Saturday, August 29, 2020

WASTAAFU WAWAASA WATUMISHI WA UMMA KUMTANGULIZA MUNGU, KUWA WAADILIFU NA KUJITUMA

Wastaafu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu wamewaasa watumishi wa umma kumtanguliza Mungu, kuwa waadilifu na kujituma ili waweze kutimiza wajibu wao sawa sawa kwa maslahi yao binafsi na Taifa kwa ujumla. 

Hayo yamebainishwa na Bw. Elias Kasuka ambaye kwa sasa amestaafu utumishi wa umma akiwa kama Afisa Kilimo Mkuu baada ya kutumika kwa miaka 35 na Bw. Godfrey Machumu ambaye kwa sasa  amestaafu utumishi wa umma akiwa kama Mhasibu  Mkuu baada ya kutumika kwa miaka 37 katika Hafla fupi ya kuwapongeza wastaafu  hao wa mwaka 2019/2020 iliyofanyika Agosti 28, 2020 Mjini Bariadi. 

“Katika Utumishi wa Umma hampashwi kukata tamaa, binafsi nimeanzia mbali nikajiendeleza sikujali umri wangu, kikubwa ni kumtanguliza Mwenyezi Mungu katika kazi zenu mtafanikiwa tu,” alisema Bw. Godfrey Machumu. 

“Siri kubwa ya kufikia mpaka kustaafu kwangu ni kufanya kazi kwa bidii na uadilifu, nilifanya kazi bila kusukumwa mfano mzuri ni kwa namna nilivyoshiriki kuandaa Maonesho ya nanenane mwaka 2018 na 2019 ; pia nawashauri mheshimu wakubwa kwa wadogo,” alisema Bw. Elias Kasuka. 

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi.Miriam Mmbaga amewapongeza wastaafu hao kwa utumishi uliotukuka mpaka kufikia kustaafu huku akitoa wito kwa watumishi wengine kuiga mema waliyojifunza kupitia utumishi wa wastaafu hao ikiwa ni pamoja na kuona umuhimu wa kujiendeleza kielimu wakiwa kazini na kujiendeleza kimaisha. 

Katika hatua nyingine Bi. Mmbaga amewaasa watumishi kuishi na watu wote vizuri huku akisisitiza umuhimu wa kuacha alama katika kazi zao wanazofanya  ili hata watakapo staafu wakumbukwe kwa alama walizoacha kwenye maeneo waliyofanyia kazi.

MWISHO

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga akimkabidhi cheti cha Utumishi uliotukuka Bw. Elias Kasuka ambaye kwa sasa amestaafu utumishi wa umma akiwa kama Afisa Kilimo Mkuu baada ya kutumika kwa miaka 35, katika Hafla fupi ya kuwapongeza wastaafu kwa mwaka 2019/2020 iliyofanyika Agosti 28, 2020 Mjini Bariadi, kushoto ni Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya utawala na Rasilimaliwatu Bw. Ekwabi Mujungu.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga akimkabidhi cheti cha Utumishi uliotukuka Bw. Godfrey Machumu ambaye kwa sasa amestaafu utumishi wa umma akiwa kama Mhasibu  Mkuu baada ya kutumika kwa miaka 37, katika Hafla fupi ya kuwapongeza wastaafu kwa mwaka 2019/2020 iliyofanyika Agosti 28, 2020 Mjini Bariadi.
Bw. Godfrey Machumu(wa pili kulia) ambaye kwa sasa  amestaafu utumishi wa umma akiwa kama Mhasibu  Mkuu baada ya kutumika kwa miaka 37,akionesha cheti cha utumishi uliotukuka alichokabidhiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu(wa pili kushoto) katika Hafla fupi ya kuwapongeza wastaafu kwa mwaka 2019/2020 iliyofanyika Agosti 28, 2020 Mjini Bariadi.

