Tuesday, December 10, 2019

WAFUNGWA 136 WAACHIWA HURU SIMIYU KUFUATIA MSAMAHA WA RAIS, WAAHIDI KUWA RAIA WEMA

Jumla ya wafungwa 136 kutoka magereza za Mkoa wa Simiyu wameachiwa huru kufuatia msamaha wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John  Pombe  Magufuli alioutoka Desemba, 2019 katika sherehe za maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara yaliyofanyika jijini Mwanza.


Akitoa taarifa hiyo mbele ya waandishi wa habari Desemba 10, 2019 Mkuu wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Simiyu, ACP. Andulile Mwasampeta amesema  anamshukuru Mhe. Rais Magufuli  kitendo hicho cha kutoa msamaha ambacho kimesaidia kupunguza msongamano kwenye magereza ya mkoa wa Simiyu.

“Ninamshukuru sana Mhe. Rais Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama kwa kutoa msamaha huu ambao umepunguza msongamano katika magereza yetu hususani gereza la Bariadi; nitumie nafasi kuwaasa wafungwa waliosamehewa kwenda kuwa raia wema na wakafanye kazi halali na wasifanye makosa yatakayowaleta tena hapa gerezani,” alisema ACP Mwasampeta.

ACP Mwasampeta ameongeza kuwa wafungwa 136 waliopata msamaha wa Rais katika mkoa wa Simiyu ni wale waliokuwa wamebakisha muda wa  siku moja hadi miezi sita miezi 12 kumaliza muda wa vifungo vyao, ambapo amebainisha kuwa wamezingatia maelekezo ya Mhe. Rais katika vigezo vya watu walioachiwa huru.

Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kwa kufanikisha zoezi la kuwaleta pamoja wafungwa wote waliopata msamaha wa  Rais kwa kutoa magari  yaliyowezesha jeshi la magereza kuwachukua katika magereza mbalimbali mkoani Simiyu na kuwaleta katika gereza la Bariadi ambapo ndipo walipoanzia safari ya kurejea majumbani kwao.

Kwa upande wao wafungwa waliopata msamaha wa Rais na kuachiwa huru wamemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kutoa msamaha huo na kuahidi kuwa raia wema watakaofanya kazi halali na kujiepusha na makosa yote yanayoweza kusababisha wakarudi tena gerezani.

“Namshukuru sana Mhe. Rais kwa msamaha huu alioutoa kwa wafungwa zaidi ya 5000 tuliokuwa magereza mbalimbali niseme tu kwamba wale wote waliokuwa wafungwa kama mimi na wakapata msamaha huu tukawe raia wema na tukachape kazi tujenge nchi yetu, “ alisema Buluba George miongoni mwa wafungwa 136 mkoani Simiyu.

“Mimi naahidi kwenda kujishughulisha na shughuli za kuniwezesha kupata kipato, nitajitahidi kufanya kazi kwa bidii ili nisije nikaletwa tena huku gerezani, namshukuru sana Rais Magufuli kwa kutupa msamaha huu,” alisema Musa Lazaro miongoni mwa wafungwa 136 mkoani Simiyu
MWISHO



Sehemu ya Wafungwa 136 kutoka  mkoa wa Simiyu  waliopata msamaha wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John  Pombe  Magufuli  wakiwa tayari kuondoka katika Gereza la Bariadi Desemba 10, 2019 mara baada  ya kuachiwa huru kufuatia msamaha huo uliotolewa na Mhe. Rais katika sherehe za miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Desemba 09, 2019 Jijini Mwanza.
Sehemu ya Wafungwa 136 kutoka  mkoa wa Simiyu  waliopata msamaha wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John  Pombe  Magufuli  wakiwa tayari kuondoka katika Gereza la Bariadi Desemba 10, 2019 mara baada  ya kuachiwa huru kufuatia msamaha huo uliotolewa na Mhe. Rais katika sherehe za miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Desemba 09, 2019 Jijini Mwanza.


