Wednesday, June 10, 2020

MRAJIS AWATAKA MAAFISA USHIRIKA KUIMARISHA USIMAMIZI WA VYAMA VYA USHIRIKA


Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania Bara, Dkt. Benson Ndiege amewataka Maafisa Ushirika kuimarisha usimamizi katika vyama vya ushirika ili kuhakikisha vyama hivyo vinatekeleza majukumu yake kwa uadilifu na kuzingatia sheria, kanuni na taratibu mbalimbali za ushirika.

Dkt. Ndiege ametoa agizo hilo wakati akizungumza na maafisa ushirika wa mkoa wa Simiyu katika kikao kilichofanyika mjini Bariadi wakati wa ziara yake ya siku moja mkoani Simiyu Juni 09, 2020.

“Wekeni mpango wa kuvitembelea vyama vya ushirika ili kuona shughuli zinazofanyika na kuweka usimamizi imara ili kuondoa dhana ya kufanya uchunguzi, ni bora kugundua tatizo kabla halijatokea na kulidhibiti kuliko kusubiri litokee na kuanza kuchukua hatua,” alisema Dkt. Ndiege.

Aidha, Dkt. Ndiege amewasisitiza Maafisa ushirika kufuatilia makusanyo ya mfuko wa usimamizi na ukaguzi kutoka Vyama vya Ushirika ili kupata fedha za kusimamia Vyama hivyo, huku akiwahakikishia kuwa fedha zote za makusanyo zitaendelea kuletwa kwao ili waongeze usimamizi na kuimarisha Ushirika.

Wakati huo huo Dkt. Ndiege ameitaka  Bodi ya Chama Kikuu cha Ushirika cha Mkoa wa Simiyu (SIMCU) kuhakikisha inaweka mipango madhubuti ya utoaji huduma kwa vyama vya msingi vya ushirika(AMCOS) na kuvisimamia kwa ukaribu zaidi na kuhakikisha vinatekeleza majukumu inavyopaswa.

Katika hatua nyingine Dkt.Ndiege ametoa wito kwa Bodi ya chama Kikuu cha ushirika mkoa wa Simiyu (SIMCU) na Chama Kikuu cha Ushirika Shinyanga (SHIRECU)  kufanya maridhiano juu ya mgawanyo wa mali ili kuendeleza uwekezaji katika mali hizo, ikiwemo viwanda vya kuchambua pamba vya Luguru, Sola na Malampaka vilivyopo Simiyu.

Mwenyekiti wa Bodi wa SIMCU Bw. Emanuel Mwerere amesema kuwa makubaliano ya mgawanyo wa mali yamechelewa kutokana na  wanachama wa SIMCU kupitia Mkutano Mkuu kukubali kupokea mali pekee kutoka SHIRECU na hawakuwa tayari  kupokea madeni, huku akibainisha kuwa hawakuchukua viwanda hivyo kwa ajili ya kukwepa hasara katika uendeshaji kutokana na hali ya viwanda hivyo ilivyo kwa sasa ambayo hairidhishi.

Kwa upande wake Mrajisi Msaidizi wa Mkoa Bw. Ibrahim Kadudu kupitia taarifa ya Ushirika ya Mkoa amesema Vyama vya Ushirika vya pamba Mkoani humo vinakabiliwa na changamoto ya malipo ya ushuru kiasi cha shilingi bilioni 3.9 na bado wakulima zaidi ya 11,047 wanadai fedha zao za pamba kiasi cha shilingi bilioni 3.4.

Naye Meneja wa Bariadi Teachers SACCOS Bw. Nchimbi Yahya akiwasilisha taarifa kwa Mrajis ameomba  fedha za akiba za wanachama wao zinazoshikiliwa na Wakurugenzi wa Halmashauri ziweze kurejeshwa, ambapo Mrajis amekiri kulifahamu suala hilo na kuahidi kulitafutia ufumbuzi.
MWISHO

 Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania Bara, Dkt. Benson Ndiege(kushoto) akizungumza na Maafisa Ushirika wa Mkoa wa Simiyu wakati wa ziara yake mkoani humo Juni 09, 2020.


 Mwenyekiti wa Bodi ya Chama kikuu cha Ushirika Mkoa wa Simiyu (SIMCU), Bw. Emanuel Mwerere akitoa taarifa ya chama hicho kwa Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania Bara, Dkt. Benson Ndiege(wan ne kulia) wakati wa ziara yake mkoani humo Juni 09, 2020.


Mrajis msaidizi wa vyama vya ushirika mkoa wa Simiyu, Bw. Ibrahim Kadudu akiwasilisha taarifa ya ushirika mkoa wa Simiyu wakati wa ziara ya Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania Bara, Dkt. Benson Ndiege mkoani humo Juni 09, 2020.


 Mjumbe wa Bodi ya Shirika la ukaguzi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) akichangia Mjumbe wa Bodi ya Shirika la ukaguzi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) akichangia hoja katika kikao cha Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania Bara, Dkt. Benson Ndiege na wajumbe wa Bodi ya Chama kikuu cha Ushirika cha mkoa wa Simiyu(SIMCU) kilichofanyika Juni09, 2020 mjini Bariadi. 


 Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania Bara, Dkt. Benson Ndiege(katikati) akizungumza na baadhi ya viongozi wa vyama vya akiba na mikopo (SACCOS) vya mjini Bariadi (hawapo pichani) wakati wa ziara yake mkoani Simiyu Juni 09, 2020.



 Baadhi ya viongozi wa vyama vya akiba na mikopo (SACCOS) vya mjini Bariadi  wakimsikiliza Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania Bara, Dkt. Benson Ndiege (hayupo pichani)  wakati wa ziara yake mkoani Simiyu Juni 09, 2020.


 Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania Bara, Dkt. Benson Ndiege(kulia) akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Chama kikuu cha Ushirika Mkoa wa Simiyu (SIMCU), Bw. Emanuel Mwerere mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya Chama hicho Mtaa wa Malambo Mjini Bariadi,  wakati wa ziara yake mkoani humo Juni 09, 2020.



 Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania Bara, Dkt. Benson Ndiege(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maafisa ushirika wa mkoa wa Simiyu wakati wa zaiara yake mkoani hapa Juni 09, 2020 (wa tatu kuchoto ni Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika mkoa wa Simiyu, Bw. Ibrahimu Kadudu.


 Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania Bara, Dkt. Benson Ndiege (wa sita kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maafisa ushirika na wajumbe wa bodi ya Chama kikuu cha Ushirika mkoa wa Simiyu(SIMCU) mara baada ya kuhitimisha kikao na wajumbe hao wakati wa ziara yake ya siku moja mkoani humo Juni 09, 2020.


 Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania Bara, Dkt. Benson Ndiege(wa nne kulia) akizungumza na ushirika na wajumbe wa bodi ya Chama kikuu cha Ushirika mkoa wa Simiyu (SIMCU) wakati wa ziara yake mkoani humo Juni 09, 2020.


 Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania Bara, Dkt. Benson Ndiege akizungumza na Maafisa Ushirika wa Mkoa wa Simiyu wakati wa ziara yake mkoani humo Juni 09, 2020.



Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania Bara, Dkt. Benson Ndiege akizungumza na Maafisa Ushirika wa Mkoa wa Simiyu(hawapo pichani) wakati wa ziara yake mkoani humo Juni 09, 2020.




0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!