 aweze kuanza kidato cha kwanza.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally yuko Mkoani Simiyu kuanzia Januari 05,2019 kwa ziara ya kikazi ya siku mbili yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM mkoani humo.
MWISHO.
 Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally akizungumza na wanachama wa CCM na wananchi katika Mji mdogo wa Lamadi, mara baada ya kuwasili Mkoani Simiyu kwa ajili ya ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM mkoani hapa Januari 05, 2019.

Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally(kulia) akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM mkoani hapa Januari 05, 2019.
 Baadhi ya viongozi wa CCM mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally(hayupo pichani)  katika kikao chake na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali  mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi Januari 05, 2019.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally(wa tano kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi na viongozi wa Serikali wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya k kikao chake na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali  mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi Januari 05, 2019.
Kutoka kushoto Mbunge wa Maswa Mashariki, mhe. Stanslaus Nyongo, Mbunge wa Itilima, Mhe. Njalu Silanga, Mbunge wa Meatu, Mhe. Salum Khamis na Mbunge wa Maswa Magharibi, Mhe. Mashimba Ndaki wakifuatilia kikao cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na viongozi na watendaji wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali  mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi Januari 05,2019 wakati wa ziara yake mkoani hapa.
Baadhi ya viongozi wa CCM wa Mkoa wa Simiyu wakicheza nyimbo za Chama wakati wakijiandaa kumpokea Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally(hayupo pichani) katika Mji mdogo wa Lamadi wilayani Busega, kwa ajili ya kuanza ziara ya siku mbili mkoani hapa Januari 05 na Januari 06 , 2019.


Wednesday, January 2, 2019

SERIKALI YAWAHAKIKISHIA WAFANYABIASHARA UPATIKANAJI WA MAJI, UMEME

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amewahakikishia wafanyabiashara mkoani hapa kuwa Serikali itatatua changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji na umeme kupitia mradi wa maji wa ziwa Victoria, uimarishwaji wa mamlaka za maji na kujengwa kwa vituo vya kupozea umeme.

Mtaka ameyasema hayo wakati ufunguzi wa hoteli ya Sweet Dreams iliyoko Mjini Bariadi na kumpongeza mfanyabiashara John Sabu kwa uwekezaji huo.

Amesema Mkoa unaendelea kuimarisha vyanzo vya maji na mamlaka za maji na kufikia mwaka 2020 maji kutoka Ziwa Victoria yatakuwa yameshafika katika makao makuu ya mkoa, huku akibainisha kuwa tatizo la umeme litatatuliwa na ujenzi wa vituo vya kupozea umeme.

“Sisi tuna mradi mkubwa wa maji wa  Ziwa Victoria ambao (kwa maelezo ya Waziri wa Maji) mpaka mwezi Februari 2019 watakuwa wametangaza zabuni ya ujenzi wa mradi huo ili maji yafike hapa, kwa kuanza mpaka kufikia mwaka 2020 maji yatakuwa yamefika makao makuu ya mkoa”

“Kwenye umeme tumezungumza na watu wa Wizara ya Nishati, tutajengewa (sub-stations) vituo viwili vya kupozea umeme, kwa kuanzia kimoja kitajengwa mwaka huu kwa hiyo tutakuwa na umeme wa uhakika” alisisitiza Mtaka.

Katika hatua nyingine Mtaka amewataka Wakuu wa Wilaya kuwalinda wafanyabiashara wakubwa na wadogo na kuwasaidia kutafsiri sheria, miongozo na taratibu zinazopaswa kuwasaidia kufanya biashara zao katika mazingira mazuri, huku akisisitiza biashara ziendelee kufanyika saa 24.

Kwa upande wao Wafanyabiashara wamempongeza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kwa kuwaruhusu kufanya biashara saa 24 na wakamuahidi kuwa wataendelea kuwekeza katika ujenzi wa vitega uchumi mbalimbali ikiwemo hoteli za kisasa na kuendelea kuwa walipa kodi waaminifu.

“Tunamshukuru Mhe. Mkuu wa mkoa kwa kuruhusu wafanyabishara tufanye biashara zetu saa 24 tunamuahidi kuwa tutaendelea kufungua biashara mbalimbali kama hoteli  ili kuondoa adha ya malazi kwa wageni wanaofika hapa mkoani, pia tutaendelea kuwa walipa kodi halali wa nchi yetu” Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Mhe. Njalu Silanga.