Sehemu ya Wafungwa 136 kutoka  mkoa wa Simiyu  waliopata msamaha wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John  Pombe  Magufuli  wakishuka kwenye magari yaliyowasafirisha kutoka magereza mbalimbali mkoani Simiyu kuwaleta Gereza la Bariadi, Desemba 10, 2019  kwa ajili ya kuruhusiwa kurejea majumbani kwao kufuatia msamaha huo uliotolewa na Mhe. Rais katika sherehe za miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Desemba 09, 2019 Jijini Mwanza.

Mkuu wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Simiyu, ACP Andulile Mwasampeta (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Desemba 10, 2019  mara baada ya kuwaachia  wafungwa 136 kufuatia msamaha wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John  Pombe  Magufuli  alioutoa katika sherehe za miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Desemba 09, 2019 Jijini Mwanza.
Bw. Buluba George miongoni mwa wafungwa 136 mkoani Simiyu waliopata msamaha wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John  Pombe  Magufuli  alioutoa katika sherehe za miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Desemba 09, 2019 Jijini Mwanza akimshukuru Mhe. Rais kwa msamaha huo mbele ya waandishi wa habari, Desemba 10, 2019.
Baadhi ya wafungwa waliopata msamaha wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John  Pombe  Magufuli wakiagana na Mkuu wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Simiyu, ACP Andulile Mwasampeta (kushoto) Desemba 10, 2019   mara baada ya kuachiwa huru kufuatia msamaha huo uliotolewa na Mhe. Rais katika sherehe za miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Desemba 09, 2019 Jijini Mwanza.
Bw. Musa Lazaro miongoni mwa wafungwa 136 mkoani Simiyu waliopata msamaha wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John  Pombe  Magufuli  alioutoa katika sherehe za miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Desemba 09, 2019 Jijini Mwanza akimshukuru Mhe. Rais kwa msamahahuo mbele ya waandishi wa habari, Desemba 10, 2019
Baadhi ya wafungwa wakitoka katika gereza la Bariadi Desemba 10, 2019 mara baada ya kuachiwa huru kufuatia msamaha wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John  Pombe  Magufuli  alioutoa katika sherehe za miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Desemba 09, 2019 Jijini Mwanza.
Mmoja wa Wafungwa  136 mkoani Simiyu waliopata msamaha wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John  Pombe  Magufuli  alioutoa katika sherehe za miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Desemba 09, 2019 Jijini Mwanza akimshukuru Mhe. Rais kwa msamahahuo mbele ya waandishi wa habari, Desemba 10, 2019

Baadhi ya wafungwa waliopata msamaha wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John  Pombe  Magufuli wakiagana na Mkuu wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Simiyu, ACP Andulile Mwasampeta (kulia) Desemba 10, 2019 mara baada ya kuachiwa kufuatia msamaha huo uliotolewa na Mhe. Rais katika sherehe za miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Desemba 09, 2019 Jijini Mwanza.

Saturday, December 7, 2019

WANAFUNZI 18,306 WACHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2019 SIMIYU

Jumla ya wanafunzi 18,306 sawa na asilimia 73.5 kati ya 24,915 waliofanya mtihani wa darasa la saba mwaka 2019 wamechaguliwa kujiunga Kidato cha Kwanza katika awamu ya kwanza mwaka 2020 katika shule za Serikali za Bweni na Kutwa.

Akitangaza matokeo hayo Desemba 06, 2019 Mjini Bariadi Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amesema idadi ya waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka 2020 imeongezeka kwa wanafunzi 5900 sawa na asilimia 23.8 ikilinganishwa na wanafunzi 12,399 waliochaguliwa mwaka 2019.
Aidha, Sagini amezitaka Halmashauri mkoani Simiyu kukamilisha miundombinu inayohitajika ili wanafunzi 6609 watakaochaguliwa awamu ya pili waweze kuripoti shuleni kabla ya 15 Februari, 2020.

