Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa amesema Serikali
inatarajia kuzindua rasmi mfuko wa watu wenye ulemavu ambao utakuwa ukishughulikia
masuala mbalimbali ya watu wenye ulemavu ikiwemo kutoa ruzuku kwa vyama vya
watu wenye ulemavu.
Mhe. Ikupa ameyasema hayo wakati akizungumza na
viongozi na watendaji wa Serikali na
watu wenye ulemavu wakati akiwa katika ziara ya kikazi wilayani humo,
Februari 26,2019.
Amesema taratibu zote zimekamilika na sasa iko
katika hatua za mwisho ili mfuko huo uweze kuzinduliwa huku akibainisha kuwa
Baraza la Ushauri kwa watu wenye Ulemavu Taifa nalo litazinduliwa hivi karibuni
kwa kuwa tayari Mwenyekiti wa Baraza hilo ameshateuliwa na Rais wa Tanzania,
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
“Tayari tumeshapata Mwenyekiti wa lile Baraza la
Ushauri kwa watu wenye ulemavu ambaye ameteuliwa na Mhe. Rais na tunaamini muda
si mrefu lile baraza litazinduliwa na litaendelea kufanya kazi kwa mujibu wa
sheria” alisema Naibu Waziri Ikupa.
Katika hatua nyingine Mhe. Ikupa amepongeza viongozi
wa Wilaya ya Meatu kwa namna wanavyoshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu
na wakati huo huo akawapongeza watu wenye ulemavu wilayani humo kutumia vema
fedha za mikopo wanazopata kutokana asilimia mbili za mapato ya ndani ya
Halmashauri kwa kuanzisha shughuli za ujasiriamali.
Aidha, ametoa wito kwa watu wenye ulemavu kujitokeza
kwa wingi kuomba mikopo hiyo ambayo haina riba ili waweze kuanzisha shughuli za
ujasiriamali zitakazowasaidia kujikwamua kiuchumi na kuondokana na utegemezi.
Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt. Joseph Chilongani amesema
Halmashauri ya Wilaya hiyo imetenga takribani shilingi milioni Sabini kwa ajili
ya kuwawezesha kiuchumi watu wenye ulemavu na akatoa wito kwao kujitokeza
kuomba mikopo ili iwasaidie kuanzisha shughuli za kuwaingizia kipato.
Kwa upande wao watu wenye ulemavu wameiomba Serikali
kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kusaidia katika utatuzi wa changamoto
mbalimbali zinazowakabili ikiwa ni pamoja na ukosefu vifaa saidizi kwa watu
wenye ulemavu na kutengeneza mazingira wezeshi shuleni kwa wanafunzi wenye
ulemavu.
“ Tunaomba Serikali yetu kwa kushirikiana na wadau
itusaidie kupata nyenzo saidizi kama fimbo nyeupe kwa wasioona, viungo bandia
na baiskeli za miguu mitatu kwa walemavu wa viungo” alisema Ndimila Luyoja
Katibu wa SHIVYAWATA wilaya ya Meatu.
“ Tunaomba vifaa saidizi vya kukuza maandishi kwa
wanafunzi wenye ualbino na pia walimu
wawape nafasi ya kukaa mbele madarasani ili waweze kuona vizuri kama wanafunzi
wengine kwa sababu wasipopata nafasi hiyo watashindwa kuona vizuri ubaoni
kutokana na wao kuwa na uoni hafifu”Mwenyekiti wa Chama cha Watu wenye ualbino
Meatu.
Naye Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Festo
Kiswaga amesema Serikali mkoani humo itaendelea kutoa kipaumbele kwa watu wenye
uelemavu ambapo amesema wataendelea kujumuishwa katika agenda ya ujenzi wa
uchumi wa viwanda kufikia uchumi wa kati mkoani humo.
Akiwa Wilayani Meatu, Mhe. Naibu Waziri amezungumza
na viongozi, watu wenye ulemavu, kuona kazi mbalimbali za watu wenye ulemavu na
kutembelea mradi wa Kitalu nyumba ili kujionea utekelezaji wake.
