Sunday, September 13, 2020

WADAU WA KILIMO SIMIYU WAJADILI MWONGOZO WA KILIMO CHA MKONGE

 Bodi ya Mkonge Tanzania imekutana na uongozi wa mkoa wa Simiyu na baadhi ya watendaji na wataalam wa kilimo kwa lengo la kujadili mwongozo wa kilimo cha mkonge mkoani hapa lengo likiwa ni kuhakikisha mkulima anazalisha mkonge bora na wenye thamani katika soko.

Akikabidhi muongozo huo kwa katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga na baadaye akawakabidhi maafisa Kilimo, Mratibu mkuu wa utafiti na masoko, Bw Hassan Kibarua amesema ni vema wataalam wa kilimo wakatoa elimu kwa wakulima wa mkonge juu ya kuzingatia ubora kuanzia uzalishaji ili usipungue thamani.

"Mkonge unatakiwa kuchakatwa si zaidi ya masaa 48 tangu kukatwa lakini kuna wakati mkulima anachakata mkonge uliokatwa zaidi ya siku tano, unakuwa umepungua ubora na unapofika sokoni unakuwa haupo kwenye daraja la ubora wa 3L ambalo lina bei ya juu, " alisema Kibarua.


RUWASA SIMIYU YAAHIDI KUONGEZA HALI YA UPATIKANAJI WA MAJI

Upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama Mkoani Simiyu unatarajiwa kuongezeka kutoka asilimia 51 ya mwaka 2019 hadi 57.4 ifikapo 0ktoba 2020 kupitia mradi wa lipa kulingana na matokeo (P4R ) hali itakayosaidia wananchi kuepukana na adha ya upatikanaji wa huduma hiyo kwa uhakika na urahisi. 

Hayo yamesemwa Septemba 11, 2020 na meneja wa wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) mhandisi Mariam Majala wakati wa makabidhiano ya mabomba yatakayotumika kutekeleza miradi ya maji Mkoani Simiyu yaliyofanyika katika ofisi za RUWASA mjini Bariadi.

“Tayari tumepokea mabomba asilimia 70 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo ambayo yana thamni ya zaidi ya shilingi milioni 800, tunaishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa mradi wa P4R na tunaamini tutakapokuwa tumelaza mabomba haya kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hii na tutakuwa tumeongeza maji kwa asilimia 6.4, kutoka asilimia 51 hadi 57.4,” alisema Mhandisi Manjala. 

Naye  Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga amewapongeza watendaji wa RUWASA Mkoa wa Simiyu kwa namna wanavyotekeleza miradi kwa kasi huku akibainisha kuwa mradi wa P4R utatoa ajira kupitia utandazaji wa mabomba hivyo akatoa wito kwa Wana Simiyu kuchangamkia fursa hiyo ya ajira pamoja

Aidha, Mmbaga ametoa wito kwa wananchi kutunza miundombinu hiyo ya maji itakayotandazwa katika maeneo hayo kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa P4R ili kuweza kuusaidia mkoa kufikia azma ya kuongeza hali ya upatikanaji wa maji.

Naye Mjumbe wa Bodi ya Zabuni ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu iliyotumika kuandaa mchakato wa manunuzi wa mabomba hayo, Bw. Ekwabi Mujungu amesema anawapongeza RUWASA kwa kununua mabomba kulinga na sifa zilizoandishwa na kupitishwa na bodi hiyo huku akisisitiza miradi kwenda kutekelezwa kwa kiwango bora ili thamani ya fedha.

MWISHO

Meneja wa Mamlaka ya Maji Vijijini na Usafi wa Mazingira (RUWASA), Mhandisi Mariam Manjala akionesha mabomba yanayotarajiwa kusambazwa katika wilaya zote kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa lipa kulingana na matokeo(P4R)  wakati wa makabidhiano ya mabomba hayo Septemba 11, 2020 Mjini Bariadi, kulia ni Katibu Tawala  wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga.