Awali akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa Hoteli ya Sweet Dreams mtoto wa Mmiliki wa hoteli hiyo, Mary John Sabu amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kwa ubunifu na ushawishi wake uliopelekea matukio mengi ya Kitaifa kufanyika mkoani Simiyu, ambayo yamechangia kuongeza mzunguko wa biashara mkoani hapa.
MWISHO
Kutoka kushoto Mfanyabiashara wa Bariadi Bw. John Sabu, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na Mwenyekiti wa Wafanyabiashara mkoa wa Simiyu, Mhe. Njalu Silanga wakiteta jambo wakati wa hafla ya ufunguzi wa Hoteli ya Sweet Dreams Mjini Bariadi.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) na Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Mkoa wa Simiyu, Mhe. Njalu Silanga wakiteta jambo wakati wa hafla ya ufunguzi wa Hoteli ya Sweet Dreams Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Mkoa wa Simiyu ambaye pia ni Mbunge wa Itilima Mhe. Njalu Silanga akizungumza na wafanyabiashara na viongozi wa mkoa huo, wakati wa hafla ya ufunguzi wa Hoteli ya Sweet Dreams Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ( wa pili kushoto) akisalimiana na Bibi. Elizabeth Mlanda mke wa Mfanyabiashara Clement Mlanda  mara  baada ya kutoa pongezi kwa Mfanyabiashara John Sabu anayemiliki Hoteli ya Sweet Dreams, wakati wa hafla ya ufunguzi wa Hoteli hiyo Mjini Bariadi.
Mfanyabiashara kutoka Mjini Bariadi Bw. Yuma akimpongeza Mfanyabiashara John Sabu anayemiliki Hoteli ya Sweet Dreams (aliyeshika kinasa sauti)wakati wa hafla ya ufunguzi wa Hoteli hiyo Mjini Bariadi.

Sehemu ya Jengo la Hoteli ya Sweet Dreams(ghorofa) iliyopo Mjini Bariadi iliyofunguliwa hivi karibuni.

Katibu Tawala wa Mkoa, Bw. Jumanne Sagini (kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Tano Mwera wakati wa hafla ya ufunguzi wa Hoteli ya Sweet Dreams Mjini Bariadi.


Baadhi ya wafanyabiashara na wadau wa maendeleo wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(hayupo pichani) wakati wa hafla ya ufunguzi wa Hoteli ya Sweet Dreams Mjini Bariadi.
Mfanyabiashara John Sabu anayemiliki Hoteli ya Sweet Dreams na mkewe wakiingia katika hafla ya ufunguzi wa Hoteli hiyo Mjini Bariadi.
Watoto wa Mfanyabiashara John Sabu anayemiliki Hoteli ya Sweet Dreams wakiwasilisha risala ya ujenzi wa hoteli hiyo katika hafla ya ufunguzi wa Hoteli hiyo Mjini Bariadi.
Mfanyabiashara John Sabu anayemiliki Hoteli ya Sweet Dreams (kushoto) akizungumza na baadhi ya wafanyabiashara wenzake katika hafla ya ufunguzi wa Hoteli hiyo Mjini Bariadi.


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akifurahia jambo katika hafla ya ufunguzi wa Hoteli hiyo Mjini Bariadi.


Kutoka kushoto Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga,  Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Mkoa wa Simiyu ambaye pia ni Mbunge wa Itilima Mhe. Njalu Silanga na Katibu Tawala wa Mkoa, Bw. Jumanne Sagini wakiteta jambo wakati wa hafla ya ufunguzi wa Hoteli ya Sweet Dreams Mjini Bariadi.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya JB wakitoa burudani wakati wa wa hafla ya ufunguzi wa Hoteli ya Sweet Dreams Mjini Bariadi.
Mfanyabiashara Bw. James Nchubi  akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ( wa pili kulia) mara  baada ya kutoa pongezi kwa Mfanyabiashara John Sabu anayemiliki Hoteli ya Sweet Dreams, wakati wa hafla ya ufunguzi wa Hoteli hiyo Mjini Bariadi.
Baadhi ya viongozi, wafanyabiashara na wadau wakifuatilia masuala mbalimbali katika hafla ya ufunguzi wa Hoteli ya Sweet Dreams Mjini Bariadi.
Sehemu ya Jengo la Hoteli ya Sweet Dreams(ghorofa) iliyopo Mjini Bariadi iliyofunguliwa hivi karibuni.

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!