Mfuko wa
Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umekabidhi hundi ya shilingi bilioni 1.5 kwa
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu, fedha ambazo ni mkopo kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda cha
Chaki Wilayani humo na kuongeza uzalishaji.
Hundi hiyo
imekabidhiwa kwa Waziri wa Nchi Ofisi Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi,
Ajira,Vijana na wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama kwa niaba ya Serikali na
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Prof.Godius Kahyarara wilayani Maswa mkoani Simiyu.
Akizungumza
wakati wa makabidhiano ya hundi hiyo Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Prof.Godius
Kahyarara amepongeza Mkoa wa Simiyu kwa kutekeleza Sera ya Ujenzi wa Uchumi wa
Viwanda kwa vitendo na kuwataka viongozi
wa mkoa huo kutokatishwa tamaa.
Amesema
NSSF kama Shirika la Umma linatekeleza sera na maelekezo ya Serikali na wametoa
mkopo huo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ili wafanye upanuzi wa kiwanda cha
chaki na kuongeza uzalshaji kwa kuwa suala la Viwanda ni la kipaumbele.
Waziri wa Nchi
Ofisi Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi, Ajira,Vijana na watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama
amesema kiwanda cha Chaki Maswa kimebeba ujumbe na dhana ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli ya kushikamanisha Uchumi wa
Viwanda na Maendeleo ya watu kwa sababu kinatumia malighafi ya hapa nchini.
Aidha,
amesema kiwanda hiki kitawanufaisha Watanzania hususani vijana wa Mkoa wa
Simiyu ambao watafanya kazi moja moja katika kiwanda na wale wataohusika katika
uchimbaji wa malighafi ambayo inapatikana maeneo mengine hapa nchini.
“Asilimia 56 ya
nguvukazi hapa Tanzania ni vijana na vijana wengi bado hawana ajira lakini
kiwanda hiki kitasaidia, kwa kuwa sehemu ya hiyo asilimia 56 wataajiriwa katika
kiwanda na wengine watapata ajira huko mkoani Singida ambako malighafi ya kutengenezea
chaki inapatikana” amesema.
Mhe.Mhagama
ameongeza kuwa kiwanda kitatatua tatizo la upatikanaji wa chaki hapa nchini,kitaokoa
fedha kwa kuwa chaki zitauzwa kwa bei nafuu na kitaongeza mapato ya fedha za
kigeni kwa kuwa chaki zitakazozalishwa zitauzwa katika soko la nje ya nchi.
Naye
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka amesema Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
imeonesha mfano katika kutekeleza agizo la Rais wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe
Magufuli la kubuni vyanzo vipya vya mapato kwa kujenga kiwanda hicho kikubwa,
ambapo amesema kufikia mwaka 2020 Halmashauri za Mkoa wa Simiyu zitakuwa mfano
kwa kuwa na miradi yake zenyewe .
“Kama Halmashauri zinakopa mabilioni
kujenga stendi, masoko kwa nini zisikope kujenga viwanda, zikatumia malighafi
ya hapa nchini zikaajiri Watanzania
wakapata kipato na nchi yetu ikanufaika; Halmashauri za Mkoa wa Simiyu
zitaajiri na kwenye miaka mitano ya Mhe.Rais tutatoa mfano wa kuwa Halmashauri zenye
miradi yake” amesema.
Kwa
upande wake Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar , Mhe.Riziki Pembe Juma amesema Zanzibar ni wadau wakubwa wa Chaki
zinazotengenezwa Maswa(Maswa Chalks), hivyo ameomba ushirikiano ulioanzishwa
kati ya Zanzibar na Simiyu udumu ili kufikia malengo katika kukuza kiwango cha
elimu na utekelezaji wa Sera ya Viwanda.
Kiwanda
cha kutengeneza chaki Wilayani Maswa kwa sasa kinazalisha katoni zaidi ya 180
kwa siku na chaki hizo zinatumika katika shule zilizopo katika maeneo tofauti
hapa nchini, ikiwa ni pamoja na mikoa
yote za Zanzibar na baadhi ya mikoa ya Tanzania bara ikiwemo Simiyu, Mwanza, Shinyanga,
Geita na Tabora.
Mkurugenzi
Mkuu wa NSSF Prof.Godius Kahyarara(kushoto) akimkabidhi Waziri wa Nchi Ofisi
Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi, Ajira,Vijana na wenye Ulemavu, Mhe. Jenista
Mhagama hundi ya shilingi bilioni 1.5 zilizotolewa na NSSF kama mkopo kwa ajili
ya upanuzi wa kiwanda cha chaki Maswa, (kulia) Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka.
Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu(wa tatu kushoto), viongozi wa Wilaya ya Maswa wakimkabidhi
Meneja wa Benki ya Azania( wa pili kulia) Hundi ya shilingi bilioni 1.5 zilizotolewa na NSSF kwa ajili ya
upanuzi wa kiwanda cha chaki wilayani humo ili aendelee na taratibu za kibenki.
Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Prof. Godius
Kahyarara(kulia) wakiteta jambo wakati
wa hafya ya makabidhiano ya hundi ya
shilingi bilioni 1.5 zilizotolewa na NSSF kama mkopo kwa ajili ya upanuzi wa
kiwanda cha chaki Wilayani Maswa.
Waziri wa
Nchi Ofisi Waziri Mkuu, Mhe.Jenista Mhagama(wa tatu kulia), Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Serikali ya Mapinduzi (wa pili kulia) katika picha ya pamoja na viongozi wa Mkoa, wilaya ya
Maswa na Vijana wa Maswa Family wanaofanya kazi katika kiwanda cha chaki.
Waziri wa Nchi Ofisi Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi, Ajira,Vijana na wenye
Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akipokea taarifa ya Upembuzi yakinifu wa panuzi
wa kiwanda cha chaki cha Maswa kutoka kwa mtalaam wa Taasisi ya Masuala ya
Kiuchumi na Kijamii(ESRF), Deodatus Sagamiko.
Waziri wa Elimu na Mafunzo
ya Amali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar , Mhe.Riziki Pembe Juma
akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakati wa hafla ya makabidhiano ya Hundi
ya shilingi bilioni 1.5 zilizotolewa na NSSF kama
mkopo kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda cha chaki Maswa.
Waziri wa
Nchi Ofisi Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi, Ajira,Vijana na wenye Ulemavu, Mhe.
Jenista Mhagama( wa pili kushoto) akiangalia kikundi cha ngoma mara mara baada
ya kuwasilisi wilayani Maswa, kwa ajili ya makabidhiano ya
Hundi ya shilingi bilioni 1.5 zilizotolewa na
NSSF kama mkopo kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda cha chaki Maswa.
Msanii
Elizabeth Maliganya (kulia) na baadhi ya waimbaji wa Kwaya ya Kanisa la AICT Bariadi
(wenye sare za vitenge) wakicheza na viongozi mbalimbali mara baada ya makabidhiano
ya hundi
ya shilingi
bilioni 1.5 zilizotolewa na NSSF kama mkopo kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda cha
chaki Maswa.
Waziri wa
nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama(wa tano kulia), Waziri wa Elimu
Zanzibar (mwenye ushungi mwekundu), mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka
(wa sita kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa wilaya ya Maswa na
wadau wengine wa maendeleo baada ya makabidhiaono ya Hundi ya
shilingi bilioni 1.5 zilizotolewa na NSSF kama mkopo kwa ajili
ya upanuzi wa kiwanda cha chaki Maswa.
Waziri wa
nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama katika picha ya pamoja na viongoziwa
mkoa na wakuu wa idara wa Halmasahuri ya Wilaya ya Maswa baada ya makabidhiaono
ya Hundi ya shilingi bilioni 1.5 zilizotolewa
na NSSF kama mkopo kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda cha chaki Maswa.
Waziri wa
Nchi Ofisi Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi, Ajira,Vijana na wenye Ulemavu, Mhe.
Jenista Mhagama akisalimiana na Mbunge wa Maswa Mashariki, mhe.Stanslaus Nyongo
mara baada ya kuwasili wilayani Maswa, kwa ajili ya makabidhiano ya
Hundi ya shilingi bilioni 1.5 zilizotolewa na
NSSF kama mkopo kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda cha chaki Maswa.
Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akitoa salamau za mkoa wakati wa hafla ya makabidhiano
ya
Hundi ya shilingi bilioni 1.5 iliyotolewa na
NSSF kama mkopo kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda cha chaki Maswa.
Baadhi ya
viongozi katika Mkoa wa Simiyu wakifuatilia masuala mbalimbali katika hafla ya makabidhiano
ya
Hundi ya shilingi bilioni 1.5 zilizotolewa na
NSSF kama mkopo kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda cha chaki Maswa.
0 comments:
Post a Comment