“Halmashauri kamilisheni miundombinu inayohitajika ili wanafunzi watakaochaguliwa awamu ya pili waweze kuripoti shule kabla ya tarehe 15 Februari 2020; nawasihi  wazazi na walezi wa wanafunzi 6609 waliokosa nafasi awamu ya kwanza kuwa wavumilivu wakati halmashauri zinaendelea kukamilisha miundombinu inayohitajika,” alisema Sagini.

Katika hatua nyingine Sagini amewapongeza wanafunzi wote waliopata nafasi ya kuchaguliwa kidato cha kwanza na kuwaasa wasifanye anasa watumie fursa hiyo kujifunza na hatimaye wakamilishe safari ya elimu, huku akiwashukuru wadau wote wa elimu wakiwemo wazazi na walimu kwa namna walivyochangia katika uendeshaji na utoaji wa elimu bora.

Ameongeza kuwa wanafunzi wote waliochaguliwa kidato cha kwanza wanapaswa kuripoti shuleni tarehe 06 Januari, 2019 huku akiwasisitiza wazazi, walezi na jamii kwa kushirikiana na viongozi wa wilaya kuhakikisha wanfunzi woe waliochaguliwa wanaripoti shuleni na kubaki shuleni mpaka watakapohitimu elimu ya kidato cha nne.

Naye Afisa elimu wa Mkoa, Mwl. Ernest Hinju amesema matokeo ya mwaka 2019 kwa darasa la saba mkoa umepata zaidi ya asilimia 86 na kuufanya mkoa kushika nafasi ya nane Kitaifa ikilinganishwa na mwaka jana ambapo mkoa ulishika nafasi ya 22 Kitaifa, jambo ambalo limeufanya mkoa kuwa miongoni mwa mikoa iliyofanya vizuri na kuwa katika nafasi 10 bora kitaifa kwa mitihani yote mikubwa mtihani wa darasa la saba, kidato cha nne(nafasi ya 9) na kidato cha sita (nafasi ya 10).

Nao baadhi ya wajumbe walitoa maoni yao kuhusu namna ya kuboresha elimu na kuwasaidia wanafunzi ambao hawajapata nafasi ya kujiunga na elimu ya sekondari ambapo walishauri ujenzi wa vyuo vya ufundi na kuongea jitihada katika michezo.

“ “Ninashauri  kila Halmashauri iweke mkakati wa kuwa na vyuo ufundi ili waanfunzi wanaokosa nafasi kujiunga na elimu ya sekondari wapate fursa ya kujifunza ufundi na waweze kujiajiri na kujikwamua kimaisha,’ alisema Afisa Elimu Taaluma Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, Mwl. Juma Athuman.

“Moja ya sababu zinazochangia kushusha kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi ni utoro, napendekeza kuwa ili kukabiliana na tatizo la utoro Halmashauri zione haja ya kuimarisha miundombinu ya michezo; wanafunzi wengi wanaopenda michezo wanajituma pia na darasani ushahidi ninao, wanamihezo wanaofanya vizuri kwenye riadha ndani ya mkoa wetu wanafanya vizuri kitaaluma,” alisema Yohana Misese.
MWISHO



 Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini  akitoa taarifa ya uchaguzi wa wanafunzi watakaoingia Kidato cha kwanza mwaka 2020 katika kikao cha Kamati ya uchaguzi wa wanafunzi watakaoingia Kidato cha kwanza, kilichofanyika Desemba 06, 2019 Mjini Bariadi.


 Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya uchaguzi wa wanafunzi watakaoingia Kidato cha kwanza mkoani Simiyu, wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini  akitoa taarifa ya uchaguzi wa wanafunzi watakaoingia Kidato cha kwanza mwaka 2020 katika kikao cha kamati hiyo kilichofanyika Desemba 06, 2019 Mjini Bariadi.


 Afisa elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju akitoa taarifa ya ufaulu kwa darasa la saba mwaka 2019 katika kikao cha Kamati ya uchaguzi wa wanafunzi watakaoingia Kidato cha kwanza, kilichofanyika Desemba 06, 2019 Mjini Bariadi.


