Wednesday, August 9, 2017

RC MTAKA:NANENANE ILENGE KUTATUA TATIZO LA NJAA NA KUWAINUA WANANCHI KIUCHUMI

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amesema Maonesho ya Sikukuu ya Wakulima (Nanenane) yalenge kuwashindanisha washiriki katika vigezo vinavyolenga kutatua tatizo la njaa na kuwainua wananchi kiuchumi badala ya kuwashindanisha kwa ujenzi wa mabanda.

Mtaka ameyasema hayo wakati akihitimisha maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa yaliyofanyika katika Uwanja wa Nyamhongolo wilaya ya Ilemela Jijini Mwanza.

Amesema Halmashauri zimekuwa zikishindanishwa na kupata tuzo na vyeti kwa kuwa na mabanda mazuri , kutembelewa na watu wengi na vigezo vingine vinavyowekwa kutathmini wakati wa maonesho, lakini wananchi katika baadhi ya maeneo hayo wanapata tatizo la njaa.

Ameongeza kuwa ipo haja kwa viongozi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa ambayo ina uhakika wa maji ya Ziwa Victoria kuweka dhamira ya kuondokana na aibu ya kuomba chakula cha msaada ili kuisaidia Serikali.

“ Ni vizuri tujiulize sana sisi viongozi wa Kanda ya Ziwa tunaokuja kwenye maonesho ya Nanenane; ni  kwa nini Mhe.Rais asiombwe chakula maeneo yasiyo na maji ya uhakika, aombwe chakula na watu wenye maji ya uhakika, ipo haja ya kuweka dhamira ya dhati  kuondokana na aibu hii” alisema Mtaka.

Aidha Mtaka amesema ili kufanya mapinduzi katika kilimo Wataalam wa Kilimo wanapaswa kuwasaidia wakulima kuondokana na kilimo cha mazoea ili waweze kulima kilimo cha kisasa chenye tija.

Sanjali na hilo Mtaka ametoa wito kwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo kuwasaidia wananchi kupata mbegu bora, mbolea na zana bora za kilimo yakiwemo matrekta ili waweze kutoka kwenye kilimo cha utamaduni(mazoea) kwenda kwenye kilimo cha kisasa chenye tija.

Mkuu huyo wa Mkoa pia ametoa rai kwa Wataalam wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kutoka Maofisini na kuwasaidia wakulima, wafugaji na wavuvi kupata elimu ya ugani ili wafanye shughuli zao kwa tija na weledi.

“Watu wa Wizara tokeni huko wizarani njooni muwafundishe watu wetu ugani...tunakwazwa sana na ninyi watu wa Wizara hasa mnapoona ni jambo jepesi kutoa maagizo kwa wakuu wa wilaya wasimamie Kilimo wakati ninyi mnajua mnaleta mbegu zisizo na kiwango,madawa mnayoleta yana changamoto ya kuwa feki” amesema Mtaka.

Ameongeza kuwa Viongozi wa kanda ya ziwa wanaomba Wizara ya Kilimo kuja na majawabu ya kudumu ya changamoto za uzalishaji wa zao la pamba hususani upatikanaji wa mbegu bora, madawa pamoja na bei ya kuuzia pamba itakayowasaidia wakulima wa pamba.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Tathmini ya Maonesho ya Nanenane, Mathayo Masele aliitangaza Halmashauri ya Wilaya ya Busega kutoka Simiyu kuwa  Halmashauri ya kwanza kati ya Halmashauri za Mikoa yote ya Kanda ya Ziwa kwa kutimiza vigezo vilivyotumika kushindanisha ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa Kauli Mbiu ya maonesho.

Akizungumzia ushindi huo Mkuu wa Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika Wilaya ya Busega, Ndg.Juma Chacha amesema Halmashauri hiyo ilitimiza vigezo vyote vya ushindani kwa asilimia 100 , ambapo ilikuwa na vitalu vya mfano kwa mazao ya chakula na biashara,mabanda ya mifugo mbalimbali, ufugaji wa samaki kwa ajili ya elimu kwa wakulima, wafugaji na wavuvi namna ya kuongeza thamani.

Naye Emmanuel Mgeta mkulima kutoka Busega aliyekuwa mshindi wa tatu kati ya wakulima wa mikoa ya kanda ya ziwa walioshindanishwa amesema maonesho ya Nanenane mwaka 2017 yamemsaidia kujifunza na kumpa hamasa ya kufanya vizuri katika uzalishaji na umuhimu wa kuyaongezea thamani mazao.


