Tuesday, August 25, 2020

SIMIYU WAMTUNUKU CHETI ALIYEKUWA RAS KUTAMBUA MCHANGO WAKE KATIKA ELIMU

Uongozi wa Mkoa wa Simiyu umemtunuku cheti cha shukrani aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini ikiwa ni kutambua mchango wake katika kukuza sekta ya elimu katika Mkoa wa Simiyu wakati wa uongozi wake, kabla ya kuteuliwa na Halmashauri Kuu ya CCM kuwa Mgombe wa Ubunge katika Jimbo la Butiama mkoani  Mara. 

Akimkabidhi cheti hicho Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga amesema  uongozi umetoa  cheti hicho kama alama katika kushukuru na  kuthamini mchango wa Ndugu Sagini  katika maendeleo ya sekta ya elimu na mkoa wa Simiyu kwa ujumla.

“Tunakutakia kila la heri na tunaahidi kuwa tutaendelea kuishi ndoto na dhamira ulizoshiriki kuzitengeneza ukiwa na Mkuu wetu wa mkoa Mhe. Anthony Mtaka ili kuhakikisha elimu inasonga mbele na mkoa wa Simiyu unakuwa nambari moja katika kila eneo,” alisema Bi. Mmbaga.

Akipokea cheti hicho aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amewashukuru viongozi wa mkoa kwa kutambua mchango wake huku akibainisha kuwa wakati wa uongozi wake kama msimamizi mkuu wa utekelezaji wa yale waliyokuwa wakikubaliana alipata ushirikiano kutoka kwa viongozi na watendaji kuanzia ngazi ya mkoa hadi wilaya.

“ Ninawashukuru sana viongozi wa mkoa mkiongozwa na kiongozi Mkuu Mhe. Mkuu wa Mkoa kwa kutambua mchango wangu, nimefarijika kuona mimi nilipotoka Simiyu kwenda kwenye shughuli za kisiasa, yale tuliyopanga kama mkoa yametimia maana mwaka juzi tulishika nafasi ya kumi, mwaka jana tukabaki hapo lakini mwaka huu nasikia mmeshika nafasi ya tatu hongereni sana, natamani lengo la kushika nafasi ya kwanza litimie,” alisema Sagini.

Aidha, Sagini ameomba Mkoa wa Simiyu ukubali kuwa marafiki wa Wilaya ya Butiama na Mkoa wa Mara kwa ujumla,  ili kuendeleza ushirikiano kati ya wilaya na mikoa jirani; huku akitoa wito kwa viongozi wa mkoa wa Simiyu kukubali na kutoa ushirikiano pale watu wa Butiama na Mara watakapohitaji kujifunza na kupata uzoefu kutoka kwao.

Jumanne Sagini aliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu mwishoni  mwa mwezi Aprili mwaka 2016 na aliachia nafasi hiyo Julai 03 mwaka huu baada ya kuanza kushiriki mchakato wa kugombea ubunge katika Jimbo la Butiama ambapo amepewa  ridhaa na Chama Cha Mapinduzi kupeperusha bendera ya Chama hicho katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2020.

MWISHO

Aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw.Jumanne Sagini (kulia) akipokea cheti maalum kutoka  Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga ambacho kimetolewa  Agosti 24, 2020 na uongozi wa mkoa kwa lengo la kutambua mchango wake katika kukuza sekta ya elimu mkoani Simiyu wakati wa uongozi wake, ambapo kwa sasa ameteuliwa na Halmashauri Kuu ya CCM  Taifa kuwa Mgombea wa Ubunge Jimbo la Butiama kupitia CCM.

Aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw.Jumanne Sagini akionesha cheti  maalum kilichotolewa  Agosti 24, 2020 na uongozi wa mkoa kwa lengo la kutambua mchango wake katika kukuza sekta ya elimu mkoani Simiyu wakati wa uongozi wake, ambapo kwa sasa ameteuliwa an Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kuwa Mgombea wa Ubunge Jimbo la Butiama kupitia CCM.

Aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw.Jumanne Sagini na mkewe Bi. Mariam Sagini wakiwa na cheti maalum kilichotolewa Agosti 24, 2020 kwa ndugu Sagini na uongozi wa mkoa wa Simiyu kwa lengo la kutambua mchango wake katika kukuza sekta ya elimu mkoani Simiyu wakati wa uongozi wake, ambapo kwa sasa ameteuliwa an Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kuwa Mgombea wa Ubunge Jimbo la Butiama kupitia CCM.

Aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw.Jumanne Sagini (kulia) akipokea cheti maalum kutoka  Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga ambacho kimetolewa  Agosti 24, 2020 na uongozi wa mkoa kwa lengo la kutambua mchango wake katika kukuza sekta ya elimu mkoani Simiyu wakati wa uongozi wake, ambapo kwa sasa ameteuliwa an Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kuwa Mgombea wa Ubunge Jimbo la Butiama kupitia CCM.

Aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw.Jumanne Sagini (aliyeshika cheti) akifurahia jambo mara baada ya kupokea cheti maalum kutoka  Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga ambacho kimetolewa  Agosti 24, 2020 na uongozi wa mkoa kwa lengo la kutambua mchango wake katika kukuza sekta ya elimu mkoani Simiyu wakati wa uongozi wake, ambapo kwa sasa ameteuliwa  na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kuwa Mgombea wa Ubunge Jimbo la Butiama kupitia CCM.

Aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw.Jumanne Sagini  akifurahia jambo na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu  mara baada ya kupokea cheti maalum kutoka  Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga ambacho kimetolewa  Agosti 24, 2020 na uongozi wa mkoa kwa lengo la kutambua mchango wake katika kukuza sekta ya elimu mkoani Simiyu wakati wa uongozi wake, ambapo kwa sasa ameteuliwa  na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kuwa Mgombea wa Ubunge Jimbo la Butiama kupitia CCM.

Aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw.Jumanne Sagini  akifurahia jambo na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu  mara baada ya kupokea cheti maalum kutoka  Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga ambacho kimetolewa  Agosti 24, 2020 na uongozi wa mkoa kwa lengo la kutambua mchango wake katika kukuza sekta ya elimu mkoani Simiyu wakati wa uongozi wake, ambapo kwa sasa ameteuliwa  na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kuwa Mgombea wa Ubunge Jimbo la Butiama kupitia CCM.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!