Bw. Elias Kasuka  ambaye kwa sasa  amestaafu utumishi wa umma akiwa kama Afisa Kilimo Mkuu  baada ya kutumika kwa miaka 35,akionesha cheti cha utumishi uliotukuka alichokabidhiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu(wa pili kushoto) katika Hafla fupi ya kuwapongeza wastaafu kwa mwaka 2019/2020 iliyofanyika Agosti 28, 2020 Mjini Bariadi.
Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya utawala na Rasilimaliwatu Bw. Ekwabi Mujungu akitoa maelezo mafupi kuhusu wastaafu wawili Bw. Elias Kasuka  ambaye kwa sasa  amestaafu utumishi wa umma akiwa kama Afisa Kilimo Mkuu  baada ya kutumika kwa miaka 35 na Bw. Godfrey Machumu ambaye kwa sasa amestaafu utumishi wa umma akiwa kama Mhasibu  Mkuu baada ya kutumika kwa miaka 37, katika Hafla fupi ya kuwapongeza wastaafu hao wa mwaka 2019/2020 iliyofanyika Agosti 28, 2020 Mjini Bariadi.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga akizungumza na watumishi wa Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Simiyu katika kikao chake na watumishi hao ambacho kilitumika kama sehemu ya kuwapongeza wastaafu wawili Bw. Elias Kasuka  ambaye kwa sasa  amestaafu utumishi wa umma akiwa kama Afisa Kilimo Mkuu  baada ya kutumika kwa miaka 35 na Bw. Godfrey Machumu ambaye kwa sasa amestaafu utumishi wa umma akiwa kama Mhasibu  Mkuu baada ya kutumika kwa miaka 37, kilichofanyika Agosti 28, 2020 Mjini Bariadi.
Kutoka kushoto Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya utawala na Rasilimaliwatu Bw. Ekwabi Mujungu, :- Bw. Elias Kasuka  ambaye kwa sasa  amestaafu utumishi wa umma akiwa kama Afisa Kilimo Mkuu  baada ya kutumika kwa miaka 35, Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga na Bw. Godfrey Machumu ambaye kwa sasa amestaafu utumishi wa umma akiwa kama Mhasibu  Mkuu baada ya kutumika kwa miaka 37, wakiagana baada ya Hafla fupi ya kuwapongeza wastaafu hao wa mwaka 2019/2020 iliyofanyika Agosti 28, 2020 Mjini Bariadi.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga (katikati kwa walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na Bw. Elias Kasuka  (wa pili kushoto walioketi) ambaye kwa sasa  amestaafu utumishi wa umma akiwa kama Afisa Kilimo Mkuu  baada ya kutumika kwa miaka 35, Bw. Godfrey Machumu (wa pili kulia) ambaye kwa sasa amestaafu utumishi wa umma akiwa kama Mhasibu  Mkuu baada ya kutumika kwa miaka 37 na mkewe pamoja na watumishi wengine wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, baada ya Hafla fupi ya kuwapongeza wastaafu hao wa mwaka 2019/2020 iliyofanyika Agosti 28, 2020 Mjini Bariadi.

Kutoka kushoto Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya utawala na Rasilimaliwatu Bw. Ekwabi Mujungu,  Bw. Elias Kasuka  ambaye kwa sasa  amestaafu utumishi wa umma akiwa kama Afisa Kilimo Mkuu  baada ya kutumika kwa miaka 35, Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga na Bw. Godfrey Machumu ambaye kwa sasa amestaafu utumishi wa umma akiwa kama Mhasibu  Mkuu baada ya kutumika kwa miaka 37, katika picha ya pamoja baada ya Hafla fupi ya kuwapongeza wastaafu hao wa mwaka 2019/2020 iliyofanyika Agosti 28, 2020 Mjini Bariadi.

Kutoka kushoto Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Uchumi na Uzalishaji, Dkt. Gamitwe Mahaza,  Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya utawala na Rasilimaliwatu Bw. Ekwabi Mujungu,  Bw. Elias Kasuka  ambaye kwa sasa  amestaafu utumishi wa umma akiwa kama Afisa Kilimo Mkuu  baada ya kutumika kwa miaka 35, Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga na Bw. Godfrey Machumu ambaye kwa sasa amestaafu utumishi wa umma akiwa kama Mhasibu  Mkuu baada ya kutumika kwa miaka 37 na Mhasibu Mkuu wa Mkoa, Bw. Francis Makombe  katika picha ya pamoja baada ya Hafla fupi ya kuwapongeza wastaafu hao wa mwaka 2019/2020 iliyofanyika Agosti 28, 2020 Mjini Bariadi.

Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya utawala na Rasilimaliwatu Bw. Ekwabi Mujungu(kulia) akiteta jambo na Bw. Godfrey Machumu ambaye kwa sasa amestaafu utumishi wa umma akiwa kama Mhasibu  Mkuu baada ya kutumika kwa miaka 37 baada ya Hafla fupi ya kuwapongeza wastaafu  wa mwaka 2019/2020 iliyofanyika Agosti 28, 2020 Mjini Bariadi.

Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya utawala na Rasilimaliwatu Bw. Ekwabi Mujungu akitoa maelezo mafupi kuhusu wastaafu wawili Bw. Elias Kasuka  ambaye kwa sasa  amestaafu utumishi wa umma akiwa kama Afisa Kilimo Mkuu  baada ya kutumika kwa miaka 35 na Bw. Godfrey Machumu ambaye kwa sasa amestaafu utumishi wa umma akiwa kama Mhasibu  Mkuu baada ya kutumika kwa miaka 37, katika Hafla fupi ya kuwapongeza wastaafu hao wa mwaka 2019/2020 iliyofanyika Agosti 28, 2020 Mjini Bariadi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga akimkabidhi zawadi ya shilingi 1,000,000/= kwa  Utumishi uliotukuka Bw. Godfrey Machumu ambaye kwa sasa amestaafu utumishi wa umma akiwa kama Mhasibu  Mkuu baada ya kutumika kwa miaka 37, katika Hafla fupi ya kuwapongeza wastaafu kwa mwaka 2019/2020 iliyofanyika Agosti 28, 2020 Mjini Bariadi.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga akimkabidhi zawadi ya shilingi 1,000,000/= kwa  Utumishi uliotukuka Bw. Elias Kasuka ambaye kwa sasa amestaafu utumishi wa umma akiwa kama Mhasibu  Mkuu baada ya kutumika kwa miaka 37, katika Hafla fupi ya kuwapongeza wastaafu kwa mwaka 2019/2020 iliyofanyika Agosti 28, 2020 Mjini Bariadi.

Bw. Elias Kasuka  ambaye kwa sasa  amestaafu utumishi wa umma akiwa kama Afisa Kilimo Mkuu  baada ya kutumika kwa miaka 35,akionesha cheti cha utumishi uliotukuka alichokabidhiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu(katikati) katika Hafla fupi ya kuwapongeza wastaafu kwa mwaka 2019/2020 iliyofanyika Agosti 28, 2020 Mjini Bariadi.

Bw. Elias Kasuka  ambaye kwa sasa  amestaafu utumishi wa umma akiwa kama Afisa Kilimo Mkuu  baada ya kutumika kwa miaka 35, akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya kupokea zawadi ya  cheti cha utumishi uliotukuka na fedha taslimu shilingi 1,000,000/=kutoka kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu(wa pili kushoto) katika Hafla fupi ya kuwapongeza wastaafu kwa mwaka 2019/2020 iliyofanyika Agosti 28, 2020 Mjini Bariadi.

Bw. Godfrey Machumu  ambaye kwa sasa  amestaafu utumishi wa umma akiwa kama Mhasibu Mkuu  baada ya kutumika kwa miaka 37, akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya kupokea zawadi ya  cheti cha utumishi uliotukuka na fedha taslimu shilingi 1,000,000/=kutoka kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu(wa pili kushoto) katika Hafla fupi ya kuwapongeza wastaafu kwa mwaka 2019/2020 iliyofanyika Agosti 28, 2020 Mjini Bariadi.
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu wakifuatilia maelezo mafupi ya wastaafu Bw. Godfrey Machumu  ambaye kwa sasa  amestaafu utumishi wa umma akiwa kama Mhasibu Mkuu  baada ya kutumika kwa miaka 37 na Bw. Elias Kasuka  ambaye kwa sasa  amestaafu utumishi wa umma akiwa kama Afisa Kilimo Mkuu  baada ya kutumika kwa miaka 35, katika Hafla fupi ya kuwapongeza wastaafu hao wa mwaka 2019/2020 iliyofanyika Agosti 28, 2020 Mjini Bariadi.
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu wakifuatilia maelezo mafupi ya wastaafu Bw. Godfrey Machumu  ambaye kwa sasa  amestaafu utumishi wa umma akiwa kama Mhasibu Mkuu  baada ya kutumika kwa miaka 37 na Bw. Elias Kasuka  ambaye kwa sasa  amestaafu utumishi wa umma akiwa kama Afisa Kilimo Mkuu  baada ya kutumika kwa miaka 35, katika Hafla fupi ya kuwapongeza wastaafu hao wa mwaka 2019/2020 iliyofanyika Agosti 28, 2020 Mjini Bariadi.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga (katikati kwa walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na Bw. Elias Kasuka  (wa pili kushoto walioketi) ambaye kwa sasa  amestaafu utumishi wa umma akiwa kama Afisa Kilimo Mkuu  baada ya kutumika kwa miaka 35, Bw. Godfrey Machumu (wa pili kulia) ambaye kwa sasa amestaafu utumishi wa umma akiwa kama Mhasibu  Mkuu baada ya kutumika kwa miaka 37 na mkewe pamoja na watumishi wengine wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, baada ya Hafla fupi ya kuwapongeza wastaafu hao wa mwaka 2019/2020 iliyofanyika Agosti 28, 2020 Mjini Bariadi.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga (katikati kwa walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na Bw. Elias Kasuka  (wa pili kushoto walioketi) ambaye kwa sasa  amestaafu utumishi wa umma akiwa kama Afisa Kilimo Mkuu  baada ya kutumika kwa miaka 35, Bw. Godfrey Machumu (wa pili kulia) ambaye kwa sasa amestaafu utumishi wa umma akiwa kama Mhasibu  Mkuu baada ya kutumika kwa miaka 37 na mkewe pamoja na watumishi wengine wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, baada ya Hafla fupi ya kuwapongeza wastaafu hao wa mwaka 2019/2020 iliyofanyika Agosti 28, 2020 Mjini Bariadi.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!