Thursday, August 15, 2019

RAS SIMIYU ASITISHA UAMUZI WA DC KUWATAKA WATUMISHI KUCHANGIA FEDHA ZA KUNUNUA MASHINE YA ULTRASOUND ILIYOIBIWA BARIADI

Uongozi wa Mkoa wa Simiyu kupitia kwa Katibu Tawala wa Mkoa, Bw. Jumanne Sagini umesitisha uamuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga, uliotolewa jana Agosti 14, 2019 ambapo watumishi wote 137 wa Hospitali ya Mji wa Bariadi walitakiwa kukatwa mishahara yao kwa ajili ya kuchangia fedha ya kununua mashine ya ULTRASOUND, iliyoibiwa katika wodi ya wazazi hospitalini hapo  badala yake ameagiza vyombo vya dola vifanye uchunguzi kubaini aliyeiba mashine hiyo na hatua stahiki zichukuliwe.


Sagini ameyasema hayo leo Agosti 15, 2019 wakati akizungumza na watumishi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Bariadi katika Ukumbi wa Hospitali hiyo Mjini Bariadi.

Amesema uongozi wa Mkoa umetafakari na kuona kuwa si watumishi wote wa hospitali hiyo wamehusika katika upotevu wa mashine hiyo kwa kuwa wanafanya kazi katika idara tofauti na baadhi yao siku ya tukio hawakuwepo, hivyo ni vema vyombo vya dola vikafanya uchunguzi kubaini waliohusika.

" Uongozi wa Mkoa tunarekebisha baadhi ya hatua zilichukuliwa na Mhe. DC jana, hili jambo haliwezi kuwa la watumishi wote 137, kama Serikali tunavyo vyombo vya dola ambavyo kuna watu wanalipwa mishahara kwa kazi hizo za kiuchunguzi, tunataka kifaa hicho kirejeshwe, vyombo hivi vifanye uchunguzi, vichukue hatua kwa watakaobainika ikiwemo kupelekwa mahakamani" amesema.

Katika hatua nyingine Sagini amewataka watumishi wa Hospitali ya Mji wa Bariadi kuimarisha mfumo wa makabidhiano ya kazi na vifaa vya kazi ili kuwepo na taarifa sahihi za wagonjwa na vifaa tiba kama utaratibu unavyotaka.

Kwa upande wao watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi wamewashukuru viongozi wa Mkoa wa Simiyu  kwa kusitisha uamuzi wa awali ambao ungewaathiri kiuchumi na kupunguza ari ya kufanya kazi hususani wale ambao hawajahusika na upotevu wa mashine hiyo.

" Tunamshukuru sana kiongozi wetu kwa msamaha aliotutolea  kwa sababu tangu jana tumelala kwa presha baada ya kuambiwa kuwa kila mtu alip, mimi uwezo wangu mdogo na mshahara wangu ni mdogo nilikuwa sioni pesa ya kulipa hicho kifaa;namshukuru Mungu kwa uamuzi wa viongozi wa mkoa yaani naongea kwa uchungu mpaka nasikia kulia kwa furaha niliyonayo" amesema Frola Katoyo Mtumishi katika idara ya dawa.

"Nimepokea vizuri uamuzi uliofanywa na viongozi wetu wa mkoa kwa sababu maanuzi yaliyotolewa jana kiuhalisia si kila mtumishi alipaswa kuhusishwa kwenye hili, maana wengine walikuwa likizo, wengine hawakuwepo kazini, hivyo ni sahihi kabisa kuviachia vyombo vya dola; nina uhakikia kuanzia leo watu watafanya kazi maana jana utendaji kazi ulipungua baada ya kupata tu taarifa kuwa wanapaswa kuchangia" alisema Simon Chisomeko Afisa Afya.

Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Mkoa wa Simiyu, Bi. Catherine Nyingi amesema Chama hicho kinaushukuru uongozi wa mkoa kwa kutambua sheria, kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma na wameiomba Serikali iendelee kuwa macho katika kusimamia sheria, kanuni na taratibu.

