Sunday, June 16, 2019

WANUNUZI WA PAMBA MLIOPEWA LESENI NA BODI NUNUENI PAMBA YA WAKULIMA KWA BEI ELEKEZI: WAZIRI HASUNGA


Waziri wa Kilimo amewaomba wanunuzi wa pamba waliopewa leseni na Bodi ya pamba wanunue pamba kwa wakulima kwa bei elekezi ya shilingi 1200 kama ilivyopangwa na kukubaliwa katika kikao cha wadau wa pamba mwezi Mei, 2019.

Waziri Hasunga ameyasema hayo Juni 15, 2019 wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu wakati alipotembelea viwanda vya kuchambua pamba, vituo vya kununulia pamba na kuzungumza na wananchi kupitia mkutano wa hadhara.

“Naomba nitumie nafasi kuwaomba wanunuzi wa pamba wenye nia njema na nchi hii waliopewa leseni na Bodi ya Pamba waje kununua pamba kwa wakulima, bei elekezi ya mwaka huu ni shilingi 1200”-alisema Waziri Hasunga.

Waziri Hasunga amevitaka vyama vya ushirika vya msingi kuzikagua mizani kwani itakapobainika kufanyika uchakachuaji wakati wa kupima hatua kali zitachukuliwa kwa mujibu wa sheria, huku akiwahakikishia wakulima kuwa changamoto zote zilizobainishwa na wakulima katika msimu wa 2018/2019 zitafanyiwa kazi.

Mkulima wa Pamba kutoka Luguru wilayani Itilima, Bw. Ngusa Lutenganeja ameishauri Serikali kupanga bei ya pamba wakati wa maandalizi ya msimu ili wakulima walime wakiwa wanafahamu bei na maandalizi ya fedha yafanyike mapema wakulima wasikopwe.

Kwa upande wake Mnunuzi wa pamba ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Itilima, Mhe. Njalu Silanga amesema imani yake ni kwamba Serikali itasimamia na kuhakikisha pamba ya wakulima inanunuliwa kwa bei elekezi ya shilingi 1200/= na wananchi wanapata fedha zao kwa wakati.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema mkoa wa Simiyu una viwanda vingi vya kuchambua pamba, ambapo ameshauri kuwa ili kuliongezea thamani zao la pamba Wizara ya Kilimo kwa  kushirikiana na wadau wengine kuona uwezekano wa kujenga kiwanda cha  kutengeneza nguo  kwa kuwa uhakika wa soko la bidhaa zitakazotengenezwa upo.

Katibu wa Chama cha Wanunuzi wa pamba nchini (TCA), Bw. Boaz Ogola ametoa wito kwa Wanunuzi wa pamba kuunga mkono juhudi za Serikali katika viwanda kwa kuwekeza kwenye viwanda vya kuongeza thamani ya pamba ili tusitegemee soko nje ambalo linayumba.
MWISHO 

Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga(wa pili kushoto) akiangalia baadhi ya mashine za kuchambua pamba zinavyofanya kazi, wakati alipotembelea kiwanda cha kuchambua pamba cha Alliance Ginnery kilichopo Kasoli wilayani Bariadi, Mkoani Simiyu Juni 15, 2019.(wa nne kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka.

