Friday, February 22, 2019

WADAU WAIOMBA EWURA KUWASAIDIA WANANCHI WANAOTUMIA CHUPA ZA MAJI KUSAFIRISHA MAFUTA

Wadau wa Nishati na Maji  mkoani Simiyu wameiomba Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kuangalia namna ya kuwasaidia wananchi wanaotumia   chupa za maji kusafirisha  mafuta vijijini na badala yake watafute njia mbadala ili kuepusha majanga ya moto na uchakachuaji wa nishati hiyo.


Wadau hao wametoa ushauri huo katika mkutano baina ya watendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) uliolenga  kuelimisha wadau Mkoani Simiyu kuhusu majukumu ya Mamlaka hiyo, uliofanyika Mjini Bariadi Februari 21, 2019.

Wakizungumza katika mkutano huo wamesema kutokuwepo vyombo maalum vya  ubebaji wa mafuta ya taa , petroli na diseli ni Moja ya tatizo kubwa, hivyo ni vema  (EWURA) ikaja na njia mbadala ya kuwawezesha wananchi kusafirisha kwa usalama nishati hiyo.

“Tunaomba EWURA isaidie kuja na namna bora, vifaa vidogo vitakavyouzwa kwa bei rahisi ili wananchi waweze kusafirisha na kuhifadhi kwa urahisi kwa sababu yanawasaidia sana” amesema Mkaguzi wa Jeshi la Zimamoto Wilaya ya Bariadi, Maulo Kigahe.

Katika hatua nyingine wadau hao wamezungumzia suala la urasimu katika kuunganishwa kwa umeme kwa wananchi katika baadhi ya ofisi za Mameneja wa TANESCO  na kuomba EWURA ione namna ya kuwasaidia wananchi wasaidiwe kupata huduma kwa wakati.

“ Kuna wananchi wakitaka  kuunganishiwa umeme majumbani kwao wanadaiwa pesa mara shilingi laki tano, mara milioni moja hivi EWURA wanayajua matatizo haya? Tukizingatia kuwa umeme ni moja ya huduma muhimu kwa mwananchi tubadilike maana hata kule vijijini tulikozaliwa tunahitaji umeme” alisema Mkuu wa  Gereza Wilaya ya Bariadi, Kajungu Massami.

Naye Saibogi Mwandu mwananchi kutoka Bariadi amesema ni vema wafanyabiashara wadogo hususani wanaouza mafuta ya petroli kwenye chupa wakapewa elimu ya namna ya kutunza mafuta hayo kwani wengi wao wamekuwa wakitunza bidhaa hiyo ndani.

Kwa upande wake Afisa Mkuu wa Mawasiliano (EWURA) makao makuu Wilfred Mwakalosi amesema EWURA katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita imeshabuni mwongozo utakaosaidia wawekezaji wa vijijini kuwekeza kwenye vituo vya gharama nafuu.

Akifunga mkutano huo Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe Festo Kiswaga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amewataka wadau wote kuwa mabalozi wazuri wa EWURA ili wasaidie kufikisha elimu waliyoipata katika maeneo yao.

Awali akifungua mkutano huo, Kiswaga amesema Mkoa wa Simiyu umejipanga katika utekelezaji wa Sera ya Viwanda kwa kujenga viwanda ikiwemo kiwanda cha vifaa tiba, kiwanda cha chaki na vingine ambavyo vitahitaji huduma za nishati na maji , hivyo ameiomba EWURA kushirikiana na Taasisi zinazohusika na utoaji wa huduma hizo katika kuhakikisha zinatolewa katika viwango vinavyokidhi mahitaji ili Mkoa uweze kufikia malengo yake katika uzalishaji katika viwanda.
MWISHO.




Baadhi ya viongozi na wadau wakiwa katika Mkutano wa kuelimisha wadau Mkoani Simiyu kuhusu majukumu ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), uliofanyika Mjini Bariadi Februari 21, 2019.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akifungua Mkutano wa kuelimisha wadau Mkoani Simiyu kuhusu majukumu ya Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka, uliofanyika Mjini Bariadi Februari 21, 2019
Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) wa Kanda ya Ziwa Mhandisi. Loden Kitumbika akiwasilisha mada katika Mkutano wa kuelimisha wadau Mkoani Simiyu kuhusu majukumu ya Mamlaka hiyo, uliofanyika Mjini Bariadi Februari 21, 2019.
Afisa Mawasiliano Mkuu kutoka  Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA), Bw. Wilfred Mwakalosi akiwasilisha mada katika Mkutano wa kuelimisha wadau Mkoani Simiyu kuhusu majukumu ya Mamlaka hiyo, uliofanyika Mjini Bariadi Februari 21, 2019.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga(kulia) na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Ekwabi Mujungu wakifuatilia kwa makini mada zikiwasilishwa katika Mkutano wa kuelimisha wadau kuhusu majukumu ya Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) Mkoani Simiyu, uliofanyika Mjini Bariadi Februari 21, 2019.
Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) wa Kanda ya Ziwa Mhandisi. Loden Kitumbika akitoa utangulizi wa lengo la Mkutano wa kuelimisha wadau kuhusu majukumu ya Mamlaka hiyo Mkoani Simiyu, uliofanyika Mjini Bariadi Februari 21, 2019.
Baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu, wakiwa katika Mkutano wa kuelimisha wadau Mkoani Simiyu kuhusu majukumu ya Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA), uliofanyika Mjini Bariadi Februari 21, 2019.
Baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu na wadau, wakiwa katika Mkutano wa kuelimisha wadau Mkoani Simiyu kuhusu majukumu ya Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA), uliofanyika Mjini Bariadi Februari 21, 2019.