Mashine ya kupima magonjwa ya ndani ya mwili wa Binadamu (ULTRASOUND MACHINE) iliripotiwa kuibiwa katika Wodi ya wazazi katika Hospitali ya Mji wa Bariadi  Agosti 05, 2019 na jana Agosti 14, 2019 Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akaagiza watumishi wote 137 wa Hospitali hiyo wakatwe fedha kwenye mishahara yao ili mashine hiyo iliyoibiwa  inunuliwe.
MWISHO



Katibu Tawala wa Mkoa  wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akizungumza na watumishi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Bariadi, leo Agosti 15, 2019 mjini Bariadi, kwa lengo la kutoa ufafanuzi juu ya kusitisha uamuzi wa watumishi hao kuchangia mashine ya ULTRASOUND iliyoibiwa Agosti 05, 2019 ambao ulitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga hapo jana  . 

Watumishi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Bariadi, wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini leo Agosti 15, 2019 mjini Bariadi, kwa lengo la kutoa ufafanuzi juu ya kusitisha uamuzi wa watumishi hao kuchangia mashine ya ULTRASOUND iliyoibiwa Agosti 05, 2019 ambao ulitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga hapo jana. 
Watumishi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Bariadi, wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini leo Agosti 15, 2019 mjini Bariadi, kwa lengo la kutoa ufafanuzi juu ya kusitisha uamuzi wa watumishi hao kuchangia mashine ya ULTRASOUND iliyoibiwa Agosti 05, 2019 ambao ulitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga hapo jana.
Baadhi ya Viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Mkoani Simiyu wakiwa katika kikao na Watumishi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Bariadi,  leo Agosti 15, 2019 mjini Bariadi, kwa lengo la kutoa ufafanuzi juu ya kusitisha uamuzi wa watumishi hao kuchangia mashine ya ULTRASOUND iliyoibiwa Agosti 05, 2019, ambao ulitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga hapo jana. 
Watumishi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Bariadi, wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini leo Agosti 15, 2019 mjini Bariadi, kwa lengo la kutoa ufafanuzi juu ya kusitisha uamuzi wa watumishi hao kuchangia mashine ya ULTRASOUND iliyoibiwa Agosti 05, 2019 ambao ulitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga hapo jana.
Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Mkoa wa Simiyu, Bi. Catherine Nyingi akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani mara baada ya kikao cha uongozi wa Mkoa wa Simiyu na Watumishi wa Watumishi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Bariadi,  leo Agosti 15, 2019 mjini Bariadi.
Mtumishi Frola Katoyo akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani mara baada ya kikao cha uongozi wa Mkoa wa Simiyu na Watumishi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Bariadi,  leo Agosti 15, 2019 mjini Bariadi.


Wednesday, August 14, 2019

JAMII YATAKIWA KUWATAMBUA, KUWATUMIA WASAIDIZI WA KISHERIA KUPATA MSAADA WA KISHERIA


Msajili wa Watoa Huduma ya Msaada wa Kisheria Tanzania, Bi. Felistas Joseph kutoka Wizara ya Katiba na Sheria ametoa wito kwa jamii kuwatambua na kuwatumia wasaidizi wa kisheria pindi wanapohitaji msaada katika masuala ya kawaida ya kisheria, ikiwemo migogoro ya ardhi, migogoro ya ndoa, utelekezaji wa familia na masuala mengine wanayokutana nayo siku kwa siku, ambao amesema wanatoa huduma hizo bila malipo yoyote.

Bi Felistas ameyasema hayo jana katika kikao cha Uundaji wa Kamati ya Uratibu wa Huduma za Msaada wa kisheria Mkoani Simiyu   kilichofanyika  Mjini Bariadi.

Amesema kada hii inatambuliwa kwa mujibu wa sheria ya msaada wa kisheria na wamefundishwa mafunzo ya awali ya sheria katika masuala ambayo wananchi wanakutana nayo siku kwa siku hivyo ni vema jamii na wadau wengine wakawatambua na kuwapokea kwa kuwa ni watu waliojitoa kuisaidia jamii bila malipo yoyote.