Meneja wa Kiwanda cha kuchambua pamba cha Alliance Ginnery kilichopo Kasoli wilayani Bariadi(kushoto) akitoa maelezo ya aina za mbegu za pamba zinazozalishwa katika kiwanda hicho kwa Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga,(wa pili kushoto) na viongozi wengine wa Mkoa wa Simiyu wakati wa ziara yake mkoani Simiyu Juni 15, 2019.
Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga(kushoto) akiangali namna taarifa za wakulima zinavyoandikwa mara baada ya pamba yao kupimwa wakati alipotembelea moja ya Chama cha Msingi Cha Ushirika (AMCOS)kilichopo kata ya Luguru wilayani Itilima, wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu, Juni 15, 2019.
Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga akiangalia baadhi ya marobota ya pamba iliyochambuliwa katika kiwanda cha NGS kilichopo Majahida wilayani Bariadi, mara baada ya kutembela kiwanda hicho wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu, Juni 15, 2019.
Mkurugenzi wa Kiwanda cha NGS kilichopo Majahida Bariadi ambaye pia ni Mbunge wa Itilima, Mhe. Njalu Silanga(wa tatu kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga (wa tatu kulia), na viongozi wengine wa Mkoa wa Simiyu wakati wa ziara ya Waziri huyo mkoani Simiyu Juni 15, 2019.
Baadhi ya viongozi na wataalam wa mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga(hayupo pichani)  wakati alipozungumza nao katika Ofisi ya Mkuu wa mkoa kabla ya kuanza ziara yake mkoani humo, Juni 15, 2019.
Mbunge wa Itilima, Mhe. Njalu Silanga akiwasilisha kero za wananchi zinazohusu kilimo kwa  Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga(kulia) katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Katika Kijiji cha Inalo Kata ya Luguru wilayani Itilima, wakati wa ziara ya Waziri huyo mkoani Simiyu Juni 15, 2019.
Mjumbe wa NEC kupitia Mkoa wa Simiyu, Mhe. Gungu Silanga akichangia hoja katika kikao cha ndani kati ya Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga na viongozi pamoja na watendaji mbalimbali, wakati wa ziara ya Waziri huyo mkoani Simiyu Juni 15, 2019.
Meneja wa Kiwanda cha kuchambua pamba cha Alliance Ginnery kilichopo Kasoli wilayani Bariadi(wa pili kulia) akitoa maelezo ya namna mbegu za pamba zinazozalishwa katika kiwanda hicho kwa Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga,(kushoto) na viongozi wengine wa Mkoa wa Simiyu wakati wa ziara yake mkoani Simiyu Juni 15, 2019.
Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga,( wa pili kushoto) akiwa na viongozi wengine wa Mkoa wa Simiyu, wakiaanagalia namna pamba inavyochambuliwa, wakati walipotembelea Kiwanda cha kuchambua pamba cha NGS kilichopo Majahida Bariadi, wakati wa ziara yake mkoani Simiyu Juni 15, 2019.
Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga,( wa pili kushoto mbele) akiwa na viongozi wengine wa Mkoa wa Simiyu, wakioneshwa mafuta yaliyotengenezwa kutoka katika pamba mbegu,, walipotembelea Kiwanda cha kuchambua pamba cha NGS kilichopo Majahida Bariadi, wakati wa ziara yake mkoani Simiyu Juni 15, 2019.
Meneja wa Kiwanda cha kuchambua pamba cha Alliance Ginnery kilichopo Kasoli wilayani Bariadi(aliyechuchumaa) akitoa maelezo ya namna pamba inavyochambuliwa katika kiwanda hicho kwa Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga,(kushoto) na viongozi wengine wa Mkoa wa Simiyu wakati wa ziara yake mkoani Simiyu Juni 15, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akitoa salamu za Mkoa, wakati wa ziara ya Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga,(kulia) mkoani Simiyu Juni 15, 2019.
Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Inalo Kata ya Luguru wilayani Itilima, wakati wa ziara yake mkoani Simiyu Juni 15, 2019.
Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga,( aliyenyosha mkono) akiwa na viongozi wengine wa Mkoa wa Simiyu, wakioneshwa mafuta yaliyotengenezwa kutoka katika pamba mbegu,, walipotembelea Kiwanda cha kuchambua pamba cha NGS kilichopo Majahida Bariadi, wakati wa ziara yake mkoani Simiyu Juni 15, 2019.
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba, Marco Mtunga(kushoto) akiwaeleza jambo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(wa pili kulia), Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga,(wa tatu kulia) na Meneja wa Alliance Ginnery, katika  ziara ya WAZIRI Hasunga katika Kiwanda cha kuchambua pamba cha Alliance Ginnery, kilichopo Kasoli wilayani Bariadi, wakati wa ziara yake mkoani Simiyu, Juni 15, 2019.
Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga(katikati) akitoka katika moja ya majengo ya kiwanda cha kuchambua pamba cha Alliance Ginnery kilichopo wakati wa ziara yake mkoani Simiyu, Juni 15, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akitoa salamu za Mkoa, wakati wa ziara ya Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga,(kulia) mkoani Simiyu Juni 15, 2019.
Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga, Meneja wa Kiwanda cha kuchambua pamba cha Alliance Ginnery na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakiteta jambo katika ziara ya Waziri Hasunga katika Kiwanda cha kuchambua pamba cha Alliance Ginnery, kilichopo Kasoli wilayani Bariadi, wakati wa ziara yake mkoani Simiyu, Juni 15, 2019.
Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga akizungumza na Baadhi ya viongozi na wataalam wa mkoa wa Simiyu katika Ofisi ya Mkuu wa mkoa kabla ya kuanza ziara yake mkoani humo, Juni 15, 2019.
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba, Marco Mtunga akifafanua jambo katika kikao cha ndani kati ya Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga na Baadhi ya viongozi na wataalam wa mkoa wa Simiyu katika Ofisi ya Mkuu wa mkoa kabla ya kuanza ziara ya Waziri huyo mkoani humo, Juni 15, 2019.
Mwenyekiti wa  CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo(kushoto) akifurahia jambo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, wakati wa ziara ya Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga (hayupo pichani) mkoani humo Juni 15, 2019.


