Mkoa
wa Simiyu umejipanga kufanya mapinduzi ya Kilimo kupitia skimu kubwa ya
Umwagiliaji inayotarajiwa kuanza kutekelezwa hivi karibuni, kwa lengo la
kuwainua wananchi Kiuchumi na kukabiliana na upungufu wa chakula.
Hayo
yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka katika kikao
kilichofanyika kati ya Viongozi na Wataalam ngazi ya Mkoa,Wilaya na wananchi wa
vijiji vya Kata ya Mwamanyili Wilayani Busega kujadili juu ya mipango ya
utekelezaji wa skimu hiyo.
Amesema katika Skimu
hiyo Halmashauri ya Wilaya ya Busega itaingia mkataba na kukopa fedha kutoka
Benki ya Maendeleo ya Kilimo(TADB) ambayo tayari imekubali kutoa mkopo huo, ili
kuwezesha ujenzi wa miundombinu ya maji kutoka Ziwa Victoria kwenda kwenye
mashamba, kuwawezesha wananchi kununua mbegu bora, mbolea, na zana bora za
kilimo.
Aidha, ameeleza kuwa
wananchi katika skimu hiyo watazalisha mpunga kwa misimu miwili kwa mwaka na
kupanda mazao mengine mbadala hususani ya jamii ya mikunde mara baada ya kuvuna
mpunga, kwa ajili ya kurutubisha Ardhi.
Mtaka amefafanua kuwa
Uongozi wa Halmashauri kwa kushirikiana na wananchi wenye mashamba katika Skimu
ya Umwagiliaji ya Mwamanyili watakaa kupanga namna bora ya urejeshaji wa mkopo
huo, ambapo amewataka wananchi kuwa waaminifu kutekeleza utaratibu watakaokubaliana.
Ameongeza kuwa kutokana
na uwepo wa Maji ya Uhakika ya Ziwa Victoria mkoa umekusudia kufanya mapinduzi
katika Sekta ya Kilimo na kujenga jamii ya watu wanaoishi kijasiriamali ili
waweze kulima kisasa na kibiashara na kuongeza tija katika uzalishaji.
“Tungehitaji tufanye mapinduzi
ya Kilimo ili hata siku Mhe.Rais atakapofanya ziara ya kikazi, anakuja kuliona
shamba la ekari 2050 za wale walioitwa maskini; tunataka Wilaya ya Busega iwe
ya mfano hapa Tanzania ambayo wananchi wake wanalima bila kutegemea mvua”
amesema Mtaka.
Kwa upande wake Diwani
wa Kata ya Mwamanyili Mhe.Charles Luhenze ametoa wito kwa wananchi wa kata hiyo
kuchangamkia fursa hiyo na kuwataka kutoa ushirikiano kwa watalaam wanaoendelea
na kazi mbalimbali za kitaalam katika eneo la Skimu hiyo kila watakapohitajika.
Naye Malibe Misalaba
Sitta mkazi Kijiji cha Nasa Ginnery kata ya Mwamanyili amemshukuru Mkuu wa Mkoa
wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka kwa juhudi alizozionesha katika kuhakikisha
wananchi wa wilaya ya Busega wanafanya Kilimo cha Umwagiliaji, hivyo akaomba
mipango iliyobaki ikamilike haraka ili Skimu hiyo ianze kutekelezwa mara moja
Paulo Buchenja mkazi wa
Kijiji cha Mwanangi kata ya Mwamanyili amesema vijana wengi wamehamasika kulima
kilimo cha Umwagiliaji wakiamini kuwa kupitia skimu hiyo watalima kisasa ambapo
wataongeza uzalishaji hali itakayopelekea kujikomboa kiuchumi.
Skimu ya Umwagiliaji Mwamanyili
Busega itatekelezwa katika eneo lenye ukubwa wa ekari 2050, wananchi watalima
kisasa(kitaalam) na kibiashara ambapo mavuno yanatarajiwa kuanzia magunia 30
hadi 40 kwa ekari.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na
wananchi wa Kata ya Mwamanyili, juu ya Skimu ya Umwagiliaji unaotarajiwa kuanza
kutekelezwa hivi karibuni katika kata hiyo Wilayani Busega.
Mkuu wa Wilaya ya
Busega, Mhe.Tano Mwera akizungumza na
wananchi wa Kata ya Mwamanyili, juu ya Skimu ya Umwagiliaji inaotarajiwa kuanza kutekelezwa
hivi karibuni katika kata hiyo Wilayani Busega.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Busega Tano Mwera wakifurahia
jambo kabla ya kuanza kikao na wananchi wa Kata ya Mwamanyili kujadiliana juu
ya Skimu ya Umwagiliaji inayotarajiwa
kuanza kutekelezwa hivi karibuni katika kata hiyo Wilayani Busega.
Diwani wa Kata ya
Mwamanyili Mhe. Charles Luhenze akizungumza na wananchi wa Kata ya Mwamanyili,
juu ya Skimu ya Umwagiliaji inaotarajiwa kuanza kutekelezwa hivi karibuni
katika kata hiyo Wilayani Busega.
Baadhi
ya wananchi wa Kata ya Mwamanyili wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony
Mtaka (hayupo pichani) katika kikao cha kujadiliana juu ya Skimu ya Umwagiliaji
inayotarajiwa kuanza kutekelezwa hivi karibuni katika kata hiyo Wilayani
Busega.
Ndg.Shadrack Yohana
Mkazi wa Kijiji cha Nasa Ginnery Kata ya Mwamanyili,akichangia jambo katika
kikao cha Viongozi wa Mkoa, Wilaya ya Busega na wananchi kilichofanyika katika
Kijiji cha Mwamanyili, kwa lengo la
kujadili juu ya Skimu ya Umwagiliaji inayotarajiwa kuanza kutekelezwa hivi
karibuni katika kata hiyo Wilayani Busega.
Baadhi ya wananchi wa
Kata ya Mwamanyili wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka
(hayupo pichani) katika kikao cha kujadiliana juu ya Skimu ya Umwagiliaji inayotarajiwa
kuanza kutekelezwa hivi karibuni katika kata hiyo Wilayani Busega.
Baadhi ya wananchi wa
Kata ya Mwamanyili wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka
(hayupo pichani) katika kikao cha kujadiliana juu ya Skimu ya Umwagiliaji inayotarajiwa
kuanza kutekelezwa hivi karibuni katika kata hiyo Wilayani Busega.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na
wananchi wa Kata ya Mwamanyili, juu ya maandalizi ya Skimu ya Umwagiliaji inayotarajiwa
kuanza kutekelezwa hivi karibuni katika kata hiyo Wilayani Busega.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na
wananchi wa Kata ya Mwamanyili, juu ya maandalizi ya Skimu ya Umwagiliaji inayotarajiwa
kuanza kutekelezwa hivi karibuni katika kata hiyo Wilayani Busega.
0 comments:
Post a Comment