Baadhi
ya wanachi Wilaya ya Maswa wakimsikiliza : Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika
viwanja vya Modeco wilayani humo.
|
Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula akisalimiana
na Mbunge wa Maswa Magharibi Mhe.Mashimba Ndaki mara baada ya kuwasili katika
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
|
Mwenyekiti
wa Baraza la Ardhi la Wilaya ya Maswa, Mhe. Mdimi Ilanga akitoa ufafanuzi wa
masaula mbalimbali yanayohusu baraza hilo katika kikao kilichofanyika Ofisi ya
Mkuu wa Wilaya ya Maswa
|
Na Stella Kalinga
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula amemtaka
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Dkt. Fredrick Sagamiko
kutoa hati miliki za viwanja kwa wakazi wa wilaya hiyo ndani ya siku 90 (hadi
kufikia tarehe 15 Februari, 2017 )
Mhe. Mabula aliyasema hayo jana alipozungumza na wananchi wa Wilaya ya Maswa katika Mkutano
wa Hadhara uliofanyika katika uwanja wa Modeco akiwa katika ziara yake wilayani
humo akitokea wilayani Bariadi
Mhe. Mabula amesema wananchi walio na Matoleo
ya Viwanja (Letter of offer) waliyopewa awali wawasilishe katika Ofisi ya
Mkurugenzi Mtendaji, ili wapatiwe hati miliki ambazo zitawasaidia kuwahakikishia
usalama wa nyumba zao kwa kupunguza hatari ya kutokea kwa migogoro isiyo ya
lazima.
Aidha,
Mhe.Mabula amesema wananchi watakapopata hati miliki hizo zitawasaidia kujikwamua
kiuchumi katika kupata mikopo ya Benki na Taasisi nyingine za kifedha kama
dhamana yao.
Kwa
upande wake Mbunge wa Maswa Magharibi Mhe.Mashimba Ndaki amesema pamoja na
Halmashauri kutoa hati hizo baadhi ya wananchi wana hati za kimila ambazo
zimekuwa zikikataliwa katika baadhi ya Taasisi
za kifedha hivyo aliomba Mhe. Naibu waziri awasaidie wananchi hao.
Akitoa
ufafanuzi juu ya suala hilo Mhe.Mabula amesema Hati za Kimila ni halali na kuna
taasisi takribani saba zinazopokea hati hizo ambapo aliahidi kuwa Wizara ya
Ardhi inaendelea kufanya mazungumzo na Taasisi nyingine za kifedha ili ziweze kuzitambua.
Wakati
huo huo Mhe. Mabula amesema Halmashauri ihakikishe inapima maeneo yote Taasisi
za Serikali na kutoa hati miliki kwa taasisi hizo ili kuepuka uvamizi
utakaopelekea migogoro katika Serikali na wananchi.
Naibu
Waziri aliongeza kuwa baada ya kupima maeneo hayo ya Taasisi za Serikali Wenyeviti
wa mitaa na vijiji wapewe ramani za maeneo
husika ili wayalinde dhidi ya uvamizi na ujenzi holela.
Sambamba
na hilo Mhe. Mabula amesema Wizara yake kwa kushirikiana na Halmashauri
itaandaa utaratibu wa kuyajengea uwezo mabaraza ya Vijiji na Kata ili yashughulikie
vema mashauri mbalimbali ya Ardhi kwa wakati na kuepuka kuliongezea mzigo
Baraza la Ardhi la Wilaya.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi la Maswa, Mhe. Mdimi Ilanga alisema
amekuwa akipokeabaadhi ya kesi ambazo zingeweza
kufanyiwa kazi na Mabaraza ya kata hivyo endapo wajumbe wa mabaraza hayo watajengewa
uwezo watasaidia kushughulikia kesi hizo.
Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula amemaliza
ziara yake ya siku mbili mkoani Simiyu ambapo alitembelea Wilaya ya Busega,
Bariadi na Maswa na kuzungumza na Watalaam wa Ardhi wa mkoa huo, kutembelea
maeneo ambayo Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) linatarajia kujenga nyuma na
kuzungumza na wananchi kupitia mikutano ya hadhara.
0 comments:
Post a Comment