Tuesday, August 25, 2020

SIMIYU WAMTUNUKU CHETI ALIYEKUWA RAS KUTAMBUA MCHANGO WAKE KATIKA ELIMU

Uongozi wa Mkoa wa Simiyu umemtunuku cheti cha shukrani aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini ikiwa ni kutambua mchango wake katika kukuza sekta ya elimu katika Mkoa wa Simiyu wakati wa uongozi wake, kabla ya kuteuliwa na Halmashauri Kuu ya CCM kuwa Mgombe wa Ubunge katika Jimbo la Butiama mkoani  Mara. 

Akimkabidhi cheti hicho Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga amesema  uongozi umetoa  cheti hicho kama alama katika kushukuru na  kuthamini mchango wa Ndugu Sagini  katika maendeleo ya sekta ya elimu na mkoa wa Simiyu kwa ujumla.

“Tunakutakia kila la heri na tunaahidi kuwa tutaendelea kuishi ndoto na dhamira ulizoshiriki kuzitengeneza ukiwa na Mkuu wetu wa mkoa Mhe. Anthony Mtaka ili kuhakikisha elimu inasonga mbele na mkoa wa Simiyu unakuwa nambari moja katika kila eneo,” alisema Bi. Mmbaga.

Akipokea cheti hicho aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amewashukuru viongozi wa mkoa kwa kutambua mchango wake huku akibainisha kuwa wakati wa uongozi wake kama msimamizi mkuu wa utekelezaji wa yale waliyokuwa wakikubaliana alipata ushirikiano kutoka kwa viongozi na watendaji kuanzia ngazi ya mkoa hadi wilaya.

“ Ninawashukuru sana viongozi wa mkoa mkiongozwa na kiongozi Mkuu Mhe. Mkuu wa Mkoa kwa kutambua mchango wangu, nimefarijika kuona mimi nilipotoka Simiyu kwenda kwenye shughuli za kisiasa, yale tuliyopanga kama mkoa yametimia maana mwaka juzi tulishika nafasi ya kumi, mwaka jana tukabaki hapo lakini mwaka huu nasikia mmeshika nafasi ya tatu hongereni sana, natamani lengo la kushika nafasi ya kwanza litimie,” alisema Sagini.

Aidha, Sagini ameomba Mkoa wa Simiyu ukubali kuwa marafiki wa Wilaya ya Butiama na Mkoa wa Mara kwa ujumla,  ili kuendeleza ushirikiano kati ya wilaya na mikoa jirani; huku akitoa wito kwa viongozi wa mkoa wa Simiyu kukubali na kutoa ushirikiano pale watu wa Butiama na Mara watakapohitaji kujifunza na kupata uzoefu kutoka kwao.

Jumanne Sagini aliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu mwishoni  mwa mwezi Aprili mwaka 2016 na aliachia nafasi hiyo Julai 03 mwaka huu baada ya kuanza kushiriki mchakato wa kugombea ubunge katika Jimbo la Butiama ambapo amepewa  ridhaa na Chama Cha Mapinduzi kupeperusha bendera ya Chama hicho katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2020.

MWISHO

Aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw.Jumanne Sagini (kulia) akipokea cheti maalum kutoka  Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga ambacho kimetolewa  Agosti 24, 2020 na uongozi wa mkoa kwa lengo la kutambua mchango wake katika kukuza sekta ya elimu mkoani Simiyu wakati wa uongozi wake, ambapo kwa sasa ameteuliwa na Halmashauri Kuu ya CCM  Taifa kuwa Mgombea wa Ubunge Jimbo la Butiama kupitia CCM.

Aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw.Jumanne Sagini akionesha cheti  maalum kilichotolewa  Agosti 24, 2020 na uongozi wa mkoa kwa lengo la kutambua mchango wake katika kukuza sekta ya elimu mkoani Simiyu wakati wa uongozi wake, ambapo kwa sasa ameteuliwa an Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kuwa Mgombea wa Ubunge Jimbo la Butiama kupitia CCM.

Aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw.Jumanne Sagini na mkewe Bi. Mariam Sagini wakiwa na cheti maalum kilichotolewa Agosti 24, 2020 kwa ndugu Sagini na uongozi wa mkoa wa Simiyu kwa lengo la kutambua mchango wake katika kukuza sekta ya elimu mkoani Simiyu wakati wa uongozi wake, ambapo kwa sasa ameteuliwa an Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kuwa Mgombea wa Ubunge Jimbo la Butiama kupitia CCM.

Aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw.Jumanne Sagini (kulia) akipokea cheti maalum kutoka  Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga ambacho kimetolewa  Agosti 24, 2020 na uongozi wa mkoa kwa lengo la kutambua mchango wake katika kukuza sekta ya elimu mkoani Simiyu wakati wa uongozi wake, ambapo kwa sasa ameteuliwa an Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kuwa Mgombea wa Ubunge Jimbo la Butiama kupitia CCM.

Aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw.Jumanne Sagini (aliyeshika cheti) akifurahia jambo mara baada ya kupokea cheti maalum kutoka  Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga ambacho kimetolewa  Agosti 24, 2020 na uongozi wa mkoa kwa lengo la kutambua mchango wake katika kukuza sekta ya elimu mkoani Simiyu wakati wa uongozi wake, ambapo kwa sasa ameteuliwa  na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kuwa Mgombea wa Ubunge Jimbo la Butiama kupitia CCM.

Aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw.Jumanne Sagini  akifurahia jambo na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu  mara baada ya kupokea cheti maalum kutoka  Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga ambacho kimetolewa  Agosti 24, 2020 na uongozi wa mkoa kwa lengo la kutambua mchango wake katika kukuza sekta ya elimu mkoani Simiyu wakati wa uongozi wake, ambapo kwa sasa ameteuliwa  na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kuwa Mgombea wa Ubunge Jimbo la Butiama kupitia CCM.

Aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw.Jumanne Sagini  akifurahia jambo na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu  mara baada ya kupokea cheti maalum kutoka  Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga ambacho kimetolewa  Agosti 24, 2020 na uongozi wa mkoa kwa lengo la kutambua mchango wake katika kukuza sekta ya elimu mkoani Simiyu wakati wa uongozi wake, ambapo kwa sasa ameteuliwa  na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kuwa Mgombea wa Ubunge Jimbo la Butiama kupitia CCM.

DARASA LA SABA, KIDATO CHA NNE SIMIYU WAAHIDI KUFUATA NYAYO ZA KIDATO CHA SITA KUBAKI TATU BORA KITAIFA

Wanafunzi wa Darasa la Saba na Kidato cha nne Mkoani Simiyu wameahidi kufuata nyayo za kidato cha Sita kuendelea kufanya vizuri katika mitihani yao ya Kitaifa na kubaki katika nafasi tatu bora Kitaifa kama walivyofanya Kidato cha Sita mwaka 2020 ambapo mkoa umekuwa wa tatu kati ya mikoa 29.

Hayo yamesemwa na baadhi ya wanafunzi wa darasa la saba shule ya msingi Somanda (B ) na kidato cha nne kutoka Shule ya sekondari Simiyu (Bariadi) waliowawakilisha wenzao katika hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihani wa kidato cha sita iliyofanyika24 Agosti 2020 Mjini Bariadi

“Tunawapongeza dada na kaka zetu  kidato cha sita kwa kufanya vizuri kwenye mtihani wao wa taifa tunaahidi kufanya vizuri kama wao;Shule yetu ya msingi Somanda B ina mkakati wa kuingia katika shule kumi bora kitaifa na kutoa wanafunzi wanne katika wanafunzi kumi bora Kitaifa,tunaahidi hatutawaangusha,”alisema Ezra Paulo mwanafunzi wa darasa la saba Somanda.

“ Matokeo ya Kidato cha Sita yametuhamasisha kujipanga zaidi kwa mwaka 2020, kupitia fursa mbalimbali ambazo tunapewa na viongozi wetu zikiwemo kambi za kitaaluma tunapata fursa ya kujisomea zaidi kuliko tukikaa majumbani, tunaahidi kufanya vizuri zaidi ya dada na kaka zetu walivyofanya ikizingatiwa kuwa shule yetu inabeba jina la mkoa,” Sarah Ndamo kutoka Simiyu Sekondari.

Kwa upande wake mwanafunzi Benard S. Benard kutoka shule ya sekondari Binza wilayani Maswa ambaye amepata daraja la kwanza pointi nne, amewaasa wanafunzi wenzake kuongeza bidii katika masomo kushirikiana na kuutumia vizuri muda wanaokuwa shuleni ili waweze kufikia malengo yao.

Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari Bariadi, Mwl. Ally Simba amesema siri kubwa ya wanafunzi wa shule hiyo kufanya vizuri zaidi na kuifanya kuwa ya kwanza kimkoa na ya 24 Kitaifa ni kufanya mitihani ya mara kwa mara huku akibainisha kuwa wamejipanga kuwa katika shule kumi bora Kitaifa na kuibadilisha shule hiyo ili iwe miongoni mwa shule maalum nchini.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe. Festo Kiswaga amesema siri kubwa ya kufanya vizuri ni mikakati iliyowekwa na mkoa pamoja na utekelezaji wake ikiwa ni pamoja na kuwajengea wanafunzi uwezo wa kujiamini huku akisisitiza kila mdau atimize wajibu wake ili mkoa uendelee kufanya vizuri.

Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju amesema mkoa umetimiza azma yake ya kutoka nafasi ya 10 mwaka 2019 na kuingia nafasi ya  tatu Kitaifa mwaka 2020 na kuongeza ufaulu kutoka GPA ya 3.0443 kufikia  2.894; huku akishauri kuwa ili Simiyu iendelee kufanya vizuri zaidi ni vema  ufundishaji makini uimarishwe zaidi..

Jumla ya wanafunzi 955 walisajiliwa kufanya mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita mwaka 2020 mkoani Simiyu, kati yao wanafunzi watano hawakufanya mtihani na katika wanafunzi 950 waliofanya mtihani, wanafunzi 208 wamepata daraja la kwanza,  507 wamepata daraja la pili, 228  daraja la tatu,  wanafunzi 06 wamepata daraja la nne  na mmoja amepata daraja sifuri.

Pamoja na kutoa shilingi laki moja kwa kila alama A iliyopatikana kwenye somo lake mwalimu aliyefanya vizuri,wanafunzi wawili waliopata daraja la kwanza pointi nne wamepewa shilingi laki mbili kila mmoja;  Mkoa pia umetambua mchango wa aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini  katika kukuza sekta ya elimu kwa kumtunuku cheti.

MWISHO


Mkuu wa Wilaya ya Bariadi. Mhe. Festo Kiswaga akimkabidhi zawadi ya shilingi laki tano Mkuu wa Shule ya sekondari Bariadi, Mwl. Ally Simba iliyotolewa kama pongezi kwa shule hiyo kushika nafasi ya kwanza kati ya shule 10 mkoani Simiyu na ambayo imeshika nafasi ya 24 Kitaifa kati ya shule zaidi ya 500, katika hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihani wa kidato cha sita ambapo mkoa wa Simiyu umeshika nafasi ya tatu Kitaifa.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi. Mhe. Festo Kiswaga akimkabidhi zawadi Mwanafunzi Benard S Benard .kutoka Shule ya Sekondari Binza wilayani Maswa aliyepata daraja la kwanza pointi nne, wakati wa hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2020 ambapo mkoa wa Simiyu umeshika nafasi ya tatu Kitaifa, iliyofanyika Agosti 24, 2020 Mjini Bariadi.


Mkuu wa Wilaya ya Bariadi. Mhe. Festo Kiswaga akimkabidhi zawadi Mwanafunzi Mussa Abdallah kutoka Shule ya Sekondari Bariadi wilayani Bariadi aliyepata daraja la kwanza pointi nne, wakati wa hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2020 ambapo mkoa wa Simiyu umeshika nafasi ya tatu Kitaifa, iliyofanyika Agosti 24, 2020 Mjini Bariadi.

Baadhi ya viongozi katika idara ya elimu, walimu, wanafunzi na wadau wa elimu wakifuatilia matukio mbalimbali katika hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2020 ambapo mkoa wa Simiyu umeshika nafasi ya tatu Kitaifa, iliyofanyika Agosti 24, 2020 Mjini Bariadi.

Baadhi ya wanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Somanda B Mjini Bariadi wakieleza malengo yao katika kufikia nafasi ya kwanza kitaifa katika Mtihani wao wa Taifa, katika hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2020 ambapo mkoa wa Simiyu umeshika nafasi ya tatu Kitaifa, iliyofanyika Agosti 24, 2020 Mjini Bariadi.
Kutoka kulia ni mwanafunzi Mussa Abdallah kutoka shule ya sekondari Bariadi, wilayani Bariadi na Benard Benard kutoka shule ya sekondari Binza wilayani Maswa waliofanya vizuri katika mtihani wa kidato cha sita kwa kupata “division one’ ya  pointi nne kila mmoja , wakiwa katika hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2020 ambapo mkoa wa Simiyu umeshika nafasi ya tatu Kitaifa, iliyofanyika Agosti 24, 2020 Mjini Bariadi.

Mkuu wa Shule ya Sekondari ya wasichana Maswa, Mwl. Kuyunga Jackson akieleza jambo katika hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2020 ambapo mkoa wa Simiyu umeshika nafasi ya tatu Kitaifa, iliyofanyika Agosti 24, 2020 Mjini Bariadi.