Saturday, June 15, 2019

SIMIYU ITAENDELEA KUSHIRIKIANA NA WALEMAVU KUHAKIKISHA WANAPATA HUDUMA KWA WAKATI: DC KISWAGA

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe. Festo Kiswaga amesema Serikali mkoani Simiyu itaendelea kufanya kazi kwa kushirikiana na watu wenye ulemavu wa makundi yote  bila kubagua na kuhakikisha wanapata huduma kwa wakati katika taasisi za Serikali wanapoenda kupata huduma.


Kiswaga ameyasema hayo Juni 13, 2019 wakati wa alipofungua kikao cha uboreshaji huduma kwa jamii ya viziwi Mkoa wa Simiyu, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, kilichofanyika Mjini Bariadi.

Amesema watu wenye ulemavu wana haki sawa na watu wengine hivyo akatoa wito kwa vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na maeneo mengine ya kutoa huduma za jamii mkoani Simiyu kufanya utaratibu wa kuweka wataalam maalum wenye uelewa wa lugha ya alama ili kuondoa changamoto ya mawasiliano kwa watu wenye ulemavu hususani viziwi.

“Vyombo vya ulinzi na usalama vihakikishe vina mtu au watu kwa ajili ya kuwasaidia viziwi kuondoa changamoto ya mawasiliano pamoja na watu wenye ulemavu kwa ujumla wanaohitaji huduma, si lazima kuajiri kwa sasa kwa kuwa suala la ajira linaweza kuchukua muda; lakini wahakikishe wana mtu wa kutoa msaada viziwi wapate huduma” alisema Kiswaga.

Aidha, Kiswaga amesisitiza umuhimu wa kutoa elimu kwa viziwi kuhusu maeneo yaliyozuiwa kama vile katika vyombo vya ulinzi (majeshi) na kushauri kuwa ikiwa wanapaswa kwenda katika maeneo hayo waombe msaada kwa watu wenye uwezo wa kuzungumza ili kuepuka watu hao kuonekana kuwa wamevunja sheria kwa kukusudia kwenda maeneo hayo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Viziwi Tanzania(CHAVITA) Mkoa wa Simiyu, Mhandi Zephania amesema viziwi wanakabiliwa na changamoto ya mawasiliano wanapoenda kupata huduma mbalimbali hivyo chama hicho kinaendelea kutoa elimu ya lugha ya alama kwa watumishi wa maeneo mbalimbali ya kutolea huduma ili kukabiliana na changamoto hiyo.

Naye Mkalimani wa lugha ya alama Bw. Jonathan Livingstone amesema Wizara ya Elimu imekubali kupokea jukumu la kusanifisha lugha ya alama iingizwe katika mitaala ifundishwe katika shule za msingi, sekondari na vyuo.

Katika hatua nyingine Kamanda wa Wilaya ya Maswa, Jonas Nyaoga amesema Jeshi la polisi limejipanga kuwahudumia viziwi kwa namna ambayo wakiwa wanahitaji huduma wanasaidiwa kwa kuhakikisha kuwa kila wanapowahoji viziwi wanatafuta watu wanaofahamu lugha ya alama ili waweze kuwatafsiria.