“Nia yetu ni kwamba jamii iweze kuwafahamu na kuwapokea wasaidizi wa kisheria, hawa ni watu wanaojitolea kwa dhati kufanya hii kazi bila kudai malipo, wanachohitaji ni ushirikiano na wadau wengine wa Serikali pamoja na wananchi; kada hii inatambuliwa rasmi chini ya sheria ya msaada wa kisheria na wameshapewa vigezo na mipaka ya kufanyia kazi” alisema.

Ameongeza kuwa  Serikali imeandaa mtaala wa kufundisha wasaidizi wa huduma za kisheria na hadi sasa takribani wasaidizi wa kisheria 4500 wamefundishwa katika kipindi cha miaka mitatu nyuma ambao wamejiunga katika vikundi na kujisajili kama mashirika ambapo hadi sasa kuna jumla ya mashirika 200.

Awali akifungua kikao cha Uundaji wa Kamati ya Uratibu ya Huduma za Msaada wa kisheria Mkoani Simiyu, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka  amesema endapo wasaidizi wa kisheria watutumiwa vizuri kero nyingi za wananchi zitatatuliwa na kufikia mwisho, huku kutoa wito kwa Wakuu wa wilaya, wabunge, madiwani na viongozi wengine kuwashirikisha wasaidizi wa kisheria katika mikutano ya hadhara ambapo wananchi huwasilisha kero zao.

Aidha, Mtaka amesema ili kuongeza uewelewa wa masuala ya msaada wa kisheria mkoani Simiyu ni vema Wizara ya Katiba na Sheria ikaona haja ya kuendela kutoa elimu kwa jamii, ambapo amewaalika kutoa elimu hiyo katika kambi za kitaaluma mkoani hapa ambazo zinatarajia kuanza mwezi Septemba, 2019 kwa kidato cha nne.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa, Bw. Jumanne Sagini amesema viongozi wa Mkoa watahakikisha kamati za uratibu wa huduma za kisheria ngazi ya wilaya zinaundwa na wasaidizi wa kisheria wanatumiwa ipasavyo.

Naye Sheikh wa Mkoa wa Simiyu, Mahamoud Kalokola amesema viongozi wa madhehebu ya dini wataendelea kutoa elimu kupitia makusanyiko ya ibada kwa waumini wao ili wananchi hususani wale ambao hawana na uwezo wa kifedha wa kuwalipa mawakili wajue kuwa wasaidizi wa kisheria wapo katika jamii na wanaweza kuwasaida kutatua changamoto zao.

Kamati ya Uratibu wa Shughuli za Huduma za Msaada wa Kisheria mkoa wa Simiyu imeundwa  na kuzinduliwa chini ya Katibu Tawala wa Mkoa ambaye ni Mwenyekiti, Msajili msaidizi(Afisa Maendeleo ya jamii Mkoa), mtaalamu wa ardhi, jeshi la polisi (dawati la jinsia) Magereza, TAKUKURU, Mahakama, Mwanasheria, Afisa wa dawati la malalamiko, viongozi wa dini na Afisa ustawi wa jamii na Afisa habari ngazi.

Wajumbe wengine ni mwakilishi wa vyombo vya habari, wawakilishi wa wadau wa maendeleo, wawakilishi wa taasisi za watoa huduma za msaada wa kisheria,Mwenyekiti wa baraza la ardhi na mwakilishi kutoka Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), ambapo kwa muundo huu huu kamati za wilaya zitaundwa ziweze kutekeleza jukumu la uratibu wa shughuli za huduma za kisheria wilayani
MWISHO