Wednesday, February 20, 2019

OMBI LA WANANCHI SIMIYU LA ENEO LA MALISHO LAPOKELEWA NA SERIKALI, LAAHIDIWA KUFIKISHWA KWA RAIS MAGUFULI

Mwenyekiti wa Timu  maalum ya mawaziri wanane ya kupitia maeneo yenye migogoro  kati ya  wananchi na maeneo ya Hifadhi, Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo na Makazi Mhe. Wiliam Lukuvi amepokea ombi la wananchi  wa wilaya tatu za mkoa wa Simiyu wanaoishi katika vijiji vinavyopakana na Pori la Akiba la Maswa  la kupewa eneo lenye urefu wa kilometa kumi, kwa ajili ya malisho na kuahidi kulifikisha kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa hatua zaidi.


Mhe. Lukuvi ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Vijiji vinavyopakana na pori la akiba la Maswa  katika mkutano wa hadhara  uliofanyika Mji mdogo wa Mwandoya wilayani Meatu.
Awali akijibu baadhi ya kero zilizowasilishwa na Mwananchi wa Wilaya ya Meatu, Bw. Deusdedith Martin  Waziri Lukuvi amesema timu hiyo imezisikia kero hizo na akaahidi kuwasilisha taarifa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na kubainisha kuwa taarifa rasmi ya majibu ya kero zao itatolewa.

Aidha, Waziri  Lukuvi amewahakikishia wananchi kuwa zoezi la kupima eneo la mita 500 kutoka kwenye mpaka wa Pori la Akiba la Maswa kuelekea kwenye vijiji vinavyopakana na Pori hilo (Buffer zone)  katika Wilaya za Meatu, Itilima na Maswa limesimamishwa mpaka litakapotolewa maelekezo.

“Hapa kulikuwa na zoezi la kupima mita 500 kutoka kwenye mpaka wa Pori la Akiba la Maswa kuingia kwa wananchi, maana yake ni kwamba kuna wananchi wengi na vijiji vingi vingeathirika ili vipishe ‘buffer zone’, ingawa ni kwa mujibu wa sheria lakini ‘buffer zone’ ile ingekula maeneo ya vijiji kwa hiyo zoezi hilo limesimamishwa”

“Zoezi hili limesimamishwa kwa mujibu wa maelekezo ya Mhe Rais baada ya kuona watu wengi maskini ambao walipaswa kupisha maeneo ya hifadhi;...... vile vile kuanzia sasa zoezi lolote la kutambua mipaka litakalofanywa na watu wa Maliasili ni lazima liwe shirikishi” alisema Waziri Lukuvi.

Awali akiwasilisha taarifa kwa niaba ya wananchi wa Wilaya ya Meatu, Bw. Deusdedit Martin aliomba Timu ya Mawaziri wanane kuwasaidia katika kutatua changamoto ya ubadilishaji wa mpaka kati ya Pori la Akiba la Maswa na Vijiji vinavyopakana, Uvamizi wa tembo katika mashamba na makazi ya watu na kukatazwa kwa wananchi kulima katika eneo la mita 60 kutoka kwenye kingo za mito.

Kwa upande wake Waziri wa Maji, Mhe. Prof.  Makame Mbarawa amewahakikishia wananchi wa Mkoa wa Simiyu upatikanaji wa uhakika wa  maji  kupitia mradi mkubwa wa Ziwa Victoria, ambapo amesema kwa sasa mradi upo  katika hatua ya kumtafuta mkandarasi.

Naye  Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe.Omari Mgumba akieleza kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha inatoa viatiifu kwa wakulima ambapo amesema hadi sasa zaidi ya chupa milioni saba zimeshasambazwa kwa wakulima katika mikoa inayolima pamba hapa nchini.

Timu ya Mawaziri wanane inayoongozwa na Waziri Lukuvi pia inajumuisha mawaziri kutoka Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Maliasili na Utalii, Mifugo na Uvuvi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Wizara ya Maji na Manaibu Waziri kutoka Wizara ya Kilimo na Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.
MWISHO
Mwenyekiti wa Timu ya Mawaziri wanane wa kisekta, Mhe. William Lukuvi akizungumza na wananchi katika Mkutano wa hadhara Mji Mdogo wa Mwandoya wilayani Meatu, baada ya timu ya mawaziri nane wa kisekta anayoiongoza kutembelea mpaka wa Pori la Akiba la Maswa na Vijiji vinavyolizunguka, Februari 19, 2019.
Wananchi wa Wilaya ya Meatu wakiwapungia mikono Timu ya Mawaziri nane wanaopitia maeneo  yenye migogoro katika wananchi na hifadhi, wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Meatu Mji mdogo  Mwandoya mara baada ya timu hiyo kutembelea na kujionea mpaka wa pori hilo, Februari 19, 2019