Katibu Tawala  wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga akizungumza wakati wa makabidhiano ya mabomba yanayotarajiwa kusambazwa katika wilaya zote kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa lipa kulingana na matokeo(P4R)  wakati wa makabidhiano ya mabomba hayo Septemba 11, 2020 Mjini Bariadi, kushoto Meneja wa Mamlaka ya Maji Vijijini na Usafi wa Mazingira (RUWASA), Mhandisi Mariam Manjala.
Sehemu ya mabomba yanayotarajiwa kusambazwa katika wilaya zote kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa lipa kulingana na matokeo(P4R)  mkoani Simiyu.

 

Mjumbe wa Bodi ya Zabuni ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu iliyotumika kuandaa mchakato wa manunuzi wa mabomba hayo, Bw. Ekwabi Mujungu akizungumza wakati wa makabidhiano ya mabomba yanayotarajiwa kusambazwa katika wilaya zote kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa lipa kulingana na matokeo(P4R)  wakati wa makabidhiano ya mabomba hayo Septemba 11, 2020.

Katibu Tawala  wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga akizungumza wakati wa makabidhiano ya mabomba yanayotarajiwa kusambazwa katika wilaya zote kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa lipa kulingana na matokeo(P4R)  wakati wa makabidhiano ya mabomba hayo Septemba 11, 2020 Mjini Bariadi, kushoto Meneja wa Mamlaka ya Maji Vijijini na Usafi wa Mazingira (RUWASA), Mhandisi Mariam Manjala

 Katibu Tawala  wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga akizungumza wakati wa makabidhiano ya mabomba yanayotarajiwa kusambazwa katika wilaya zote kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa lipa kulingana na matokeo(P4R)  wakati wa makabidhiano ya mabomba hayo Septemba 11, 2020 Mjini Bariadi, wa pili kushoto Meneja wa Mamlaka ya Maji Vijijini na Usafi wa Mazingira (RUWASA), Mhandisi Mariam Manjala                 

 


Friday, September 11, 2020

KITUO CHA AFYA LUKUNGU CHATAKIWA KUIMARISHA MFUMO WA UKUSANYAJI, USIMAMIZI WA MAPATO

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Khamis Kulemba ameutaka uongozi wa Kituo cha Afya Lukungu wilayani Busega kuimarisha ukusanyaji na usimamizi wa mapato (kudhibiti upotevu wa mapato) ili kuongeza mapato yatakayosaidia kununua dawa na kuboresha miundombinu kwa lengo la kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

Dkt. Kulemba ameyasema hayo Septemba 10, 2020 katika nyakati tofauti wakati wa ziara ya usimamizi shirikishi iliyofanyika katika kituo hicho, ambapo moja ya malengo ya ziara ilikuwa ni kukagua mifumo ya ukusanyaji wa mapato na hali ya utoaji wa huduma za afya kwa ujumla wake.

“Imarisheni mfumo wa ukusanayaji mapato nataka wakati ujao mapato yaongezeke mara mbili ya sasa, mkumbuke kuwa kwa kadri tunavyodhibiti upotevu wa mapato ndiyo tutakavyoboresha utoaji wa huduma; tutaweza kununua dawa na kufanya maendeleo ya kituo chetu hali itakayochangia kuongeza ufanisi katika huduma zinazotolewa kwa wananchi,” alisema Kulemba.

Ameongeza kuwa Uongozi wa Kituo hicho unapaswa kuhakikisha kuwa mfumo wa GoT-HOMIS unaohusika na usimamizi na uendeshaji wa vituo vya kutolea huduma za afya unafungwa na kufanya kazi kituoni hapo, ili kudhibiti aina yoyote ya upotevu wa mapato kwa kuwa taarifa ya kila huduma na mapato zitaingizwa katika mfumo huo.

Naye Afisa Afya kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu amesema pamoja na kuimarisha mfumo wa mapato uongozi huo uboreshe mazingira kwa kusafisha mara kwa mara maeneo ya kituo hicho pamoja na kupanda bustani za maua.

Akizungumza kwa niaba ya watumishi wa idara ya afya wilaya ya Busega, Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya amesema watatekeleza maelekezo yote yaliyotolewa na mganga mkuu wa mkoa ili kutimiza azma ya serikali ya kutoa huduma zinazotakiwa kwa wananchi na kwa wakati.