Kauli Mbiu ya Nane nane mwaka 2017 ni “ZALISHA KWA TIJA MAZAO YA KILIMO,MIFUGO NA UVUVI ILI KUFIKIA UCHUMI WA KATI” ambapo  Mikoa ya Kanda ya Ziwa Simiyu, Mwanza, Geita, Mara, Shinyanga na Kagera imeadhimisha katika Uwanja wa Nyamhongo Ilemela jijini Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na baadhi ya watumishi wa MEDA Economic Development Associates inayojishughulisha na uzalishaji wa mbegu bora za Muhogo wakati alipokagua banda lao katika Maadhimisho ya Nanenane Kanda ya Ziwa katika Uwanja wa Nyamhongolo Wilaya ya Ilemela Jijini Mwanza
Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) Kanda ya Ziwa,Martin Malima akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu baadhi ya bidhaa zilizokamatwa kutokana na kutokidhi ubora wa kutumiwa na binadamu mara alipotembelea banda la mamlaka hiyo katika Maonesho ya Nanenane  Kanda ya Ziwa katika Uwanja wa Nyamhongolo Ilemela Jijini Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akimkabidhi Mkuu wa Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika Halmashauri ya wilaya ya Busega,Juma Chacha zawadi ya kombe na cheti baada ya Halmashauri hiyo kushika nafasi ya kwanza miongoni mwa Halmashauri za Mikoa ya kanda ya Ziwa katika Maonesho ya Nanenane  Kanda ya Ziwa katika Uwanja wa Nyamhongolo Ilemela Jijini Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akipita kuona mashamba darasa ya zao la vitunguu yaliyopandwa kwa kutumia mbolea  aina ya Yara katika Maonesho ya Nanenane  Kanda ya Ziwa katika Uwanja wa Nyamhongolo Ilemela Mkoani Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wananchi waliohudhuria katika Maonesho ya Nanenane  Kanda ya Ziwa katika Uwanja wa Nyamhongolo Ilemela Jijini Mwanza.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini (mwenye miwani) akipata maelezo kutoka kwa watalaam wa Kilimo mara baada ya kutembelea Banda la Halmashauri ya Wilaya ya Busega na kuona vitalu vya baadhi ya mazao ya Kilimo na biashara, katika Maonesho ya Nanenane  Kanda ya Ziwa katika Uwanja wa Nyamhongolo Ilemela Jijini Mwanza.
Mkuu wa Wilaya ya Magu, Mhe.Hadija Nyembo ambaye pia Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Ilemela akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika Kilele cha Maonesho ya Nanenane  Kanda ya Ziwa ili azungumze na wananchi katika Uwanja wa Nyamhongolo Ilemela Jijini Mwanza,
Baadhi ya Wasanii wa Ngoma aina ya Gobogobo kutoka Wilaya ya Misungwi Mwanza wakicheza na nyoka wakati wakitoa burudani kwenye  Kilele cha Maonesho ya Nanenane  Kanda ya Ziwa katika Uwanja wa Nyamhongolo Ilemela Jijini Mwanza.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini (wa pili kulia) akipata maelezo kutoka kwa wataalam kuhusu asali bora baada ya kutembelea Banda la Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, kwenye Maonesho ya Nanenane  Kanda ya Ziwa katika Uwanja wa Nyamhongolo Ilemela Jijini Mwanza.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini (katikati) akipata maelezo kutoka kwa watalaam wa Kilimo kuhusu zao la dengu mara baada ya kutembelea Banda la Halmashauri ya Wilaya ya Busega na kuona vitalu vya baadhi ya mazao ya Kilimo na biashara, kwenye Maonesho ya Nanenane  Kanda ya Ziwa katika Uwanja wa Nyamhongolo Ilemela Jijini Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka  akifuatilia taarifa kwenye kipeperushi mara baada ya kutembelea Banda la Benki ya Maendeleo yaKilimo (TADB) wakati wa Kilele cha Maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa Uwanja wa Nyamhongolo Ilemela Jijini Mwanza , (wa pili kulia) Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa TADB Augustino Matutu Chacha.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akipata zana maelezo na watumishi wa kampuni ya KIRASA inayojihusisha na uuzaji wa matrekta  wakati alipotembela kuona  zana hizo(hazipo pichani) kwenye Kilele cha Maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa Uwanja wa Nyamhongolo Ilemela Jijini Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akimkabidhi Mkulima Emmanuel Mgeta kutoka wilaya ya Busega zawadi ya cheti na fedha taslimu baada ya mkulima huyo kushika nafasi ya tatu wakulima walioshindanishwa kutoka katika Halmashauri za Mikoa ya kanda ya Ziwa kwenye Maonesho ya Nanenane  Kanda ya Ziwa katika Uwanja wa Nyamhongolo Ilemela Jijini Mwanza.
Wasanii kutoka Wilaya ya Ilemela Mwanza wakitoa burudani kwenye  Kilele cha Maonesho ya Nanenane  Kanda ya Ziwa katika Uwanja wa Nyamhongolo Ilemela Jijini Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akimkabidhi Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa TADB Augustino Matutu Chacha zawadi ya kombe na cheti baada ya Benki hiyo  kushika nafasi ya kwanza kati ya  Taasisi zilizoshindanishwa katika Maonesho ya Nanenane  Kanda ya Ziwa katika Uwanja wa Nyamhongolo Ilemela Jijini Mwanza..
Wasanii wa kundi la Futuhi kutoka Mwanza wakitoa burudani kwenye  Kilele cha Maonesho ya Nanenane  Kanda ya Ziwa katika Uwanja wa Nyamhongolo Ilemela Jijini Mwanza.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini(wapili kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mjasiliamali anayetengeneza bidhaa za ngozi ikiwani njia ya kuongezea thamani mazao ya mifugo baada ya kutembelea Banda la Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, kwenye Kilele cha Maonesho ya Nanenane  Kanda ya Ziwa katika Uwanja wa Nyamhongolo Ilemela Jijini Mwanza.
Baadhi ya Viongozi kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa waliohudhuria Kilele cha Maonesho ya Nanenane  Kanda ya Ziwa katika Uwanja wa Nyamhongolo Ilemela Jijini Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(wa pili kulia mstari wa mbele) na viongozi wengine kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa wakifurahi na kucheza muzika mara baada ya kuhitimisha Maonesho ya Nanenane  Kanda ya Ziwa katika Uwanja wa Nyamhongolo Ilemela Jijini Mwanza.

