Friday, August 7, 2020

SERIKALI YAANDAA MFUMO MAALUM KUWASAIDIA WAJASIRIAMALI

Katika kuwawezesha wanawake na vijana katika sekta ya biashara serikali imesema imeandaa mfuko maalum utakaowasaidia wajasiriamali wanaopata mafunzo katika taasisi mbalimbali kama SIDO na VETA kwa kuwapa mikopo ya mtaji 

Hayo yamebainishwa na waziri wa viwanda na biashara, Mhe. Innocent Bashungwa kwenye kongamano la biashara na kilimo biashara kwa wanawake na vijana mkoani Simiyu lililofanyika Agosti 05, 2020 katika Viwanja vya nanenane Nyakabindi Bariadi Simiyu.

Waziri Bashungwa amesema serikali inafanya kila jitihada kuwawezesha wanawake na vijana kwani wanatambua kuwa nguvu kazi kubwa ya taifa inatokana na makundi hayo.

Katika hatua nyingine Bashungwa amewaagiza katibu mkuu wa wizara ya viwanda na biashara na kushirikiana na wa wizara ya kilimo kuhakikisha kliniki ya biashara inayotembea kufanya kazi kwa ufanisi.

Kwa upande wake Dkt Never Zehaya kutokana chuo Kikuu cha Nelson Mandela aliyegundua viuatilifu vya wadudu wahalibifu wanaoshambulia mazao mbalimbali ya wakulima ameiomba serikali kupunguza uagizaji wa dawa hizo nje ya nchi na badala yake kununua zinazotengenezwa nchino lengo likiwa ni kuwapa nguvu na uwezo wa uzalishaji mkubwa.

 Ombi hilo alilitolewa wakati mawaziri wawili walipotembelea banda lake akiwemo wa viwanda na biashara Innocent Bashungwa na wa kilimo Japhet Hasunga lililopo kwenye maonesho ya nane nane kitaifa Nyakabindi mjini Bariadi mkoani Simiyu.

 Dkt Zehaya kuliko serikali kutumia fedha nyingi kuagiza viuatilifu nje ya nchi ambavyo mara nyingi vimekuwa vikiripotiwa na kulalamikiwa na wakulima kutoua wadudu hao waharibifu bora kutumia vya ndani ambavyo amesema havina gharama kubwa na vinafanya vizuri shambani.

 Aidha ameongeza kuwa serikali ikiwezesha dawa za ndani za kuulia wadudu waharibifu sambamba na kuhakikisha kunakuwa na soko la uhakika itawasaidia kuzalisha kwa wingi hatua itakayowawezesha kukuza uchumi wao na taifa kwa ujumla.

 "badala ya kuagiza viuatilifu (madawa za kuulia wadudu ) ambazo zimejaa kemikali na bado kuna wakati haziui wadudu ni vyema ipunguze kuagiza nje badala yake inunue nchini kwani dawa za ndani ni nzuri na zinaua wadudu"alisema Dkt Zehaya.

MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!