Shekhe wa mkoa wa Simiyu, Mahamoud Kalokola akieleza jambo katika hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2020 ambapo mkoa wa Simiyu umeshika nafasi ya tatu Kitaifa, iliyofanyika Agosti 24, 2020 Mjini Bariadi.


Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga akieleza jambo katika hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2020 ambapo mkoa wa Simiyu umeshika nafasi ya tatu Kitaifa, iliyofanyika Agosti 24, 2020 Mjini Bariadi.

Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Somanda Bw. Timotheo Alfred akieleza jambo katika hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2020 ambapo mkoa wa Simiyu umeshika nafasi ya tatu Kitaifa, iliyofanyika Agosti 24, 2020 Mjini Bariadi.

Katibu wa CCM Mkoa wa Simiyu, Bi. Haula Kachwamba  akieleza jambo katika hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2020 ambapo mkoa wa Simiyu umeshika nafasi ya tatu Kitaifa, iliyofanyika Agosti 24, 2020 Mjini Bariadi.

Baadhi ya viongozi kutoka katika Vyombo vya Ulinzi na Usalama mkoa wa Simiyu wakifuatilia matukio mbalimbali katika hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2020 ambapo mkoa wa Simiyu umeshika nafasi ya tatu Kitaifa, iliyofanyika Agosti 24, 2020 Mjini Bariadi.

Mkuu wa Wilaya ya Maswa, mhe. Aswege Kaminyoge akieleza jambo katika hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2020 ambapo mkoa wa Simiyu umeshika nafasi ya tatu Kitaifa, iliyofanyika Agosti 24, 2020 Mjini Bariadi.

Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt. Joseph Chilongani  akieleza jambo katika hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2020 ambapo mkoa wa Simiyu umeshika nafasi ya tatu Kitaifa, iliyofanyika Agosti 24, 2020 Mjini Bariadi.


Baadhi  ya wanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari ya Simyu Mjini Bariadi, wakieleza malengo yao katika kufikia nafasi ya kwanza kitaifa katika Mtihani wao wa Taifa, katika hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2020 ambapo mkoa wa Simiyu umeshika nafasi ya tatu Kitaifa, iliyofanyika Agosti 24, 2020 Mjini Bariadi.

Mmoja wa walimu katika shule ya sekondari ya wasichana Maswa akipokea zawadi kutoka Mkuu wa Wilaya ya Bariadi. Mhe. Festo Kiswaga katika hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2020 ambapo mkoa wa Simiyu umeshika nafasi ya tatu Kitaifa, iliyofanyika Agosti 24, 2020 Mjini Bariadi.

Baadhi ya walimu, wanafunzi na wadau wa elimu wakifuatilia matukio mbalimbali katika hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2020 ambapo mkoa wa Simiyu umeshika nafasi ya tatu Kitaifa, iliyofanyika Agosti 24, 2020 Mjini Bariadi.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi. Mhe. Festo Kiswaga akimkabidhi zawadi Mwalimu wa Somo la Kiswahili katika shule ya sekondari Bariadi, Mwl. Makame S. Makame kutokana na yeye kufanya vizuri katika somo lake, katika hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihani wa kidato cha sita ambapo mkoa wa Simiyu umeshika nafasi ya tatu Kitaifa, iliyofanyika Agosti 24, 2020 Mjini Bariadi.

Baadhi ya viongozi katika idara ya elimu, walimu, wanafunzi na wadau wa elimu wakifuatilia matukio mbalimbali katika hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2020 ambapo mkoa wa Simiyu umeshika nafasi ya tatu Kitaifa, iliyofanyika Agosti 24, 2020 Mjini Bariadi.



Mkuu wa Wilaya ya Bariadi. Mhe. Festo Kiswaga akimkabidhi zawadi mmoja wa walimu kutoka shule ya sekondari Bariadi , katika hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihani wa kidato cha sita ambapo mkoa wa Simiyu umeshika nafasi ya tatu Kitaifa, iliyofanyika Agosti 24, 2020 Mjini Bariadi.

Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Tanzania mkoa wa Simiyu, Mwl. Kulwa Dwese akieleza jambo katika hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2020 ambapo mkoa wa Simiyu umeshika nafasi ya tatu Kitaifa, iliyofanyika Agosti 24, 2020 Mjini Bariadi.