Sunday, August 6, 2017

NAIBU SPIKA AFUNGUA MASHINDANO YA MBIO ZA BAISKELI MKOANI SIMIYU

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson amefungua Mashindano ya Mbio za Baiskeli na Ngoma za Asili Mjini Bariadi(Simiyu Jambo Festival) ambayo yamehudhuriwa na Maelfu ya Wananchi wa Mkoa wa Simiyu.

Mashindano hayo ya mbio za baiskeli yamehusisha kilometa 200 wanaume, kilomita 80 wanawake ambapo pia  walemavu waliweza kushindania katika umbali wa kilomita tano.

Akizungumza baada ya kufungua mashindano hayo Dkt.Tulia pamoja na kuupongeza Mkoa wa Simiyu kuandaa mashindano hayo amesema, ipo michezo nchini haijapewa kipaumbele lakini ikitumiwa vizuri inaweza kutoa ajira ukiwemo mchezo wa mbio za baiskeli; ambapo ametoa wito kwa viongozi wa mikoa mingine pia kuwekeza katika michezo mbalimbali ili kuwasaidia wananchi kupata kipato.

“Lililofanyika Simiyu ni jambo jema sasa hivi watu watakuwa wanajua kuwa wakijifua vizuri kwenye baiskeli na ngoma za jadi wanakuja kushiriki mashindano ya Baiskeli na  ngoma Simiyu, nitoe wito kwa viongozi wengine kufikiria mambo mengine yanayoweza kuwasaidia wananchi katika maeneo yao kupata ajira na kujipatia kipato” alisema.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amesema mkakati wa mkoa huo ni kurasimisha tamaduni zote na kuhusianisha na shughuli za Utalii ndani ya mkoa huo.

