Waziri Mkuu
Jamhuri ya Muungan, Mhe. Kassim Majaliwa(Mb), ameupongeza Mkoa wa Simiyu kwa
kuwa mmoja kati ya Mikoa ya mfano katika kutekeleza agizo lake la mwaka jana
alilolitoa kupitia michezo hiyo la kuanzishwa kwa shule maalumu za michezo.
Waziri Mkuu
ameyasema hayo Juni 10, 2019 wakati wa ufunguzi wa Mashindano ya UMISSETA
Kitaifa katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona Mjini Mtwara.
Mkoa wa
Simiyu umejenga Shule ya Sekondari itakayokuwa kituo cha kukuza vipaji vya
wanafunzi katika michezo. “Naagiza mwakani wanafunzi wote walioonesha vipaji
katika michezo watakaofaulu Mtihani wa Elimu ya Msingi wapangwe katika shule
hiyo ili wakakuze vipaji vyao.”
Wanamichezo
kutoka Mkoa wa Simiyu wakiingia kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona kushiriki
katika Ufunguzi wa Michezo ya UMISETA uliofanywa na Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa, Juni 10, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka ( wa tatu kulia) akiwa nabaadhi ya wataalam wakiangalia
baadhi ya mawe yaliyotolewa katika eneo unapojengwa uwanja wa mpira wa miguu
katika Shule ya Sekondari Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka na baadhi ya wananchi
wa Kata ya Malambo wakishuhudia zoezi la
kutoa mawe katika eneo unapojengwa uwanja wa mpira wa miguu katika Shule ya
Sekondari Simiyu.
0 comments:
Post a Comment