Mwenyekiti wa Timu ya Mawaziri wanane, Mhe. William Lukuvi akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mjini Mdogo wa Mwandoya wilayani Meatu, mara baada ya Timu ya mawaziri wanane wanaopitia maeneo yenye migogoro kati ya wananchi na  hifadhi,  mara baada ya timu hiyo kutembelea na kujionea mpaka wa pori la Akiba la Maswa, Februari 19, 2019
Bw. Deusdedit Martin akiwasilisha taarifa ya mapendekezo ya wananchi kwa Mwenyekiti wa Timu ya Mawaziri wanane, Mhe. William Lukuvi wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mji Mdogo wa Mwandoya wilayani Meatu, mara baada ya timu hiyo kutembelea mpaka wa pori la Akiba la Maswa na Vijiji vinavyolizunguka, Februari 19, 2019
Mwenyekiti wa Timu ya Mawaziri wanane, Mhe. William Lukuvi(wa pili kushoto) akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo (katikati) na Mjumbe wa NEC, Mhe. Gungu Silanga(wa pili kulia), baada ya mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mji Mdogo wa Mwandoya wilayani Meatu, mara baada ya timu hiyo kutembelea mpaka wa pori la Akiba la Maswa na Vijiji vinavyolizunguka, Februari 19, 2019.(kushoto) Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba na (kulia) Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi.
Meneja wa Pori la Akiba la Maswa, Bw.Lusato Masinde akijibu baadhi ya hoja kutoka kwa Mwenyekiti wa Timu ya Mawaziri wanane, Mhe. William Lukuvi katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Mji Mdogo wa Mwandoya wilayani Meatu, baada ya timu hiyo kutembelea mpaka wa pori la Akiba la Maswa na Vijiji vinavyolizunguka, Februari 19, 2019
Baadhi ya wajumbe wa timu ya mawaziri wanane wa kisekta, Kutoka kulia Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina, Waziri wa Nchi, OR-TAMISEMI, Sulemani Jafo, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira,Mussa Sima na Waziri wa Maji, Pro. Makame Mbarawa wakiwa katika mkutano wa Hadhara Mji Mdogo wa Mwandoya wilayani Meatu, baada ya timu hiyo kutembelea mpaka wa pori la Akiba la Maswa na Vijiji vinavyolizunguka, Februari 19, 2019.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi(kushoto) akifurahia jambo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika mkutano wa Hadhara Mji Mdogo wa Mwandoya wilayani Meatu, baada ya timu ya mawaziri nane wa kisekta ikiongozwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi kutembelea mpaka wa pori la Akiba la Maswa na Vijiji vinavyolizunguka, Februari 19, 2019.
Wasanii  kutoka wilayani Meatu wakitoa burudani katika mkutano wa Hadhara Mji Mdogo wa Mwandoya wilayani Meatu, baada ya timu ya mawaziri wanane wa kisekta ikiongozwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi kutembelea mpaka wa pori la Akiba la Maswa na Vijiji vinavyolizunguka, Februari 19, 2019.
Bw. Peter Ndekeja mwananchi kutoka wilayani Meatu akitoa malalamiko yake kwa Mwenyekiti wa Timu ya Mawaziri wanane wa kisekta, Mhe. William Lukuvi wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mji Mdogo wa Mwandoya wilayani Meatu, mara baada ya timu hiyo kutembelea mpaka wa pori la Akiba la Maswa na Vijiji vinavyolizunguka, Februari 19, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wananchi katika Mkutano wa hadhara Mji Mdogo wa Mwandoya wilayani Meatu, baada ya timu ya mawaziri wanane wa kisekta ikiongozwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi kutembelea mpaka wa pori la Akiba la Maswa na Vijiji vinavyolizunguka, Februari 19, 2019.


Mwenyekiti wa Timu ya Mawaziri wanane, Mhe. William Lukuvi akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mjini Mdogo wa Mwandoya wilayani Meatu, mara baada ya Timu ya mawaziri wanane wanaopitia maeneo yenye migogoro wananchi na hifadhi, mara baada ya timu hiyo kutembelea na kujionea mpaka wa pori la akiba la Maswa, Februari 19, 2019

Baadhi ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakifuatilia Mkutano wa hadhara uliofanyika Mji Mdogo wa Mwandoya wilayani Meatu, baada ya timu ya mawaziri wanane wa kisekta ikiongozwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi kutembelea mpaka wa pori la Akiba la Maswa na Vijiji vinavyolizunguka, Februari 19, 2019.
Baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Meatu wakifuatilia Mkutano wa hadhara uliofanyika Mji Mdogo wa Mwandoya wilayani Meatu, baada ya timu ya mawaziri nane wa kisekta ikiongozwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi kutembelea mpaka wa pori la Akiba la Maswa na Vijiji vinavyolizunguka, Februari 19, 2019.
Kutoka kushoto Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka,Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. Mussa Sima na Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt. Joseph Chilongani, wakifurahia jambo katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Mji Mdogo wa Mwandoya wilayani Meatu, baada ya timu ya mawaziri wanane wa kisekta ikiongozwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi kutembelea mpaka wa pori la Akiba la Maswa na Vijiji vinavyolizunguka, Februari 19, 2019.



