Mabaraza
ya Madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Busega na Meatu Mkoani Simiyu
yameridhia Halmashauri hizo kukopa shilingi bilioni 17.1 kutoka Benki ya
Maendeleo ya Kilimo (TADB), kwa ajili ya kutekeleza Miradi mikubwa miwili ya Maendeleo.
Maridhiano
hayo yamefikiwa katika Vikao vya dharura vya mabaraza ya madiwani
vilivyofanyika kwa nyakati tofauti, ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Busega imepanga
kukopa shilingi bilioni 10.7 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa Kilimo cha
Umwagiliaji katika Bonde la Mwamanyili (eneo la ekari 2050) na Meatu shilingi bilioni 6.4 kwa ajili ya
upanuzi wa kiwanda cha maziwa(MEATU MILK).
Akiwasilisha taarifa ya Maendeleo ya Mpango wa
Kilimo cha Umwagiliaji Wilayani Busega, Afisa Mipango wa Wilaya hiyo Josephat
Joseph, amesema hadi sasa kazi za upimaji wa mashamba na njia ya kupita bomba
la maji, kupima udongo, kusanifu mfereji mkuu kwenye chanzo, sehemu ya
kuchukulia maji, nyumba za pampu, mifereji ya kuingiza na kutolea maji,kuandaa
michoro na gharama za mradi zimeshakamilika.
Aidha, amesema
katika utekelezaji wa mradi huu Halmashauri ndiyo msimamizi mkuu wa mradi na itajenga
miundombinu yote ya umwagiliaji, hivyo itaingia makubaliano na wakulima wa
Mwamanyili kupitia umoja wao watakaounda katika kutekeleza shughuli za mradi.
Nao wakulima wa
Bonde la Mwamanyili wamesema wameupokea mradi huo kwa mikono miwili na kwa sasa
wamesitisha shughuli zote za Kilimo katika bonde hilo, ili kupisha shughuli nyingine
za maandalizi ya ujenzi wa miundombinu ya mradi huo.
“ Tunawashukuru viongozi
wetu kwa kutusaidia kupata mkopo wa kutekeleza mradi huu naupokea kwa mikono
miwili tena natamani uanze haraka, sasa hivi hatutalima maeneo yetu tunapisha
wataalam waendelee na shughuli za maandalizi ya mradi ili wakikamilisha tu
tuanze ” alisema Joseph Mayala.
Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amesema kutekelezwa
kwa mradi huo, kutaiandikia historia wilaya ya BUSEGA kwa
kuwainua wananchi kiuchumi na kuondokana na aibu ya kuomba chakula cha msaada
Serikalini, ambapo amesisitiza kuwa utakuwa mradi wa pekee ambao mnyororo wake
wa thamani utaonekana kupitia mazao yatakayolimwa hususani mpunga.
Kwa upande wa
Mradi wa Upanuzi wa Kiwanda cha Maziwa Meatu, Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Fabian Manoza amesema kuelekea upanuzi wa
kiwanda hicho, Halmashauri imekusudia kuongeza idadi ya wafugaji wanaopeleka
maziwa kiwandani kutoka 45 wa sasa na kufikia wafugaji 400 wakubwa ambao wanafuga
ng’ombe wa kisasa.
Mikakati mingine
ni kununua mtambo mpya wa kuchakata maziwa wenye uwezo wa kuchakata lita elfu
15,000 kwa siku, kununua Mitamba 1000 na kuandaa shamba la malisho lenye
miundombinu muhimu pamoja na kuongeza soko la MEATU MILK kwa kuingia mikataba
na mawakala na kuweka maduka katika baadhi ya miji mikubwa.
Wafugaji wa
Wilaya ya Meatu wamesema wameupokea mradi wa upanuzi wa kiwanda cha maziwa
wilayani humo kwa furaha, kwani utawasaidia kuongeza upatikanaji wa soko la
uhakika la maziwa.
Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Mhe.Pius Machungwa ametoa wito kwa wafugaji kukubali
kubadilika na kuanza kufuga kisasa kulingana na jinsi wanavyoshauriwa na
wataalam ili kuongeza tija.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema Serikali
mkoani humo imejipanga kutafuta majawabu
ya changamoto za wafugaji kwa kuwasaidia kufuga kisasa, ikiwa ni pamoja na
kuwashauri kupima maeneo yao na kuyawekea miundombinu muhimu kama mabwawa,
visima, majosho na mashamba ya malisho.
“Kiwanda mnachokihitaji
hapa kitatumia lita 15,000 kwa siku, mnapaswa kuweka mikakati mizuri ya ng’ombe
wenu ili muwe na uhakika wa maziwa, nayazungumza haya ili kila mmoja aone
umuhimu wa kiwanda; tuwasaidie wafugaji wafuge kisasa na kwa tija” alisema
Mtaka.
