Mkuu wa Simiyu Mhe.
Anthony J. Mtaka amepiga marufuku tabia ya viongozi wa kimila kuwaadhibu
wananchi wanaobanika kuwa kuwa na makosa
kupita mabaraza ya kimila maaarufu kama
DAGA SHIDA na badala yake amewataka
watumie vyombo vya Serikali vinavyotambulika kisheria.
Mtaka alitoa agizo hilo
alipozungumza na wananchi wa kijiji cha Ikindilo kata ya Ikindilo tarafa ya
Bumela wilayani Itilima, ambapo ameitaka Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani
Itilima, kulisimamia suala hilo kwa kuwa limekuwa likiwadharirisha wananchi na wale
watakaobainika kukaidi agizo hilo, wafikishwe kwenye vyombo vya sheria na
kuchukuliwa hatua.
“Mkuu wa Wilaya na
wajumbe wako kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya, simamieni suala hili na mhakikishe
linakomeshwa kabisa. Naagiza hili kwa
mkoa mzima sitaki kusikia kitu kinachoitwa daga shida. Hatuwezi kuacha wananchi
wanateseka, watumishi wetu tunaowaleta kuwatumikia wananchi nao wanateseka na
mifumo kandamizi kama hii wakati vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vipo”alisema
Mtaka
Aidha, Mkuu huyo wa
Mkoa aliwataka wananchi watakaoitwa kwa ajili ya kwenda kuadhibiwa na viongozi
wa mabaraza ya kimila maarufu kama Sumbantale wasikubali na wawatake viongozi
hao wa kimila kuwashtaki katika ofisi za
Serikali au katika Vituo vya polisi ikiwa watajiridhisha kuwa wana makosa.
Mfumo wa daga shida
umekuwa ukitumwa katika maeneo mengi mkoani Simiyu, ambapo wananchi hususani watumishi wa umma wamekuwa
wakiadhibiwa na viongozi wa kimila kwa kuwataka kulipa faini ya fedha , mazao,
wanyama na kupigwa pale wanapoonekana kwenda
kinyume na matakwa yao ya kimila na wakati mwingine wamekuwa wakizushiwa .
Wakati huo huo Mtaka
amewataka wazazi na walezi kuacha mara
moja tabia ya kuwakatisha masomo watoto
wao wa kike na kuwaozesha kwa kuwa wakiendelea kufanya hivyo watachukuliwa
hatua kali za kisheria.
“Ole wake mzazi au
mlezi atakayemtoa mtoto shule na akaenda
kumuozesha,ajue ameamua kuhamishia maisha yake toka nyumbani kwenda jela, hilo
halina mjadala. Mtoto wa shule ni wako kwa kuwa umemzaa lakini akiwa shule toka
darasa la kwanza mpaka kidato cha sita
ni mali ya serikali” alisema Mtaka.
0 comments:
Post a Comment