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (katikati) akizungumza na wadau wa Huduma za Msaada wa Kisheria Mkoani Simiyu, wakati wa kikao cha Uundaji wa Kamati ya Uratibu wa Huduma za Msaada wa kisheria Mkoani humo  kilichofanyika Agosti 13, 2019   Mjini Bariadi.
Katibu Tawala wa  Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (kushoto) akizungumza na wadau wa Huduma za Msaada wa Kisheria Mkoani Simiyu, wakati wa kikao cha Uundaji wa Kamati ya Uratibu ya Huduma za Msaada wa kisheria Mkoani humo kilichofanyika Agosti 13, 2019    Mjini Bariadi.
Msajili wa Watoa Huduma ya Msaada wa Kisheria Tanzania, Bi. Felistas Joseph(kulia) kutoka Wizara ya Katiba na  Sheria  akiwasilisha mada katika kikao cha Uundaji wa Kamati ya Uratibu ya Huduma za Msaada wa kisheria Mkoani Simiyu kilichofanyika Agosti 13, 2019   Mjini Bariadi, kutoka kushoto ni  Katibu Tawala wa  Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka.
Mwakilishi wa Taasisi za watoa huduma za msaada wa kisheria mkoani Simiyu akichangia hoja katika kikao cha Uundaji wa Kamati ya Uratibu ya Huduma za Msaada wa kisheria Mkoani humo kilichofanyika Agosti 13, 2019   Mjini Bariadi.
Wakili wa Serikali Lilian Kilembe kutoka Wizara ya katiba na Sheria akiwasilisha mada katika katika kikao cha Uundaji wa Kamati ya Uratibu ya Huduma za Msaada wa kisheria Mkoani Simiyu kilichofanyika  Agosti 13, 2019   Mjini Bariadi
Baadhi ya wajumbe wa kikao cha Uundaji wa Kamati ya Uratibu ya Huduma za Msaada wa kisheria Mkoani Simiyu kilichofanyika Agosti 13, 2019  Mjini Bariadi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati akifungua kikao hicho.
Baadhi ya wajumbe wa kikao cha Uundaji wa Kamati ya Uratibu ya Huduma za Msaada wa kisheria Mkoani Simiyu kilichofanyika  Agosti 13, 2019 Mjini Bariadi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati akifungua kikao hicho.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu na Mwenyekiti wa Kamati ya Uratibu ya Huduma za Msaada wa kisheria  Mkoa, Bw. Jumanne Sagini (katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa kikao cha Uundaji wa Kamati hiyo kilichofanyika Agosti 13, 2019  Mjini Bariadi.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu na Mwenyekiti wa Kamati ya Uratibu ya Huduma za Msaada wa kisheria  Mkoa, Bw. Jumanne Sagini (katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa kikao cha Uundaji wa Kamati hiyo kilichofanyika  Agosti 13, 2019 Mjini Bariadi.
\

Baadhi ya wajumbe wa kikao cha Uundaji wa Kamati ya Uratibu ya Huduma za Msaada wa kisheria Mkoani Simiyu kilichofanyika  Agosti 13, 2019 Mjini Bariadi wakimsikiliza Mratibu Msaidizi wa Huduma za Kisheria Ngazi ya Mkoa ambaye pia ni Afisa Maendeleo wa Mkoa, Bw. Fadhili Wilhem wakati akiwasilisha mada katika kikao hicho.

Baadhi ya wajumbe wa kikao cha Uundaji wa Kamati ya Uratibu ya Huduma za Msaada wa kisheria Mkoani Simiyu kilichofanyika  Agosti 13, 2019 Mjini Bariadi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati akifungua kikao hicho.
Baadhi ya wajumbe wa kikao cha Uundaji wa Kamati ya Uratibu ya Huduma za Msaada wa kisheria Mkoani Simiyu kilichofanyika  Agosti 13, 2019 Mjini Bariadi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati akifungua kikao hicho.

Monday, August 12, 2019

DKT BASHIRU ATOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI AJALI YA MOTO MOROGORO


Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally ametoa salamu za rambirambi na kuwaombea majeruhi na waliofariki katika ajali ya moto Mkoani Morogoro, huku akitoa wito kwa wananchi kuwa zinapotokea ajali wawe wepesi wa kuokoa watu na mali za waliopata ajali badala ya kukimbilia kuchukua vitu ili kuepusha madhara.

Dkt. Bashiru ametoa salamu hizo wakati akizungumza na viongozi wa CCM wilayani Meatu katika kikao cha Ndani kilichofanyika Ukumbi wa CCM Mjini Mwanhuzi Agosti 11, 2019 ambapo amewaombea marehemu wote wapumzike kwa amani na majeruhi wapate afya njema ili waendelee na shughuli za ujenzi wa Taifa.

