Saturday, May 9, 2020

WORLD VISION YAKABIDHI VIFAA VYA KUJIKINGA NA CORONA SIMIYU


Shirika lisilo la kiserikali la World Vision limekabidhi msaada wa vifaa vya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona pamoja na Jengo la zahanati kwa uongozi wa mkoa wa Simiyu vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 95.7.

Akikabidhi msaada huo jana Mei 08, 2020 kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini katika kijiji cha Wigelekelo wilayani Maswa, Meneja wa World Vision Kanda ya Ziwa, Bw. John Massenza amesema pamoja na zahanati wamekabidhi mipira ya kuvaa mikononi, vitakasa mikono,vipaza sauti, barako na mavazi maalum ya wataalam wa afya.

"Pamoja na zahanati leo tunakabidhi mipira ya kuvaa mikononi boksi 500,vitakasa mikono lita 200,vipaza sauti 26 kwa wahudumu wa afya ngazi za jamii na mavazi  ya kujikinga na maambukizi 60 na barakoa aina ya N95, vyote vikiwa na thamani ya shilingi 95,755,000/=, "alisema Massenza.

Aidha, ameongeza kuwa shirika hilo kwa kushirikiana na ofisi ya mganga mkuu wa mkoa wa Simiyu na waganga wakuu wa wilaya litaendelea kutoa misaada ya vifaa , vitendea kazi, kutoa mafunzo kwa watumishi wa afya na kuhakikisha wanasambaza elimu ya kujikinga na ugonjwa wa homa ya mapafu (COVID 19) inayosababishwa na virusi vya Corona. .

" Shirika limeendelea kutoa elimu ya kujikinga na ugonjwa wa homa ya mapafu  kwa njia ya matangazo na tumewezesha mafunzo kwenye makundi tofauti ya watu ambayo yatasambaza elimu hii kwa jamii mfano wa makundi hayo ni viongozi wa dini,wahudumu wa afya ,viongozi wa  serikali,  "alisema Massenza.

Akipokea vifaa hivyo pamoja na zahanati Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw Jumanne Sagini ameishukuru World Vision kwa msaada huo ambao umetolewa kwa Halmashauri zote sita pamoja na kuwa  shirika hilo linafanya kazi na halmashauri ya wilaya ya Maswa na Itilima; huku akibainisha kuwa vifaa kinga hivyo vitawajengea ujasiri watoa huduma za afya kuwahudumia watakaobainika kuwa na maambukizi ya Virusi vya Corona.

Naye mganga mkuu wa mkoa wa Simiyu,Dkt.Festo Dugange amesema wamekuwa wakitekeleza afua mbalimbali za kuhakikisha wananchi wanakuwa salama dhidi ya ugonjwa wa COVID 19  kwa kutoa elimu ya namna ya kujikinga, huku akiongeza kuwa mkoa upo vizuri na tayari umeshatenga vituo endapo watapatikana washukiwa wa ugonjwa huo.

Akiongea kwa niaba ya wakurugenzi wa halmashauri mkurugenzi mtendaji wa  halmashauri ya wilaya ya Maswa, Dkt. Frederick Sagamiko amelishukuru shirika hilo kwa kuwa msaada mkubwa kwenye shughuli za maendeleo mkoani hapo hususani katika wilaya ya Itilima na Maswa ambapo kwa Maswa mbali na kuwajengea zahanati pia limesaidia katika ujenzi wa kiwanda cha viazi lishe na wilaya ya Itilima kiwanda cha sabuni.

Kwa upande wao wananchi wa kijiji cha Wigelekelo wakiwemo Mbuke Kemakema na Mashauri Ngeme wamelipongeza shirika hilo kwa ujenzi wa zahanati ambayo itawasaidia kupata huduma za afya karibu  kwani awali walikuwa wakitembea umbali mrefu kufuata huduma za afya.
MWISHO



:- Meneja wa World Vision Kanda ya Ziwa, Bw. John Massenza akimkabidhi Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini(kulia) baadhi ya mabosi yenye mipira ya kuvaa mikononi inayotumiwa na watoa huduma za afya ambayo ni sehemu ya vifaa kinga vilivyotolewa msaada na Shirika lisilo la Kiserikali la World Vision kwa Mkoa wa Simiyu kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona, makabidhiano hayo yamefanyika katika kijiji cha Wigelekelo wilayani Maswa, Mei 08, 2020.

