Saturday, May 25, 2019

WAKULIMA WAKIWEZESHWA ZANA BORA ZA KILIMO WATALIMA KWA TIJA ZAIDI: KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali ametoa wito kwa viongozi wilayani Meatu kuwasaidia wakulima wa pamba  kupata zana bora za kilimo ili kuongeza tija  katika uzalishaji  na wilaya hiyo iendelee kuwa kinara katika uzalishaji wa zao la pamba nchini.


Ndg. Ali ameyasema hayo wakati Mwenge wa Uhuru ulipopita na kukagua  Shamba la Mbegu bora ya pamba lenye ukubwa wa ekari 13 katika Kijiji cha Mwabusalu ambapo alimpongeza mkulima Jidayi Charles na kumtunuku cheti cha kumtambua kama mkulima bora.

“Ninampongeza sana Bwana Jidayi maana ni wazee wachache sana wanaojihusisha na kilimo ni vizuri mkachukua jitihada za makusudi kumsaidia apate zana za kisasa, kama analima ekari 13 akiwa hana trekta nina uhakika akiwezeshwa atafanya vizuri zaidi, kama mmeshaanza utaratibu wa kumpatia mkopo uharakishwe ili kiwango cha uzalishaji kiweze kuongeza zaidi” alisema Mzee  Mkongea Ali.

Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt. Joseph Chilongani amesema wilaya ya Meatu ndiyo wilaya kinara katika uzalishaji wa pamba nchini ambapo amebainisha kuwa katika msimu wa mwaka 2018/2019 ilizalisha takribani kilo milioni 31 za pamba na akaeleza kuwa mkakati wa wilaya ni kuendelea kuwasaidia wakulima kwa utaalam na mikopo za kununua zana bora ili waweze kuzalisha kwa tija  zaidi.

Akitoa taarifa ya mradi wa shamba hilo, Afisa Kilimo wa Wilaya ya Meatu, Bw.Thomas Shilabu amesema uzalishaji wa zao la pamba unakabiliwa na changamoto ya baadhi ya wakulima kulima wa kilimo cha mazoea kwa kusia mbegu na kupalilia maotea.

Kwa upande wake Bw. Jidayi Charles amesema kwa sasa anatumia trekta ya kukodi kulima shamba lake lenye ukubwa wa ekari 13 ambalo linachangia kuchelewesha uandaaji wa shamba kwa kuwa linatumiwa na wakulima wengi, lakini endapo atakapata trekta lake litamrahisishia kuandaa shamba mapema na kwa urahisi zaidi.

Pamoja na kutembelea mradi wa shamba za kuzalisha mbegu bora za pamba, Mwenge wa Uhuru ukiwa Wilayani Meatu umezindua vyumba viwili vya maabara shule ya Sekondari Mwandoya, kutembelea mradi wa maji wa SangaItiinje na kupanda miti katika Chanzo cha maji, kukagua klabu ya wanafunzi ya wapinga RUSHWA na Klabu ya wanafunzi ya kupambana na mimba za utotoni shule ya msingi Isengwa.

Wakati mwenge wa uhuru ulipopita kuona shughuli za klabu ya mapambano dhidi ya mimba za utotoni, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru ameupongeza uongozi wa wilaya ya Meatu kuanzisha klabu hizo shuleni na akatoa wito kwa wataalam wa Ustawi wa Jamii na Dawati la jinsia na vyombo vya dola kutowahurumia wote wanaobanika kusababisha mimba za utotoni.

Aidha, ulifungua Nyumba ya kulala wageni TS Lodge, kukagua shughuli za kikundi cha vijana wajasiriamali, kukagua shughuli za mapambano dhidi ya rushwa, mapambano dhidi ya mimba za utotoni na mapambano dhidi ya malaria.
MWISHO


Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali  akikagua shamba la mbegu bora za pamba katika Kijiji cha Mwabusalu wilayani Meatu, Mei 23, 2019.
Sehemu ya shamba la mbegu bora za pamba ekari 13 linalomilikiwa na Mkulima Jidayi Charleas wilayani Meatu, lililotembelewa na kukaguliwa na mbio za Mwenge wa Uhuru Mei 23, 2019 wilayani humo.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali  akifungua Vyumba viwili vya maabara katika shule ya sekondari Mwandoya wilayani Meatu, Mei 23, 2019.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali  akipanda mti katika chanzo cha maji cha Mradi wa maji wa SangaItinje wilayani Meatu, Mei 23, 2019.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali   akiwa na wakimbiza mwenge wa Uhuru wengine wakikagua pampu ya maji katika Mradi wa maji wa Sanga Itinje wilayani Meatu, Mei 23, 2019.
Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt. Joseph Chilongani (kulia) akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dkt. Seif Shekalaghe katika Kijiji cha Sangaitinje wilayani Meatu, Mei 23, 2019.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali  (mwenye galoni la maziwa ya Meatu(Meatu Milk) akiangalia bidhaa za maziwa zinazozalishwa katika kiwanda cha Meatu Milk kinachomilikiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo, Mei 23, 2019.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali akimkabidhi cheti Mwenyekiti wa Klabu ya Wapinga Rushwa katika shule ya Msingi Isengwa, wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo, Mei 23, 2019.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali  (kulia) akiangalia burudani kutoka kwa Wanachama wa Klabu ya Kupinga Mimba za Utotoni katika shule ya Msingi Isengwa, wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo, Mei 22, 2019.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali  ( wa tatu kulia) akizungumza na kikundi vijana wanaotengeneza Batiki Mjini Mwanhuzi wilayani Meatu, wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo, Mei 23, 2019
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali  akizungumza na Wanachama wa klabu ya Kupinga mimba za Utotoni katika Shule ya Msingi Isengwa wilayani Meatu, wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo, Mei 23, 2019.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali  akiangalia mazoezi kwa vitendo ya wanafunzi wa shule ya sekondari Mwandoya wilayani Meatu, wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo, Mei 23, 2019.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali  akiangalia mazoezi kwa vitendo ya wanafunzi wa shule ya sekondari Mwandoya wilayani Meatu, wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo, Mei 23, 2019.
Sehemu ya mbele ya Vyumba vya maabara vilivyozinduliwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru Mei 23, 2019 katika shule ya sekondari Mwandoya wilayani Meatu.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali akizungumza na wanachama wa Klabu ya Wapinga Rushwa katika shule ya Msingi Isengwa, wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo, Mei 23, 2019.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali akisaini cheti cha Klabu ya Wapinga Rushwa katika shule ya Msingi Isengwa, wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo, Mei 23, 2019.
Baadh ya vikundi vya vijana vya wilaya ya Meatu vilivyokaguliwa na mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo, Mei 23, 2019.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali akitoa ujumbe wa mbio za Mwenge wa Uhuru mara baada ya kuzindua vyumba viwili vya maabara katika Shule ya Sekondari Mwandoya wilayani Meatu, Mei 23, 2019.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali, wakimbiza Mwenge wa Uhuru wengine na baadhi ya viongozi wa wilaya ya Meatu wakiwa katika picha ya pamoja na Wanachama wa klabu ya Kupinga mimba za Utotoni katika Shule ya Msingi Isengwa wilayani Meatu, wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo, Mei 23, 2019.
Nyumba ya pampu na jenereta katika Mradi wa Maji wa SangaItinje wilayani Meatu ambao ulitembelewa na Mbio za Mwenge wa Uhuru Mei 23, 2019 wilayani humo.
Sehemu ya Vyumba vya maabara vilivyozinduliwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru Mei 23, 2019 katika shule ya sekondari Mwandoya wilayani Meatu.

MWENGE WA UHURU KUPITIA MIRADI 34 YENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 8.8 MKOANI SIMIYU


Mwenge wa Uhuru mwaka 2019 umeanza mbio zake Mei 22, 2019 Mkoani Simiyu ambapo unatarajia kupitia miradi 34 kutoka katika sekta binafsi, maji, elimu, afya, viwanda, kilimo, barabara, maendeleo ya jamii na hifadhi ya mazingira ambayo ina thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 8.8.