“Natoa pole kufuatia vifo vya wenzetu waliofariki katika ajali ya moto kule Mkoani Morogoro tuendelee kuwaombea waliotangulia  mbele ya haki wapumzike kwa amani na wale majeruhi waweze kupata afya na kurejea katika shughuli za kujenga Taifa”

“Kama Mwenyekiti wetu na Rais wetu alivyosema, ni vizuri tunapopata majanga kama haya ya ajali wote tuwe wepesi wa kuokoa waliopata ajali na mali badala ya kukimbilia kuchukua vitu kuepusha madhara makubwa”  alisema Dkt. Bashiru.

Akizungumza na Viongozi wa CCM wilayani Meatu, Dkt. Bashiru amewataka viongozi hao kutoa taarifa za watu wanao nunua pamba kwa njia ya Umachinga,  pasipo kutumia utaratibu unaotakiwa wa kupitia vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS) kwa bei elekezi ya shilingi 1200/= ili waweze kuchukuliwa hatua.

Kwa upande wake  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa fedha za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo afya, elimu, maji na ujenzi huku akiwashukuru wabunge wa wilaya ya Meatu(Jimbo la Kisesa na Jimbo la Meatu) kwa namna wanavyojitoa binafsi na kupitia mifuko ya majimbo kuunga mkono juhudi za Serikali katika maendeleo.

Naye Mbunge wa Jimbo la Meatu, Mhe. Salum Khamis amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Dkt. John Magufuli kukubali kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Draja la Sibiti ambalo ujenzi wake umerahisisha mawasiliano na utachangia katika kukua kwa uchumi wa wilaya ya Meatu, mkoa wa Simiyu na mikoa jirani.

Mara baada ya kuhitimisha kikao cha ndani na viongozi wa CCM Wilaya ya Meatu,  Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally alipata fursa ya kutembelea na kuona ujenzi wa Daraja la Sibiti ikiwa ni ukaguzi wa utekelezaji wa Ilani ya CCM ambapo alipongeza Serikali kwa ujenzi wa daraja hilo ambalo linaiunganisha mikoa ya Simiyu na Singida.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Bw. Fabian Manoza amesema kutokana na ujenzi wa Daraja la Mto  Sibiti Halmashauri ina mpango wa kupanua stendi ya Mjini Mwanhuzi kwa kuwa magari mengi yameanza kupita Meatu kupitia daraja hilo.
MWISHO
Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. BashIru Ally akizungumza na viongozi wa CCM na wananchi katika kikao cha ndani kilichofanyika Katika Ukumbi wa  CCM Mjini Mwanhuzi Wilayani Meatu, Agosti 11, 2019.
Baadhi ya viongozi wa CCM wilayani Meatu wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. BashIru Ally katika kikao cha ndani kilichofanyika Katika Ukumbi wa  CCM Mjini Mwanhuzi Wilayani Meatu, Agosti 11, 2019
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe, Anthony Mtaka akiwasilisha taarifa ya Serikali katika kikao cha ndani cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. BashIru Ally na viongozi wa CCM ngazi ya tawi hadi Mkoa, kilichofanyika Katika Ukumbi wa  CCM Mjini Mwanhuzi Wilayani Meatu, Agosti 11, 2019.
Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt.Joseph Chilongani akiwasilisha taarifa ya Serikali katika kikao cha ndani cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na viongozi wa CCM ngazi ya tawi hadi Mkoa, kilichofanyika Katika Ukumbi wa  CCM Mjini Mwanhuzi Wilayani Meatu, Agosti 11, 2019.
Mbunge wa Jimbo la Kisesa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina akitoa salamu kwa niaba ya wananchi wa jimbo la Kisesa  katika kikao cha ndani cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na viongozi wa CCM ngazi ya tawi hadi Mkoa, kilichofanyika Katika Ukumbi wa  CCM Mjini Mwanhuzi Wilayani Meatu, Agosti 11, 2019.
Mbunge wa Jimbo la Meatu, Mhe. Salum Khamis akitoa salamu kwa niaba ya wananchi,  katika kikao cha ndani cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. BashIru Ally na viongozi wa CCM ngazi ya tawi hadi Mkoa, kilichofanyika Katika Ukumbi wa  CCM Mjini Mwanhuzi Wilayani Meatu, Agosti 11, 2019.
Baadhi ya Viongozi wa Chama na Serikali wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally katika kikao cha ndani kilichofanyika Katika Ukumbi wa  CCM Mjini Mwanhuzi Wilayani Meatu, Agosti 11, 2019.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Meatu, Mhe. Juma Mwiburi akitoa neon la shukrani mara kabla ya kuhitimisha kikao cha ndani kati ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. BashIru Ally na viongozi wa CCM ngazi ya tawi hadi Mkoa, kilichofanyika Katika Ukumbi wa  CCM Mjini Mwanhuzi Wilayani Meatu, Agosti 11, 2019
.Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally aakipokea zawadi ya Batiki iliyotengenezwa na kikundi cha Umoja wa Vijana wa CCM wialaya ya Meatu mara baada ya kuhitisha kkao chake na viongozi wa CCM kilichofanyika Katika Ukumbi wa  CCM Mjini Mwanhuzi Wilayani Meatu, Agosti 11, 2019.