“Position(Nafasi) ya Mkoa wa Simiyu kwenye nchi ni kukuza tamaduni na sanaa zetu kama moja ya eneo litakalotuunganisha na sekta ya Utalii, tumezungukwa na mapori ya akiba na mbuga za wanyama, tungehitaji watalii wanapokuja kwenye maeneo hayo wapate ladha ya tofauti kiwemo utamaduni wa Mtanzania”

Mtaka ameongeza kuwa wasanii wote watatambuliwa na baadae kujengewa uwezo  kupitia watalaam wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(Kitivo cha sanaa),Chuo cha Sanaa Bagamoyo na vyuo vya michezo ili waweze kufanya kazi zao kibiashara na kuimarisha uchumi wao.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Food Products,Mhe.Salum Khamis ambaye ndio Mdhamini wa mashindano ya Baiskeli na ngoma za Asili (Simiyu Jambo Festival) amesema ataendelea kudhamini mashindano kama hayo Mkoani Simiyu ili kuwawezesha wananchi kuinua kipato kupitia vipaji vyao.

 Naye mshindi wa kwanza mbio za kilometa 80 (wanawake) Raulensia Luzuba kutoka Mwanza ameomba mashirika na makampuni mbalimbali kuwadhamini ili waweze  kujengewa uwezo na kuandaliwa kushiriki katika mashindano ya Kimataifa.

Masunga Duba mshindi wa mbio za kilometa 200(wanaume)kutoka Simiyu amesema pamoja na wafadhili kudhamini mashindano wawasaidie  pia wachezaji kupata baiskeli za kisasa zitakazowasaidia kwenda kwa kasi inayotakiwa.

Mashindano ya baiskeli Mkoani Simiyu yameshirikisha wachezaji kutoka mikoa ya Simiyu, Mwanza, Shinyanga,Arusha na Mbeya, ambapo ushindi kwa upande wa wanaume umechukuliwa na Hamisi Hussein(Arusha) ambaye amejishindia pikipiki, wa pili ni Masunga Duba(Simiyu) kitita cha shilingi 1,000,000/= wa tatu Richard Laizer(Arusha) .shilingi 500,000/= na zawadi nyingine zimetolewa kwa mshindi wa nne mpaka wa 15.

Kwa upande wa wanawake mshindi wa kwanza  Raulensia Luzuba kutoka Mwanza amejipatia shilingi 500,000/=, mshindi wa pili Tatu Malulu(Mwanza) shilingi 400,000/= na wa tatu ni Vumilia Mwinamila(Simiyu) shilingi 300,000/= na zawadi nyingine zimetolewa kwa mshindi wa nne mpaka wa 10.


