Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ameitaka Kamati ya Ulinzi na Usalama ya
Wilaya ya Meatu mkoani humo, ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo,Dkt. Joseph
Chilongani kutekeleza kwa weledi, uadilifu na haki zoezi la kuondoa mifugo kwenye
maeneo ya hifadhi litakaloanza September 04, 2017.
Mtaka
ametoa kauli hiyo mara baada ya viongozi wa Serikali na Chama Mkoa na Wilaya,
Wataalam, wafugaji na wadau wa uhifadhi na Utalii kukutana na kujadili suala la
uondoaji mifugo katika Maeneo ya Hifadhi, yakiwemo ya Pori la Akiba la Maswa, Ranchi ya MWIBA na
Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori (WMA) Makao wilayani Meatu.
“Mkafanye zoezi hili
kwa weledi mkubwa na haki, lisije likawa zoezi la kuwaonea watu, kufanya
utapeli kwa kujifanya mnachukua ng’ombe kwa ajili ya kutaifisha halafu
mkagawana; viongozi na wote mtakaohusika mkalisimamie kwa makini sana suala
hili” alisisitiza Mtaka
Mkuu wa Wilaya ya Meatu Mhe.Joseph
Chilongani amesema baada ya makubaliano yaliyofikiwa kati ya viongozi, wafugaji
na wadau wa uhifadhi na utalii ametoa muda wa siku nne na kufikia Septemba 04
mwaka huu, wafugaji wawe wametoa mifugo katika maeneo ya hifadhi kwa hiari.
Dkt.Chilongani amebainisha kuwa Viongozi
wa Wilaya ya Meatu walikutana na wafugaji katika maeneo yao na kuwatahadhalisha
juu ya uingizwaji wa mifugo kwenye maeneo ya hifadhi, ili kuwasaidia waepuke
adhabu ya kifungo na mifugo yao kutaifishwa kwa kuwa kuingiza mifugo hifadhini ni
makosa kwa mujibu wa sheria.
“Maandalizi yote yako tayari, timu za
kutekeleza zoezi hili zote zipo, nitoe muda wa siku hizi zilizobaki ili kufikia
Jumatatu ya tarehe 04 zoezi la kuondoa mifugo kwenye Pori la Akiba la Maswa,
Ranchi ya MWIBA na WMA ya Makao lianze, tulishawapa wafugaji muda wa kutosha tulipokuwa
tukipita kwenye vijiji kuzungumza nao juu ya madhara ya kuingiza mifugo hifadhini” amesema.
Kwa upande wake Meneja wa Pori la Akiba
la Maswa Lasato Masinde amezitaja baadhi ya changamoto za kuingiza mifugo
katika maeneo ya Hifadhi kuwa ni ushindani wa malisho na maji kati ya
wanyamapori na wafugwao,ongezeko la ujangili, kuuwawa kwa wanyamapori hasa
walao nyama, magonjwa na mmonyoko wa udongo kutokana na wafugaji kukata miti.
Aidha, Masinde amefafanua kuwa suala la
uingizwaji wa mifugo katika hifadhi linachangiwa pia na baadhi ya viongozi wa
vijiji wasiokuwa waadilifu ambao hupokea fedha kwa wafugaji na kuwaruhusu
kuingiza mifugo yao, jambo ambalo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka
amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Meatu kuwachukulia hatua stahiki
wale wote watakaobainika kujihusisha na uhalifu huo.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa wito kwa wafugaji kupima maeneo yao wanayomiliki
na kuyawekea miundombinu ya mifugo kama vile visima vya maji na mabwawa,
majosho na mashamba ya malisho ili waweze kufuga kisasa na kuondokana na adha
ya kuhangaika kutafuta maji na malisho.
Katika kikao hicho wafugaji kwa pamoja
wamekubali kutoa mifugo katika maeneo ya
hifadhi na kukubaliana na ushauri wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu wa kupima maeneo
yao na kuweka miundombinu, hivyo wameomba watalaam wa Ardhi na Mifugo waweze
kuwasaidia namna wanavyoweza kutumia maeneo yao kufuga kisasa.
|
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na viongozi, watalaam,wafugaji na wadau
mbalimbali wa uhifadhi katika kikao maalum cha kujadili suala la kuondoa mifugo
katika Pori la akiba la Maswa, Ranchi ya MWIBA na Jumuiya ya Hifadhi ya
Wanyamapori ya Makao wilayani Meatu.