Akizungumza mara baada ya kupokea Mwenge wa Uhuru kutoka Mwanza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema katika thamani hiyo ya miradi ambayo ni shilingi 8, 878,598,412.25 shilingi 904,170,725.00 ni nguvu za wananchi, Halmashauri shilingi 428, 403,532.63, Serikali Kuu ni shilingi 5, 992,582,072.37, wahisani shilingi 1,256,475,082.25 na sekta Binafsi shilingi 296,967,000.00

Akizungumzia Ujumbe wa Mwenge wa Uhuru mwaka 2019 “MAJI NA HAKI YA KILA MTU TUTUNZE VYANZO VYAKE NA TUKUMBUKE KUSHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA” Mtaka amesema, wastani wa upatikanaji maji Simiyu ni asilimia 50.4 ambao unahudumia wakazi 817, 968  na kubainisha kuwa Serikali inaendelea kuhamasiha wananchi kulinda vyanzo vya maji ili kuwezesha upatikanaji wa huduma hiyo.

Aidha, amesema Mkoa wa Simiyu umejipanga na unaendelea kuandaa mazingira mazuri ya amani na utulivu, yatakayowezesha wananchi kutumia haki yao ya kidemokrasia kushiriki kikamilifu katika mchakato mzima wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2019.

Kwa upande wake Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali  amewataka viongozi wa mkoa wa Simiyu na wilaya zote mkoani humo kuhakikisha taarifa zote za miradi ya maendeleobitakayopitiwa na Mwenge wa uhuru ziwepo eneo la mradi na wataalam wote wanaohusika na miradi hiyo wawepo.

Baada ya kupokelewa Mkoani Simiyu Mwenge wa Uhuru umeanza mbio zake wilayani Maswa ambapo umepitia mradi wa urasimishaji wa makazi Malampaka, ukaguzi wa ujenzi wa barabara za lami Mjini Maswa, mradi wa maji Nyashimba, Kiwanda cha viazi lishe Njiapanda, vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja Kijiji cha Mwadila.

Aidha, Mwenge wa Uhuru ulitembelea na kuona shughuli za wajasiriamali na kutoa hundi za wajasiriamali, kuzindua klabu za kutokomeza rushwa na dawa za kulevya, kuzindua kampeni ya tokomeza malaria na kukagua shughuli za utoaji elimu ya kuhimiza upimaji wa VVU/UKIMWI.
Mwenge wa Uhuru takimbiza kwa mua wa siku sita mkoani Simiyu Mei 22 mpaka Mei 27, 2019 na Mei 28, 2019 utakabidhiwa mkoani Mara.
MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(mwenye fulana nyeupe) akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongela katika kijiji cha Jihu wilayani Maswa, Mei 22, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(mwenye fulana nyeupe) akipokea hati ya makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongela katika kijiji cha Jihu wilayani Maswa, Mei 22, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kulia) akimkabidhi  Mwenge wa Uhuru  Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe  katika kijiji cha Jihu wilayani Maswa, Mei 22, 2019 ikiwa ndiyo wilaya ya kwanza kuanza Mbio za Mwenge wa Uhuru mkoani Simiyu.
Mhandisi wa Maji wa Wilaya ya Maswa  akitoa maelezo kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali kabla ya kuweka jiwe la msingi mradi maji wa Nyashimba katika Kijiji cha Nyashimba wilayani Maswa, Mei 22, 2019.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali akifungua vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja ya mwalimu  Mkuu katika shule ya sekondari Mwadila Mei 22, 2019.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali akiangali baadhi ya machapisho yanayotumika na wanachama wa Klabu yaMapambano dhidi ya Rushwa katika shule ya sekondari Lalago wilayani Maswa kutoa elimu ya vita dhidi ya rushwa kabla ya kuzindua klabu hiyo, Mei 22, 2019
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali(wa nne kushoto)  na wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa wengine wakiangalia mbegu za  viazi lishe, kabla ya kuweka jiwe la msingi Kiwanda cha kusindika Viazilishe katika Kijiji cha Njiapanda wilayani Maswa, Mei 22, 2019.
Baadhi ya Askari wa Jeshi la Polisi na Vijana wa Skauti mkoani Simiyu wakipita na Mwenge wa uhuru katika moja ya barabara zinazojengwa  kwenye mtandao wa Kilomita 1.5 katika Mji wa Maswa, ambapo mradi huo ulikaguliwa na Mbio za mwenge wa Uhuru Mei 22, 2019.
Mbunge wa Maswa mashariki na Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Stanslaus Nyongo akizungumza na wananchi, wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani Maswa, Mei 22, 2019.
Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dkt. Seif Shekalaghe akizungumza na wananchi, wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani Maswa, Mei 22, 2019.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali(wa pili kulia)  akiwasiliza wanawake wajasiriamali wa wilayani Maswa, wakati alipopita kukagua kazi zinazofanywa na wanawake hao baada ya kuwezeshwa na Halmashauri kuwezeshwa mikopo inayotoka na asilimia nne ya mapato ya ndani, wakati wa mbio za mwenge wa Uhuru wilayani humo Mei 22, 2019.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali akimkabidhi hati ya kiwanja Mkazi wa Malampaka, Bw. Martini Kamuzora mara baada ya kuzindua zoezi la urasimishaji wa makazi ya wananchi katika Mji wa Malampaka, Mei 22, 2019.
Moja ya mabanda yaliyoandaliwa na Halmashauri ya Wilaya ya Maswa kutoa elimu kwa wananchi juu ya vita dhidi ya dawa za kulevya kupitia Klabu ya kupiga vita dawa za kulevya shule ya sekondari Lalago, wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo Mei 22, 2019.
Wanachama wa Klabu ya kupiga vita dawa za kulevya kutoka shule ya Sekondari Lalago wakitoa maelezo kwa Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali, kabla ya kuzinduliwa kwa klabu hiyo wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo Mei 22, 2019.
Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ndg. Latifa Khamis Juwakali akitoa ujumbe wa Mwenge kwa wananchi wa Lalago wilayani Maswa(hawapo pichani), Mei 22, 2019.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali akizungumza na wanawake wajasiriamali wanaojihusisha na kilimo cha pamba alipokuwa akikagua kazi wanazofanya wanawake hao, wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani Maswa, Mei 22, 2019.