Mkuu wa Shule ya Sekondari Bariadi mkoani Simiyu, Mwl. Ally Simba akieleza jambo katika hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2020 ambapo mkoa wa Simiyu umeshika nafasi ya tatu Kitaifa, iliyofanyika Agosti 24, 2020 Mjini Bariadi.

Kutoka kushoto Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Afisa Elimu wa Mkoa, Mwl. Ernest Hinju na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga wakiteta jambo kabla ya kukabidhi zawadi kwa walimu na wanafunzi, katika hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2020 ambapo mkoa wa Simiyu umeshika nafasi ya tatu Kitaifa, iliyofanyika Agosti 24, 2020 Mjini Bariadi.

Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe. Benson Kilangi  akieleza jambo katika hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2020 ambapo mkoa wa Simiyu umeshika nafasi ya tatu Kitaifa, iliyofanyika Agosti 24, 2020 Mjini Bariadi.

Baadhi ya wanafunzi wa shule za sekondari wilayani Bariadi wakifuatilia matukio mbalimbali katika hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2020 ambapo mkoa wa Simiyu umeshika nafasi ya tatu Kitaifa, iliyofanyika Agosti 24, 2020 Mjini Bariadi.

Baadhi ya Makatibu Tawala wa Wilaya mkoa wa Simiyu wakiteta jambo katika hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2020 ambapo mkoa wa Simiyu umeshika nafasi ya tatu Kitaifa, iliyofanyika Agosti 24, 2020 Mjini Bariadi.

Baadhi ya wanafunzi wa shule za  msingi wilayani Bariadi wakifuatilia matukio mbalimbali katika hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2020 ambapo mkoa wa Simiyu umeshika nafasi ya tatu Kitaifa, iliyofanyika Agosti 24, 2020 Mjini Bariadi.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga(kushoto) akipokea cheti cha shukrani kwa naiba ya aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini kwa kutambua mchango wake katika kuinua kiwango cha elimu mkoa wa Simiyu wakati wa uongozi wake, katika hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2020 ambapo mkoa wa Simiyu umeshika nafasi ya tatu Kitaifa, iliyofanyika Agosti 24, 2020 Mjini Bariadi


Thursday, August 13, 2020

DC MASWA AZINDUA KAMPUNI ITAKAYOSIMAMIA VIWANDA VYA HALMASHAURI

Mkuu wa wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu, Mhe. Aswege Kaminyoge amezindua bodi ya Kampuni ya Ng'hami (Ng'hami Industries Company Ltd), ambayo iko chini ya Halmashauri ya wilaya ya Maswa itakayoendesha viwanda vinavyomilikiwa na halmashauri hiyo.

Akizindua bodi ya wakurugenzi wa kampuni hiyo jana katika ukumbi wa Halmashauri ya Maswa mkuu huyo wa wilaya amesema uzinduzi wa bodi hiyo unaashiria utekelezaji wa dhamira njema ya kuwa na viwanda vya kimkakati ndani na nje ya Mkoa wa Simiyu.

Kaminyoge amesema matokeo ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati kwa sekta ya viwanda Wilayani Maswa yameanza kuonekana dhahiri kwa vitendo na kukuza uchumi wa wananchi wao kwa ujumla.

Bodi hiyo itasimamia viwanda vitano ambavyo ni kiwanda cha kusindika Unga lishe wa viazi,Kiwanda cha Chaki,Kiwanda cha vifungashio ,kiwanda cha unga wa gypsum na cha kutenga madaraja ya mchele.

MWISHO










WORLD VISION YATOA MSAADA WA VITANDA NA MAGODORO SIMIYU SEKONDARI

Shirika lisilokuwa la kiserikali la World Vision Tanzania limekabidhi vitanda 100 na magodoro 100 katika shule ya sekondari Simiyu wenye thamani ya shilingi milioni 26.6.

Akikabidhi msaada huo kaimu meneja wa klasta ya Nzega, Bi. Gilselda Balyagati  amesema kuwa shirika hilo limeamua kuunga jitihada za serikali ya awamu ya tano za kuhakikisha watoto wanapata elimu bora ngazi ya shule ya Msingi na sekondari ambapo kupitia mradi wa Kanadi  limeweza kupata fedha kiasi za kusapoti ununuzi wa vitanda na magodoro kwa wanafunzi wa bweni hasa wasichana ili kuwawezesha kusoma katika mazingira bora.

Aidha, Balyagati amesema kuwa lengo la kutoa msaada huo ni kuchangia na kusaidia juhudi za kuwalinda wasichana dhidi ya vishawishi na mapambano dhidi ya ndoa na mimba za utotoni, huku akibainisha kuwa katika mkoa wa Simiyu shirika hilo lina miradi 5 kwenye  afya na maji.