Baadhi ya wananchi waliopata huduma za matibabu katika kituo cha afya Lukungu wameupongeza uongozi wa kituo kwa namna ulivyoboresha utoaji wa huduma na kuomba hali ya upatikanaji wa dawa iimarishwe zaidi na miundombinu ya kutoa huduma ikiwemo huduma za upasuaji, wodi za kulaza wagonjwa ziongezwe  ili wapate huduma zote kituoni hapo.

“ Kwa upande wa huduma mimi nimehudumiwa vizuri, nimepokelewa vizuri na wauguzi wamenisikiliza baada ya kunisikiliza nimeenda kwenye vipimo na nilivyorudi kwa daktari amenieleza tatizo langu akaniandikia dawa,  nashukuru dawa zote nilizoandikiwa nimepewa,” Mandege William Manyama, mkazi wa Kijiji cha Lukungu.

“Huduma zote nilizokuwa nazihitahitaji nimezipata na nimehudumiwa ndani ya muda mfupi, ombi langu serikali ione namna ya kuongeza huduma hasa za kulaza wagonjwa ili tuipate hapa hapa badala ya kupelekwa kwenye vituo vingine na hospitali,” alisema Daud Moshi mkazi wa Kijiji cha Lukungu.

MWISHO


Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Khamis Kulemba(katikati) akitoa maelekezo kwa  baadhi ya watoa huduma za afya katika kituo cha Afya Lukungu wilayani Busega wakati akiwa katika ziara ya usimamizi shirikishi katika kituo hicho Septemba 10,  2020.

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Khamis Kulemba(kulia) akifanya ukaguzi katika wodi ya wazazi katika kituo cha Afya Lukungu wilayani Busega wakati akiwa katika ziara ya usimamizi shirikishi katika kituo hicho Septemba 10,  2020.

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Khamis Kulemba akitoa maelekezo kwa  baadhi ya watoa huduma za afya katika kituo cha Afya Lukungu wilayani Busega wakati akiwa katika ziara ya usimamizi shirikishi katika kituo hicho Septemba 10,  2020.

Mfamasia wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega akichangia jambo katika kikao kati ya Timu ya Usimamizi wa Huduma za Afya ya Mkoa wa Simiyu na Wilaya ya Busega pamoja na watumshi wa Kituo cha Afya Lukungu wakati wa ziara ya usimamizi shirikishi katika kituo hicho Septemba 10, 2020.

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Khamis Kulemba(katikati) akitoa maelekezo kwa  baadhi ya watoa huduma za afya katika kituo cha Afya Lukungu wilayani Busega wakati akiwa katika ziara ya usimamizi shirikishi katika kituo hicho Septemba 10,  2020.

Baadhi ya wananchi wakisubiri huduma katika kituo cha Afya Lukungu wilayani Busega.

Jengo la huduma za wagonjwa wa nje katika Kituo cha Afya cha Lukungu wilayani Busega

Baadhi ya watoa huduma za afya katika kituo cha afya cha Lukungu wakimsikiliza Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Khamis Kulemba(hayupo pichani) wakati akitoa maelekezo kwa  watoa huduma hao wakati akiwa katika ziara ya usimamizi shirikishi katika kituo hicho Septemba 10,  2020.

Afisa Afya katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu  akichangia jambo katika kikao kati ya Timu ya Usimamizi wa Huduma za Afya ya Mkoa wa Simiyu na Wilaya ya Busega pamoja na watumshi wa Kituo cha Afya Lukungu wakati wa ziara ya usimamizi shirikishi katika kituo hicho Septemba 10, 2020.

Afisa Afya katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu  akichangia jambo katika kikao kati ya Timu ya Usimamizi wa Huduma za Afya ya Mkoa wa Simiyu na Wilaya ya Busega pamoja na watumshi wa Kituo cha Afya Lukungu wakati wa ziara ya usimamizi shirikishi katika kituo hicho Septemba 10, 2020.

Moja ya majengo ya kutolea huduma katika kituo cha Afya Lukungu wilayani Busega.

Wodi ya wazazi katika kituo cha Afya Lukungu wilayani Busega.



Baadhi ya Maafisa wa Idara ya Afya mkoa wa Simiyu na Wilayani ya Busega na watoa huduma za afya katika kituo cha afya cha Lukungu wakimsikiliza Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Khamis Kulemba(hayupo pichani) wakati akitoa maelekezo kwa  watoa huduma hao wakati akiwa katika ziara ya usimamizi shirikishi katika kituo hicho Septemba 10,  2020.


Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Khamis Kulemba na Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Busega wakifuatilia kikao cha Idara ya Afya mkoa wa Simiyu na Wilayani ya Busega na watoa huduma za afya katika kituo cha afya cha Lukungu kilichofanyika wakati wa ziara ya usimamizi shirikishi katika kituo hicho Septemba 10,  2020.

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Khamis Kulemba(kulia) akitoa maelekezo kwa  baadhi ya watoa huduma za afya katika kituo cha Afya Lukungu wilayani Busega wakati akiwa katika ziara ya usimamizi shirikishi katika kituo hicho Septemba 10,  2020.

Wednesday, September 9, 2020

RAS SIMIYU ATAKA MAJENGO YA UPASUAJI, WODI YA WAZAZI HOSPITALI YA WILAYA BUSEGA YAKAMILISHWE

     Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Bw. Anderson Njiginya kutoa fedha kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa majengo ya upasuaji na wodi ya wazazi katika Hospitali ya Wilaya ili kuboresha hali ya utoaji wa huduma kwa wananchi katika hospitali hiyo. 

Mmbaga ametoa agizo hilo Septemba 09, 2020 wakati zoezi la usimamizi shirikishi alipotembelea hospitali hiyo kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo hayo ambayo yanapaswa kukamilika na kuanza kutoa huduma ifikapo Septemba 30, 2020.

“Nampongeza Mkurugenzi kwa kujiongeza, badala ya kusubiri kibali kutoka HAZINA kulipa fedha za kukamilisha ujenzi wa majengo haya, amejiwekea utaratibu wa kuwalipa mafundi wetu, nimeelekeza kuwa aongeze kiwango anachotoa kwa kila juma ili kuongeza kasi ya ujenzi na hatimaye majengo haya yaweze kukamilika na kutumika kwa huduma kusudiwa,” alisema Mmbaga.

Aidha, Mmbaga ameongeza kuwa ukamilishaji wa majengo hayo uende sambamba na utunzaji wa mazingira ambao utajumuisha upandaji miti, bustani za maua na utunzaji wa miti asili huku akitoa pongezi kwa Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri hya Wilaya ya Busega kwa usimamizi mzuri katika ujenzi wa hospitali hiyo na kumuagiza Mkurugenzi kumthibitisha katika cheo chake.

Wakati huo huo Mmbaga ameelekeza Timu ya usimamizi wa afya ngazi ya wilaya (CHMT) kuimarisha usimamizi katika mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) uliboreshwa hususani watoa huduma ngazi ya jamii wanaohusika katika usajili ili wananchi waweze kupata huduma zilizokusudiwa  na serikali.

Katika hatua nyingine Mmbaga ametembelea kikundi kinachojihusisha kilimo cha umwagiliagi kilichopo kijiji cha Chamgasa na kuelekeza wataalam wa fedha na uchumi waweze kutoa elimu kwa wakulima hao juu ya utunzaji na matumizi ya fedha ili wanapopewa mikopo na wadau waweze kutekeleza miradi ambayo itakuwa endelevu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Bw. Anderson Njiginya amesema atahakikisha fedha zinatolewa kwa wakati kwa mafundi wanaoendelea na ujenzi wa majengo ya Upasuaji na wodi ya wazazi katika hospitali ya wilaya ili shughuli za ujenzi zisikwame.

Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Khamis Kulemba ameipongeza Timu ya usimamizi wa afya ngazi ya wilaya (CHMT) kwa namna inavyotekeleza majukumu yake huku akisisitiza watumishi wote wa afya kuendelea kutoa huduma stahiki  kwa wananchi.

Nao baadhi ya watumishi wa afya katika kituo cha afya Lukungu wameomba miundombinu katika vituo vya kutolea huduma za afya iboreshwe ili kutoa huduma kulingana na hadhi za vituo hivyo na wananchi wapate huduma wanazotarajia kuzipata katika vituo husika.

MWISHO.