Kikao cha kujadili uboreshaji wa huduma za jamii kwa viziwi mkoani Simiyu kilijumuisha viongozi wa Chama cha Viziwi(CHAVITA) Mkoa wa Simiyu, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya zote tano za Mkoa wa Simiyu.
MWISHO
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akifungua kikao cha uboreshaji huduma kwa jamii ya viziwi mkoa wa Simiyu kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Mhe. Anthony Mtaka, kilichofanyika Juni 13, 2019 Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa Chama cha Viziwi Tanzania(CHAVITA) Mkoa wa Simiyu, Bw. Mhandi Zephania akitoa taarifa ya Chama hicho katika kikao cha uboreshaji huduma kwa jamii ya viziwi mkoa wa Simiyu kilichofanyika Juni 13, 2019 Mjini Bariadi.
Mkalimani wa lugha ya alama Jonathan Livingstone akifafanua jambo katika katika kikao cha cha uboreshaji huduma kwa jamii ya viziwi mkoa wa Simiyu kilichofanyika Juni 13, 2019 Mjini Bariadi
Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Maswa, akichangia hoja katika kikao cha cha uboreshaji huduma kwa jamii ya viziwi mkoa wa Simiyu kilichofanyika Juni 13, 2019 Mjini Bariadi.
:- Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (wa tano kushoto mbele) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kikao cha uboreshaji huduma kwa jamii ya viziwi mkoa wa Simiyu, kilichofanyika Juni 13, 2019 Mjini Bariadi mara baada ya kufunga kikao hicho.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Bariadi, Bibi. Veronica Kinyemi, akichangia hoja katika kikao cha uboreshaji huduma kwa jamii ya viziwi mkoa wa Simiyu kilichofanyika Juni 13, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya wajumbe wa Kikao cha uboreshaji huduma kwa jamii ya viziwi mkoa wa Simiyu kilichofanyika Juni 13, 2019 Mjini Bariadi wakifuatilia hoja mbalimbali katika kikao hicho.
Baadhi ya Viongozi wa Serikali Mkoani Simiyu na baadhi ya viziwi Mkoani Simiyu wakimsikiliza Bw. Jonathan Livingstone (mkalimani wa lugha ya alama) wakati akiwasilisha taarifa katika kikao cha uboreshaji huduma kwa jamii ya viziwi mkoa wa Simiyu, kilichofanyika Juni 13, 2019 Mjini Bariadi.


Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt. Joseph Chilongani akichangia hoja katika kikao cha uboreshaji huduma kwa jamii ya viziwi mkoa wa Simiyu kilichofanyika Juni 13, 2019 Mjini Bariadi.

Baadhi ya Viongozi wa Serikali Mkoani Simiyu na baadhi ya viziwi Mkoani Simiyu wakifuatilia masuala mbalimbali yaliyowasilishwa katika kikao cha uboreshaji huduma kwa jamii ya viziwi mkoa wa Simiyu, kilichofanyika Juni 13, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akiagana na Mwenyekiti wa Chama cha Viziwi Tanzania(CHAVITA) Mkoa wa Simiyu, Bw. Mhandi Zephania mara baada ya kufunga kikao cha uboreshaji huduma kwa jamii ya viziwi mkoa wa Simiyu kilichofanyika Juni 13, 2019 Mjini Bariadi.

Thursday, June 13, 2019

NIDHAMU YATAJWA KUWA MSINGI WA MAFANIKIO KATIKA MICHEZO NA ELIMU SIMIYU


Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Ekwabi Mujungu amewataka wanafunzi walimu na maafisa elimu walio katika kambi ya Michezo ya UMITASHUMTA Ngazi ya mkoa kudumisha nidhamu wakati wote watakapokuwa katika kambi hiyo ili Mkoa uweze kufanya vizuri katika michezo na elimu kwa ujumla.

Mujungu ameyasema hayo Juni 12, 2019 wakati akifungua Mashindano ya UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, ambayo kwa mwaka 2019 yanaongozwa na Kauli Mbiu “MICHEZO NA SANAA KWA ELIMU BORA PIA NI AJIRA”.