Walemavu mshindi wa kwanza Emmanuel Mtemi amejipatia shilingi 200,000/= wa pili Masunga Sendama shilingi 150,000/= na wa tatu Saguda Sospeter shilingi 100,000/=wote kutoka mkoa wa Simiyu na zawadi nyingine zimetolewa kwa mshindi wa nne na wa tano.
Naibu Spika wa Bunge la  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson (mwenye bendera nyeupe kulia) akifungua mashindano ya Mbio za Baiskeli Mkoa wa Simiyu(Simiyu Jambo Festival) kwa kuruhusu washirikuanza mashindano hayo Mjini Bariadi.
Naibu Spika wa Bunge la  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson (wa pili kushoto) akimkabidhi ufunguo wa pikipiki mshindi wa kwanza kilometa 200 (wanaume), Hamisi Hussein kutoka Arusha katika mashindano ya Baiskeli yaliyofanyika Mjini Bariadi (kulia) ni Mkurugenzi Kampuni ya Jambo Food Products ambayo ni mdhamini, Mhe.Salum Khamis akimpongeza Mshindi huyo
Naibu Spika wa Bunge la  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson (mwenye baiskeli wa pili kulia) akiwa na viongozi wa Mkoa na baadhi ya Wabunge wa Mkoa wa Simiyu na Viti Maalum kutoka nje ya Mkoa kwa ajili ya kufungua mashindano ya baiskeli yaliyofanyika Mjini Bariadi.
Mkurugenzi Kampuni ya Jambo Food Products, Mhe.Salum Khamis ambaye ndio mdhamini wa mashindano ya baiskeli na ngoma za asili yalliyofanyika Mkoani Simiyu, akimkabidhi Mshindi wa kwanza mbio za Kilometa 80 (wanawake) Raulensia Luzuba kutoka mkoani Mwanza zawadi ya shilingi laki tano taslimu.
Rais wa Chama cha Baiskeli Taifa, Godfrey Mhagama akimkabidhi mshindi wa kwanza katika mbio za kilometa 10 (walemavu) katika mashindano ya Baiskeli na ngoma za asili (Simiyu Jambo Festival) yaliyofanyika Mjini Bariadi Simiyu.
Naibu Spika wa Bunge la  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson akimkabidhi ufunguo wa pikipiki mshindi wa kwanza (wanaume) katika mashindano ya Baiskeli yaliyofanyika Mjini Bariadi kilometa 200, Hamisi Hussein kutoka Arusha
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja na washindi watatu wa mbio za Kilometa 10 (walemavu) na viongozi wa Mkoa wa Simiyu na baadhi kutoka nje ya mkoa wa Simiyu, mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya baiskeli na Ngoma za Asili(Simiyu Jambo Festival) Mjini Bariadi.
Mshindi wa tatu mbio za baiskeli kilometa 80(wanawake), Vumilia Mwinakila kutoka Mkoa wa Simiyu akicheza wimbo wa Kisukuma pamoja na  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson baada ya kupokea kitita cha shilngi laki tatu.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja na washindi watatu wa mbio za Kilometa 80(wanawake) na viongozi wa Mkoa wa Simiyu na baadhi kutoka nje ya mkoa wa Simiyu, mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya baiskeli na Ngoma za Asili(Simiyu Jambo Festival) Mjini Bariadi.
Baadhi Washiriki wa mashindano ya mbio za Baiskeli kilometa 200 wanaume (kulia) wakiendelea kuchuana vikali kushindania pikipiki na fedha taslimu.
mshindi wa kwanza kilometa 200 (wanaume), Hamisi Hussein kutoka Arusha akipanda kwenye pikipiki yake aliyokabidhiwa baada ya kuibuka mshindi dhidi ya wenzake katika mashindano ya Baiskeli yaliyofanyika Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Wa pili kutoka kushoto Katibu Tawala mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini, Mbunge wa Busega, Mhe.Raphael Chegeni , Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson wakiwa wamembeba nyoka wa kikundi cha wasanii wa ngoma ya asili ya Kisukuma.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson akimpongeza Bibi.Tatu Malulu kutoka Mwanza kwa kuwa mshindi wa pili mbio za kilometa 80 (wanawake) katika mashindano ya Baiskeli yaliyofanyika Mkoani Simiyu.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson akizungumza na waandishi wa habari katika mahojiano maalum mara baada ya kuwapokea washiriki wa mashindano ya mbio za baiskeli wa makundi yote(wanaume, wanawake na walemavu) yaliyofanyika Bariadi Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthny Mtaka akizungumza na waandishi wa habari katika mahojiano maalum mara baada ya kuwapokea washiriki wa mashindano ya mbio za baiskeli wa makundi yote(wanaume, wanawake na walemavu) yaliyofanyika Bariadi Mkoani Simiyu.
Mshindi wa kwanza mbio za baiskeli kilometa 200 (wanaume), Hamisi Hussein kutoka Arusha(mwenye pikipiki) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi  na washindi wenzake, mshindi wa pili Masunga Duba kutoa Simiyu(wa tatu kushoto mstari wa pili) na wa tatu Richard Laizer (wa pili kulia mstari wa pili).
Kikundi cha ngoma ya asili cha Wagalu kikitoa burudani kwa wananchi na viongozi waliofika kushuhudia mashindano ya baiskeli na ngoma za asili (Simiyu Jambo Festival) Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Kikundi cha ngoma ya asili cha Wagalu kikitoa burudani kwa wananchi na viongozi waliofika kushuhudia mashindano ya baiskeli na ngoma za asili (Simiyu Jambo Festival) Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali pamoja na mamanju wa vikundi vya Wagika na Wagalu Mkoani Simiyu, mara baada ya mashindano ya baiskeli na ngoma za asili kumalizika Mjini Bariadi.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson(kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Kushoto wakiteta jambo wakati wakiwasubiri washiriki wa mashindano ya mbio za baiskeli yaliyofanyika Mjini Bariadi, kufika katika kituo cha mwisho.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson(wa tatu kushoto) akicheza pamoja na baadhi ya  viongozi wa Mkoa wa Simiyu na waimbaji kutoka Kata ya Bumela Wilayani Itilima wakati wa kuhitimisha mashindano ya baiskeli na ngoma za asili (Simiyu Jambo Festival) Mjini Bariadi.
Baadhi ya wasanii wa Kikundi cha ngoma ya asili cha Wagika wakitoa burudani kwa wananchi na viongozi waliofika kushuhudia mashindano ya baiskeli na ngoma za asili (Simiyu Jambo Festival) Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson(wa nne kulia) akicheza pamoja na baadhi ya  viongozi wa Mkoa wa Simiyu na Msanii Elizabeth Maliganya(wa tatu kulia) kutoka Bariadi wakati wa kuhitimisha mashindano ya baiskeli na ngoma za asili (Simiyu Jambo Festival) Mjini Bariadi.
Msanii Elizabeth Maliganya kutoka Bariadi akitoa burudani pamoja na wasanii wenzake wakati wa kuhitimisha mashindano ya mbio za  baiskeli na ngoma za asili (Simiyu Jambo Festival) Mjini Bariadi.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson akiwahutubia wananchi wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya kuhitimishwa kwa mashindano ya mbio za  baiskeli na ngoma za asili (Simiyu Jambo Festival) Mjini Bariadi.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson akisalimia na Katibu Tawala wa Wilaya ya Bariadi, Albert Rutaihwa ara baada ya kuwasili kwa ajili ya kufungua mashindano ya baiskeli yaliyofanyika Mjini Bariadi mkoani Simiyu.

