Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amesema Maonesho ya Sikukuu ya Wakulima (Nanenane) yalenge
kuwashindanisha washiriki katika vigezo vinavyolenga kutatua tatizo la njaa na
kuwainua wananchi kiuchumi badala ya kuwashindanisha kwa ujenzi wa mabanda.
Mtaka ameyasema
hayo wakati akihitimisha maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa yaliyofanyika katika
Uwanja wa Nyamhongolo wilaya ya Ilemela Jijini Mwanza.
Amesema
Halmashauri zimekuwa zikishindanishwa na kupata tuzo na vyeti kwa kuwa na
mabanda mazuri , kutembelewa na watu wengi na vigezo vingine vinavyowekwa kutathmini
wakati wa maonesho, lakini wananchi katika baadhi ya maeneo hayo wanapata tatizo
la njaa.
Ameongeza
kuwa ipo haja kwa viongozi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa ambayo ina uhakika wa maji
ya Ziwa Victoria kuweka dhamira ya kuondokana na aibu ya kuomba chakula cha
msaada ili kuisaidia Serikali.
“
Ni vizuri tujiulize sana sisi viongozi wa Kanda ya Ziwa tunaokuja kwenye
maonesho ya Nanenane; ni kwa nini
Mhe.Rais asiombwe chakula maeneo yasiyo na maji ya uhakika, aombwe chakula na
watu wenye maji ya uhakika, ipo haja ya kuweka dhamira ya dhati kuondokana na aibu hii” alisema Mtaka.
Aidha
Mtaka amesema ili kufanya mapinduzi katika kilimo Wataalam wa Kilimo wanapaswa kuwasaidia
wakulima kuondokana na kilimo cha mazoea ili waweze kulima kilimo cha kisasa
chenye tija.
Sanjali
na hilo Mtaka ametoa wito kwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo kuwasaidia wananchi
kupata mbegu bora, mbolea na zana bora za kilimo yakiwemo matrekta ili waweze
kutoka kwenye kilimo cha utamaduni(mazoea) kwenda kwenye kilimo cha kisasa
chenye tija.
Mkuu
huyo wa Mkoa pia ametoa rai kwa Wataalam wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
kutoka Maofisini na kuwasaidia wakulima, wafugaji na wavuvi kupata elimu ya
ugani ili wafanye shughuli zao kwa tija na weledi.
“Watu
wa Wizara tokeni huko wizarani njooni muwafundishe watu wetu ugani...tunakwazwa
sana na ninyi watu wa Wizara hasa mnapoona ni jambo jepesi kutoa maagizo kwa
wakuu wa wilaya wasimamie Kilimo wakati ninyi mnajua mnaleta mbegu zisizo na
kiwango,madawa mnayoleta yana changamoto ya kuwa feki” amesema Mtaka.
Ameongeza
kuwa Viongozi wa kanda ya ziwa wanaomba Wizara ya Kilimo kuja na majawabu ya
kudumu ya changamoto za uzalishaji wa zao la pamba hususani upatikanaji wa
mbegu bora, madawa pamoja na bei ya kuuzia pamba itakayowasaidia wakulima wa
pamba.
Katika
hatua nyingine Mwenyekiti wa Tathmini ya Maonesho ya Nanenane, Mathayo Masele aliitangaza
Halmashauri ya Wilaya ya Busega kutoka Simiyu kuwa Halmashauri ya kwanza kati ya Halmashauri za Mikoa
yote ya Kanda ya Ziwa kwa kutimiza vigezo vilivyotumika kushindanisha ikiwa ni
pamoja na utekelezaji wa Kauli Mbiu ya maonesho.
Akizungumzia
ushindi huo Mkuu wa Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika Wilaya ya Busega,
Ndg.Juma Chacha amesema Halmashauri hiyo ilitimiza vigezo vyote vya ushindani
kwa asilimia 100 , ambapo ilikuwa na vitalu vya mfano kwa mazao ya chakula na
biashara,mabanda ya mifugo mbalimbali, ufugaji wa samaki kwa ajili ya elimu kwa
wakulima, wafugaji na wavuvi namna ya kuongeza thamani.
Naye
Emmanuel Mgeta mkulima kutoka Busega aliyekuwa mshindi wa tatu kati ya wakulima
wa mikoa ya kanda ya ziwa walioshindanishwa amesema maonesho ya Nanenane mwaka
2017 yamemsaidia kujifunza na kumpa hamasa ya kufanya vizuri katika uzalishaji
na umuhimu wa kuyaongezea thamani mazao.
Kauli
Mbiu ya Nane nane mwaka 2017 ni “ZALISHA KWA TIJA MAZAO YA KILIMO,MIFUGO NA
UVUVI ILI KUFIKIA UCHUMI WA KATI” ambapo Mikoa ya Kanda ya Ziwa Simiyu, Mwanza, Geita,
Mara, Shinyanga na Kagera imeadhimisha katika Uwanja wa Nyamhongo Ilemela
jijini Mwanza.
