Thursday, April 8, 2021

MALALAMIKO YA WACHIMBAJI, WENYE MASHAMBA MGODI WA BULUMBAKA BARIADI YASHUGHULIKIWE: RAS SIMIYU

 

Uongozi wa mkoa wa Simiyu umetoa siku saba kwa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi na Ofisi ya Madini Mkoa wa Simiyu kupitia malalamiko na hoja zote za wachimbaji wadogo, wamiliki wa mashamba na wadau wengine katika mgodi wa dhahabu wa Bulambaka wilayani Bariadi na kuhakikisha shughuli za uchimbaji wa madini unafanyika kwa mujibu wa sheria. 

Hayo yameelezwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga mara baada ya kiongozi huyo na viongozi wengine wa mkoa kuzungumza na wananchi hao waliofika  katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Aprili 08, 2021 Mjini Bariadi ili kupata ufumbuzi wa malalamiko yao.

“ Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Simiyu imepokea wachimbaji na wadau mbalimbali wanaofanya kazi katika mgodi wa Bulumbaka na kuwasikiliza baada ya kutoka kwa Mkuu wa Wilaya; hoja za wachimbaji ni pamoja na wao kutokubaliana na utaratibu wa utoaji leseni kwa kikundi kilichopewa leseni kufanya kazi katika eneo lile, ambapo baadhi ya wanakikundi wamedai kuwa hawakitambua kwa kuwa hawakushirikishwa,”

“Baada ya kuwasiliza pamoja na hoja nyingine tumeona hili suala bado liko ndani ya uwezo wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya hivyo nimetoa siku saba kwa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya  na ofisi ya madini mkoa wa Simiyu, wapitie hoja zote na kutoa ushauri na kufanyia kazi yale yote wanayoweza kuyafanyia kazi kwenye ngazi yao kuhakikisha uchimbaji madini ufanyike kwa mujibu wa sheria,” alisema Mmbaga.

Nao baadhi ya wamiliki wa mashamba na wachimbaji wadogo ambao ni wananchi walioko eneo la mgodi la Bulumbaka wamesema:

“Baadhi ya wenye mashamba hawajui leseni hii ilivyopatikana maana maana hawakushirikishwa, sisi wananchi ambao pia ni wachimbaji wadogo  tunaomba  haki itendeke, hatutaki mtu yeyote anyanyaswe,” alisema Bw.Masuke Sahani mkazi wa Bulumbaka

“ Sisi tuna kilio kikubwa na mgodi wetu tumeshangaa kwamba Mwananyanzala amepata leseni wakati sisi tuna muda mrefu tunatafuta hiyo leseni kwa watu wa madini hatujapata, tunaomba Mkuu wa Wilaya atusaidie sisi wakazi wa Bulumbaka tupate haki yetu,” alisema Monica Daniel mmoja wa wamiliki wa mashamba Bulumbaka.

Awali akizungumzia na wananchi hao walipofika ofisini kwake, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga amesema malalamiko ya wananchi hao ameyapokea, ambapo amebainisha kuwa maagizo aliyayatoa awali hayakufuatwa hivyo akawaomba wauone uongozi wa mkoa ambao nao baadaye ukaelekeza  ofisi yake iyashaghulikie kwa kuwa yako ndani ya uwezo wake.

Mmiliki wa leseni katika eneo la Bulumbaka Seni Mwananyanzala amesema kuwa leseni yake ilitolewa kihalali ambapo alifafanua kuwa leseni hiyo ilisainiwa tarehe 19 Machi 2021.

MWISHO

 

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga akitoa kauli ya mkoa kuhusu namna ya kushughulikia hoja na malalamiko ya wachimbaji wadogo na wamiliki wa mashamba katika eneo la mgodi wa Dhahabu wa Bulumbaka wilayani Bariadi waliofika kuona na uongozi wa mkoa Aprili 08, 2021 Mjini Bariadi  ili kupata ufumbuzi wa malalamiko yao. 

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akiwasiliza wachimbaji wadogo na wamiliki wa mashamba katika eneo la mgodi wa Dhahabu wa Bulumbaka wilayani Bariadi waliofika kumuona  Aprili 08, 2021 ofisini kwake Mjini Bariadi  ili kupata ufumbuzi wa malalamiko yao.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akiwasiliza wachimbaji wadogo na wamiliki wa mashamba katika eneo la mgodi wa Dhahabu wa Bulumbaka wilayani Bariadi waliofika kumuona  Aprili 08, 2021 ofisini kwake Mjini Bariadi  ili kupata ufumbuzi wa malalamiko yao.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akiwasiliza wachimbaji wadogo na wamiliki wa mashamba katika eneo la mgodi wa Dhahabu wa Bulumbaka wilayani Bariadi waliofika kumuona  Aprili 08, 2021 ofisini kwake Mjini Bariadi  ili kupata ufumbuzi wa malalamiko yao.

Baadhi ya wachimbaji wadogo na wamiliki wa mashamba katika eneo la mgodi wa Dhahabu wa Bulumbaka wilayani Bariadi wakisubiri kumuona Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (hayupo pichani) waliofika kumuona  Aprili 08, 2021 ofisini kwake Mjini Bariadi  ili kupata ufumbuzi wa malalamiko yao.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!