Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula(Mb), ameziagiza Halmashauri nchini, kuyatambua
na kuyatolea taarifa maeneo yanayohodhiwa
na watu bila kuendelezwa na yale ambayo hayakupatikana kihalali ili Wizara
iweze kuchukua hatua stahiki.
Naibu Waziri huyo
ameyasema hayo alipotembelea eneo la hekta 13 katika Kijiji cha Kalago, Kata ya
Lamadi, Wilayani Busega lililokuwa linamilikiwa na Mwekezaji Hermati Pateli
kinyume cha sheria, ambaye amefutiwa hati na Serikali, kisha Halmashauri ya
Busega Mkoani Simiyu kuanza ujenzi wa mradi wa maji katika eneo hilo utakaonufaisha
vijiji vinne vya kata ya Lamadi.
Mhe.Mabula amesema Halmashauri zinapaswa
kutambua maeneo yasiyoendelezwa na yanayomilikiwa kinyume cha sheria na
kuwasilisha taarifa katika Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi ili yaweze
kuyarejesha kwa wananchi na kupangiwa matumizi mengine yenye manufaa zaidi kwa
jamii.
“Maeneo yote yaliyohodhiwa ambayo
hayajaendelezwa na ambayo pengine hayakupatikana kihalali, ni jukumu la
Halmashauri kuyatambua na kuleta taarifa
zake Wizarani ili Wizara iweze kuchukua hatua ya kuweza kuyarudisha katika
matumizi kwa Umma na yaweze kufaidisha watu wengi zaidi badala ya mtu mmoja”
amesema Naibu Waziri Angelina Mabula
Aidha,Naibu Waziri Mabula amebainisha sababu zilizopelekea Mwekezaji Hermati Pateli kufutiwa hati ya eneo hilo na Serikali kuwa ni udanganyifu
wa Uraia pamoja na upatikanaji wa hati ambao haukuzingatia sheria na taratibu za
nchi.
Naibu Waziri huyo
amesema eneo lililokuwa linamilikiwa na Mwekezaji huyo isivyo halali ambalo
limefutiwa hati miliki limegawanyika katika ploti mbili, ploti Namba 01 na
Namba 02 Block C lenye ukubwa wa hekta
7.62 na Block Namba 03 C hekta 5.45.
Akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula(Mb), Mhandisi Mshauri wa
Mradi wa Maji wa Lamadi kutoka Kampuni ya EAU Consult, Baraka Felix amesema
Tanki la Maji litakalojengwa katika eneo hilo litakuwa na uwezo wa kuzalisha
mita za ujazo 3000 kwa siku.
Naye Mkurugenzi Mtendaji
wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Anderson Njiginya amesema Mradi wa Maji wa Lamadi unaojengwa katika eneo hilo
utawanufaisha wananchi wa Vijiji Vinne vya Kalago, Lamadi, Lukungu na Mwabayanda.
Mradi huu wa maji unaojengwa katika eneo hili lililokuwa
linamilikiwa isivyo halali na Mwekezaji Pateli, utagharimu kiasi cha Yuro
milioni 2.8, na unatarajiwa kukamilika ifikapo Mei, 2019.
Mhandisi
Baraka Felix kutoka Kampuni ya EAU Consult akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula(Mb)(kulia) alipotembelea
eneo la hekta 13 katika Kijiji
cha Kalago, Kata ya Lamadi, Wilayani Busega lililokuwa linamilikiwa na Mwekezaji
Hermati Pateli kinyume cha sheria, ambaye amefutiwa hati na Serikali
Mhandisi Baraka Felix kutoka Kampuni ya EAU Consult akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula(Mb)(kulia) alipotembelea kuona Ujenzi wa Ofisi ya Mamlaka ya Maji Lamadi itakayosimamia mradi wa maji wa Lamadi unaojengwa katika eneo lililokuwa linamilikiwa na Mwekezaji Hermati Pateli kinyume cha sheria, ambaye amefutiwa hati na Serikali
Mhandisi Baraka Felix kutoka Kampuni ya EAU Consult akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula(Mb)(kulia) alipotembelea kuona Ujenzi wa Ofisi ya Mamlaka ya Maji Lamadi itakayosimamia mradi wa maji wa Lamadi unaojengwa katika eneo lililokuwa linamilikiwa na Mwekezaji Hermati Pateli kinyume cha sheria, ambaye amefutiwa hati na Serikali
Naibu Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula(Mb)akizungumza na waandishi
wa habari katika mahojiano maalum mara
baada ya kutembelea eneo la hekta 13 katika Kijiji cha
Kalago, Kata ya Lamadi, Wilayani Busega lililokuwa linamilikiwa na Mwekezaji
Hermati Pateli kinyume cha sheria, ambaye amefutiwa hati na Serikali.
Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula(Mb) akipokea
maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega,
Anderson Njiginya wakati alipotembelea eneo la hekta 13 katika Kijiji cha Kalago, Kata ya
Lamadi, Wilayani Busega lililokuwa linamilikiwa na Mwekezaji Hermati Pateli
kinyume cha sheria, ambaye amefutiwa hati na Serikali.
Naibu Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula(Mb) (wa pili kushoto) akizungumza
na baadhi ya Viongozi wa Wilaya ya Busega mara baada ya kutembelea eneo la hekta 13 katika Kijiji cha Kalago, Kata ya Lamadi, Wilayani Busega lililokuwa
linamilikiwa na Mwekezaji Hermati Pateli kinyume cha sheria, ambaye amefutiwa
hati na Serikali, (kushoto) Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe.Tano Mwera.
Msajili Msaidizi wa
Baraza la Ardhi Kanda ya Ziwa, Dorothy Moses akitoa ufafanuzi juu ya hoja
mbalimbali zilizowasilishwa na watumishi wa Idara ya Ardhi katika kikao cha
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb)
na watumishi hao Wilayani Busega(hawapo pichani).
0 comments:
Post a Comment