Friday, May 10, 2019

MWAUWASA, BENNET CONTRACTORS WASAINI MKATABA UJENZI WA MRADI WA MAJI WA BILIONI 1.8 BUSEGA

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi. Anthony Sanga  na Mkurugenzi wa Kampuni ya  Bennet Contractors Sabato Boaz kutoka Mwanza, wamesaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa Maji wa Nyashimo wilayani Busega utakaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 1.8.

Mkataba wa Mradi huo utakaonufaisha vijiji vya Bukabile, Mwagulanja na Bulima na kuhudumia wananchi 20,030 , umesainiwa Nyashimo wilayani Busega na kushuhudiwa na wananchi, viongozi wa Chama na Serikali wa Wilaya ya Busega na Mkoa wa Simiyu, wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka.

Akizungumza na wananchi na viongozi waliofika kushuhudia zoezi hilo Mtaka amemtaka Mkandarasi Kampuni ya  Bennet Contractors kuzingatia muda na viwango katika utekelezaji wa mradi huo, huku akisisitiza kuhakikisha mradi huo unawanufaisha wananchi wanaozunguka eneo la mradi kwa kutoa ajira za muda na ununuzi wa vifaa vya ujenzi.

“Mkataba unaonesha mradi huu ni wa miezi 15, nikuombe mkandarasi miezi 15ni mingi tungehitaji tunapoanza maandalizi ya kutengeneza ilani ya CCM mwaka 2020 tuzungumzie utekelezaji wa ilani siyo mpango; tunahitaji jamii yetu inufaike kupitia mradi huu, vijana wapate ajira, mama ntilie wapike chakula na baadhi ya vifaa vya ujenzi vinunuliwe kwenye maduka ya hapa” alisema Mtaka.

Ameongeza kuwa Serikali imetoa zaidi ya shilingi bilioni 16.4  kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maji wilayani Busega, ikiwa ni pamoja na Mradi wa Lamadi, Kiloleli, Mwamanyili na ukarabati wa visima maeneo mbalimbali, ambayo itakapokamilika  itaongeza hali ya upatikanaji wa maji safi na salama Busega kutoka asilimia 39 ya sasa na kufikia asilimia 74.

