Saturday, December 15, 2018

SIMIYU YAIDHINISHIWA BILIONI 13 MATENGENEZO YA BARABARA, MIRADI YA MAENDELEO

Mkoa wa Simiyu umeidhinishiwa jumla ya shilingi bilioni 13.1 kwa ajili ya matengenezo ya barabara na  miradi ya maendeleo katika bajeti ya mwaka 2018/2019.

Hayo yamebainishwa na Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS)'Mkoa wa Simiyu, Mhandisi. Albert Kent wakati akiwasilisha taarifa katika Kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa, kilichofanyika Desemba 14, 2018 Mjini Bariadi.

Kent amesema kati ya fedha hizo shilingi bilioni 11.461 zimeidhinishwa kwa ajili ya matengenezo ya barabara kutoka katika mfuko wa barabara na shilingi bilioni 1.595 utekelezaji wa miradi 12  ya maendeleo  yenye urefu wa kilometa 78.2.

Aidha, Kent amezungumzia maendeleo ya ujenzi wa daraja la mto Sibiti na kubainisha kuwa ujenzi wake umefikia asilimia 85 na jitihada zinaendelea kufanyika, ili ifikapo mwezi Machi, 2019 liwe limekamilika kama ilivyoelekezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli mwezi Septemba, 2018 wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja hilo.

Naye Mratibu wa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA), Mhandisi. Salvatory Yambi amesema katika bajeti ya mwaka 2018/2019 Mkoa wa Simiyu umeidhinishiwa jumla ya shilingi bilioni 5.4  na kubainisha kuwa hadi sasa TARURA inaendelea kutekeleza miradi 29 yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 3.6 ambayo ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.

Awali akifungua kikao cha Bodi ya Barabara kwa niaba ya Mwenyekiti wa kikao hicho na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga amepongeza TANROADS na TARURA kwa kazi kubwa wanayoifanya mkoani humo, hususani katika kusimamia ujenzi na matengenezo barabara hali iliyochangia kuufungua mkoa na kuchochea kukua kwa uchumi.

Akichangia hoja katika kikao hicho, Mbunge wa Bariadi, Mhe. Andrew Chenge ameshauri kuwepo na uhusiano wa karibu kati ya TARURA na Halmashauri hususani katika maandalizi ya Bajeti, ili vipaumbele vya TARURA vizingatie vipaumbele vya Halmashauri ambao ndio wanaokutana na  wananchi moja kwa moja na kujua mahitaji yao.

Naye Katibu Tawala wa Mkoa Simiyu, Jumanne Sagini ametoa wito kwa Wakurugenzi wa halamshauri kutenga fedha kwa ajili ya matengenezo ya barabara ambazo haziko chini ya TARURA hususani katika kipindi hiki cha maandalizi ya bajeti.

Katika kikao hiki pia wajumbe mbalimbali walipata nafasi ya kuchangia hoja ambazo zililenga kuboresha miundombinu ya barabara na madaraja, masuala yote ambayo Mhandisi Kent alieleza kuwa yatafanyiwa kazi na yanayohitaji hatua zaidi kutoka katika wizara yenye dhamana yatafikishwa.

"Nashauri wananchi washirikishwe katika zoezi la uwekaji wa alama za vivuko wakati barabara ya Maswa-Bariadi itakapokamilika ili viwekwe mahali penye uhitaji" Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe

"Ili daraja la Sibiti liweze kuleta tija zaidi tunaomba TANROADS iandae mpango wa dharura wa kujenga daraja la Mto Itembe ili kuwaondolea adha wananchi  waweze kuvuka kutoka eneo moja  kwenda kwingine pindi mvua zinaponyesha." Mhe. Leah Komanya, Mbunge wa Viti Maalum CCM.

Mwenyekiti Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mhe. Robert Lweyo ameshauri  ijengwe  round about (mzunguko) Mjini Bariadi katika makutano ya barabara ya Ngulyati-Bariadi, Lamadi- Bariadi na Maswa-Bariadi, jambo ambalo Mhandisi Kent aliahidi kuliandikia barua na na kuliwasilisha katika wizara yenye dhamana na ujenzi.
MWISHO

Meneja wa Wakala wa Barabara(TANROADS) Mkoa wa Simiyu, Mhandisi. Albert Kent akiwasilisha taarifa yake ya Mkoa katika kikao cha Bodi ya barabara , kilichofanyika Desemba 14, 2018 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akifungua kikao cha bodi ya barabara kwa niaba ya Mwenyekiti wa kikao hicho, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(hayupo pichani), kilichofanyika Desemba 14, 2018 Mjini Bariadi. 
Mratibu wa Wakala wa Barabara mijini na Vijijini(TARURA)Mkoa wa Simiyu, Mhandisi. Salvatory Yambi taarifa yake ya Mkoa katika kikao cha Bodi ya barabara , kilichofanyika Desemba 14, 2018 Mjini Bariadi.


Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akifafanua jambo katika kikao cha Bodi ya barabara , kilichofanyika Desemba 14, 2018 Mjini Bariadi.


Baadhi ya wajumbe wa Kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Simiyu wakifuatilia kwa makini masuala mbalimbali yaliyokuwa yakijadiliwa katika kikao hicho, Desemba 14, 2018 Mjini Bariadi.
Mbunge wa Jimbo la Bariadi, Mhe. Andrew Chenge akichangia hoja katika kikao cha Bodi ya barabara mkoa wa Simiyu , kilichofanyika Desemba 14, 2018 Mjini Bariadi.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Simiyu, Mhe. Leah Komanya akichangia hoja katika kikao cha Bodi ya barabara , kilichofanyika Desemba 14, 2018 Mjini Bariadi.
Baadhi ya wajumbe wa Kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Simiyu wakifuatilia kwa makini masuala mbalimbali yaliyokuwa yakijadiliwa katika kikao hicho, Desemba 14, 2018 Mjini Bariadi.


Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera(kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt.Seif Shekalaghe wakitelezana jambo, katika kikao cha Bodi ya barabara mkoa wa Simiyu , kilichofanyika Desemba 14, 2018 Mjini Bariadi.

Baadhi ya wajumbe wa Kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Simiyu wakifuatilia kwa makini masuala mbalimbali yaliyokuwa yakijadiliwa katika kikao hicho, Desemba 14, 2018 Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo(kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Bariadi, Mhe. Andrew Chenge wakiangalia kwa makini taarifa zilizopo katika makablasha , wakati wa kikao cha Bodi ya barabara mkoa wa Simiyu , kilichofanyika Desemba 14, 2018 Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa Halamshauri ya Mji wa Bariadi, Mhe. Robert Lweyo akichangia hoja katika kikao cha Bodi ya barabara mkoa wa Simiyu , kilichofanyika Desemba 14, 2018 Mjini Bariadi.
Baadhi ya wajumbe wa Kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Simiyu wakifuatilia kwa makini masuala mbalimbali yaliyokuwa yakijadiliwa katika kikao hicho, Desemba 14, 2018 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe akichangia hoja katika kikao cha Bodi ya barabara mkoa wa Simiyu , kilichofanyika Desemba 14, 2018 Mjini Bariadi.


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Simiyu, Deusdedit Nsimeki akichangia hoja katika kikao cha Bodi ya barabara mkoa wa Simiyu , kilichofanyika Desemba 14, 2018 Mjini Bariadi.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!