Katibu tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga akizungumza na baadhi wajumbe wa Timu ya usimamizi wa masuala ya afya mkoa wa Simiyu na wilaya ya Busega wakati wa ziara ya Katibu Tawala wa Mkoa iliyolenga kufanya usimamizi shirikishi katika hospitali hiyo kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo hayo ambayo yanapaswa kukamilika na kuanza kutoa huduma ifikapo Septemba 30, 2020.
Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega akitoa maelezo kwa Katibu tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga katika jengo la mionzi la Hospitali ya Wilaya hiyo wakati wa ziara ya Katibu Tawala wa Mkoa iliyolenga kufanya usimamizi shirikishi katika hospitali hiyo kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo hayo ambayo yanapaswa kukamilika na kuanza kutoa huduma ifikapo Septemba 30, 2020.

TAFADHALI TAZAMA PICHA MBALIMBALI KATIBU TAWALA WA MKOA AKIWA KATIKA USIMAMIZI SHIRIKISHI, ALIPOKUTANA NA WATUMISHI IDARA YA AFYA, KIKUNDI CHA UMWAGILIAJI CHAMGASA NA PICHA ZA BAADHI YA MAJENGO YA HOSPITALI YA WILAYA YA BUSEGA



















Thursday, September 3, 2020

RAS SIMIYU AWATAKA WAAJIRI SEKTA BINAFSI KUWASILISHA MADENI YA MICHANGO YA WAAJIRIWA NSSF

 Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga leo amefanya kikao na  Uongozi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF na baadhi ya waajiri wa sekta binafsi mkoani Simiyu kwa lengo la kujadili ulipaji wa madeni ya michango ya waajiriwa NSSF, ambapo katika kikao hicho imeazimiwa kuwa waajiri wote wa sekta binafsi wanaodaiwa wahakikishe wanalipa madeni hayo kwa wakati. 

Akizungumza na waajiri wa sekta binafsi katika kikao hicho Bi Mmbaga amesema suala malipo ya michango ya mfuko wa hifadhi ya jamii ni suala la kisheria na lina manufaa kwa pande zote mbili (waajiri na waajiriwa), hivyo ni vema  NSSF iendelee  kutoa elimu ili kila upande ujue na utimize wajibu wake. 

“Jambo hili lipo kisheria na lina faida kwa pande zote mbili mwajiri na mwajiriwa, kwa mwajiri kwamba hatasumbuliwa kwamba amekiuka sheria lakini mwajiriwa akiwa mwajiri  anayelipiwa michango yake ya pensheni  atatambua kuwa mwajiri wake anajali maslahi yake,”alisema Mmbaga. 

Aidha, Mmbaga amesema azimio jingine la kikao hicho ni  Mfuko wa hifadhi ya jamii NSSF Mkoa wa Simiyu kuhakikisha kuwa unatoa vitambulisho vya waajiriwa ambao waajiri wao wametimiza masharti ya kuanza kuwalipia michango ya mfuko wa hifadhi ya jamii mpaka kufikia Septemba 10, 2020 . 

Wakati huo huo Mmbaga amesema Mkoa utaendelea kufanya vikao  na wadau angalau mara tatu  kwa mwaka kwa lengo la kuelimieshana na kujadiliana masuala mbalimbali ikiwemo namna sahihi ya utatuzi wa changamoto mbalimbali ili waweze wadau waweze kufanya kazi zao kwa tija na kuendana na dira ya mkoa yenye lengo la kuwa mkoa shindani kiuchumi.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF, Bw. Nuru Mmbaga amesema  ni wajibu wa kila mwajiri katika sekta binafsi kulipa michango ya mfuko wa hifadhi ya jamii kwa kutoa asilimia 10 ya mshahara ghafi wa mwajiriwa nay eye mwajiri kulipia asilimia 10 pia kwa mujibu wa sheria.

Naye Mwanasheria wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Mwanahamisi Kawega amesisitiza umuhimu wa waajiri kulipa madeni ya michango ya waajiriwa wao kwa mfuko wa hifadhi ya jamii NSSF ili waajiri wao waweze kupata haki na stahili zao mathalani mafao ya uzazi.

Kwa upande wao waajiri wa sekta binafsi walioshiriki katika kikao hicho wameshukuru uongozi wa Mkoa kuitisha kikao hicho ambapo wamekiri kuwa wako tayari kulipa madeni yote halali ya michango ya waajiriwa wao huku wakisisitiza elimu iendelee kutolewa kwa waajiri na waajiriwa ili wawe na uelewa wa pamoja kuhusu haki na wajibu wao katika masuala ya hifadhi ya jamii.