Mwenyekiti wa Timu ya Mawaziri wanane wa kisekta, Mhe. William Lukuvi akiteta jambo na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi(kushoto) katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Mji Mdogo wa Mwandoya wilayani Meatu, baada ya timu ya mawaziri wanane wa kisekta ikiongozwa na Mhe.Lukuvi kutembelea mpaka wa pori la Akiba la Maswa na Vijiji vinavyolizunguka, Februari 19, 2019.

IGP SIRRO: JESHI LA POLISI HALITAWAFUMBIA MACHO WATAKAOBAINIKA KUJIHUSISHA NA MAUAJI YA WATOTO LAMADI


Mkuu wa Jeshi la Polisi hapa nchini IGP Simon Sirro amesema Jeshi la Polisi halitawafumba macho wale wote watakaobainika kuhusika katika mauaji ya watoto katika Kata ya Lamadi wilayani Busega na badala yake litawashughulikia kwa mujibu wa sheria.

Inspekta wa Polisi Sirro ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Lamadi Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Kisesa Kijiji cha Lamadi, kufuatia matukio ya mauaji yaliyoripotiwa mwishoni mwa mwaka jana na hivi karibuni.

IGP Sirro amewatoa hofu wananchi wa Lamadi na kuwasihi kuendelea kuliamini jeshi la Polisi kuwa liko imara na kuwahakikishia kwamba Serikali yao ipo kazini kuhakikisha mauaji hayo yanakomeshwa.

Amesema mauaji hayo yamekuwa yakihusishwa na imani za kishirikina na ramli chonganishi hivyo akawataka waganga wa jadi wanaojihusisha na ramli chonganishi kuacha mara moja maana ni kinyume na sheria, huku akiwataka waganga ambao bado hawajasajiliwa kwa mujibu wa sheria wafanye hivyo haraka.

“Tutawashughulikia wote wanaotaka kuwafanya wana Lamadi wasiishi kwa amani, kwa sababu tunaamini waliofanya haya ni wanaopiga ramli chonganishi ambao ni wachache, nitumie nafasi hii kuwataka waganga ambao hawajasajiliwa kwenda kujisajili haraka, msipojisajili tutawachukulia hatua pia” alisema

Aidha, Sirro ametoa wito kwa jamii kuachana na imani za kishirikiana, mila na desturi potofu ambazo amesema zinarudisha nyuma maendeleo, badala yake akataka elimu iendelee kutolewa kwa jamii ili iweze kubadilika.

Katika hatua nyingine IGP Sirro aliwataka wananchi na viongozi Mkoa Simiyu kushirikiana na jeshi hilo, huku akisisitiza  kuwa ushirikiano watakaotoa kwa polisi ndiyo utasaidia wahusika wote kukamatwa.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka  amesema kufuatia mauaji hayo Serikali imeshawafikisha mahakamani watuhumiwa wa mauaji ya watoto.

Aidha, Mtaka amebainisha kuwa kabla ya watuhumiwa kufikishwa mahakamani Serikali kupitia vyombo vyake vya dola ilisimamia zoezi la upigaji kura za siri ambazo wananchi waliomba wapige ili kuwabaini wauaji hao ambalo lilifanyika 13 Februari, 2019.
MWISHO.
Mkuu wa Jeshi la Polisi hapa nchini IGP Simon Sirro

Friday, February 15, 2019

WANANCHI WAPIGA KURA ZA SIRI KUBAINI WATUHUMIWA WA MAUAJI YA WATOTO BUSEGA

Wananchi wa Kata ya Lamadi Wilayani Busega mkoani Simiyu wamepiga kura za siri kwa lengo la kubaini watuhumiwa wa mauaji ya watoto yaliyotokea hivi karibuni wilayani humo.

Wakizungumza katika zoezi hilo lililofanyika Februari 14, 2019  katika Kitongoji cha Kisesa Kijiji cha Lamadi wananchi hao wamesema kuwa  wamelipokea vizuri zoezi hilo na kubainisha kuwa kura hizo zitasaidia Vyombo vya Dola katika kufanya uchunguzi na kuwabaini wauaji wa watoto wilayani humo

“Zoezi hili nimelipokea vizuri na nina imani litatusaidia kuwapata wauaji wa watoto wetu na naishukuru Serikali kuona haja ya kuwashirikisha wananchi maana mauaji haya ya watoto yametusikitisha sana wakazi wa Lamadi” alisema Modesta Andrea mkazi wa Lamadi

“ Tukio hili la kupiga kura za siri mimi naona ni zuri kwa sababu naamini kuna baadhi ya wananchi wanaweza wakawa wanafahamu watu waliofanya mauaji ya watoto na kama ikitokea kuna watu wakaandikwa labda kwa sababu ya fitina tunaamini vyombo vyetu vya dola vitachuja na kuchunguza na mwishowe wauaji watabainika tu; tunaomba wakibainika sheria ifuate mkondo wake” alisema Elisha Daniel mkazi wa Lamadi.

