Monday, June 17, 2019

UJENZI WA TAWI LA IFM SIMIYU UTAMALIZIKA SEPTEMBA 2019: PROFESA SATTA


Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Prof. Tadeo Satta  amewahakikisha wananchi wa Mkoa wa Simiyu na mikoa jirani kuwa ujenzi wa awali wa  tawi la Chuo hicho mkoani Simiyu ,unatarajia kukamilika  mwezi Septemba mwaka huu na kuanza kudahili wanafunzi katika mwaka wa masomo 2019/2020 .

Profesa  Satta ameyasema hayo Juni 17, 2019 wakati wa hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa Tawi la Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Simiyu katika kijiji cha Sapiwi wilaya ya Bariadi.

Profesa  Satta  amesema kujengwa kwa kituo hicho kipya cha mafunzo kutachangia kuongeza udahili na  kubainisha kuwa katika mpango mkakati wa chuo mwaka 2016/2017 hadi mwaka 2020/2021, chuo kimejipanga kuongeza kutoa mafunzo kwa wateja wake hasa katika mikoa ya Dodoma, Mwanza na Simiyu inayotarajiwa kuchukua mikoa ya kanda ya ziwa mpaka Tabora.

Ameongeza kuwa azma ya chuo ni kuanza kudahili wanafunzi katika mwaka wa masomo 2019/2020 kuanzia ngazi ya cheti  na matarajio ni kuhamisha wanafunzi wa ngazi ya cheti na stashahada kutoka Mwanza kuja Simiyu ili Mwanza zibaki kozi za jioni wanazosoma watu wanaotoka kazini.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amempongeza Makamu Mkuu wa Chuo IFM, Prof. Tadeo Satta kwa kuwa mtendaji wa mipango aliyoipanga na kutimiza ahadi ya kuanza kujenga tawi hilo mwaka huu, huku akitoa wito kwa  wananchi wote kuchangamkia  fursa mbalimbali ikiwemo ujenzi wa hosteli, migahawa na nyumba za kupangisha watumishi.

“Tawi la Chuo cha IFM linajengwa Sapiwi watu wote wanaalikwa kuchangamkia fursa na wachangamikiaji wa fursa wa kwanza ni wana Sapiwi wenyewe, tungehitaji kupata hosteli, migahawa ya chakula, maeneo ya watu kunywa vinywaji na tutawaambia TANROADS waone namna ya kuweka “stendi” maana hapa Sapiwi kitakuwa kituo kikubwa” alisisitiza Mtaka.

Aidha, Mtaka amewahakikishia viongozi wa Chuo cha IFM kuwa viongozi wa Mkoa wataendelea kushirikiana nao  katika kuhakikisha azma ya kukamilisha ujenzi kwa wakati ikiwa ni pamoja na kuwezesha mkandarasi kufanya kazi saa 24 kwa kuhakikisha kuna ulinzi  na miundombinu ya umeme inakuwepo katika eneo la ujenzi.

Naye Mayunga Juma Mkazi wa kijiji cha Sapiwi amesema wananchi wa Sapiwi wanashukuru  uwepo wa ujenzi huo kwani umesaidia kutoa ajira na kuwawezesha kupata fedha za kujikimu kimaisha.

Kwa upande wake Msimamizi wa Ujenzi huo kutoka Chuo cha Mafunzo ya Ufundi (VETA) Kagera,   Baluye Mitinje  ameahidi kusimamia na kuhakikisha ujenzi unafanyika usiku na mchana ili ukamilike kwa wakati.

Ujenzi wa awali wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha Tawi la Sapiwi utagharimu kiasi cha shilingi milioni mia tisa na sabini na moja .