|
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na baadhi ya watumishi wa MEDA Economic
Development Associates inayojishughulisha na uzalishaji wa mbegu bora za Muhogo
wakati alipokagua banda lao katika Maadhimisho ya Nanenane Kanda ya Ziwa katika
Uwanja wa Nyamhongolo Wilaya ya Ilemela Jijini Mwanza
Afisa Uhusiano wa
Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) Kanda ya Ziwa,Martin Malima akimuonesha Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu baadhi ya bidhaa zilizokamatwa kutokana na kutokidhi ubora wa
kutumiwa na binadamu mara alipotembelea banda la mamlaka hiyo katika Maonesho
ya Nanenane Kanda ya Ziwa katika Uwanja
wa Nyamhongolo Ilemela Jijini Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akimkabidhi Mkuu wa Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
Halmashauri ya wilaya ya Busega,Juma Chacha zawadi ya kombe na cheti baada ya
Halmashauri hiyo kushika nafasi ya kwanza miongoni mwa Halmashauri za Mikoa ya
kanda ya Ziwa katika Maonesho ya Nanenane
Kanda ya Ziwa katika Uwanja wa Nyamhongolo Ilemela Jijini Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akipita kuona mashamba darasa ya zao la vitunguu
yaliyopandwa kwa kutumia mbolea aina ya
Yara katika Maonesho ya Nanenane Kanda
ya Ziwa katika Uwanja wa Nyamhongolo Ilemela Mkoani Mwanza.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wananchi waliohudhuria
katika Maonesho ya Nanenane Kanda ya
Ziwa katika Uwanja wa Nyamhongolo Ilemela Jijini Mwanza.
Katibu Tawala Mkoa wa
Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini (mwenye miwani) akipata maelezo kutoka kwa watalaam
wa Kilimo mara baada ya kutembelea Banda la Halmashauri ya Wilaya ya Busega na
kuona vitalu vya baadhi ya mazao ya Kilimo na biashara, katika Maonesho ya
Nanenane Kanda ya Ziwa katika Uwanja wa
Nyamhongolo Ilemela Jijini Mwanza.
Mkuu wa Wilaya ya Magu,
Mhe.Hadija Nyembo ambaye pia Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Ilemela akizungumza kabla
ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ambaye alikuwa Mgeni
Rasmi katika Kilele cha Maonesho ya Nanenane
Kanda ya Ziwa ili azungumze na wananchi katika Uwanja wa Nyamhongolo
Ilemela Jijini Mwanza,
Baadhi ya Wasanii wa
Ngoma aina ya Gobogobo kutoka Wilaya ya Misungwi Mwanza wakicheza na nyoka
wakati wakitoa burudani kwenye Kilele
cha Maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa katika
Uwanja wa Nyamhongolo Ilemela Jijini Mwanza.
Katibu Tawala Mkoa wa
Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini (wa pili kulia) akipata maelezo kutoka kwa wataalam
kuhusu asali bora baada ya kutembelea Banda la Halmashauri ya Wilaya ya
Itilima, kwenye Maonesho ya Nanenane
Kanda ya Ziwa katika Uwanja wa Nyamhongolo Ilemela Jijini Mwanza.
Katibu Tawala Mkoa wa
Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini (katikati) akipata maelezo kutoka kwa watalaam wa
Kilimo kuhusu zao la dengu mara baada ya kutembelea Banda la Halmashauri ya
Wilaya ya Busega na kuona vitalu vya baadhi ya mazao ya Kilimo na biashara, kwenye
Maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa
katika Uwanja wa Nyamhongolo Ilemela Jijini Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akifuatilia taarifa kwenye kipeperushi mara
baada ya kutembelea Banda la Benki ya Maendeleo yaKilimo (TADB) wakati wa
Kilele cha Maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa Uwanja
wa Nyamhongolo Ilemela Jijini Mwanza
, (wa pili kulia) Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa TADB Augustino Matutu
Chacha.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akipata zana
maelezo na watumishi wa kampuni ya KIRASA inayojihusisha na uuzaji wa
matrekta wakati alipotembela kuona zana hizo(hazipo pichani) kwenye Kilele cha
Maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa Uwanja wa Nyamhongolo
Ilemela Jijini Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akimkabidhi Mkulima Emmanuel Mgeta kutoka wilaya ya Busega
zawadi ya cheti na fedha taslimu baada ya mkulima huyo kushika nafasi ya tatu
wakulima walioshindanishwa kutoka katika Halmashauri za Mikoa ya kanda ya Ziwa
kwenye Maonesho ya Nanenane Kanda ya
Ziwa katika Uwanja wa Nyamhongolo Ilemela Jijini Mwanza.
Wasanii kutoka Wilaya
ya Ilemela Mwanza wakitoa burudani kwenye
Kilele cha Maonesho ya Nanenane
Kanda ya Ziwa katika Uwanja wa Nyamhongolo Ilemela Jijini Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akimkabidhi Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa TADB
Augustino Matutu Chacha zawadi ya kombe na cheti baada ya Benki
hiyo kushika nafasi ya kwanza kati
ya Taasisi zilizoshindanishwa katika Maonesho
ya Nanenane Kanda ya Ziwa katika Uwanja
wa Nyamhongolo Ilemela Jijini Mwanza..
Wasanii wa kundi la
Futuhi kutoka Mwanza wakitoa burudani kwenye
Kilele cha Maonesho ya Nanenane
Kanda ya Ziwa katika Uwanja wa Nyamhongolo Ilemela Jijini Mwanza.
Katibu Tawala Mkoa wa
Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini(wapili kulia) akipata maelezo kutoka kwa
Mjasiliamali anayetengeneza bidhaa za ngozi ikiwani njia ya kuongezea thamani
mazao ya mifugo baada ya kutembelea Banda la Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, kwenye
Kilele cha Maonesho ya Nanenane Kanda ya
Ziwa katika Uwanja wa Nyamhongolo Ilemela Jijini Mwanza.
Baadhi ya Viongozi
kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa waliohudhuria Kilele cha Maonesho ya
Nanenane Kanda ya Ziwa katika Uwanja wa
Nyamhongolo Ilemela Jijini Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka(wa pili kulia mstari wa mbele) na viongozi wengine kutoka
Mikoa ya Kanda ya Ziwa wakifurahi na kucheza muzika mara baada ya kuhitimisha
Maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa
katika Uwanja wa Nyamhongolo Ilemela Jijini Mwanza.
|
0 comments:
Post a Comment