Saturday, August 5, 2017

WANANCHI WAHIMIZWA KWENDA KUSHUHUDIA MASHINDANO YA BAISKELI NA NGOMA ZA ASILI AGOSTI 06

Wananchi Mkoani Simiyu wamehimizwa kwenda kushuhudia mashindano ya Baiskeli na Ngoma za Asili yatakayofanyika kesho Jumapili katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mratibu wa Mashindano hayo yanayotambulika kama Simiyu Jambo Festival ambayo yanadhaminiwa na Kampuni ya Jambo Food Products, Ndg.Kulwa Mtebe amesema washiriki wa mbio za baiskeli kutoka mikoa mbalimbali wameshawasili Mjini Bariadi na wamejiandaa vizuri kwa ajili mashindano.

Aidha, amesema Mgeni Rasmi katika tukio hilo(Simiyu Jambo Festival) la Kihistoria Mkoani Simiyu ambaye ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.Tulia Ackson ameshawasili Mkoani kwa ajili ya mashindano hayo.

Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Simiyu, Edson Mwakihaba amesema Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani limejipanga kikamilifu kuhakikisha kwamba watumiaji wa barabara wanazingatia sheria za usalama barabarani na askari watakuwepo katika vituo vyote ambavyo washiriki wa mbio za baiskeli watapita.

Rais wa Chama cha Baiskeli Taifa Godfrey Mhagama amesema Chama hicho kupitia kamati yake ya Ufundi kitakahikisha kanuni na taratibu za mchezo wa mbio za baiskeli zinasimamiwa na kufuatwa katika mashindano hayo.

Mhagama ameongeza kuwa Wachezaji wahakikishe wanacheza katika viwango vinavyotakiwa kwa kuwa vigezo vyote vitavyozingatiwa ikiwa ni pamoja na kasi ya mchezaji na muda anaoutumia katika kukamilisha mbio kwa umbali uliopangwa, ambayo pia itakuwa ni njia ya kupata wachezaji wanaoweza kuwakilisha Taifa katika Mashindano ya Olimpiki.

Kwa upande wake Meneja Masoko wa Kampuni ya Jambo Food Products Anthony Paul amewahakikishia washiriki kuwa zawadi zote zilizopangwa kwa washindi katika makundi yote matatu (wanaume, wanawake, walemavu) ziko tayari ambayo ni pikipiki itakayotolewa kwa mshindi wa kwanza(wanaume) na fedha taslimu zaidi ya shilingi Milioni nane zitakazotolewa kwa washindi wengine.

Naye Emmanuel Mollel mshiriki wa mashindano ya mbio za Baiskeli kutoka mkoa wa Arusha amesema washiri kutoka katika mkoa huo wamejipanga kikamilifu na kiushindani kuhakikisha wanapata ushindi.

Tatu Malulu mshiriki wa mbio za Kilometa 80 kutoka katika Mkoa wa Mwanza amesema amekuwa akifanya mazoezi siku zote ambayo yamemuimarisha hivyo akathibitisha kuwa kutokana na maandalizi hayo anatarajia ushindi na ametoa wito kwa Wachezaji kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi siku zote maana ndio siri ya kufanikiwa kwao.