MWISHO
Naibu Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella
Ikupa(katikati) akizungumza na viongozi na watendaji wa Wilaya ya Meatu pamoja
na watu wenyeulemavu wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi wilayani humo,
Februari 26, 2019.
Naibu Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa(wa
tatu kulia) akiangalia baadhi ya kazi za wajasiriamali wenye ulemavu , wakati
akiwa katika ziara yake ya kikazi wilayani humo, Februari 26, 2019.
Naibu Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella
Ikupa(aliyeshika mkeka kushoto) akiangalia baadhi ya kazi za wajasiriamali
wenye ulemavu , wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi wilayani humo,
Februari 26, 2019.
Mkuu wa Wilaya ya
Meatu, Mhe. Dkt. Joseph Chilongani akimkaribisha Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa mara baada
ya kuwasili Mjini Mwanhuzi Meatu wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi wilayani
humo, Februari 26, 2019.
Mwenyekiti wa
SHIVYAWATA Wilaya ya Meatu ambaye pia ni
mlemavu wa macho, Bw. Charles Hilu akiwasilisha changamoto za watu wenye
ulemavu kwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa (wa pili
kulia) wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi wilayani humo, Februari 26,
2019.
Baadhi ya watoto wenye
ulemavu wa kusikia wilayani Meatu wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella
Ikupa(hayupo pichani) kwa usaidizi wa Mkalimani wa lugha ya alama, wakati wa ziara ya kikazi ya kiongozi huyo wilayani
humo, Februari 26, 2019.
Naibu Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa
akitoka katika Kitalu Nyumba(Green House)
kilichopo Mwanhuzi Wilayani Meatu mara baada ya kukikagua, wakati akiwa katika ziara yake ya
kikazi wilayani humo, Februari 26, 2019.
Afisa Kilimo wa Wilaya
ya Meatu Bw. Thomas Shilabu akitoa maelezo juu ya mfumo wa umwagiliaji uliowekwa katika Mradi wa Kitalu nyumba
(green house) unaotekelezwa na Vijana ;
kwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu
wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi wilayani
humo, Februari 26, 2019.
Mbunge wa Viti maalum
Mkoa wa Simiyu (CCM) Mhe. Leah Komanya akizungumza katika kikao cha Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe.
Stella Ikupa na viongozi wa Wilaya ya Meatu, wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu
Waziri huyo wilayani humo, Februari 26,
2019.
Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Mhe. Pius Machungwa akizungumza katika kikao
cha Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye
Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa na viongozi wa Wilaya ya Meatu na watu wenye
ulemavu, wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo wilayani humo, Februari 26, 2019.
Baadhi ya Viongozi na
watu wenye ulemavu wilayani Meatu wakiwa katika kikao na Naibu Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa ,
wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo
wilayani humo, Februari 26, 2019.
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka, ambaye
ni Mkuu wa Wilaya ya Bariadi , Mhe. Festo Kiswaga akizungumza na viongozi wa
wilaya ya Meatu na baadhi ya watu wenye ulemavu katika kikao cha Naibu Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella
Ikupa , wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo wilayani humo, Februari 26, 2019.
Baadhi
ya Viongozi na watu wenye ulemavu wilayani Meatu wakiwa katika kikao na Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe.
Stella Ikupa , wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo wilayani humo, Februari 26, 2019
Baadhi ya Viongozi na
watu wenye ulemavu wilayani Meatu wakiwa katika Kitalu nyumba kilichopo
Mwanhuzi wakati Naibu Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa alipotembelea kujionea utekelezaji wa Mradi
wa Kitalu Nyumba katika ziara ya kikazi wilayani humo, Februari 26, 2019.
Naibu Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa
(katikati) akizungumza naviongozi wa Wilaya ya Meatu, mara baada ya kuwasili
wilayani humo kwa ziara ya kikazi, Februari 26, 2019.
0 comments:
Post a Comment