 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mhe. Robert Lweyo akichangia hoja katika katika kikao cha Kamati ya uchaguzi wa wanafunzi watakaoingia Kidato cha kwanza, kilichofanyika Desemba 06, 2019 Mjini Bariadi.


 Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akichangia hoja katika katika kikao cha Kamati ya uchaguzi wa wanafunzi watakaoingia Kidato cha kwanza, kilichofanyika Desemba 06, 2019 Mjini Bariadi.


 Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya uchaguzi wa wanafunzi watakaoingia Kidato cha kwanza mkoani Simiyu, wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini  akitoa taarifa ya uchaguzi wa wanafunzi watakaoingia Kidato cha kwanza mwaka 2020 katika kikao cha kamati hiyo kilichofanyika Desemba 06, 2019 Mjini Bariadi.


 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Bw. Anderson Njiginya akichangia hoja katika katika kikao cha Kamati ya uchaguzi wa wanafunzi watakaoingia Kidato cha kwanza, kilichofanyika Desemba 06, 2019 Mjini Bariadi.


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Bw. Melkizedeck Humbe  akichangia hoja katika katika kikao cha Kamati ya uchaguzi wa wanafunzi watakaoingia Kidato cha kwanza, kilichofanyika Desemba 06, 2019 Mjini Bariadi.

Thursday, December 5, 2019

VIONGOZI WA UMMA WATAKIWA KUEPUKA MGONGANO WA KIMASLAHI KATIKA MAAMUZI WANAYOFANYA

Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela amewataka viongozi wa Umma kuangalia maslahi ya nchi katika maamuzi wanayofanya kwa kuwa kutanguliza maslahi binafsi kunasababisha mgongano wa kimaslahi unaopelekea kuiumiza nchi.


Jaji Nsekela ameyasema hayo  wakati akizungumza na viongozi wa Umma katika mafunzo ya maadili na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi  kwa Viongozi wa Umma mkoani Simiyu ambayo  yamefanyika Desemba 04, 2019 Mjini Bariadi.

"Viongozi wa Umma wanapaswa kuzingatia kanuni na taratibu katiia maamuzi wanayofanya , ambazo zitasaidia kusiwepo mgongano wa kimaslahi ili kutenganisha matakwa binafsi  na maslahi ya Umma katika kutekeleza majukumu, wakitanguliza maslahi binafsi wanaliumiza Taifa," alisema Jaji Nsekela.

Akizungumzia suala la ahadi ya uadilifu ambayo viongozi wa Umma hukiri mara baada ya kupewa nyadhifa mbalimbali na kuapishwa, Jaji Nsekeka amesema viongozi wa Umma wasikiri ahadi hiyo kama kasuku badala yake wawe waumini wazuri wa yale wanayoyakiri ikiwa ni pamoja na kufanya kazi zao kwa uadilifu.

Aidha, Jaji Nsekela amesema Viongozi wa Umma wanapaswa kuwa wakweli  na wajaze kwa uhalali Tamko la Mali na Madeni huku akiwasisitiza kuondokana na dhana kwamba matakwa ya kisheria ya kujaza tamko hilo yanalenga kuwafilisi Mali zao kwa kuwa hakuna sheria inayozuia kiongozi wa Umma kuwa na Mali isipokuwa sheria inamtaka amiliki Mali halali zilizopatikana kwa njia halali.

Katika hatua nyingine Jaji Nsekela amewatahadharisha viongozi wa Umma kuachana na tabia ya kupokea zawadi kutoka kwa wanaowahudumia kwa kuwa jambo hilo ni kichocheo kikubwa cha rushwa, maana wao wanalipwa mishahara kwa kazi wanazofanya.

Awali akifungua mafunzo kwa Viongozi wa Umma mkoani Simiyu, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema mafunzo hayo yatawasaidia  na kuwakumbusha viongozi hao kutoka huduma kwa wananchi kwa uadilifu pasipo upendeleo kwa kigezo cha dini, ukabila, kujuana na kutekeleza majukumu yao kwa wakati.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Lamadi wilaya ya Busega, Mhe. Laurent Bija amesema ili viongozi wa Umma waendelee kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu ni vema taasisi na mifumo dhabiti ya usimamizi ikaimarishwa na iwe endelevu.