“Tunashukuru kwa kikao kizuri ambacho umekuwa na mjadala mzuri, sisi tuko tayari kulima madeni hayoa lakini kinachotakiwa ni NSSF kutusaidia kutoa namba za utambulisho maana watumishi wetu wengi  walikataa fedha zao kukatwa kutokana na kutokuwa na namba, tunaombba namba zitolewe kwa wakati,” alisema Bi.Tina Chenge Mkurugenzi wa Madina Bakery Company.

“Tunaomba elimu kwetu na kwa watu wetu iendelee kutolewa maana tunafanya kazi tofauti na tunaajiri watu kwa namna tofauti mfano katika viwanda kuna waajiriwa tunakuwa nao kwa miezi miwili au mitatu, nashauri tukae chini tuangale madeni yote halali tulipe na NSSF itoe kadi za utambulisho kwa waajiriwa wetu ambao tuanze kuwalipia michango yao mara moja,” alisema Gungu Silanga Mkurugenzi kampuni ya Nsagali.

MWISHO

 

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga akizungumza na  baadhi ya waajiri wa sekta binafsi mkoani Simiyu katika kikao maalum kilichofanyika Septemba 03, 2020 kwa lengo la kujadili ulipaji wa madeni ya michango ya waajiriwa katika Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF.

Kaimu Meneja wa  Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF Mkoa wa Simiyu, Bw. Nuru Mmbaga akiwasilisha mada katika kikao kati ya Katibu Tawala wa mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga na  baadhi ya waajiri wa sekta binafsi mkoani Simiyu katika kikao maalum kilichofanyika Septemba 03, 2020 kwa lengo la kujadili ulipaji wa madeni ya michango ya waajriwa katika Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF.

Mwanasheria wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Mwanahamisi Kawega akitoa ufafanuzi wa kisheria wa masuala mbalimbali katika katika kikao kati ya Katibu Tawala wa mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga na  baadhi ya waajiri wa sekta binafsi mkoani Simiyu katika kikao maalum kilichofanyika Septemba 03, 2020 kwa lengo la kujadili ulipaji wa madeni ya michango ya waajriwa katika Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga(kulia) akiteta jambo na Mwanasheria wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Mwanahamisi Kawega katika kikao kati yake na  baadhi ya waajiri wa sekta binafsi mkoani Simiyu katika kikao maalum kilichofanyika Septemba 03, 2020 kwa lengo la kujadili ulipaji wa madeni ya michango ya waajriwa katika Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF.

Bi. Tina Chenge mmoja wa waajiri wa sekta binafsi akichangia hoja katika kikao kati ya Katibu Tawala wa mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga na  baadhi ya waajiri wa sekta binafsi mkoani Simiyu katika kikao maalum kilichofanyika Septemba 03, 2020 kwa lengo la kujadili ulipaji wa madeni ya michango ya waajriwa katika Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF.

Bw. Gungu Silanga  mmoja wa waajiri wa sekta binafsi akichangia hoja katika kikao kati ya Katibu Tawala wa mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga na  baadhi ya waajiri wa sekta binafsi mkoani Simiyu katika kikao maalum kilichofanyika Septemba 03, 2020 kwa lengo la kujadili ulipaji wa madeni ya michango ya waajriwa katika Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF.

Kaimu Meneja wa  Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF Mkoa wa Simiyu, Bw. Nuru Mmbaga akiwasilisha mada katika kikao kati ya Katibu Tawala wa mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga na  baadhi ya waajiri wa sekta binafsi mkoani Simiyu katika kikao maalum kilichofanyika Septemba 03, 2020 kwa lengo la kujadili ulipaji wa madeni ya michango ya waajriwa katika Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF.

Kaimu Meneja wa  Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF Mkoa wa Simiyu, Bw. Nuru Mmbaga akiwasilisha mada katika kikao kati ya Katibu Tawala wa mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga na  baadhi ya waajiri wa sekta binafsi mkoani Simiyu katika kikao maalum kilichofanyika Septemba 03, 2020 kwa lengo la kujadili ulipaji wa madeni ya michango ya waajriwa katika Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF.


Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!