Zaidi ya washiriki 160 kutoka katika mikoa ya Simiyu, Shinyanga, Mwanza, Geita na Arusha wanatarajia kushiriki mashindano hayo ambayo yatagawanyika katika makundi matatu; wanaume Kilometa 200, wanawake Kilometa 80 na Watu wenye Uemavu Kilometa 05.
Baadhi ya Washiriki wa mashindano ya baiskeli wanawake kutoka wakisikiliza maswali kutoka kwa waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa mahojiano maalum juu ya maandalizi ya mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika Jumapili ya tarehe 06/08/2017 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(mwenye pikipiki) akiwa na pikipiki itakayotolewa kwa mshindi wa kwanza kwa Kilometa 200 pamoja na baadhi ya washiriki wa mashindano ya mbio za baiskeli yatakayofanyika Jumapili ya tarehe 06/08/2017 Mjini Bariadi.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Jambo, Anthony Paul akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) pikipiki aina ya SHINERAY itakayotolewa na Kampuni hiyo ambayo ni Wadhamni wa Mashindano ya Baiskeli kwa mshindi wa kwanza wanaume yatakayofanyika  Jumapili ya tarehe 06/08/2017, Mjini Bariadi.
Rais wa Chama cha Baiskeli Taifa Godfrey Mhagama ( wa tatu kulia) akizungumza na viongozi wa Chama hicho Mkoa wa Simiyu kuhusu masuala mbalimbali ya maandalizi ya mashindano ya baiskeli yatakayofanyika Jumapili ya tarehe 06/08/2017 Mjini Bariadi.
Rais wa Chama cha Baiskeli Taifa Godfrey Mhagama akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mahojiano maalum juu ya maandalizi ya mashindano ya Mbio za Baiskeli yatakayofanyika Jumapili ya tarehe 06/08/2017 Mjini Bariadi.
Mratibu wa Mashindano ya Baiskeli na ngoma za Asili yanayotambulika kama Simiyu Jambo Festival, Kulwa Mtebe akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mahojiano maalum juu ya maandalizi ya mashindano ya Mbio za Baiskeli yatakayofanyika Jumapili ya tarehe 06/08/2017 Mjini Bariadi.
Mkuu wa  Usalama Barabarani Mkoa wa Simiyu, Edson Mwakihaba akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mahojiano maalum juu ya hali ya usalama wa barabarani wakati wa mashindano ya Mbio za Baiskeli yatakayofanyika Jumapili ya tarehe 06/08/2017 Mjini Bariadi.
Mshiriki wa Mashindano ya Baiskeli kutoka Mkoa wa Arusha, Emmanuel Mollel akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mahojiano maalum juu ya maandalizi ya mashindano ya Mbio za Baiskeli yatakayofanyika Jumapili ya tarehe 06/08/2017 Mjini Bariadi.




WAKUU WA SHULE WATAKIWA KUWA WABUNIFU KUONGEZA UFAULU

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amewataka Wakuu wa Shule mkoani humo kuongeza ubunifu ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi katika shule zao.

Mtaka ameyasema hayo wakati alipokuwa akifunga mafunzo ya siku mbili kwa wakuu wa shule zote za Sekondari yaliyofanyika Mjini Bariadi katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Bariadi

 Amesema wakuu wa shule wanatakiwa kuwa wabunifu hususani katika mbinu mbalimbali zitakazosaidia kuwaandaa vizuri kitaaluma wanafunzi ikiwa ni pamoja na mazoezi na mitihani ya kujipima ya mara kwa mara, zitasaidia wanafunzi kufanya vizuri katika mitihani ya ndani na kitaifa.

“Kiongozi lazima uwe mbunifu, Mkiwa wabunifu kwenye shule watoto watafanya vizuri,mnapaswa kubuni mbinu na mikakati mbalimbali kwenye majaribio ya darasani, mitihani ya kujipima na  kubuni namna ya kuwapa motisha walimu wenu wapende kazi na kujiona ni wanafamilia katika shule mlizopo” amesema Mtaka.

Aidha, amewataka wakuu hao wa shule kujiwekea utaratibu wa kupita mara kwa mara madarasani kukagua kwa lengo la kujiridhisha, ikiwa walimu wanatimiza wajibu wao wa kuwafundisha wanafunzi kama inavyotakiwa badala ya kusubiri kuletewa taarifa.