Halmashauri ya
Wilaya ya Busega na Meatu zinatarajia kupata Mkopo kutoka Benki ya Maendeleo ya
Kilimo ambayo imekubali kutoa mikopo hiyo ili kuunga mkono juhudi za Viongozi
na wananchi wa mkoa wa Simiyu katika kuleta maendeleo.
|
Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (katikati) akizungumza na Madiwani na baadhi ya
wafugaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu(hawapo pichani) katika
kikao cha dharura cha Baraza la Madiwani, kilichofanyika Mjini Mwanhuzi kwa
lengo la kujadili maombi ya mkopo kwa ajili upanuzi wa kiwanda cha maziwa
wilayani humo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu,
Mhe.Pius Machungwa akifungua kikao dharura cha Baraza la Madiwani
kilichofanyika Mjini Mwanhuzi kwa lengo la kujadili maombi ya mkopo kwa ajili
upanuzi wa kiwanda cha maziwa wilayani humo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega,
Mhe.Vumi Magoti(wa pili kulia)akizungumza na Madiwani na baadhi ya wakulima wa
Busega(hawapo pichani) katika kikao cha dharura cha Baraza la Madiwani
kilichofanyika Nyashimo kwa lengo la kujadili maombi ya mkopo kwa ajili kutekeleza
Mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji katika Bonde la Mwamanyili Wilayani humo
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Ndg.Fabian Manoza akizungumza na
Madiwani na baadhi ya wafugaji wa Halmashauri hiyo (hawapo pichani) katika kikao cha dharura cha Baraza la
Madiwani, kilichofanyika Mjini Mwanhuzi kwa lengo la kujadili maombi ya mkopo
kwa ajili upanuzi wa kiwanda cha maziwa wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya
ya Meatu, Mhe.Dkt.Joseph Chilongani akizungumza
na Madiwani na baadhi ya wafugaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu (hawapo
pichani) katika kikao cha dharura cha
Baraza la Madiwani, kilichofanyika Mjini Mwanhuzi kwa lengo la kujadili suala
la maombi ya mkopo kwa ajili upanuzi wa kiwanda cha maziwa wilayani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka
(katikati) akizungumza na Madiwani na baadhi ya wakulima Bonde la Mwamanyili wa
Halmashauri ya Wilaya ya Busega (hawapo pichani) katika kikao cha dharura cha
Baraza la Madiwani, kilichofanyika Nyashimo kwa lengo la kujadili suala la
maombi ya mkopo kwa ajili kutekeleza Mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji katika
Bonde la Mwamanyili Wilayani humo.
Afisa Mipango
kutoa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Ndg.Josephat Joseph akiwasilisha taarifa
ya Maendeleo ya Mpango wa Kilimo cha Umwagiliaji katika Bonde la Mwamanyili kwa
viongozi, madiwani na baadhi ya wakulima (hawapo pichani) katika kikao cha dharura
cha baraza la madiwani kilichofanyika kwa lengo la kujadili maombi ya mkopo kwa
ajili ya kutekeleza mradi huo wilayani Busega.
Madiwani na baadhi ya Wafugaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
wakifuatilia mjadala kuhusu suala la maombi ya Mkopo kwa ajili ya Upanuzi wa
Kiwanda cha Maziwa Wilayani Meatu katika kikao cha dharura cha Baraza
kilichofanyika Mjini Mwanhuzi.
Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na Viongozi wa Wilaya ya Meatu (baadhi
hawapo pichani) alipotembelea eneo lililoandaliwa kwa ajili ya kuanzisha shamba
la malisho ya mifugo wanaotarajiwa kununuliwa na Halmashauri hiyo kwa ajili ya
kuwezesha upatikanaji wa maziwa katika
kiwanda cha maziwa wilayani humo.
Diwani wa Kata
ya Mwamishali katika Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Mhe.Christopher Ndamo
akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa kikao cha
dharura cha Baraza la Madiwani, kilichofanyika kwa lengo la kujadili suala la
maombi ya mkopo kwa ajili upanuzi wa kiwanda cha maziwa wilayani humo.
Diwani wa Kata
ya Mwamanyili, Mhe.Charles Luyenze akichangia hoja katika kikao cha cha dharura
cha Baraza la Madiwani kilichofanyika kwa lengo la kujadili suala la maombi ya
mkopo kwa ajili ya kutekeleza Mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji katika Bonde la
Mwamanyili wilayani Busega.
Mmoja wa
Wafugaji kutoka Wilaya ya Meatu, akizungumza na waandishi wa habari mara baada
ya kumalizika kwa kikao cha dharura cha Baraza la Madiwani, kilichofanyika kwa
lengo la kujadili suala la maombi ya mkopo kwa ajili upanuzi wa kiwanda cha
maziwa wilayani humo.
Baadhi ya
Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega wakifuatilia mjadala kuhusu suala
la maombi ya Mkopo kwa ajili ya Utekelezaji wa Mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji
katika Bonde la Mwamanyili wilayani humo, katika cha dharura cha Baraza la
Madiwani kilichofanyika hivi karibuni katika makao makuu ya wilaya hiyo
Nyashimo.
Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa
Wilaya ya Busega (meza kuu) na watendaji mbalimbali wa Wilaya hiyo baada
ya kikao cha dharura cha Baraza la Madiwani kilichofanyika kwa lengo la
kujadili suala la maombi ya mkopo kwa ajili ya kutekeleza Mradi wa Kilimo cha
Umwagiliaji katika Bonde la Mwamanyili wilayani humo.
Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa
Wilaya ya Busega (meza kuu) na madiwani wa Halmashauri hiyo baada ya
kikao cha dharura cha Baraza la Madiwani kilichofanyika kwa lengo la kujadili
suala la maombi ya mkopo kwa ajili ya kutekeleza Mradi wa Kilimo cha
Umwagiliaji katika Bonde la Mwamanyili wilayani humo.
Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa
Wilaya ya Busega (meza kuu) na baadhi ya wakulima baada ya kikao cha dharura
cha Baraza la Madiwani kilichofanyika kwa lengo la kujadili suala la maombi ya mkopo
kwa ajili ya kutekeleza Mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji katika Bonde la
Mwamanyili wilayani humo.
|
0 comments:
Post a Comment