Baadhi ya Viongozi wa Chama na Serikali wa Mkoa wa Simiyu na wilaya ya Meatu wakiimba mara baada ya  Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally kuhitimisha kikao chake cha ndani na viongozi hao kilichofanyika Katika Ukumbi wa  CCM Mjini Mwanhuzi Wilayani Meatu, Agosti 11, 2019.
Kutoka Kulia Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe, Anthony Mtaka na Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt.Joseph Chilongani wakiwa katika Daraja la mto Sibiti.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally, akizungumza na baadhi ya viongozi wa Chama na Serikali mara baada ya kukagua daraja la Sibiti wakatri akihitimisha ziara yake mkoani Simiyu, Agosti 11, 2019.



Sehemu ya Daraja la Mto Sibiti linalounganisha mikoa ya Simiyu na Singida.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally, akipewa maelezo na viongozi wa Chama na Serikali wilayani Meatu na Mkoani Simiyu wakati alipotembelea daraja la Sibiti mara baada ya kuhitimisha ziara yake Mkoani Simiyu, Agosti 11, 2019.

Sunday, August 11, 2019

DKT. BASHIRU: MAJENGO YOTE MAPYA YA CHAMA NA SERIKALI YAWE NA MIUNDOMBINU YA KUVUNA MAJI YA MVUA

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt.Bashiru Ally  amewataka wataalam wa ujenzi kuzingatia miundombinu ya uvunaji wa maji ya mvua katika usanifu wa majengo yote ya Chama na Serikali yanayoendela kujengwa hapa nchini, ili kupunguza gharama za uendeshaji zinazotumika kununua/kulipia maji  na kuwa na uhakika wa upatikanaji wa huduma ya maji katika majengo hayo.

Ameyasema hayo Agosti 10, 2019  wakati akikagua maendeleao ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Bariadi  na wakati akiweka jiwe la msingi ujenzi wa Ofisi ya CCM wilaya ya Busega mkoani Simiyu.

Amesema ikiwa majengo yote yatakuwa na miundombinu ya kuvuna maji ikiwa ni pamoja na kuwa na matenki imara ya kuhifadhia maji hayo, inapotokea maji yakakatika tunatumia maji yaliyovunwa lakini pia gharama za kuendesha ofisi hususani za kulipia huduma zinapungua.

“Naelekeza nchini nzima majengo yote mapya ya Chama kuanzia yale ya tawi, biashara na ofisi tuyasanifu kwa kuzingatia Miundombinu ya uvunaji wa maji ya mvua, na ndani ya Serikali nimemshauri waziri wa maji kuwa miongoni mwa mambo tunayotakiwa kuyafanya kukabiliana na changamoto ya maji ni ubunifu” alisema Dkt. Bashiru

Kuhusu zao la pamba amewataka viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuanzia ngazi ya tawi kuhakikisha wanafuatilia mwenendo wa ununuzi wa zao la pamba na kuwasilisha taarifa kwake lengo likiwa ni kuhakikisha wakulima wanapata haki yao.