Naye Mbunge wa Busega, Dkt. Raphael Chegeni amesema pamoja na mradi wa Nyashimo Serikali inatekeleza miradi mingine ya maji wilayani Busega ukiwepo wa Kiloleri Mradi wa Lamadi, hivyo akasisitiza wananchi kulinda na kutunza miradi hiyo ili iwanufaishe.

Nao wananchi wamesema“Tunashukuru kuletewa huu mradi tulikuwa tunapata adha ya maji tulikuwa tunanunua kwenye madumu na kufua ziwani, lakini endapo mradi huu uliosainiwa mkataba leo ukikamilika itakuwa ni neema kwetu hasa sisi wakina mama ambao ndiyo tunapata tabu zaidi na familia zetu” Sara Nanyori mkazi wa kijiji cha Bulima.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi. Anthony Sanga  amesema mradi wa Nyashimo ni utekelezaji wa ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliyoitoa kwa wananchi na unafadhiliwa kwa asilimia 100 na fedha za Serikali ya Tanzania.
Mkurugenzi wa Kampuni ya  Bennet Contractors(Mkandarasi) Sabato Boaz kutoka Mwanza, amesema pamoja na kwamba mkataba unaonesha utekelezaji ni miezi 15, kampuni yake inatarajia kutekeleza kwa ubora na kwa muda mfupi kadri itakavyowezekana ili kuleta  huduma ya maji safi na salama haraka kwa wananchi wa Nyashimo.
MWISHO


Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza(MWAUWASA), Mhandisi. Anthony Sanga  (kushoto) na  Mkurugenzi wa Kampuni ya Bennet Contractors, Sabato Boaz  kutoka Jijini Mwanza  wakibadilishana  nakala za mkataba waliosaini Mei 10, 2019 wilayani Busega ,  kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa Maji wa Nyashimo na kushuhudiwa na viongozi wa Chama na Serikali wa Wilaya ya Busega na Mkoa wa Simiyu, wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa, Mhe. Anthony Mtaka (mwenye suti ya rangi ya kijivu)  ambao utakaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 1.8