“Ili tuweze kufanya vizuri katika michezo na Elimu kwa ujumla napenda kusisitiza nidhamu ya usimamizi wakati wa mashindano, kambi na ngazi ya Taifa; ni lazima kuwe na nidhamu binafsi kwenu ninyi wachezaji na wasimamizi wanaowasimamia, kama hakuna nidhamu tusitarajie matokeo mazuri” alisema Mujungu.

Aidha, Mujungu ametoa wito kwa Wakurugenzi wa Halmashauri mkoani hapa kuwawezesha Walimu wa michezo kupata mafunzo ili waweze kujua vema sheria za michezo mbalimbali kwa lengo la kuwasaidia wanafunzi kufahamu michezo hiyo na kuamua michezo hiyo kwa haki.

Katika hatua nyingine ametoa wito kwa Wakurugenzi wa Halmashauri kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo katika kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya michezo ikiwa ni pamoja na upungufu wa miundombinu ya viwanja, walimu wa michezo na ratiba ya michezo kutofuatwa.

Awali akitoa taarifa ya mashindano ya UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa mwaka 2019, Kaimu Afisa Elimu wa mkoa, Mwl. Onesmo Simime amesema mashindano hayo yatashirikisha michezo ya aina sita ambayo ni riadha, mpira wa miguu, mpira wa wavu, mpira wa mikono, mpira wa pete(wavulana na wasichana kwa michezo yote mitano) na fani za ndani.

Kwa upande wake Kaimu Afisa michezo wa Mkoa, Bw. Charles Maganga amesema kupitia mashindano haya ya UMITASHUMTA mwaka 2019 Walimu kwa kushirikiana na Maafisa Michezo waliopo kambini watahakikisha wanachagua wachezaji wazuri watakaounda timu ya Mkoa yenye ushindani na matarajio yao ni kufanya vizuri katika mashindano ya Kitaifa.

Naye mwanamichezo (mwanafunzi) Jeremia Boniface Jeremia kutoka Halamshauri ya Wilaya ya Bariadi akizungumza kwa niaba ya wenzake amesema matarajio yao ni Mkoa wa Simiyu kufanya vizuri kwa kuwa wameandaliwa vizuri na kaahidi kuwa watakuwa na nidhamu wakati wote wa mashindano hayo.
MWISHO
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Ekwabi Mujungu akizungumza na wanafunzi wa shule za Msingi walio katika Kambi ya Mashindano ya UMITASHUMTA Kimkoa katika shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa wakati wa  ufunguzi wa Mashindano hayo Juni 12, 2019.
Kaimu Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl. Onesmo Simime akitoa taarifa ya mashindano ya UMITASHUMTA mwaka 2019 ambayo yanayoendelea  katika shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa.
Baadhi ya wachezaji kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Maswa wakipita mbele ya Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Ekwabi Mujungu wakati wa Ufunguzi wa mashindano ya UMITASHUMTA Kimkoa katika shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa wakati wa  ufunguzi wa Mashindano hayo Juni 12, 2019.
Baadhi ya wachezaji wa Mpira wa Miguu kutoka Halmashauri ya Mji wa  Bariadi na Halmashauri ya Wilaya ya Meatu wakiwa katika mashindano ya UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa ambayo yanaendelea katika shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa.