“Sasa hivi Chama lazima kiwe mbele ya Serikali kutetea haki za wavuja jasho, nchi nzima machinery (watendaji wote ) ya chama lazima ifuatilie ununuzi wa mazao ya wakulima na mimi nipate taarifa za kila siku; maneno yamesemwa mengi tangu mwezi wa tano, mwezi wa sita na wa saba  tumekaa vikao mwezi huu wa nane ni vitendo” alisema.

Kwa upade wake Mbunge wa Busega Mhe. Dkt. Raphael Chegeni amemshukuru Katibu Mkuu wa CCM Taifa Dkt. Bashiru Ally kwa kuielekeza Serikali kuimarisha usimamizi wa suala la ununuzi wa pamba, ambapo hadi sasa limeanza kupata ufumbuzi kwa wanunuzi kupewa fedha na benki kwa ajili ya kununua pamba kwa wakulima kwa  bei elekezi ya shilingi 1200/=

Akitoa salamu za Serikali Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka ametoa wito kwa wananchi wa Wilaya ya Busega kutumia faida ya kuwa na Ziwa Victoria kufanya shughuli za uvuvi kwa kutumia vizimba na mabwawa na wakati huo huo amewataka kujihusisha na kilimo cha umwagiliaji ili kujihakishia usalama wa chakula.

Akiwa Wilayani Bariadi, Dkt. Bashiru alitembelea eneo la ujenzi wa Tawi la Chuo cha usimamizi wa Fedha(IFM) kijiji cha Sapiwi na kupongeza viongozi na wananchi wa Kijiji hicho kwa kuwa na matumizi bora ya ardhi ya kijiji chao jambo ambalo limepelekea kijiji  kutoa eneo kwa ajili ya ujenzi wa chuo hicho ambacho kitawaletea manufaa wao kama jamii ya Sapiwi na Taifa kwa ujumla na kuwataka viongozi wengine kuiga mfano huo.

Dkt. Bashiru yuko katika ziara yake ya kikazi mkoani Simiyu kwa ajili ya masuala mbalimbali ya Chama na kufuatilia suala la mwenendo wa ununuzi wa pamba.
MWISHO.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally akizungumza na viongozi wa Chama na Serikali na baadhi ya wananchi Agosti 10, 2019 wakati wa ziara yake wilayani Busega.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally(wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Chama na Serikali  baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Ofisi ya CCM Wilaya Busega Agosti 10, 2019 wakati wa ziara yake wilayani Busega.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally(wa PILI kulia mbele) akiwa na baaadhi ya viongozi wa Chama na Serikali  akikagua jengo la Ofisi ya CCM Wilaya ya Busega, baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi ofisi hiyo Agosti 10, 2019 wakati wa ziara yake wilayani Busega.
Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega akitoa maelezo juu ya mchoro wa jengo la Ofisi ya CCM Wilaya ya Busega, ambalo liliwejkewa jiwe la msingi na  Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally Agosti 10, 2019.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo na Mbunge wa Jimbo la Busega, Dkt. Raphael Chegeni wakifurahia jambo wakati wa Ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally Agosti 10, 2019 wilayani humo.



Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally akizungumza na viongozi wa Chama na Serikali na baadhi ya wananchi Agosti 10, 2019 wakati wa ziara yake wilayani Busega.