Naye Katibu wa Idara ya Ukuzaji Maadili  kutoka Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Bw. Waziri Kipacha amesema ikitokea kiongozi wa Umma amekiuka masharti yaliyopo kwenye Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, hatua ya kwanza ni Sekretarieti ya Maadili kufanya uchunguzi wa awali.
MWISHO



Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela akiwasilisha mada katika mafunzo ya  maadili na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi  kwa Viongozi wa Umma kutoka katika Taasisi mbalimbali za Umma mkoani Simiyu , yaliyofanyika Desemba 04, 2019 Mjini Bariadi.



Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akifungua mafunzo  ya maadili na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi  kwa viongozi wa Umma mkoani humo yaliyoendeshwa na Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela(wa tatu kushoto), Desemba 04,2019.



Baadhi ya Viongozi wa Umma wakimsikiliza Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela (hayupo pichani) akiwasilisha mada katika mafunzo ya  maadili na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi  kwa Viongozi wa Umma kutoka katika Taasisi mbalimbali za Umma mkoani Simiyu , yaliyofanyika Desemba 04, 2019 Mjini Bariadi.


Katibu wa Idara ya Ukuzaji Maadili  kutoka Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Bw. Waziri Kipacha akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali yaliyoulizwa na Viongozi katika mafunzo  ya maadili na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi  kwa viongozi wa Umma mkoani Simiyu yakiyoendeshwa na Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela(kushoto), ambayo yamefanyika  Desemba 04,2019 Mjini Bariadi.

Mkuu wa Wakala wa Ununuzi Serikalini (GPSA), Bw. Honest  Kahumba akichangia hoja katika mafunzo  ya maadili na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi  kwa viongozi wa Umma mkoani Simiyu yakiyoendeshwa na Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela(hayupo pichani), ambayo yamefanyika  Desemba 04,2019 Mjini Bariadi.
Diwani wa Kata ya Lamadi wilayani Busega, Mhe. Laurent Bija akichangia hoja katika mafunzo  ya maadili na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi  kwa viongozi wa Umma mkoani Simiyu yakiyoendeshwa na Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela(hayupo pichani), ambayo yamefanyika  Desemba 04,2019 Mjini Bariadi.
Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela (wa tatu kushoto) akiwa  katika picha ya pamoja na baadhi ya Mahakimu wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya mafunzo ya  maadili na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi  kwa Viongozi wa Umma kutoka katika Taasisi mbalimbali za Umma mkoani Simiyu , yaliyofanyika Desemba 04, 2019 Mjini Bariadi.

Baadhi ya Viongozi wa Umma wakimsikiliza Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela (hayupo pichani) akiwasilisha mada katika mafunzo ya maadili na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi  kwa Viongozi wa Umma kutoka katika Taasisi mbalimbali za Umma mkoani Simiyu , yaliyofanyika Desemba 04, 2019 Mjini Bariadi.

Baadhi ya Viongozi wa Umma wakimsikiliza Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela (hayupo pichani) akiwasilisha mada katika mafunzo ya maadili na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi  kwa Viongozi wa Umma kutoka katika Taasisi mbalimbali za Umma mkoani Simiyu , yaliyofanyika Desemba 04, 2019 Mjini Bariadi.



Baadhi ya Viongozi wa Umma wakimsikiliza Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela (hayupo pichani) akiwasilisha mada katika mafunzo ya maadili na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi  kwa Viongozi wa Umma kutoka katika Taasisi mbalimbali za Umma mkoani Simiyu , yaliyofanyika Desemba 04, 2019 Mjini Bariadi.


