Sunday, August 2, 2020

MAVUNDE AAGIZA HALMASHAURI KUTENGA MAENEO KWA SHUGHULI ZA UZALISHAJI ZA VIJANA, WANAWAKE

 Naibu Waziri ofisi ya waziri mkuu kazi, vijana na ajira Mhe. Anthony Mavunde ameziagiza halmashauri zote nchini kutenga maeneo maalum kwa ajili ya shughuli za uzalishaji mali kwa vijana na wanawake..

Naibu Waziri Mavunde ameyasema hayo Agosti 02, 2020 ambayo imetengwa maalum kwa ajili ya kuhamasisha Program ya Kilimo awamu ya pili (ASDP II) baada ya kutembelea mabanda ya maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2020,  katika viwanja vya Nyakabindi Bariadi mkoani Simiyu.

“Mhe. Waziri Mkuu wa awamu ya tatu alitoa maelekezo ya kutenga maeneo hayo, awamu ya nne akaja Mzee Pinda Novemba 2014 likaja azimio la kila mkoa kutenga maeneo maalum kwa ajili ya shughuli za uzalishaji mali kwa vijana na wanawake, mpaka sasa zimetengwa hekari 203,000 tu ambazo bado hazitoshi kulingana na ukubwa wa nchi yetu,” alisema Mavunde

Naibu waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu kazi, vijana na ajira Mhe. Anthony Mavunde( wa tatu kushoto) akiwa na viongozi wengine wakiangalia moja ya teknolojia ya uoteshaji wa mimea pasipo kutumia udongo Agosti 02, 2020 wakati alipotembeela mabanda mbalimbali ya maonesho katika  maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2020,  katika viwanja vya Nyakabindi Bariadi mkoani Simiyu.
HABARI KATIKA PICHA MHE. MAVUNDE AKIWA AMEONGOZA NA VIONGOZI WENGINE ALIPOTEMBELEA MABANDA MBALIMBALI KATIKA MAONESHO YA NANENANE KITAIFA 2020 NYAKABINDI BARIADI SIMIYU. AIDHA ZIPO PICHA ZA MIFUGO NA MAJENGO MBALIMBALI ALIYOYATEMBELEA. PIA TAZAMA PICHA ZA KATIBU TAWALA WA MKOA SIMIYU, BI. MIRIAM MMBAGA AKITEMBELEA MABANDA MBALIMBALI  
















0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!