Akizungumza na wananchi wa Lamadi mara baada ya zoezi hilo kukamilika, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka amesema kufanyika kwa zoezi hilo hatua ya kwanza ya uchunguzi wa mauaji ya watoto wilayani humo, huku akiwahakikishia wananchi kura walizopiga zitahesabiwa na vyombo vya dola mkoani humo.

“Kupiga kura za siri si kwamba tumeshindwa kufanya upelelezi, hii ni hatua ya kwanza ya sisi kufanya uchunguzi wetu, kura hizi zitahesabiwa na vyombo vya dola mkoani Simiyu ambavyo ni Usalama wa Taifa, Uhamiaji, Jeshi la Magereza, Jeshi la Wananchi JWTZ (Mkoa wa Simiyu), Jeshi la Zimamoto, Jeshi la Polisi na TAKUKURU na baadaye taarifa itatolewa.

Aidha, Mtaka amesema wajibu wa kwanza wa Serikali ni kulinda watu wake kuhakikisha wananchi wanaishi kwa amani ili waweze kufanya vema shughuli za maendeleo.

Sambamba na hilo Mtaka amesema Serikali Mkoani Simiyu itahakikisha inayafanyia kazi masuala mbalimbali yaliyosemwa na wananchi katika mkutano huo ikiwa ni pamoja na malalamiko dhidi ya utendaji wa baadhi ya viongozi na watendaji wa Serikali  na kubainisha kuwa  hatua stahiki zitachukuliwa dhidi ya wale wote watakaobainika kwenda kinyume katika kuwatumikia wananchi.

“Niwahakikishie kuwa Serikali itayafanyia kazi yote yaliyosemwa na wananchi katika Mkutano wa hadhara uliofanyika hapa Lamadi, kama kuna wakubadilishwa watabadilishwa, wa kuwajibishwa watawajibishwa, wakuhamishwa watahamishwa naomba mniamini” alisisitiza Mtaka.

Kwa upande wake Mbunge wa Busega, Dkt. Raphael Chegeni ametoa pole kwa wazazi wote waliopoteza watoto wao katika mauaji ya watoto na kuahidi kutoa rambirambi shilingi 500,000/= kwa kila familia ilikutwa na msiba huku akilaani vikali vitendo vya mauaji ya kinyama ambayo yamekatisha ndoto za watoto hao.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera amewashukuru wananchi wa Lamadi kwa  namna walivyojitokeza katika zoezi la kupiga kura za siri na kwa namna walvyolifanya kwa amani na utulivu.
MWISHO


Baadhi ya wananchi wa Lamadi wakiweka karatasi zao za kura za siri zilizopigwa katika zoezi maalum la wananchi wa Lamadi  kupiga kura za siri lililofanyika katika Kitongoji cha Kisesa,   kwa ajili ya kubaini watuhumiwa wa mauaji ya watoto yaliyotokea hivi karibuni wilayani humo.



Bi.Modesta Andrea kutoka kijiji cha Itongo Kata ya Lamadi wilayani Busega mkoani Simiyu akipiga  kura ya siri katika zoezi maalum la kupiga kura za siri lililowahusisha  wananchi wa Lamadi  lililofanyika katika Kitongoji cha Kisesa Februari 14, 2019  kwa ajili ya kubaini watuhumiwa wa mauaji ya watoto yaliyotokea hivi karibuni wilayani humo.




Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wananchi wa Lamadi wilayani Busega mara baada ya kukamilika kwa zoaezi la wananchi kupiga kura za siri kubaini watuhumiwa wa mauaji ya watoto yaliyotokea hivi karibuni wilayani humo, ambalo limefanyika katika Kitongoji cha Kisesa Kijiji cha Lamadi Februari 14,2019.