Baadhi ya wachezaji kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi  wakipita mbele ya Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Ekwabi Mujungu wakati wa Ufunguzi wa mashindano ya UMITASHUMTA Kimkoa katika shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa wakati wa  ufunguzi wa Mashindano hayo Juni 12, 2019.
Baadhi ya wachezaji kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi  wakipita mbele ya Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Ekwabi Mujungu wakati wa Ufunguzi wa mashindano ya UMITASHUMTA Kimkoa katika shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa wakati wa  ufunguzi wa Mashindano hayo Juni 12, 2019.
Baadhi ya wachezaji kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi wakipita mbele ya Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Ekwabi Mujungu wakati wa Ufunguzi wa mashindano ya UMITASHUMTA Kimkoa katika shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa wakati wa  ufunguzi wa Mashindano hayo Juni 12, 2019.
Baadhi ya wachezaji kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Busega wakipita mbele ya Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Ekwabi Mujungu wakati wa Ufunguzi wa mashindano ya UMITASHUMTA Kimkoa katika shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa wakati wa  ufunguzi wa Mashindano hayo Juni 12, 2019.
Baadhi ya wachezaji kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Meatu wakipita mbele ya Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Ekwabi Mujungu wakati wa Ufunguzi wa mashindano ya UMITASHUMTA Kimkoa katika shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa wakati wa  ufunguzi wa Mashindano hayo Juni 12, 2019.
Baadhi ya wachezaji kutoka Halmashauri ya Mji wa Bariadi wakipita mbele ya Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Ekwabi Mujungu wakati wa Ufunguzi wa mashindano ya UMITASHUMTA Kimkoa katika shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa wakati wa  ufunguzi wa Mashindano hayo Juni 12, 2019.
Baadhi ya wachezaji kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Itilima wakipita mbele ya Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Ekwabi Mujungu wakati wa Ufunguzi wa mashindano ya UMITASHUMTA Kimkoa katika shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa wakati wa  ufunguzi wa Mashindano hayo Juni 12, 2019.
Baadhi ya Maafisa Elimu na Michezo mkoani Simiyu, wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa Mashindano ya UMITASHUMTA mwaka 2019 ambayo yanayoendelea  katika shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, kutoka kwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Ekwabi Mujungu(hayupo pichani).


WAZIRI MKUU APONGEZA SIMIYU KUJENGA SHULE YA MICHEZO

Waziri Mkuu Jamhuri ya Muungan, Mhe. Kassim Majaliwa(Mb), ameupongeza Mkoa wa Simiyu kwa kuwa mmoja kati ya Mikoa ya mfano katika kutekeleza agizo lake la mwaka jana alilolitoa kupitia michezo hiyo la kuanzishwa kwa shule maalumu za michezo.


Waziri Mkuu ameyasema hayo Juni 10, 2019 wakati wa ufunguzi wa Mashindano ya UMISSETA Kitaifa katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona Mjini Mtwara.

Mkoa wa Simiyu umejenga Shule ya Sekondari itakayokuwa kituo cha kukuza vipaji vya wanafunzi katika michezo. “Naagiza mwakani wanafunzi wote walioonesha vipaji katika michezo watakaofaulu Mtihani wa Elimu ya Msingi wapangwe katika shule hiyo ili wakakuze vipaji vyao.”

                             Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. , Kassim Majaliwa 
Wanamichezo kutoka Mkoa wa Simiyu wakiingia kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona kushiriki katika Ufunguzi wa Michezo ya UMISETA uliofanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Juni 10, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ( wa tatu kulia) akiwa nabaadhi ya wataalam wakiangalia baadhi ya mawe yaliyotolewa katika eneo unapojengwa uwanja wa mpira wa miguu katika Shule ya Sekondari Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka  na baadhi ya wananchi wa Kata ya Malambo  wakishuhudia zoezi la kutoa mawe katika eneo unapojengwa uwanja wa mpira wa miguu katika Shule ya Sekondari Simiyu.


Tuesday, June 4, 2019

SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA KUMBUSHENI VIONGOZI, WATUMISHI KUTIMIZA WAJIBU WAO: RC MTAKA


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu amesema ni vema Sekreatarieti ya Maadili ya viongozi wa Umma iendelee kuwakumbusha viongozi na watumishi wa umma nchini kutimiza wajibu wao ili kuweza kufikia malengo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  na Serikali.

Mtaka ameyasema hayo Juni 03, 2019 Mjini Bariadi, wakati akifungua mafunzo kwa Viongozi wa Umma mkoani Simiyu, ambayo yameandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora.

Amesema ikiwa kila mmoja katika Utumishi wa Umma atatimiza wajibu wake na kwa kuzingatia mgawanyo wa uongozi ulivyo ndani ya nchi; jamii na nchi kwa ujumla wake itaweza kufikia malengo yaliyowekwa na Serikali katika nyanja mbalimbali kwa wakati.