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka  mara baada ya kupokea msaada huo na kuukabidhi kwenye uongozi wa shule ya Sekondari Simiyu, Mkuu wa wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga ameishukuru World Vision kwa msaada huo na kuwataka  wanafunzi kutumia msaada huo wa  magodoro na vitanda kuongeza ari ya kujisomea na baadaye waweze kufikia malengo yao.

 

Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga  Afisa wa Mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju amesema vitanda hivyo vitasaidia kuboresha mazingira ya kujisomea kwa wanafunzi kwa kuwa shule hiyoimeteuliwa kama kituo cha kambi za kitaaluma.

Hinju ameongeza  kuwa kupitia juhudi serikali ya mkoa na wadau watoto wameweza kukaa kambi  na hivyo kupata muda wa kutosha kujisomea na kusaidia kupunguza daraja 0 kwenye matokeo ya kidato cha 4 mwaka 2019 na hatimaye  kwenye mtihani wa taifa na kufanikiwa kuingia kwenye nafasi ya 5 bora kitaifa.

Kwa upande wake mwl wa shule ya Sekondari Simiyu Vestina Sedekia  alilishukuru shirika hilo kwa kutoa msaada huo na kuongeza  kuwa wamewasaidia wanafunzi  hususan wasiokuwa na uwezo wa kuwa nayo.

 "msaada huu ni wa muhimu unakuta familia ina godoro moja la kulalia watoto hata 4 hivyo inakua vigumu mtoto anayetaka kwenda bweni (kambi) kubeba lile godoro na awaache wenzake hawana la kulalia hivyo msaada huo ni wa muhimu "alisema mwl Sedekia

 

 

Wednesday, August 12, 2020

DKT GWAJIMA AAGIZA MIKOA YOTE NCHINI KUFANYA UKAGUZI WA VITUO VYA AFYA

" Mikoa yote fanyeni ukaguzi katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya kama mlivyofanya kwa vichache na mkagundua matatizo mengi kwenye usimamizi wa mfumo wa ugavi na ikaonekana bayana kwamba mkiongeza usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi mnaziba mianya ya watu fulani ambao wanadhani vituo hivyo ni shamba la bibi," 

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima.katika kikao kazi kilichowahusisha Viongozi mbalimbali, wataalam wa afya mkoa wa Simiyu pamoja na baadhi ya wataalam kutoka Wizara ya Afya, katika kikao kazi kilichofanyika Agosti 11, 2020 Mjini Bariadi kwa lengo la kufanya tathmini ya utekelezaji wa ukaguzi wa dawa na mapato katika vituo vya kutolea huduma za afya. 

Aidha, Dkt. Gwajima amesema taarifa ya ukaguzi huo unapaswa kufanyika kila robo inapokamilika na taarifa iwasilishwe wiki mbili baadaye na kufafanua kuwa taarifa ya awali itapokelewa Oktoba 15 baada ya kukamilika kwa robo ya kwanza ya mwezi Juni-Septemba mwaka 2020/2021. 

Ameongeza kuwa ukaguzi huo ufanywe na wataalam waliobobea kwenye masuala ya ukaguzi wakiwemo wakaguzi wa ndani na maafisa ugavi ambapo amesisitiza wataalam hao wawezeshwa kufika katika vituo hivyo na kupata nafasi ya kufanya ukaguzi katika mifumo mbalimbali ya uedneshaji wa vituo hivyo ili waweze kubaini baadhi ya matatizo ya kimifumo pia. 

Katika hatua nyingine Dkt, Gwajima amewataka wakurugenzi wa Halmashauri  kufungua maduka ya dawa jamii katika vituo vya kutolea huduma za afya ili kuongeza hali ya upatikanani wa dawa na mapato. 

Wakati huo huo Dkt. Gwajima ameupongeza mkoa wa Simiyu kwa kufanya vizuri katika eneo la ukaguzi na ufuatiliaji jambo ambalo limechangia kuongeza hali ya upatikanaji wa dawa na mapato ya vituo kuongeza hadi mara tano ya mapato ya awali. 

Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa rai kwa Wafamasia mkoani hapa kujitathmini katika utendaji kazi wao ili kuhakikisha kuwa wanadhibiti matumizi ya dawa na vifaa tiba katika vituo vya kutolea huduma za afya. 