Baadhi ya wananchi wa Lamadi wilayani Busega wakiendelea kupiga kura za siri na wengine wakisubiri kauli ya Serikali mara baada ya kupiga kura hizo zilizokuwa na lengo la kubaini watuhumiwa wa maujai ya watoto yaliyotokea hivi karibuni wilayani Busega, zoezi la kupiga kura limefanyika katika Kitongoji cha Kijiji cha Lamadi Februari 14,2019.
 Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera akizungumza na wananchi wa Lamadi wilayani Busega mara baada ya kukamilika kwa zoezi  la wananchi kupiga kura za siri kubaini watuhumiwa wa mauaji ya watoto yaliyotokea hivi karibuni wilayani humo, ambalo limefanyika katika Kitongoji cha Kisesa Kijiji cha Lamadi Februari 14,2019.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo akizungumza na wananchi wa Lamadi wilayani Busega mara baada ya kukamilika kwa zoezi  la wananchi kupiga kura za siri kubaini watuhumiwa wa mauaji ya watoto yaliyotokea hivi karibuni wilayani humo, ambalo limefanyika katika Kitongoji cha Kisesa Kijiji cha Lamadi Februari 14,2019.
Kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera, Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt. Joseph Chilongani na Mbunge wa Busega, Dkt. Raphael Chegeni wakiteta jambo katika mkutano maalum ambao wananchi wa Lamadi wilayani Busega, wamepiga kura za siri kubaini watuhumiwa wa mauaji ya watoto yaliyotokea hivi karibuni, zoezi ambalo limefanyika katika Kitongoji cha Kisesa Kijiji cha Lamadi Februari 14,2019.
Mzee Fulile Msikule akichangia hoja katika mkutano maalum ambao wananchi wa Lamadi wilayani Busega, wamepiga kura za siri kubaini watuhumiwa wa mauaji ya watoto yaliyotokea hivi karibuni, zoezi ambalo limefanyika katika Kitongoji cha Kisesa Kijiji cha Lamadi Februari 14,2019.
Mzee Alfred Nanai akichangia hoja katika mkutano maalum ambao wananchi wa Lamadi wilayani Busega, wamepiga kura za siri kubaini watuhumiwa wa mauaji ya watoto yaliyotokea hivi karibuni, zoezi ambalo limefanyika katika Kitongoji cha Kisesa Kijiji cha Lamadi Februari 14,2019.
Mbunge wa Busega, Dkt. Raphael Chegeni akizungumza na wananchi wa Lamadi wilayani Busega mara baada ya kukamilika kwa zoezi  la wananchi kupiga kura za siri kubaini watuhumiwa wa mauaji ya watoto yaliyotokea hivi karibuni wilayani humo, ambalo limefanyika katika Kitongoji cha Kisesa Kijiji cha Lamadi Februari 14,2019.

Thursday, February 14, 2019

WANAFUNZI WALIOONGOZA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2018 SIMIYU WAKIRI KAMBI ZA KITAALUMA ZIMEWASAIDIA


Wanafunzi wa shule za Serikali (kata) Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu, Ibrahim Buyungumya kutoka Shule ya Sekondari Nkololo , aliyeongoza kimkoa kwa kupata daraja la kwanza alama (points)  saba na Kwandu Maduhu  wa Biashara Sekondari aliyepata daraja la kwanza alama kumi na moja, wamekiri kuwa kambi za kitaaluma zimechangia  kuongeza ufaulu wao katika Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2018.

Wanafunzi hao wameyasema hayo katika hafla ya kuwapongeza walimu waliofanikisha na wanafunzi waliofanya vizuri katika Matokeo ya mtihani wa Taifa wa Kidato cha nne mwaka 2018  Kimkoa na kuufanya mkoa kushika nafasi ya Tisa Kitaifa, iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Nkololo wilayani Bariadi, Februari 13, 2019.

Wanafunzi hao wamesema pamoja na kumuomba Mungu, juhudi zao binafsi za kujisomea, jitihada za walimu, malezi kutoka kwa wazazi wanakiri kambi za kitaaluma zilizofanyika mkoani Simiyu kwa madarasa yote ya mitihani ziliwasaidia kuwaandaa na mtihani huo wa Taifa, huku wakisisitiza kambi hizo ziwe endelevu  na wakapendekeza kuwa kwa mwaka 2019 ziongezewe muda na zianze mapema zaidi.

“ Namshukuru Mungu kunifanikisha kupata daraja la kwanza alama saba, nawashukuru walimu wangu, wazazi wangu kwa namna walivyokuwa msaada kwangu; pia kipekee namshukuru Mkuu wetu wa Mkoa kwa kutuletea kambi,  zimetusaidia sana maana tulipata nafasi ya kukutana na wanafunzi wenzetu na walimu mahiri kutoka shule mbalimbali na zilitusaidia kuelewa masomo kwa mawanda mapana zaidi” alisema Ibrahimu Buyungumya.

“Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kupata daraja la kwanza alama 11, nawashukuru wazazi, walimu pia nashukuru uwepo wa kambi za kitaaluma ambazo zilitusaidia sana kujiandaa vema na mtihani wetu, nashauri kambi hizi zianze mapema na muda uongezwe  ili ziwasaidie wadogo zetu wafaulu vizuri zaidi yetu sisi” alisema Kwandu Maduhu.

Mkuu wa Shule ya sekondari Biashara, Mwl. Mathias Joseph ambaye shule yake ilifanya vzuri kwa kupata alama A 23 na alama B 79 amesema pamoja na kambi za kitaaluma siri nyingine ya kufanya vizuri ni jitihada zilizofanywa na walimu pamoja na usimamizi mzuri wa mikakati iliyowekwa na idara ya Elimu na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, ikiwa ni pamoja na kufanya mazoezi na mitihani ya mara kwa mara.

Akizungumza katika hafla ya kuwapongeza walimu waliofanikisha na wanafunzi waliofanya vizuri katika Matokeo ya mtihani wa Taifa wa  Kidato cha nne mwaka 2018 katika mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka  amewapongeza viongozi, walimu, wanafunzi, wazazi na wadau wote wa elimu mkoani humo, kwa jitihada walizofanya  katika kuongeza ufaulu.

Aidha, Mtaka ameelekeza kamati zote za shule zikutane na wazazi wa wanafunzi wa madarasa ya mtihani ili wakubaliane juu ya wanafunzi hao kuanza kambi za kitaaluma na wazazi hao wachangie chakula ambacho watoto wao wangekula wakiwa majumbani kwao kitumike wakiwa kambini.

