Tuesday, April 7, 2020

TUTATUMIA WASULUHISHI KUTATUA MIGOGORO NGAZI YA VIJIJI, MTAA NA KATA: MPANJU

Wizara ya Katiba na Sheria, imeandaa utaratibu  wa kutumia  wasuluhishi  na watatuzi wa   migogoro ngazi ya vijiji na mitaa kote  nchini  kabla ya wananchi kufikisha mashauri yao mahakamani.

Hayo yamesemwa jana na Naibu Katibu Mkuu Wzara ya Katiba na Sheria Bw. Amon Mpanju wakati akihitimisha mafunzo ya msaada wa kisheria kwa viongozi wanawake ,watumishi wanawake wasio viongozi na makundi mbalimbali ya wanawake wakiwemo wajasiriamali ambayo yamelenga kuwajengea  uelewa mpana wa masuala ya kisheria.

"Hawa watu tutawasajili rasmi tutawatambua ili watusaidie kutatua migogoro kwenye familia, migogoro ya ardhi, ugomvi na kadhalika, lengo hasa ni kuwa na mfumo unaoweza kumfikia mwananchi kutatua migogoro pasipo na ulazima wa kwenda mahakamani ambako kimsingi wananchi wamekuwa wakipoteza muda na rasilimali nyingi," alisema Mpanju.

Aidha, Mpanju amesema lengo la Serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha wananchi hususani wale wa pembezoni na wasio na uwezo wa kumudu gharama za kutafuta mawakili wa kusimamia mashauri yao wanapata huduma za kisheria, ambapo amesema kupitia Sheria namba 1 ya Huduma za msaada wa kisheria ya mwaka 2017 Wizara ya Katiba na Sheria imesajili Taasisi na watoa huduma za kisheria kupitia kwa wasaidizi wa kisheria.

Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu, Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony  Mtaka amesema wizara ya katiba na sheria imekuwa msaada  kwa utoaji elimu ya sheria mkoani Simiyu na kuabinisha kuwa mafunzo hayo yatawasaidia washiriki kujua namba ya kushughulikia masuala na changamoto mbalimbali katika jamii.

Katika hatua nyingine Mtaka ameeleza kuwa mkoa wa Simiyu umepanga kutumia mabweni ya Shule za sekondari za Serikali kuwahifadhi washukiwa wa maambukizi ya Virusi vya Corona ambapo amewatoa hofu wakazi wa Simiyu kuwa kabla ya shule kufunguliwa mabweni yatakayotumika kwa kazi hiyo yatapuliziwa dawa endapo itabainika yalihifadhi watu wenye maambukizi.

Sambamba na hilo Mtaka ametoa ofa kwa walimu wa Mkoa wa Simiyu watakaokuja na ubunifu ambao utawasaidia wanafunzi kujisomea wakiwa nyumbani katika kipindi hiki ambacho shule zimefungwa kwa ajili ya tahadhari ya maambukizi ya virusi vya Corona.

Wawezeshaji wa mafunzo ya msaada wa kisheria wamesema, "mafunzo haya yamewasaidia sana watumishi na viongozi mbalimbali wanawake walioshiriki,walikuwa hawajui vitu vingi mfano, wengine walikuwa hawajui masuala ya sheria zandoa,mirathi na wengine walikuwa hawajui wanapata wapi huduma za msaada wa kisheria; tunaomba mafunzo kama haya yawe yanatolewa mara kwa mara kuwasaidia wananchi kujua sheria na haki zao” mwezeshaji wa. mafunzo Bibi. Eddah Maliki.

"Tumekutana na makundi mbalimbali ya wanawake katika mada za  haki za binadamu, ukatili wa kijinsia, sheria ya ndoa, mirathi, sheria ya huduma za msaada wa kisheria; tumebainia kuna uhitaji wa elimuya masuala ya kisheria na ukatili wa kijinsia ni changamoto kubwa katika jamii, washiriki wameomba wanaume pia wapewe mafunzo haya ili washirikiane kuondoa ukatili wa kijinsia katika jamii," alisema George Mollel Wakili kutoka Wizaraya Katiba na Sheria.

