Saturday, September 22, 2018

RC SIMIYU AZINDUA TTCL RUDI NYUMBANI KUMENOGA MKOANI SIMIYU


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amezindua kampeni ya Shirika la Simu Tanzania (TTCL) Rudi Nyumbani Kumenoga mkoani humo na kuipongeza TCCL kwa kuboresha huduma zake na kuwa miongoni mwa mashirika ya Serikali yanayotoa gawio kwa Serikali, fedha ambazo zinasaidia kuboresha huduma za jamii na miundombinu.

Akizindua kampeni hiyo jana jioni Septemba 21, 2018 Mjini Bariadi, amesema kwa mara ya kwanza TTCL imetoa gawio kwa serikali fedha ambazo sehemu zimewezesha ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ulioanza na Jengo la Wagonjwa wa nje (OPD), ujenzi wa Barabara, miundombinu mingine pamoja na huduma mbalimbali kwa jamii.

Aidha, Mtaka ametoa wito kwa wananchi kutumia huduma za TTCL na kumuomba Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Bw. Waziri Kindamba kufungua ofisi mkoani Simiyu, kumleta meneja na kuongeza watumishi ili kuongeza wigo wa utoaji wa huduma.

Ameongeza kuwa  Mtendaji Mkuu wa TTCL aimarishe mfumo wa intaneti zaidi ili kuwezesha mpango wa mkoa wa Simiyu wa kufundisha kupitia teknolojia ambapo mtandao wa intaneti utahitajika kwa kiasi kikubwa.

“Tungehitaji tuone wanafunzi wa Simiyu wasome saa 24, wanafunzi wasio na walimu wa kutosha wa sayansi tutajenga vyumba vya madarasa vitakavyowezesha wao kusoma kupitia mfumo wa teknolojia, Mtendaji Mkuu wa TTCL imarisha mtandao wa TTCL wanafunzi wapate intaneti ili tuweze kurahisisha ufundishaji kwenye miji mikuu ya wilaya zetu” alisema.

Wakitoa maoni yao huduma za TTCL baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Simiyu wamesema walikuwa hawazitumii lakini baada ya shirika hilo kuboresha huduma zake hasa za mtandao wa intaneti wameanza kuzitumia na wakaomba ziendelee kuboreshwa zaidi.

“ Mimi nilikuwa sijawahi kutumia mtandao wa TTCL nilikuwa natumia mitandao mingine tu lakini nilivyoona matangazo nikasema ngoja nijaribu, nikaenda kununua laini na kuanza kutumia, napenda kutumia zaidi intaneti yao  iko vizuri” alisema Emmanuel Elias mkazi wa Bariadi

Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Bw. Waziri Kindamba ametoa wito kwa Watanzania wote kurudi nyumbani na kuendelea kutumia huduma za TTCL kwa kuwa kadri wanavyotumia huduma hizo wanazalisha faida ambayo itaendelea kutumika hapa nchini kwa maendeleo ya nwananchi na Taifa kwa ujumla.

Aidha, kutokana na Taarifa ya kuwa na siku nne za maombolezo kwa Taifa ililotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kufuatia ajali ya Kivuko cha MV Nyerere huko Ukerewe Mkoani Mwanza, Mkurugenzi Kindamba amesema TTCL haitaendelea na kampeni hiyo RUDI NYUMBANI KUMENOGA mpaka siku hizo zipite ili kuungana na Watanzania wengine kuomboleza juu ya msiba huu wa Taifa.

“Mhe. Rais ametangaza siku nne za maombolezo kuanzia tarehe 21 Septemba  hadi Septemba 24, 2018  kufuatia ajali ya kuzama kwa Kivuko cha MV Nyerere, tulikuwa tumepanga kuanza na Simiyu, twende Kahama halafu Tabora lakini kwa sababu ya msiba huu uliotugusa Watanzania wote na kwa kuwa  Shirika hili ni la Watanzania na sisi tumeguswa hivyo itabidi shughuli hii tuisitishe kwa muda; Mungu awarehemu wenzetu waliotangulia na majeruhi wapone haraka” alisema.
MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa mkoa huo pamoja na baaadhi ya Viongozi wa Shirika la Simu Tanzania (TTCL) katika Uzinduzi wa Kampeni ya Rudi Nyumbani Kumenoga uliofanyika Mjini Bariadi jioni ya Septemba 21, 2018.
Kutoka kushoto Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mtendajii Mkuu wa TTCL Bw. Waziri Kindamba na Mkuu wa Wilaya ya itilima, Mhe. Benson Kilangiwakifurahia jambo wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Rudi Nyumbani Kumenoga uliofanyika Mjini Bariadi jioni ya Septemba 21, 2018.


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kulia)akimweleza jambo Mtendajii Mkuu wa TTCL Bw. Waziri Kindamba katika Uzinduzi wa Kampeni ya Rudi Nyumbani Kumenoga mkoani Simiyu uliofanyika Mjini Bariadi jioni ya Septemba 21, 2018.
Mtendajii Mkuu wa TTCL Bw. Waziri Kindamba(aliyenyosha mkono) akitambulisha rasmi Kampeni ya Rudi Nyumbani Kumenoga kwa wananchi wa mkoa wa Simiyu. katika Uzinduzi wa Kampeni hiyo uliofanyika Mjini Bariadi jioni ya Septemba 21, 2018.



Baadhi ya wananchi wa Mji wa Bariadi mkoani Simiyu walioshiriki katika Uzinduzi wa Kampeni ya Rudi Nyumbani Kumenoga uliofanyika Mjini Bariadi jioni ya Septemba 21, 2018.

  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na baadhi ya wananchi wa Mji wa Bariadi mkoani humo walioshiriki katika Uzinduzi wa Kampeni ya Rudi Nyumbani Kumenoga uliofanyika Mjini Bariadi jioni ya Septemba 21, 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizindua Kampeni ya Rudi Nyumbani Kumenoga ya TTCL Mjini Bariadi, jioni ya Septemba 21, 2018.
Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Aslay akitoa burudani kwa wananchi wa Mji wa Bariadi mkoani Simiyu walioshiriki katika Uzinduzi wa Kampeni ya Rudi Nyumbani Kumenoga uliofanyika Mjini Bariadi jioni ya Septemba 21, 2018.




Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Shilole akitoa burudani kwa wananchi wa Mji wa Bariadi mkoani Simiyu walioshiriki katika Uzinduzi wa Kampeni ya Rudi Nyumbani Kumenoga uliofanyika Mjini Bariadi jioni ya Septemba 21, 2018.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!