“Nilishatoa maelekezo na nayarudia; kamati za shule zikae na wazazi wakubaliane madarasa yote ya mtihani watoto waanze kambi za kitaaluma na wazazi wachangie chakula kile kile ambacho watoto wangekula wakiwa nyumbani, ili watoto wapate nafasi nzuri ya kusoma na kujiandaa na mtihani wa Taifa” alisema Mtaka.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu, Enock  Yakobo ametoa wito kwa wazazi mkoani humo kuhimiza watoto kusoma ili waweze kufikia ndoto zao akakemea tabia ya baadhi ya wazazi kuwaachisha masomo watoto wa kike na kuwaozesha.

Jumla ya wanafunzi 7094 kati yao wavulana ni 4224 na wasichana  2875 walifanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne mwaka 2018 mkoani Simiyu na kuwezesha mkoa kushika nafasi ya tisa Kitaifa kati ya mikoa 31, ambapo umepanda kwa nafasi mbili ikilinganishwa na mwaka 2017 ambapo ulishika nafasi ya 11 Kitaifa.

Katika pongezi zilizotolewa kwa walimu na wanafunzi mwanafunzi wa kiume aliyeongoza Kimkoa amezawadiwa shilingi milioni Moja, mwanafunzi bora wa kike shilingi laki  tano (wote wamefunguliwa akaunti) na kuahidiwa kupewa mahitaji yote muhimu watakapochaguliwa kidato cha tano, huku walimu sitini kila mwalimu  akipewa shilingi elfu ishirini kwa kila alama A iliyopatikana kwenye somo lake.

MWISHO
Mwanafunzi kutoka Shule ya Kata Nkololo aliyefanya vizuri  kwa kupata daraja la kwanza (pointi saba) na kushika nafasi ya kwanza kimkoa katika mtihani wa Taifa wa Kidato cha nne mwaka 2018 Ibrahimu Buyungumya(kushoto) na Mwanafunzi  wa Kike Kwandu Maduhu kutoka Shule ya Sekondari Biashara aliyefanya vizuri kwa kupata daraja la kwanza (pointi 11) katika mtihani huo na kuongoza kimkoa (wasichana), wakionesha kadi zao za akaunti ambazo wamekabidhiwa (katika hafla maalum ya kuwapongeza iliyofanyika shule ya Sekondari Nkololo wilayani Bariadi Februari13, 2019 ) baada ya kufunguliwa akaunti na kuwekewa zawadi hizo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(katikati) akizungumza jambo na  Mwanafunzi kutoka Shule ya Kata Nkololo aliyeongoza kimkoa katika mtihani wa Taifa wa Kidato cha nne mwaka 2018 kwa kupata  daraja la kwanza(pointi saba) ,Ibrahimu Buyungumya(kushoto) na Mwanafunzi  wa Kike Kwandu Maduhu kutoka Shule ya Sekondari Biashara aliyeongoza kwa upande wa wasichana  kwa kupata daraja la kwanza (pointi 11) katika mtihani huo, baada ya hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri kimkoa, iliyofanyika katika shule ya sekondari Nkololo wilayani Bariadi Februari 13, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(mwenye suti kulia) akishuhudia wanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Nkololo wilayani Bariadi  wakifanya mazoezi kwa vitendo wakati wa hafla ya kuwapongeza walimu waliofanikisha na wanafunzi waliofanya vizuri katika Mtihani wa Kidato cha nne mwaka 2018 iliyofanyika kimkoa shuleni hapo, Februari 13, 2019.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(kushoto) akiteta jambo na Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju, wakati wa hafla ya kuwapongeza walimu waliofanikisha na wanafunzi waliofanya vizuri katika Mtihani wa Kidato cha nne mwaka 2018 iliyofanyika kimkoa, katika shule ya sekondari Nkololo wilayani Bariadi Februari 13, 2019. 


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(wa pili kushoto) akiwakabidhi zawadi ya ngao viongozi wa Halmashauri ya mji wa Bariadi ambayo iliongoza kimkoa na kushika nafasi ya tisa kati ya halmashauri zaidi ya 185 nchini katika mtihani wa Taifa wa Kidato cha nne mwaka 2018, (kushoto na wa pili kushoto) ni wanafunzi walifanya vizuri Kimkoa kutoka shule za Serikali), wakati wa hafla ya kuwapongeza walimu waliofanikisha na wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihani huo iliyofanyika kimkoa katika shule ya sekondari Nkololo wilayani Bariadi Februari 13, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (wa nne kushoto mbele) katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa mkoa na Halmashauri ya Mji wa Bariadi , walimu wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, wanafunzi walawili walioongoza  katika matokeo ya mtihani wa Taifa wa kidato cha nne mwaka 2018 Kimkoa na wazazi wao, baada ya hafla ya kuwapongeza walimu waliofanikisha na wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihani huo iliyofanyika kimkoa katika shule ya sekondari Nkololo wilayani Bariadi Februari 13, 2019.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo akizungumza na viongozi, walimu, wazazi na wanafunzi katika hafla ya kuwapongeza walimu waliofanikisha na wanafunzi waliofanya vizuri katika Mtihani wa Kidato cha nne mwaka 2018 iliyofanyika kimkoa, katika shule ya sekondari Nkololo wilayani Bariadi Februari 13, 2019.

