Wakazi wa kijiji cha
Ikindilo wilayani Itilima wamelishukuru Shirika la dini la Life Minisry kwa
kuwatoa katika adha ya maji iliyokuwa ikiwakabili kwa kuwachimbia kisima kirefu
chenye thamani ya shilingi milioni 50.
Akizungumza mara baada
ya uzinduzi wa kisima hicho uliofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
. J. Mtaka , mkazi wa kijiji cha Ikindilo bibi . Monica Malugu alisema kisima
hicho kimewasadia kuondokana na ashida ya kufuata maji kwa mwendo mrefu.
“Nawashukuru sana
wafadhili kwa kutukumbuka wana Ikindilo kwa kutuchimbia kisima hiki, tulikuwa
tunafuata mbali yaani tulikuwa tunatembea zaidi ya masaa matatu. Tulikuwa
tunaamka usiku kwenda kufuata maji na
wakati mwingine tukichelewa kurudi tunapigwa na waume zetu” alisema Bibi
Monica.
Akitoa shukrani kwa
niaba ya Serikali, Mkuu wa mkoa wa Simiyu amesema Serikali inatambua na
kuthamini mchango wa mashirika ya dini katika maendeleo ya nchi ya Tanzania na
watu wake na akaahidi kuulinda mradi huo na miradi mingine ya Life Ministry
inayotekelezwa katika mkoa wa Simiyu.
Aidha, Mtaka alisema
wafadhili kama hao wamekuwa wadau wakubwa wa maendeleo tangu uhuru hivyo aliwahakikishia kuwa watapata ushirikiano wa
kotosha kutoka kwa Viongozi wa Serikali ngazi ya kijiji hadi Mkoa pale
watakapohitaji kutekeleza miradi mingine
ya maendeleo.
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa Life Ministry Tanzania Bw.Dismas Shekalaghe aliwataka wakazi wa
Ikindilo kukilinda na kukitunza kisima hicho na miundombinu yake ili kiwanufaishe
kwa kuwapa huduma ya maji safi iliyo
endelevu, ambapo walaihidi kukifanyia ukarabati kila baada ya mwaka mmoja.
Shirika la Life
Ministry linafanya kazi katika nchi zaidi ya 198 duniani, Pamoja na kuchimba
visima vitatu katika mkoa wa Simiyu wanatarajia
kuwasaidia wananchi katika maeneo
mengine, hususani kilimo cha mboga mboga
ili kuwakwamua katika umasikini.
0 comments:
Post a Comment