Mkuu huyo wa Mkoa pia amewaasa wakuu hao wa shule kuwa na uongozi shirikishi ambao unajali pande zote kwa maana ya walimu, wanafunzi na wazazi ili waweze kujua kero na masuala mbalimbali yasiyowaridhisha na waweze kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa taratibu kuyapatia suluhu.

Vile vile Mtaka amesisitiza wakuu wa shule kufanya vikao na wazazi kwa kuwa wazazi wanayo nafasi kubwa ya kuchangia wanafunzi kufanya vizuri, hivyo akawataka wavitumie vikao kupata maoni ya wazazi katika masuala mbalimbali ya kuboresha maendeleo ya wanafunzi kitaaluma.

Sanjali na hilo amewataka Wakuu hao wa Shule kuzingatia sheria, kanuni , taratibu na kuchukua hatua stahiki pale inapobidi ikiwa ni pamoja na kutowaruhusu wanafunzi wajawazito au waliojifungua kuendelea na masomo.

Kwa upande wake Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl.Julius Nestory amesema katika mafunzo hayo ya siku mbili wakuu wa shule wameelimishwa juu ya sheria zote nne za Elimu, falsafa,nyaraka,kanuni mbalimbali za Elimu na sera mpya ya Elimu.

Nestory amebainisha pia kuwa wakuu  wa shule hao wamepewa mafunzo ya utunzaji wa nyaraka za Serikali, udhibiti wa vitendo vya rushwa, kusimamia shule na taaluma pamoja na utunzaji wa takwimu sahihi ambapo amewataka wakuu wa shule hao kutumia sheria zilizopo katika kusimamia shule kupitia mipango thabiti itakayotoa matokeo chanya.

Naye Magebu Bugacha Mkuu wa Shule ya Sekondari Mwantimba ameshukuru uongozi wa Mkoa kuona umuhimu wa kuwaandalia wakuu wa shule mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo ambayo yatawasaidia na kuwapa uzoefu katika kuendesha na kusimamia shule zao.

Akitoa shukrani kwa niaba ya Maafisa Elimu wa Wilaya za Mkoa huo, Afisa Elimu wa Wilaya ya Meatu, Mwl.Estomia Makyara amesema maelekezo yote ya Mkuu wa Mkoa aliyoyatoa wakati akifunga mafunzo hayo kwa Wakuu wa shule yatatekelezwa kwa uadilifu, ili mkoa wa Simiyu uwe ni miongoni mwa mikoa mitatu bora kwa ufaulu katika mitihani ya Kitaifa.


Jumla ya Wakuu wa shule 152 kutoka katika Halmashauri zote sita za Mkoa wa Simiyu wamepata  mafunzo hayo ambayo yalilenga kuwajengea uwezo katika usimamizi na uendeshaji wa shule za Sekondari.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na Wakuu wa Shule (hawapo pichani) wakati wa kufunga mafunzo yao ya siku mbili yaliyofanyika Mjini Bariadi, (kulia) Afisa Elimu Mkoa, Mwl.Julius Nestory.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na Wakuu wa Shule (hawapo pichani) wakati wakufunga mafunzo yao ya siku mbili yaliyofanyika Mjini Braiadi(wa pili kulia) Adili Elinipenda Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Simiyu.
Afisa Elimu wa Wilaya ya Meatu, Mwl.Estomia Makyara akitoa shukrani kwa niaba ya Maafisa Elimu wa Wilaya za Mkoa wa Simiyu wakati wa kufunga mafunzo ya siku mbili kwa Wakuu wa Shule (hawapo pichani)yaliyofanyika Mjini Bariadi.
Baadhi ya Wakuu wa Shule za Sekondari Mkoani Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka (hayupo pichani)alipozungumza nao wakati akifunga mafunzo ya siku mbili Mjini Bariadi.
Baadhi ya Maafisa Elimu wa Wilaya za Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka (hayupo pichani) akizungumza na Wakuu wa Shule wakati akifunga mafunzo yao ya siku mbili Mjini Bariadi.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mwagala wilayani Maswa akitoa shukrani kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka kwa hotuba aliyoitoa wakati wa kufunga mafunzo ya Wakuu wa Shule yaliyofanyika Mjini Bariadi.

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!