Mkuu wa Wilaya ya
Meatu, Dkt.Joseph Chilongani akizungumza na viongozi, watalaam,wafugaji na
wadau mbalimbali wa uhifadhi katika kikao maalum cha kujadili suala la kuondoa
mifugo katika Pori la akiba la Maswa, Ranchi ya MWIBA na Jumuiya ya Hifadhi ya
Wanyamapori ya Makao wilayani humo.
Baadhi ya viongozi na
watalaam wa Mkoa wa Simiyu na Wilaya ya Meatu,wafugaji na wadau mbalimbali wa
uhifadhi wakifuatilia hoja mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa katika kikao
maalum cha kujadili suala la kuondoa mifugo katika Pori la akiba la Maswa, Ranchi
ya MWIBA na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao wilayani Meatu.
Meneja wa Pori la Akiba
la Maswa, Lusato Masinde akiwasilisha taarifa yake kwa viongozi na watalaam wa
Mkoa wa Simiyu na Wilaya ya Meatu,wafugaji na wadau mbalimbali wa uhifadhi
katika kikao maalum cha kujadili suala la kuondoa mifugo katika Pori la akiba
la Maswa, Ranchi ya MWIBA na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao
wilayani Meatu.
Katibu
wa Jumuiya ya Hifadhi ya Wanayamapori ya Makao, Robert Simon akiwasilisha
taarifa yake kwa viongozi na watalaam wa Mkoa wa Simiyu na Wilaya ya
Meatu,wafugaji na wadau mbalimbali wa uhifadhi katika kikao maalum cha kujadili
suala la kuondoa mifugo katika Pori la akiba la Maswa, Ranchi ya MWIBA na
Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao wilayani Meatu.
Mhifadhi kutoka Ranchi
ya MWIBA, Julius Makaroti akiwasilisha
taarifa ya ranchi hiyo kwa viongozi na watalaam wa Mkoa wa Simiyu na Wilaya ya
Meatu,wafugaji na wadau mbalimbali wa uhifadhi katika kikao maalum cha kujadili
suala la kuondoa mifugo katika Pori la akiba la Maswa, Ranchi ya MWIBA na
Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao wilayani Meatu.
Katibu wa CCM Mkoa wa
Simiyu, Ndg.Donald Magesa akizungumza na viongozi, watalaam,wafugaji na wadau
mbalimbali wa uhifadhi katika kikao maalum cha kujadili suala la kuondoa mifugo
katika Pori la akiba la Maswa, Ranchi ya MWIBA na Jumuiya ya Hifadhi ya
Wanyamapori ya Makao wilayani Meatu.
Mwenyekiti wa CCM
wilaya ya Meatu, Mhe.Juma Mwiburi akizungumza na viongozi, watalaam,wafugaji na
wadau mbalimbali wa uhifadhi katika kikao maalum cha kujadili suala la kuondoa
mifugo katika Pori la akiba la Maswa, Ranchi ya MWIBA na Jumuiya ya Hifadhi ya
Wanyamapori ya Makao wilayani Meatu.
Mmoja wa wafugaji wa
Wilaya ya Meatu akichangia hoja katika kikao kilichofanyika wilayani Meatu
kujadili suala la kuondoa mifugo katika Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya
Makao, Pori la Akiba la Maswa na Ranchi ya Mwiba wilayani humo.
Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Mhe.Pius Machungwa akichangia hoja katika kikao
kilichofanyika wilayani Meatu kujadili suala la kuondoa mifugo katika Jumuiya
ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao, Pori la Akiba la Maswa na Ranchi ya Mwiba
wilayani humo.
Mwenyekiti wa Kijiji
cha Makao wilayani Meatu na ambaye pia ni mfugaji, Anthony Philipo akichangia
hoja katika kikao kilichofanyika wilayani Meatu kujadili suala la kuondoa
mifugo katika Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao, Pori la Akiba la
Maswa na Ranchi ya Mwiba wilayani humo.
Mwanasheria wa
Halmashauri ya Wilaya ya Meatu,Said Samba akifafanua jambo katika kikao kilichofanyika
Mjini Mwanhuzi kujadili suala la kuondoa
mifugo katika Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao, Pori la Akiba la
Maswa na Ranchi ya Mwiba wilayani humo.
Mhifadhi
kutoka Shirika la Frankfoot, Sylevester Bwasama akifafanua jambo katika kikao
kilichofanyika Mjini Mwanhuzi kujadili
suala la kuondoa mifugo katika Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao, Pori
la Akiba la Maswa na Ranchi ya Mwiba wilayani humo.
|
0 comments:
Post a Comment