Jumla ya vikundi 16 vya wanawake na vijana vilivyopo katika kata
36 Wilayani Maswa Mkoani Simiyu vimepatiwa mkopo wa
shilingi Milioni 50 kwa ajiri ya kuboresha kilimo cha pamba katika maeneo yao.
Vikundi hivyo ambavyo hujishughulisha na kilimo cha
pamba vimepokea hundi hiyo katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Maswa, wakati wa uzinduzi wa msimu wa kilimo wa mwaka 2017/2018.
Akizindua msimu wa kilimo na kukabidhi hundi kwa vikundi hivyo Mkuu wa
Wilaya ya Maswa Dkt Seif Shekalage alisema halmashauri imetekeleza sera ya
kuwawezesha vijana na wanawake kwa kuwajengea uwezo katika kujiletea maendeleo
ya kujikomboa na umaskini.
Alisema halmashauri imefanikiwa kutekeleza sera hiyo ya kutoa asilimia 5
kwa wanawake na 5 kwa vijana ili kuhakikisha wanajenga uchumi na
kipato cha kila mwananchi wa Wilaya hiyo.
Dk Shekalage aliongeza kuwa akinamama na vijana wanapaswa kutambua matumizi
sahihi na makusudio ya mkopo waliopokea ili uweze kuwanufaisha katika shughuli
zao za kilimo.
Aidha kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Maswa Roggers Limo alisema kwa
kipindi cha miaka mitatu iliyopita 2013/2014 hadi 2016/2017 Wilaya yao ilitoa
mkopo wa kiasi cha shilingi Mil 75,955,000 kwa vikundi vya
wanawake na shilingi 105,182,500 kwa vikundi vya
vijana ambapo Milioni 30,162 ,500 ni mapato ya ndani ya Halmashauri.
Hata hivyo Afisa kilimo wa Wilaya hiyo Christopher Simwimba alivitaka
vikundi hivyo kutumia mkopo huo ipasavyo na kuhakikisha kabla ya kuanza kupanda
katika mashamba yao ni lazima waondoe mazalia ya pamba yaliyokuwa yamebaki ili
yasije kuharibu pamba mpya itakayopandwa.
Simwimbi pia aliwasihi wakulima hao kupitia vikundi vyao kutumia mbolea ya
samadi ili kurutubisha udongo wa mashamba yao sambamba na kupanda kitaalamu wa
kuzingatia sentimeta 90 hadi 40 kwa kila mstari .
Nao baadhi wa wanakikundi vya vikundi hivyo wameishukuru Halmashauri hiyo
kwa jitihada wanazozifanya za kuhakikisha wanainua na kufufua kilimo cha zao la
pamba ambalo limeonekana kushuka kwa kiwango cha uzalishaji.
Haji Mwarabu mwanakikundi kutoka katika kikundi cha Huruma katika kata ya
Mataba aliihakikishia Halmashauri hiyo kupitia Mkurugenzi mtendaji wa
Halmashauri yao Dkt Fredrick Sagamiko kuwa watautumia vizuri mkopo huo ili
waweze kubadilisha maisha yao kupitia kilimo cha pamba.
Baadhi ya wanavikundi vya vijana na wanawake Wilayani Maswa ,watendaji
wa Halmashauri na Baadhi ya madiwani wakiwa katika uzinduzi wa msimu wa Kilimo
mwaka 2017/2018 na utoaji wa hundi ya shilingi Milioni 50 kwa vikundi
vya wanawake na vijana .
Baadhi ya wanavikundi vya vijana na wanawake Wilayani Maswa ,watendaji
wa Halmashauri na Baadhi ya madiwani wakiwa katika uzinduzi wa msimu wa Kilimo
mwaka 2017/2018 na utoaji wa hundi ya shilingi Milioni 50 kwa vikundi
vya wanawake na vijana .
Mkuu wa Wilaya ya Maswa Maswa Dkt Seif Shekalage (kushoto)akijiandaa zoezi
la uzinduzi wa ugawaji wa mbegu kwa wakulima katika uzinduzi wa msimu wa kilimo
Mkuu wa Wilaya ya Maswa Maswa Dkt Seif Shekalage (KATIKATI) akiwa katika
picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Mhe.Lucas
Mwaniyuki ,pamoja na baadhi ya madiwani wa halmashauri ya maswa mara baada ya
makabidhiano ya hundi ya Milioni 50 kwa vikundi 16 vya wanawake na vijana vinavyojihusisha
na kilimo.
Mkuu wa Wilaya ya Maswa Maswa Dkt Seif Shekalage akimkabidhi mbegu za pamba
aina ya YKM08 mwanakikundi cha mama na mtoto ni familia kutoka katika kata ya Kadeto
Veronica Seloli wakati wa uzinduzi wa msimu wa kilimowilayani humo.
0 comments:
Post a Comment