Mkuu wa Shule ya Sekondari Biashara Mwalimu Mathias Joseph akionesha zawadi ya shilingi 460,000/= iliyotolewa kama motisha kwa walimu wa shule hiyo waliofanikisha kutoa jumla ya  alama A 23  katika Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha nne mwaka 2018, wakati wa hafla ya kuwapongeza walimu waliofanikisha na wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihani huo iliyofanyika kimkoa katika shule ya sekondari Nkololo wilayani Bariadi Februari 13, 2019.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akizungumza na viongozi, walimu, wazazi na wanafunzi katika hafla ya kuwapongeza walimu waliofanikisha na wanafunzi waliofanya vizuri katika Mtihani wa Kidato cha nne mwaka 2018 iliyofanyika kimkoa, katika shule ya sekondari Nkololo wilayani Bariadi Februari 13, 2019.
Mwanafunzi kutoka Shule ya Kata Nkololo aliyefanya vizuri  kwa kupata daraja la kwanza (pointi saba)na kushika nafasi ya kwanza kimkoa katika Matokeoya  mtihani wa Taifa wa Kidato cha nne mwaka 2018 Ibrahimu Buyungumya, katika hafla ya kuwapongeza walimu waliofanikisha na wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihani huo iliyofanyika kimkoa katika shule ya sekondari Nkololo wilayani Bariadi Februari 13, 2019.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Nkololo wakishangilia jambo, katika hafla ya kuwapongeza walimu waliofanikisha na wanafunzi waliofanya vizuri katika Matokeo ya  Mtihani wa Kidato cha nne mwaka 2018 iliyofanyika kimkoa, katika shule ya sekondari Nkololo wilayani Bariadi Februari 13, 2019

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (wa nne kushoto mbele) katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa mkoa na Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi , walimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, wanafunzi wawili walioongoza  katika mtihani wa Taifa wa kidato cha nne mwaka 2018 kimkoa na wazazi wao, baada ya hafla ya kuwapongeza walimu waliofanikisha na wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihani huo iliyofanyika kimkoa katika shule ya sekondari Nkololo wilayani Bariadi Februari 13, 2019. .
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (wa tano kushoto mbele) katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa mkoa na Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, walimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, wanafunzi wawili walioongoza katika mtihani wa Taifa wa kidato cha nne mwaka 2018 Kimkoa na wazazi wao, baada ya hafla ya kuwapongeza walimu waliofanikisha na wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihani huo iliyofanyika kimkoa katika shule ya sekondari Nkololo wilayani Bariadi Februari 13, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (wa tano kushoto mbele) katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa mkoa na Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, walimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, wanafunzi wawili walioongoza  katika matokeo ya  mtihani wa Taifa wa kidato cha nne mwaka 2018 kimkoa na wazazi wao, baada ya hafla ya kuwapongeza walimu waliofanikisha na wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihani huo iliyofanyika kimkoa katika shule ya sekondari Nkololo wilayani Bariadi Februari 13, 2019.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi (CCM) Mkoa wa Simiyu, Jackson Yuma akizungumza na viongozi, walimu, wazazi na wanafunzi katika hafla ya kuwapongeza walimu waliofanikisha na wanafunzi waliofanya vizuri katika matokeo ya  Mtihani wa Kidato cha nne mwaka 2018 iliyofanyika kimkoa, katika shule ya sekondari Nkololo wilayani Bariadi Februari 13, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (mwenye skafu ) akiwa ameongoza na baadhi ya viongozi waliompokea  katika shule ya sekondari Nkololo na kumuongoza   kueleka eneo la hafla ya kuwapongeza walimu waliofanikisha na wanafunzi waliofanya vizuri katika matokeo ya  Mtihani wa Kidato cha nne mwaka 2018 iliyofanyika kimkoa, katika shule ya sekondari Nkololo wilayani Bariadi Februari 13, 2019.
Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt. Joseph Chilongani akizungumza na viongozi, walimu, wazazi na wanafunzi katika hafla ya kuwapongeza walimu waliofanikisha na wanafunzi waliofanya vizuri katika Mtihani wa Kidato cha nne mwaka 2018 iliyofanyika kimkoa, katika shule ya sekondari Nkololo wilayani Bariadi Februari 13, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(katikati) akizungumza jambo na  Mwanafunzi kutoka Shule ya Kata Nkololo aliyeongoza kimkoa katika mtihani wa Taifa wa Kidato cha nne mwaka 2018 kwa kupata  (pointi saba) ,Ibrahimu Buyungumya(kushoto) na Mwanafunzi  wa Kike Kwandu Maduhu kutoka Shule ya Sekondari Biashara aliyeongoza kwa upande wa wasichana  kwa kupata daraja la kwanza (pointi 11) katika mtihani huo, baada ya hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri kimkoa, iliyofanyika katika shule ya sekondari Nkololo wilayani Bariadi Februari 13, 2019.kuliani Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga.




Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!