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akifungua mafunzo  ya maadili na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi  kwa viongozi wa Umma mkoani humo yaliyoendeshwa na Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela(wa pili kushoto),  ambayo yamefanyika Mjini Bariadi Desemba 04,2019.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akifunga mafunzo ya maadili na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi  kwa viongozi wa Umma mkoani humo (kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka) yaliyoendeshwa na Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela(kushoto),  ambayo yamefanyika Mjini Bariadi Desemba 04, 2019.
Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela (wa tatu kushotowalioketi) akiwa  katika picha ya pamoja na baadhi ya Wakuu wa Idara wa Halmashauri za Mkoa wa Simiyu mara baada ya mafunzo ya maadili na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi  kwa Viongozi wa Umma kutoka katika Taasisi mbalimbali za Umma mkoani Simiyu , yaliyofanyika Desemba 04, 2019 Mjini Bariadi.
Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela (wa tatu kushotowalioketi) akiwa  katika picha ya pamoja na baadhi ya Wakuu wa Taasisi za Umma Mkoa wa Simiyu mara baada ya mafunzo ya  maadili na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi  kwa Viongozi wa Umma kutoka katika Taasisi mbalimbali za Umma mkoani Simiyu , yaliyofanyika Desemba 04, 2019 Mjini Bariadi.

Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela (wa tatu kushotowalioketi) akiwa  katika picha ya pamoja na baadhi ya Wakurugenzi wa Halmashauri na Makatibu Tawala wa Wilaya za Mkoa wa Simiyu mara baada ya mafunzo ya maadili na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi  kwa Viongozi wa Umma kutoka katika Taasisi mbalimbali za Umma mkoani Simiyu , yaliyofanyika Desemba 04, 2019 Mjini Bariadi.

Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela (wa tatu kushotowalioketi) akiwa  katika picha ya pamoja na baadhi ya Wakuu wa Seksheni na Vitengo wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya mafunzo ya maadili na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi  kwa Viongozi wa Umma kutoka katika Taasisi mbalimbali za Umma mkoani Simiyu , yaliyofanyika Desemba 04, 2019 Mjini Bariadi.

Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela (wa tatu kushotowalioketi) akiwa  katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Ulizni na Usalama ya Mkoa wa Simiyu mara baada ya mafunzo ya maadili na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi  kwa Viongozi wa Umma kutoka katika Taasisi mbalimbali za Umma mkoani Simiyu , yaliyofanyika Desemba 04, 2019 Mjini Bariadi.
Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela (wa tatu kushotowalioketi) akiwa  katika picha ya pamoja na baadhi ya Madiwani kutoka katika Halmashauri za Mkoa wa Simiyu mara baada ya mafunzo ya maadili na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi  kwa Viongozi wa Umma kutoka katika Taasisi mbalimbali za Umma mkoani Simiyu , yaliyofanyika Desemba 04, 2019 Mjini Bariadi.

Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela (wa tatu kushoto walioketi) akiwa  katika picha ya pamoja na baadhi ya Madiwani kutoka katika Halmashauri za Mkoa wa Simiyu mara baada ya mafunzo ya maadili na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi  kwa Viongozi wa Umma kutoka katika Taasisi mbalimbali za Umma mkoani Simiyu , yaliyofanyika Desemba 04, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya Viongozi wa Umma wakimsikiliza Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela (hayupo pichani) akiwasilisha mada katika mafunzo ya maadili na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi  kwa  Viongozi wa Umma kutoka katika Taasisi mbalimbali za Umma mkoani Simiyu , yaliyofanyika Desemba 04, 2019 Mjini Bariadi.
Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela (kulia) akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, kwa ajili ya kutoa mafunzo ya maadili na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi  kwa kwa Viongozi wa Umma kutoka katika Taasisi mbalimbali za Umma mkoani Simiyu , yaliyofanyika Desemba 04, 2019 Mjini Bariadi.

Baadhi ya Viongozi wa Umma wakimsikiliza Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela (hayupo pichani) akiwasilisha mada katika mafunzo ya maadili na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi  kwa Viongozi wa Umma kutoka katika Taasisi mbalimbali za Umma mkoani Simiyu , yaliyofanyika Desemba 04, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya Viongozi wa Umma wakimsikiliza Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela (hayupo pichani) akizungumza na viongozi wa Umma, wakati alipowasili Mjini Bariadi  kutoa mafunzo ya maadili na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi  kwa   Viongozi wa Umma kutoka katika Taasisi mbalimbali za Umma mkoani Simiyu , yaliyofanyika Desemba 04, 2019 Mjini Bariadi.

Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela (katikati)akizungumza na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya  kuwasili Mjini Bariadi, kwa ajili ya kutoa mafunzo ya maadili na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi  kwa  kwa Viongozi wa Umma kutoka katika Taasisi mbalimbali za Umma mkoani Simiyu , yaliyofanyika Desemba 04, 2019 Mjini Bariadi.

Tuesday, December 3, 2019

SERIKALI YAWAFICHUA WATOTO 16,000 WENYE ULEMAVU WALIOFICHWA NA KUWAANDIKISHA SHULE


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa amesema Serikali imewafichua na kuwatambua jumla ya watoto 16,000 wenye ulemavu wa aina mbalimbali waliokuwa na umri wa kwenda shule katika mikoa yote hapa nchini waliokuwa wamefichwa na kuwaandikisha shule kulingana na mahitaji yao ya msingi.

Naibu waziri Ikupa ameyasema hayo Desemba 03, 2019 katika Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.

“Watoto wenye mahitaji maalum waliokuwa wamefichwa Serikali imewatambua na kuwaandikisha shule kulingana na mahitaji yao ya msingi, watoto 16,000 wametambuliwa kutoka mikoa na halmashauri zote nchini isipokuwa Halmashauri tisa tu ambazo hazijafikiwa kwa kuwa zoezi hili ni endelevu kadri bajeti itakavyoruhusu nazo zitafikiwa,”alisema Ikupa.

Aidha akijibu baadhi ya changamoto zilizowasilishwa na  Shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu (SHIVYAWATA) kuhusiana na kutengewa bajeti  ndogo amesema kuwa tayari serikali imetenga milioni 30 kwa ajili ya kuliwezesha baraza la watu wenye ulemavu  kufanya kazi kwa ufanisi, huku akitoa wito kwa wadau mbalimbali kuendelea kuongeza nguvu katika kuwasaida watu wenye ulemavu hususani walio katika maeneo ya pembezoni.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri  Ikupa ametoa wito kwa vyama vya siasa nchini kutenga nafasi maalum za uwakilishi bungeni kwa watu wenye ulemavu kama kilivyofanya Chama Cha Mapinduzi( CCM), huku akiwasisitiza wenye ulemavu na wao kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi badala ya kusubiri nafasi maalum pekee.

Awali akiwasilisha taarifa ya Mkoa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe. Benson Kilangi amesema Simiyu inawathamini na kuwajali watu wenye ulemavu huku akibainisha kuwa Halmashauri zimetenga zaidi ya shilingi milioni 231 katika mwaka wa fedha 2019/2020 kwa ajili ya kutoa mikopo isiyo na riba kwa watu wenye ulemavu na kuwataka kuchangamkia fursa hiyo ili wajikwamue kiuchumi.

Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Bibi. Tungi Mwanjala ameiomba Serikali   kuviwezesha viwanda vya ndani kutengeneza vifaa saidizi kwa watu wenye ulemavu ili kupunguza gharama zitokanazo na kodi ya kuagiza vifaa hivyo nje ya nchi.

Naye mmoja wa Watu wenye ulemavu Bi Nuru Awadh amesema katika kipindi hiki cha Serikali ya Awamu ya Tano watu wenye ulemavu wameaminiwa  katika nafasi mbalimbali na sheria nyingi zinazowahusu watu wenye ulemavu zitakelezwa kwa vitendo.

Maadhimisho ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu mwaka 2019 yanaongozwa na Kauli Mbiu inayosema: “HAMASISHA USHIRIKI WA WATU WENYE UELMAVU NA UONGOZI WAO: TEKELEZA AGENDA ENDELEVU 2030” 
**Mwisho**


Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa(kushoto) akizungumza na  watu wenye ulemavu  wakati alipotembelea mabanda yao kuona shughuli wanazofanya, katika Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa(wa tatu kushoto) akizungumza na wananchi na watu wenye ulemavu kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini, katika Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.

Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa(kushoto) akizungumza jambo na Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu nchini(SHIVYAWATA), Bi. Tungi Mwanjala katika Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.


Baadhi ya watu wenye ulemavu wakimsikiliza Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa(hayupo pichani) katika Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.


Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa(kushoto) akipokea maelezo kutoka kwa alemavu wasioona  kwenye banda lao , katika Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.

Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa(wa pili kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe. Benson Kilangi fedha  zilizotolewa na wadau mbalimbali kwa ajili kuwaunga mkono watu wenye ulemavu  katika shughuli zao za uzalishaji(kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka), katika Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.


Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa(wa nnekushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa Mkoa wa Simiyu, Viongozi wa SHIVYAWATA na Maafisa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, mara baada ya kuhitimisha Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) akitoa salamu za Mkoa kwa Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa(wa pili kushoto) mara tu baada ya kuwasili Mjini Bariadi kwa ajili ya Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.


Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu nchini(SHIVYAWATA), Bi. Tungi Mwanjala akiwasilisha taarifa ya SHIVYAWATA katika Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.

Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa(kulia) akimkabidhi mmoja wa watu wenye ulemavu sehemu ya  fedha  zilizotolewa na wadau mbalimbali kwa ajili kuwaunga mkono katika shughuli zao za uzalishaji, katika Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anaye shughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa(kulia) akipokea zawadi ya sabuni ya maji kutoka kwa mmoja wa watu wenye ulemavu, katika Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa(wa pili kulia) akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya kupokea taarifa ya mkoa kabla ya kueleka katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa(kulia) akipokea zawadi kutoka kwa mmoja wa watu wenye ulemavu, katika Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa(wa nnekushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi waandamizi wa Mkoa wa Simiyu na  Viongozi wa SHIVYAWATA, mara baada ya kuhitimisha Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa(kulia) akipokea zawadi kutoka kwa mmoja wa watu wenye ulemavu, katika Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Msanii Elizabeth Maliganya akiimba wimbo wenye ujumbe maalum kwa ajili ya watu wenye ulemavu, katika Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) akifurahia jambo na Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa mara baada ya kiwasili Mjini Bariadi kwa ajili ya Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa(kuhoto) akikaribisha katika banda la watu wenye ualbino wakayti alipotembelea mabanda ya watu wenye ulemavu kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na walemavu, katika Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa(wa nnekushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi waandamizi wa Mkoa wa Simiyu, Viongozi wa SHIVYAWATA na Maafisa Usatawi wa Jamii Mkoa wa Simiyu, mara baada ya kuhitimisha Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.

Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa(wa nnekushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi waandamizi wa Mkoa wa Simiyu na  Viongozi wa SHIVYAWATA, mara baada ya kuhitimisha Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anaye shughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa(katikati akizungumza na wananchi na watu wenye ulemavu kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini, katika Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.

Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa(kulia) akipokea zawadi kutoka kwa mmoja wa watu wenye ulemavu, katika Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa(kulia) akimkabidhi mmoja wa watu wenye ulemavu sehemu ya  fedha  zilizotolewa na wadau mbalimbali kwa ajili kuwaunga mkono katika shughuli zao za uzalishaji, katika Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa(wa tano kushoto walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi waandamizi wa Mkoa wa Simiyu, Viongozi wa SHIVYAWATA na wadau wa watu wenye ulemavu, mara baada ya kuhitimisha Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.

Baadhi ya viongozi na watendaji kutoka mkoa wa Simiyu na kutoka SHIVYAWATA wakifuatila mambo mbalimbali yaliyokuwa yakiendela wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anaye shughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa(kulia) akipokea zawadi kutoka kwa mmoja wa watu wenye ulemavu, katika Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anaye shughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa(kulia) akipokea zawadi kutoka kwa mmoja wa watu wenye ulemavu, katika Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Kaimu katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Gamitwe Mahaza akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe. Benson Kilangi, katika Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!