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi. Anthony Sanga  (kushoto) na  Mkurugenzi wa  Kampuni ya Bennet Contractors Sabato Boaz  kutoka Jijini Mwanza  wakitia saini  mkataba wa ujenzi wa mradi wa Maji wa Nyashimo Mei 10, 2019 wilayani Busega na kushuhudiwa na viongozi wa Chama na Serikali wa Wilaya ya Busega na Mkoa wa Simiyu, wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(mwenye suti ya rangi ya kijivu)  ambao utakaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 1.8.
Kutoka kushoto Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza(MWAUWASA), Mhandisi. Anthony Sanga,   Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na Mbunge wa Busega, Dkt. Raphael  Chegeni wakielekea eneo maalum la utiaji saini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa Nyashimo wilayani Busega kati ya MWAUWASA na Mkandarasi Kampuni ya Bennet Contractors kutoka Jijini Mwanza.
Baadhi ya wananchi wa kata ya Nyashimo wakifuatilia zoezi la  utiaji saini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa Nyashimo wilayani Busega kati ya MWAUWASA na Mkandarasi Kampuni ya Bennet Contractors kutoka Jijini Mwanza, mradi utakaogharimu shilingi bilioni 1.8 na kuwanufaisha wananchi wa Kata ya Nyashimo.
Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera akitoa neno la shukrani wakati wa  kusaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa Nyashimo wilayani Busega kati ya MWAUWASA na Mkandarasi Kampuni ya Bennet Contractors kutoka Jijini Mwanza, mradi utakaogharimu shilingi bilioni 1.8 na kuwanufaisha wananchi wa Kata ya Nyashimo.
Mbunge wa Busega, Dkt. Raphael  Chegeni akizungumza na wananchi wa Kata ya Nyashimo wakati wa kusaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa Nyashimo wilayani Busega kati ya MWAUWASA na Mkandarasi Kampuni ya Bennet Contractors kutoka Jijini Mwanza, mradi utakaogharimu shilingi bilioni 1.8 na kuwanufaisha wananchi wa Kata ya Nyashimo.
Mwananchi kutoka kata ya Nyashimo akifurahia jambo na Diwani wa Kata hiyo Mhe. Mickness Mahela wakati wa  zoezi la  kusaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa Nyashimo wilayani Busega kati ya MWAUWASA na Mkandarasi Kampuni ya Bennet Contractors kutoka Jijini Mwanza, mradi utakaogharimu shilingi bilioni 1.8 na kuwanufaisha wananchi wa Kata ya Nyashimo.
Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Wajumbe wa Bodi ya MWAUWASA wakifuatilia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea kabla ya zoezi la kusaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa Nyashimo wilayani Busega kati ya MWAUWASA na Mkandarasi Kampuni ya Bennet Contractors kutoka Jijini Mwanza, mradi utakaogharimu shilingi bilioni 1.8 na kuwanufaisha wananchi wa Kata ya Nyashimo.
Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Wajumbe wa Bodi ya MWAUWASA wakifuatilia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea kabla ya zoezi la kusaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa Nyashimo wilayani Busega kati ya MWAUWASA na Mkandarasi Kampuni ya Bennet Contractors kutoka Jijini Mwanza, mradi utakaogharimu shilingi bilioni 1.8 na kuwanufaisha wananchi wa Kata ya Nyashimo.
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Nyashimo wakiwa wamejipanga kwa lengo la kutoa kero zao kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(kulia) kabla ya kuanza kwa zoezi la kusaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa Nyashimo wilayani Busega kati ya MWAUWASA na Mkandarasi Kampuni ya Bennet Contractors kutoka Jijini Mwanza, mradi utakaogharimu shilingi bilioni 1.8 na kuwanufaisha wananchi wa Kata ya Nyashimo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(kulia) akitoa ufafanuzi wa moja ya kero iliyowasilishwa na mkazi wa Kata ya Nyashimo, kabla ya kushuhudia  zoezi la  kusaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa Nyashimo wilayani Busega kati ya MWAUWASA na Mkandarasi Kampuni ya Bennet Contractors kutoka Jijini Mwanza, mradi utakaogharimu shilingi bilioni 1.8 na kuwanufaisha wananchi wa Kata ya Nyashimo.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Ekwabi Mujungu akitambulisha viongozi wa mkoa walifika kushuhudia zoezi la kusaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa Nyashimo wilayani Busega kati ya MWAUWASA na Mkandarasi Kampuni ya Bennet Contractors kutoka Jijini Mwanza, mradi utakaogharimu shilingi bilioni 1.8 na kuwanufaisha wananchi wa Kata ya Nyashimo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akimkaribisha Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Busega, Komredi. kueleza juu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM wilayani humo, kabla ya kushuhudia  zoezi la  kusaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa Nyashimo wilayani Busega kati ya MWAUWASA na Mkandarasi Kampuni ya Bennet Contractors kutoka Jijini Mwanza, mradi utakaogharimu shilingi bilioni 1.8 na kuwanufaisha wananchi wa Kata ya Nyashimo.
Baadhi ya wananchi wa kata ya Nyashimo wakifuatilia zoezi la  kusaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa Nyashimo wilayani Busega kati ya MWAUWASA na Mkandarasi Kampuni ya Bennet Contractors kutoka Jijini Mwanza, mradi utakaogharimu shilingi bilioni 1.8 na kuwanufaisha wananchi wa Kata ya Nyashimo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na wananchi wa Kata ya Nyashimo, kabla ya kushuhudia  zoezi la  kusaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa Nyashimo wilayani Busega kati ya MWAUWASA na Mkandarasi Kampuni ya Bennet Contractors kutoka Jijini Mwanza, mradi utakaogharimu shilingi bilioni 1.8 na kuwanufaisha wananchi wa Kata hiyo
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(kulia) akiwahamasisha viongozi kumchangia mama mwenye uhitaji na pichani ni baadhi ya viongozi waliojitokeza kumsaidia mama huyo, kabla ya kushuhudia  zoezi la kusaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa Nyashimo wilayani Busega kati ya MWAUWASA na Mkandarasi Kampuni ya Bennet Contractors kutoka Jijini Mwanza, mradi utakaogharimu shilingi bilioni 1.8 na kuwanufaisha wananchi wa Kata ya Nyashimo.


Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!