Baadhi ya viongozi wa Chama na Serikali wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally akizungumza na viongozi wa Chama na Serikali na baadhi ya wananchi Agosti 10, 2019 wakati wa ziara yake wilayani Busega.
Mbunge wa Jimbo la Busega, Dkt. Raphael Chegeni akizungumza kwa niaba ya wananchi  wakati  wa Ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally Agosti 10, 2019 wilayani humo.
Mbunge wa Bariadi, Mhe. Andrew Chenge akizungumza kwa niaba ya wananchi  wakati  wa Ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally Agosti 10, 2019 wilayani humo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, James John  akimkabidhi Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally taarifa ya ujenzi wa hospitali ya wilaya Agosti 10, 2019 wakati wa ziara yake wilayani Bariadi.
Moja ya majengo ya Hospitali ya Wilaya ya Bariadi ambayo yako katika hatua za ukailishaji.
Baadhi ya wananchi wakiwa wanashangilia jambo katika kikao cha ndani cha Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally na viongozi wa Chama na Serikali Agosti 10, 2019 wakati wa ziara yake wilayani Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akatoa salamu za wilaya ya Bariadi katika kikao cha  ndani  cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na watendaji na watumishi wa Chama na Serikali wilaya Agosti 10, 2019
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe.Enock Yakobo  akifurahia jambo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, wakati  wa Ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally Agosti 10, 2019.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akiwasilisha taarifa ya Mkoa wa Simiyu, wakati  wa Ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally Agosti 10, 2019.
Mkuu wa Wilaya ya Busega  , Mhe. Tano Mwera akiwasilisha taarifa ya Wilaya ya Busega, wakati  wa Ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally Agosti 10, 2019.
Mjumbe wa NEC  kupitia Mkoa wa Simiyu, Bw. Gungu Silanga akikabidhi Mbunge wa Bariadi shuka za kulalia wagonjwa kwa Mbunge  wa Bariadi, Mhe. Andrew Chenge(kulia) wakati wa Ziara ya Katibu mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally wilayani Bariadi, Agosti 10, 2019.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally Agosti 10, 2019 akipokea maelezo ya namna ya kutunzwa mazingira katika eneo ilipojengwa Ofisi ya CCM Wilaya ya Busega wakati wa ziara yake  Wilayani Busega, Agosti 10, 2019.


Mbunge wa Busega Dkt. Raphael Chegeni  akiwasalimia wananchi na wanachama  Chama cha Mapinduzi. wakati wa Ziara ya Katibu mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally wilayani Busega, Agosti 10, 2019.
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally akizungumza na viongozi wa Chama na Serikali na baadhi ya wananchi Agosti 10, 2019 wakati wa ziara yake wilayani Busega.
Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Simiyu kupitia CCM, Mhe. Ester Midimu akisalimia wananchi wakati wa Ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally Agosti 10,2019 wilayani Busega.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, ENOCK Yakobo akitoa neno la shukrani  kwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally baada ya kuzungumza na viongozi wa Chama na Serikali na wananchi Agosti 10, 2019 wakati wa ziara yake wilayani Bariadi.
Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Simiyu kupitia CCM, Mhe. Leah Komanya akisalimia wananchi wakati wa ziaraya Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally Agosti 10,2019 wilayani Busega.
Baadhi ya viongozi wa Chama na Serikali wakicheza pamoja na wanakwaya ya Sayuni wilayani Busega wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally Agosti 10,2019 wilayani Busega.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally akizungumza na viongozi wa Chama na Serikali na baadhi ya wananchi Agosti 10, 2019 wakati wa ziara yake wilayani Bariadi.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally akizungumza na viongozi wa Chama na Serikali na baadhi ya wananchi  katika Kijiji cha Sapiwi  wilayani Bariadi Agosti 10, 2019 wakati alipotembelea na kujionea hali ya ujenzi wa  Tawi jipya la  Chuo cha usimamizi wa fedha (IFM) wilayani Bariadi.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka( kushoto)  akimuongoza Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally akizungumza na viongozi wa Chama na Serikali na baadhi ya wananchi  katika Kijiji cha Sapiwi  wilayani Bariadi Agosti 10, 2019 wakati alipotembelea na kujionea hali ya ujenzi wa  Tawi jipya la  Chuo cha usimamizi wa fedha (IFM) wilayani Bariadi.
Baadhi ya viongozi wa Chama na Serikali wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally akizungumza na viongozi wa Chama na Serikali na baadhi ya wananchi Agosti 10, 2019 wakati wa ziara yake wilayani Busega.

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!