“Ni vizuri Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ikiendelea kuwakumbusha watu wote wanaofanya kazi zinazoihusu jamii kutimiza wajibu wao, kila mmoja akitimiza wajibu wake yapo mambo mengi sana sisi kama jamii, mkoa na kwa namna ambavyo uongozi na mgawanyiko wa .nchi yetu ulivyo tutafikia malengo yetu kwa wakati” alisema Mtaka.

Aidha, ametoa wito kwa viongozi wa Umma ambao ni watoa maamuzi katika maeneo yao ya kazi kuwa makini katika kutoa maamuzi na wahakikishe wanafanya maamuzi kwa wakati.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Msaidizi Sekteratieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, Bw. Gerald Mwaitebele amesema viongozi wa Umma wanapaswa kutoa maamuzi kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo iliyowekwa ili kutoiletea hasara Serikali.

Ameongeza kuwa Sekretarieti ya Maadili kwa Viongozi wa Umma itaendelea kutoa elimu kwa viongozi wa umma juu ya umuhimu wa kuzingatia misingi ya uadilifu katika uongozi na endapo ikitokea kiongozi yeyote atakengengeuka na kutofuata maadili sheria itachukua mkondo wake.

Kwa upande wake Hakimu mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio ameshukuru Sekretarieti ya Maadili kwa kutoa mafunzo ya maadili  kwa viongozi wa Umma na akatoa wito kwa viongozi hao kuwa waadilifu, kutekeleza majukumu yao na kutojilimbikizia mali kinyume na taratibu na maadili ya viongozi wa Umma.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Bahame Kaliwa ametoa wito kwa Sekretarieti ya Maadili kwa viongozi wa Umma kutoa elimu ya maadili kila viongozi wapya wanapoteuliwa au kuchaguliwa, hususani madiwani wanapochaguliwa na kuunda Mabaraza mapya ya madiwani ili wajue misingiya uadilifu inayopaswa kuwaongoza katika kazi zao
MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na Viongozi wa Umma mkoani humo, wakati akifungua mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya Viongozi wa Umma mkoani Simiyu wakifuatilia  mafunzo yaliyoandaliwa kwa ajili yao na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akizungumza na viongozi wa Umma Mkoani humo, wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi
Kaimu Katibu Msaidizi Sekteratieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, Bw. Gerald Mwaitebele, akizungumza na viongozi wa Umma Mkoani Simiyu, wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi hiyo, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
Afisa Maadili kutoka Sekteratieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, Bw. Onesmo Msalangi akizungumza na viongozi wa Umma Mkoani Simiyu, wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi hiyo, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya Viongozi wa Umma mkoani Simiyu wakifuatilia  mafunzo yaliyoandaliwa kwa ajili yao na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.

Hakimu mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio akichangia hoja wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora kwa viongozi wa Umma Mkoani Simiyu, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
Mwenyekitia wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mhe. Robert Lweyo akichangia hoja wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora kwa viongozi wa Umma Mkoani Simiyu, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
Katibu Tawala Msaidizi Seksheni ya Menejimenti ya Serikali za Mitaa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Maganga Simon akichangia hoja wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora kwa viongozi wa Umma Mkoani Simiyu, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
Makamu Mwenyekiti wa Halamashauri ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Bahame Kaliwa akichangia hoja wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora kwa viongozi wa Umma Mkoani Simiyu, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Somanda, Mhe. Said Majaja akichangia hoja wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora kwa viongozi wa Umma Mkoani Simiyu, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
Kaimu Katibu Msaidizi Sekteratieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, Bw. Gerald Mwaitebele, akizungumza na viongozi wa Umma Mkoani Simiyu, wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi hiyo, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa umma mkoani humo, mara baada ya kufungua mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora kwa viongozi hao , ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa umma mkoani humo, mara baada ya kufungua mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora kwa viongozi hao , ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa umma mkoani humo, mara baada ya kufungua mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora kwa viongozi hao , ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya waandishi wa habari mkoani humo( waliosimama, kulia ni Afisa Habari Mkoa) , mara baada ya kufungua mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora kwa viongozi wa Umma , ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!