Naye mmojawa washiriki wa mafunzo haya, Angelina Daudi kutoka Ofisi ya. Dawati la Jinsia, Jeshi la Polisi wilaya ya Itilima amesema mafunzo haya yamemuongezea uelewa katika masuala yanayohusu haki za wanawake,mirathi na sheria ya ndoa na elimu aliyoipata itamsaidia kuboresha kazi yake na kuomba mafunzo haya yawe yanatolewa mara kwa mara..
MWISHO

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Bw. Amon Mpanju akizungumza na baadhi ya viongozi wanawake na makundi mbalimbali ya wanawake jana mkoani Simiyu wakati wa kuhitimisha mafunzo ya huduma za msaada wa kisheria yaliyofanyika Mjini Bariadi kwa muda wa siku tano.

Baadhi ya wanawake viongozi na wanawake wa makundi mbalimbali wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Bw. Amon Mpanju (hayupo pichani) wakati akihitimisha  mafunzo ya huduma za msaada wa kisheria kwa kundi hilo, yaliyofanyika Mjini Bariadi kwa muda wa siku tano.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na baadhi ya viongozi wanawake na makundi mbalimbali ya wanawake jana mkoani Simiyu wakati wa kuhitimisha mafunzo ya huduma za msaada wa kisheria yaliyofanyika Mjini Bariadi kwa muda wa siku tano.

Wakili kutoka Wizara ya Katiba na Sheria. George Mollel akitoa mafunzo kwa baadhi ya viongozi wanawake na makundi mbalimbali ya wanawake jana mkoani Simiyu wakati wa kuhitimisha mafunzo ya huduma za msaada wa kisheria yaliyofanyika Mjini Bariadi kwa muda wa siku tano.
 Mkuu wa Shule ya Msingi Ibulyu, Mwl. Adela Mkusi akizungumzia manufaa ya mafunzo ya humdma za kisheria yaliyotolewa kwa baadhi ya wanawake viongozi, watumishi wanawake na wajasiriamali mkoani Simiyu, wakati wa kuhitimisha mafunzo hayo yaliyofanyika kwa muda wa siku tano Mjini Bariadi.

 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) akizugumza na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Bw. Amon Mpanju ofisini kwake mara baada ya kuwasili mjini Bariadi jana kwa ajili ya kuhitimisha mafunzo ya huduma za msaada wa kisheria kwa viongozi wanawake, watumishi na wajasriamali wanawake mkoani Simiyu, ambayo yamefanyika kwa muda wa siku tano Mjini Bariadi.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) akizugumza na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Bw. Amon Mpanju ofisini kwake mara baada ya kuwasili mjini Bariadi jana kwa ajili ya kuhitimisha mafunzo ya huduma za msaada wa kisheria kwa viongozi wanawake, watumishi na wajasriamali wanawake mkoani Simiyu, ambayo yamefanyika kwa muda wa siku tano Mjini Bariadi.

Baadhi ya wanawake viongozi na wanawake wa makundi mbalimbali wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Bw. Amon Mpanju (hayupo pichani) wakati akihitimisha  mafunzo ya huduma za msaada wa kisheria kwa kundi hilo, yaliyofanyika Mjini Bariadi kwa muda wa siku tano.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) akizugumza na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Bw. Amon Mpanju ofisini kwake mara baada ya kuwasili katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Kusekwa Memorial kwa ajili ya kuhitimisha mafunzo ya huduma za msaada wa kisheria kwa viongozi wanawake, watumishi na wajasriamali wanawake mkoani Simiyu, ambayo yamefanyika kwa muda wa siku tano Mjini Bariadi.

Wakili kutoka Wizara ya Katiba na Sheria. George Mollel akitoa mafunzo kwa baadhi ya viongozi wanawake na makundi mbalimbali ya wanawake jana mkoani Simiyu wakati wa kuhitimisha mafunzo ya huduma za msaada wa kisheria yaliyofanyika Mjini Bariadi kwa muda wa siku tano.

Baadhi ya wanawake viongozi na wanawake wa makundi mbalimbali wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Bw. Amon Mpanju (hayupo pichani) wakati akihitimisha  mafunzo ya huduma za msaada wa kisheria kwa kundi hilo, yaliyofanyika Mjini Bariadi kwa muda wa siku tano.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!