MWISHO

 Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM, Prof.Tadeo Satta akitoa maelezo kwa Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kuhusu ramani ya majengo ya Kituo kipya cha chuo hicho kinachojengwa katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi Mkoani Simiyu, wakati wa uzinduzi wa ujenzi huo Juni 17, 2019,
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wananchi wa Sapiwi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ujenzi wa Kituo kipya cha Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFMkinachojengwa Kata ya Sapiwi wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, iliyofanyika Juni 17, 2019 kijijini Sapiwi.
Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM, Prof. Prof.Tadeo Satta akizungumza na wananchi wa Sapiwi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ujenzi wa Kituo kipya cha Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kinachojengwa Kata ya Sapiwi wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, iliyofanyika Juni 17, 2019 kijijini Sapiwi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) akifurahia jambo na Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM, Prof. Tadeo Satta wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ujenzi wa Kituo kipya cha Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kinachojengwa Kata ya Sapiwi wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, iliyofanyika Juni 17, 2019 kijijini Sapiwi.
Mkuu wa Mkoa wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga  akizungumza na wananchi wa Sapiwi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ujenzi wa Kituo kipya cha Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kinachojengwa Kata ya Sapiwi wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, iliyofanyika Juni 17, 2019 kijijini Sapiwi/
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Sapiwi Wilayani Bariadi wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika hafla ya uzinduzi wa  Ujenzi wa Kituo kipya cha Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kinachojengwa Kata ya Sapiwi wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, iliyofanyika Juni 17, 2019 kijijini Sapiwi.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari  Sapiwi Wilayani Bariadi wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika hafla ya uzinduzi wa  Ujenzi wa Kituo kipya cha Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kinachojengwa Kata ya Sapiwi wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, iliyofanyika Juni 17, 2019 kijijini
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi wakishuhudia zoezi la uchimbaji msingi wa baadhi ya majengo ya Kituo kipya cha Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM kinachojengwa Kata ya Sapiwi wialayni bariadi mkoani Simiyu, wakati wa uzinduzi wa ujenzi huo  Juni 17, 2019.
Kikundi cha sanaa kikitoa burudani katika hafla ya uzinduzi wa  Ujenzi wa Kituo kipya cha Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kinachojengwa Kata ya Sapiwi wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, iliyofanyika Juni 17, 2019 kijijini Sapiwi.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe. Festo Kiswaga ( mwenye suti ya kahawia) akicheza na baadhi ya wananchi wa kata ya  Sapiwi kufurahia ujenzi wa kituo kipya cha Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) , katika hafla ya uzinduzi wa  Ujenzi wa Kituo hicho kinachojengwa Kata ya Sapiwi wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, iliyofanyika Juni 17, 2019 kijijini Sapiwi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Bariadi, Mhe.Richard Buyamba akizungumza na wananchi wa Sapiwi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ujenzi wa Kituo kipya cha Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kinachojengwa Kata ya Sapiwi wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, iliyofanyika Juni 17, 2019 kijijini Sapiwi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka( wa nne kushoto) akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Ujenzi wa Ujenzi wa Kituo kipya cha Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kinachojengwa Kata ya Sapiwi wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, iliyofanyika Juni 17, 2019 kijijini Sapiwi.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Donatus Weginah akitambulisha baadhi ya viongozi  wa Mkoa huo,  wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ujenzi wa Kituo kipya cha Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kinachojengwa Kata ya Sapiwi wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, iliyofanyika Juni 17, 2019 kijijini Sapiwi.
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Sapiwi wakiangalia ramani ya majengo ya Kituo kipya cha Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kinachojengwa katika Kata ya Sapiwi wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, mara baada ya hafla ya uzinduzi wa ujenzi huo iliyofanyika Juni 17, 2019 kijijini Sapiwi.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akiwaonesha baadhi ya wananchi wa kata ya Sapiwi ramani ya majengo ya Kituo kipya cha Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kinachojengwa katika Kata ya Sapiwi wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, mara baada ya hafla ya uzinduzi wa ujenzi huo iliyofanyika Juni 17, 2019 kijijini Sapiwi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka( wa tatu kushoto) akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Ujenzi wa Ujenzi wa Kituo kipya cha Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kinachojengwa Kata ya Sapiwi wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, iliyofanyika Juni 17, 2019 kijijini Sapiwi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka( wa tano kushoto) na baadhi ya viongozi wengine wakizungumza jambo  mara baada ya kukagua eneo unapochimbwa msingi wa majengo ya Kituo kipya cha Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kinachojengwa katika Kata ya Sapiwi wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, wakati wa hafla ya uzinduzi wa ujenzi huo iliyofanyika Juni 17, 2019 kijijini Sapiwi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu na Chuo cha usimamizi wa fedha(IFM), mara baada ya hafla ya uzinduzi wa ujenzi  wa Kituo kipya cha Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kinachojengwa katika Kata ya Sapiwi wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, wakati wa hafla ya uzinduzi wa ujenzi huo iliyofanyika Juni 17, 2019kijini Sapiwi.
Baadhi ya wananchi na viongozi wakishuhudia zoezi la kuchimba msingi wa baadhi ya majengo ya Kituo kipya cha Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM kinachojengwa Kata ya Sapiwi wialayni bariadi mkoani Simiyu, wakati wa uzinduzi wa ujenzi huo  Juni 17, 2019.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!