Mkuu wa mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony John Mtaka amehimiza wataalam wa uvuvi kuanzisha mradi wa ufugaji wa samaki katika mabwawa ili kuwahakikishia wananchi wa mkoa wa Simiyu upatikanaji wa
kitoweo pamoja na kutoa fursa ya ajira kwa vijana.
Mkuu wa Mkoa ametoa kauli
hiyo katika kikao alichofanya kati ya viongozi wa taasisi za serikali, binafsi,
timu za menejimenti za Mamlaka za Serikali za Mitaa (CMT), viongozi wa dini,
vyama vya siasa na wadau wengine wa maendeleo kilichofanyika mwanzoni wa wiki
hii, katika ukumbi wa K.K.K.T Bariadi.
Alisema Ofisi yake
itatafuta wataalam wa ufugaji wa samaki kutoka chuo cha Ukiriguru cha jijini
Mwanza ambao watafanya tathmini na kutoa ushauri wa kitaalamu ili kufanikisha
lengo hilo.
“Hatuwezi kuendelea
kutegemea samaki kutoka sehemu nyingine wakati tuna mabwawa katika mkoa wetu
ambayo yanafaa kabisa kwa ufugaji wa samaki na kuwaongezea fursa ya ajira
vijana wetu,” alisema Mtaka.
Baadhi ya viongozi
walioshiriki kikao hicho walisema watamuunga mkono Mkuu huyo wa mkoa kwa
kuwahamasisha vijana kushirikiana na Serikali katika kutekeleza mradi huo.
0 comments:
Post a Comment