Aidha, Mtaka amesema ni vema viongozi wote katika ngazi ya wilaya na mkoa kuhakikisha anatimiza wajibu wake na katika utoaji wa huduma za afya ndani ya mkoa  ikiwa ni pamoja na kufuatilia taarifa za ukaguzi wa dawa na mapato katika vituo vya kutolea huduma za afya. 

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Festo Dugange amesema katika kipindi cha Januari hadi julai 2020 mkoa huu umefanya ukaguzi katika vituo 42 vya huduma

Kati ya vituo 119 kubaini kasoro mbalimbali ikiwa ni pamoja na ujazaji hafifu wa leja, thamani ya dawa kutoingizwa katika vitabu na kasi ya matukio kukosekana kwa dawa. 

Dkt. Dugange  amemeongeza kuwa baada ya ukaguzi huo kumekuwa na udhibiti wa upotevu wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi, kuongezeka kwa wateja vituoni  na mapato yameonezeka; ambapo mapato ya mwezi Januari kwa vituo 22 yalikuwa shilingingi 37, 349, 762 kabla ya ukaguzi na kufikia 78,778,964 mwezi Julai baada ya ukaguzi. 

Naye Mkaguzi Mkuu wa ndani wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Mika Mollel amesema ili wakaguzi wa ndani waweze kufanya kazi yao vizuri ni vema wakapewa nafasi ya kuingia katika mifumo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mifumo ya dawa na ukusanyaji wa mapato huku akiomba waaajiri kuwawezesha wakaguzi hao kutekeleza majukumu yao. 

Mwenyekiti wa CCM, Mhe. Enock Yakobo ametoa rai kwa Halmashauri zote mkoani Simiyu kuhakikisha kuwa zinakuwa na rekodi sahihi ya dawa na jambo la hali ya upatikanaji wa dawa lijadiliwe katika vikao vya halmashauri na watakaohusika katika upotevu wa dawa na mapato wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria.

 

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na Viongozi mbalimbali, wataalam wa afya mkoa wa Simiyu pamoja na baadhi ya wataalam kutoka Wizara ya Afya, katika kikao kazi kilichofanyika Agosti 11, 2020 Mjini Bariadi kwa lengo la kufanya tathmini ya utekelezaji wa ukaguzi wa dawa na mapato katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akifungua kikao kikao kazi  cha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima, Viongozi mbalimbali, wataalam wa afya mkoa wa Simiyu pamoja na baadhi ya wataalam kutoka Wizara ya Afya,  kilichofanyika Agosti 11, 2020 Mjini Bariadi kwa lengo la kufanya tathmini ya utekelezaji wa ukaguzi wa dawa na mapato katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga akifunga  kikao kikao kazi  cha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima, Viongozi mbalimbali, wataalam wa afya mkoa wa Simiyu pamoja na baadhi ya wataalam kutoka Wizara ya Afya,  kilichofanyika Agosti 11, 2020 Mjini Bariadi kwa lengo la kufanya tathmini ya utekelezaji wa ukaguzi wa dawa na mapato katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Mganga Mkuu wa Mkoa, Dkt. Festo Dugange akionesha cheti alichokabidhiwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI kama pongezi kwa kuwa mkoa wa pili  katika usimamizi wa huduma za afya, katika  kikao kikao kazi  cha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima, Viongozi mbalimbali, wataalam wa afya mkoa wa Simiyu pamoja na baadhi ya wataalam kutoka Wizara ya Afya,  kilichofanyika Agosti 11, 2020 Mjini Bariadi kwa lengo la kufanya tathmini ya utekelezaji wa ukaguzi wa dawa na mapato katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Baadhi ya wajumbe wakifuatilia kikao kikao kazi  cha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima, Viongozi mbalimbali, wataalam wa afya mkoa wa Simiyu pamoja na baadhi ya wataalam kutoka Wizara ya Afya,  kilichofanyika Agosti 11, 2020 Mjini Bariadi kwa lengo la kufanya tathmini ya utekelezaji wa ukaguzi wa dawa na mapato katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Baadhi ya wajumbe wakifuatilia kikao kikao kazi  cha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima, Viongozi mbalimbali, wataalam wa afya mkoa wa Simiyu pamoja na baadhi ya wataalam kutoka Wizara ya Afya,  kilichofanyika Agosti 11, 2020 Mjini Bariadi kwa lengo la kufanya tathmini ya utekelezaji wa ukaguzi wa dawa na mapato katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Simiyu (mbele) na baadhi ya wajumbe wakifuatilia kikao kazi  cha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima, Viongozi mbalimbali, wataalam wa afya mkoa wa Simiyu pamoja na baadhi ya wataalam kutoka Wizara ya Afya,  kilichofanyika Agosti 11, 2020 Mjini Bariadi kwa lengo la kufanya tathmini ya utekelezaji wa ukaguzi wa dawa na mapato katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Mkurugenzi wa Tiba na Kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto akichangia hoja katika kikao kazi  cha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima, Viongozi mbalimbali, wataalam  wa afya mkoa wa Simiyu pamoja na baadhi ya wataalam kutoka Wizara ya Afya,  kilichofanyika Agosti 11, 2020 Mjini Bariadi kwa lengo la kufanya tathmini ya utekelezaji wa ukaguzi wa dawa na mapato katika vituo vya kutolea huduma za afya.
Mkaguzi wa Ndani wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima akichangia hoja katika kikao kazi  cha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima, Viongozi mbalimbali, wataalam  wa afya mkoa wa Simiyu pamoja na baadhi ya wataalam kutoka Wizara ya Afya,  kilichofanyika Agosti 11, 2020 Mjini Bariadi kwa lengo la kufanya tathmini ya utekelezaji wa ukaguzi wa dawa na mapato katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akichangia hoja katika kikao kazi  cha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima, Viongozi mbalimbali, wataalam  wa afya mkoa wa Simiyu pamoja na baadhi ya wataalam kutoka Wizara ya Afya,  kilichofanyika Agosti 11, 2020 Mjini Bariadi kwa lengo la kufanya tathmini ya utekelezaji wa ukaguzi wa dawa na mapato katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, Bi. Elizabeth Gumbo akichangia hoja katika kikao kazi  cha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima, Viongozi mbalimbali, wataalam  wa afya mkoa wa Simiyu pamoja na baadhi ya wataalam kutoka Wizara ya Afya,  kilichofanyika Agosti 11, 2020 Mjini Bariadi kwa lengo la kufanya tathmini ya utekelezaji wa ukaguzi wa dawa na mapato katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Aswege Kaminyoge akichangia hoja katika kikao kazi  cha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima, Viongozi mbalimbali, wataalam  wa afya mkoa wa Simiyu pamoja na baadhi ya wataalam kutoka Wizara ya Afya,  kilichofanyika Agosti 11, 2020 Mjini Bariadi kwa lengo la kufanya tathmini ya utekelezaji wa ukaguzi wa dawa na mapato katika vituo vya kutolea huduma za afya.




