Saturday, August 29, 2020

SIMIYU YAAHIDI KUSHIRIKI KIKAMILIFU MAULIDI YA KITAIFA MWAKA 2020 MKOANI KAGERA

Mkoa wa Simiyu umeahidi kushiriki kikamilifu katika maandalizi ya Maulidi ya Kitaifa inayotarajia kufanyika Oktoba mkoani Kagera. 

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Tawala wa mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga Agosti 28, 2020 wakati akizungumza na baadhi ya viongozi wa BAKWATA wa Mikoa ya Simiyu na Kagera waliomtembelea ofisini kwake kwa lengo la kuomba ushirikiano na mkoa wa Simiyu kushiriki katika kufanikisha Maulidi hiyo.

“Tumelipokea jambo hili kwa mikono miwili na tunaahidi kulifanyia kazi kwa wepesi kwa kushirikiana na viongozi, ninaomba kupitia Katibu wa BAKWATA  wa Mkoa wetu tutakaa pamoja tuone namna tutakavyolitekeleza na baadaye tutalifanyia maamuzi ndani ya muda mfupi tu ili maandalizi yaendelee,” alisema Bi. Mmbaga.

Kwa upande wake Sheikh wa Mkoa wa Kagera, Haruna Kichwabuta amesema ili sherehe ya Maulidi Kitaifa iweze kufanikiwa inahitaji ushirikiano wa Viongozi wa mikoa jirani jambo ambalo limekuwa likifanyika wakati wote huku akisisitiza kuwa anashukuru mkoa wa Simiyu kuonesha utayari wa kushiriki kufanikisha siku hiyo.

“Tumetoka Kagera tukiwa na Baraka zote za Mhe. Mkuu wa Mkoa wetu na alituhakikishia kuwa ameshawasiliana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Simiyu hivyo tunategemea kupata ushirikiano kutoka Simiyu kwa kuwa sisi ni mikoa jirani, kama mlivyoshiriki mwaka jana  kupitia kwa Mhe. Mkuu wa Mkoa Mhe. Mtaka Mkoani Mwanza naamini hata mwaka huu tutakuwa pamoja ,” alisema Sheikh Kichwabuta.

MWISHO

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga (kulia) akizungumza na baadhi ya viongozi wa BAKWATA mkoa wa Simiyu na Kagera ambao wamemtembelea ofisini kwake kwa lengo la kuomba ushirikiano na mkoa wa Simiyu katika kufanikisha  maandalizi ya Maulidi ya Kitaifa inayotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 2020 mkoani Kagera.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga ( wa pili kulia) akifurahia jambo na Sheikh wa Mkoa wa Simiyu, Mahamoud Kalokola mara baada ya mazungumzo kati yake na viongozi wa BAKWATA  wa Mikoa ya Simiyu na Kagera yaliyolenga kuomba ushirikiano na mkoa wa Simiyu katika kufanikisha  maandalizi ya Maulidi ya Kitaifa inayotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 2020 mkoani Kagera.

Sheikh wa Mkoa wa Simiyu, Mahamoud Kalokola akitoa taarifa ya utangulizi kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga (kushoto)  juu ya ujumbe wa viongozi wa BAKWATA  wa Mikoa ya Simiyu na Kagera uliofika ofisini kwake kuomba ushirikiano na mkoa wa Simiyu katika kufanikisha  maandalizi ya Maulidi ya Kitaifa inayotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 2020 mkoani Kagera.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa BAKWATA mkoa wa Simiyu na Kagera mara baada ya mazungumzo kati yake na viongozi hao na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu yaliyolenga kuomba ushirikiano na mkoa wa Simiyu katika kufanikisha  maandalizi ya Maulidi ya Kitaifa inayotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 2020 mkoani Kagera.

Sheikh wa mkoa wa Kagera, Haruna Kichwabuta akisalimiana na Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju mara baada ya mazungumzo kati ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga na viongozi wa BAKWATA  wa Mikoa ya Simiyu na Kagera yaliyolenga kuomba ushirikiano na mkoa wa Simiyu katika kufanikisha  maandalizi ya Maulidi ya Kitaifa inayotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 2020 mkoani Kagera.

Baadhi ya viongozi wa BAKWATA  wa Mikoa ya Simiyu na Kagera wakiwa ofisini kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu kwa ajili ya mazungumzo yaiyolenga kuomba ushirikiano na mkoa wa Simiyu katika kufanikisha  maandalizi ya Maulidi ya Kitaifa inayotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 2020 mkoani Kagera.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga (kulia) akizungumza na baadhi ya viongozi wa BAKWATA mkoa wa Simiyu na Kagera ambao wamemtembelea ofisini kwake kwa lengo la kuomba ushirikiano na mkoa wa Simiyu katika kufanikisha  maandalizi ya Maulidi ya Kitaifa inayotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 2020 mkoani Kagera.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!