Meneja wa World Vision Kanda ya Ziwa, Bw. John Massenza akitoa maelezo kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini(kulia) kuhusu mavazi maalum kwa watoa huduma yatakayovaliwa wakati wa kuwahudumia watakaobainika kuwa na maambukizi ya Corona ikiwa ni sehemu ya vifaa kinga vilivyotolewa msaada na Shirika lisilo la Kiserikali la World Vision kwa Mkoa wa Simiyu kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona, makabidhiano hayo yamefanyika katika kijiji cha Wigelekelo wilayani Maswa, Mei 08, 2020.
 

Meneja wa World Vision Kanda ya Ziwa, Bw. John Massenza akimkabidhi kipaza sauti Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini(kulia) ambavyo vitatumiwa na watoa huduma ngazi ya jamii kutoa eleimu kwa wananchi ikiwa ni sehemu ya msaada na Shirika lisilo la Kiserikali la World Vision kwa Mkoa wa Simiyu kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona, makabidhiano hayo yamefanyika katika kijiji cha Wigelekelo wilayani Maswa, Mei 08, 2020.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini  akiangalia moja ya vitakasa mikono vilivyotolewa na Shirika lisilo la Kiserikali la World Vision kwa Mkoa wa Simiyu kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona, katika  makabidhiano yaliyofanyika katika kijiji cha Wigelekelo wilayani Maswa, Mei 08, 2020.
 
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini  akiwa na viongozi wengine wakitoka kukagua jengo la zahanati ya Wigelekelo iliyojengwa na Shirika lisilo la Serikali la World Vision kwa kushitrikiana na wananchi na kukabidhiwa kwa serikali Mei 08, 2020 Wilayani Maswa.

 Sehemu ya mbele ya jengo la zahanati ya Wigelekelo iliyojengwa na Shirika lisilo la Serikali la World Vision kwa kushitrikiana na wananchi na kukabidhiwa kwa serikali Mei 08, 2020 Wilayani Maswa.


Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini  (kulia) na Meneja wa World Vision Kanda ya Ziwa, Bw. John Massenza wakisaini hati za makabidhiano ya msaada wa  zahanati pamoja na vifaa kinga  dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona vilivyotolewa na Shirika lisilo la Serikali la World Vision kwa Mkoa wa Simiyu katika Kijiji cha Wigelekelo wilayani Maswa, Mei 08, 2020.
 Mganga mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Festo Dugange akizungumza kabla ya kumkaribisha Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini kutoa salamu za mkoa wakati wa makabidhiano ya msaada wa  zahanati pamoja na vifaa kinga  dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona vilivyotolewa na Shirika lisilo la Serikali la World Vision kwa Mkoa wa Simiyu katika Kijiji cha Wigelekelo wilayani Maswa, Mei 08, 2020.


Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini  akiwa na viongozi wengine katika ukaguzi wa jengo la zahanati ya Wigelekelo iliyojengwa na Shirika lisilo la Serikali la World Vision kwa kushitrikiana na wananchi na kukabidhiwa kwa serikali Mei 08, 2020 Wilayani Maswa.
 
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akimuuliza jambo Meneja wa World Vision Kanda ya Ziwa, Bw. John Massenza baada ya kukabidhiwa vifaa kinga  vilivyotolewa na Shirika lisilo la Kiserikali la World Vision kwa Mkoa wa Simiyu kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona, katika  makabidhiano yaliyofanyika katika kijiji cha Wigelekelo wilayani Maswa, Mei 08, 2020.


Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akipewa maelezo juu ya vifaa kinga  vilivyotolewa na Shirika lisilo la Kiserikali la World Vision kwa Mkoa wa Simiyu kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona, katika  makabidhiano yaliyofanyika katika kijiji cha Wigelekelo wilayani Maswa, Mei 08, 2020.
 

Baadhi ya vifaa kinga vilivyotolewa msaada kwa mkoa wa Simiyu Simiyu kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona, katika  makabidhiano yaliyofanyika katika kijiji cha Wigelekelo wilayani Maswa, Mei 08, 2020.





Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akipokea maelezo kutoka kwa Meneja wa World Vision Kanda ya Ziwa, Bw. John Massenza baada ya kukabidhiwa vifaa kinga  vilivyotolewa na Shirika lisilo la Kiserikali la World Vision kwa Mkoa wa Simiyu kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona, katika  makabidhiano yaliyofanyika katika kijiji cha Wigelekelo wilayani Maswa, Mei 08, 2020. 

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!