Mkaguzi Mkuu wa ndani wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Mika Mollel akichangia hoja katika kikao kazi  cha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima, Viongozi mbalimbali, wataalam  wa afya mkoa wa Simiyu pamoja na baadhi ya wataalam kutoka Wizara ya Afya,  kilichofanyika Agosti 11, 2020 Mjini Bariadi kwa lengo la kufanya tathmini ya utekelezaji wa ukaguzi wa dawa na mapato katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Mkuu wa wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera  akichangia hoja katika kikao kazi  cha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima, Viongozi mbalimbali, wataalam  wa afya mkoa wa Simiyu pamoja na baadhi ya wataalam kutoka Wizara ya Afya,  kilichofanyika Agosti 11, 2020 Mjini Bariadi kwa lengo la kufanya tathmini ya utekelezaji wa ukaguzi wa dawa na mapato katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Mkuu wa wilaya ya Itilima, Mhe. Benson Kilangi  akichangia hoja katika kikao kazi  cha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima, Viongozi mbalimbali, wataalam  wa afya mkoa wa Simiyu pamoja na baadhi ya wataalam kutoka Wizara ya Afya,  kilichofanyika Agosti 11, 2020 Mjini Bariadi kwa lengo la kufanya tathmini ya utekelezaji wa ukaguzi wa dawa na mapato katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Baadhi ya viongozi wakiwa katika kikao kazi cha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima, Viongozi mbalimbali, wataalam  wa afya mkoa wa Simiyu pamoja na baadhi ya wataalam kutoka Wizara ya Afya,  kilichofanyika Agosti 11, 2020 Mjini Bariadi kwa lengo la kufanya tathmini ya utekelezaji wa ukaguzi wa dawa na mapato katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza katika kikao kazi  cha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima, Viongozi mbalimbali, wataalam  wa afya mkoa wa Simiyu pamoja na baadhi ya wataalam kutoka Wizara ya Afya,  kilichofanyika Agosti 11, 2020 Mjini Bariadi kwa lengo la kufanya tathmini ya utekelezaji wa ukaguzi wa dawa na mapato katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!