Serikali ya Tanzania kwa
kushirikiana na Serikali ya Ujerumani, Mfuko wa Mabadiliko tabia nchi
(CGF) na wananchi, imetenga kiasi cha shilingi bilioni 375.4 kutekeleza
Mradi wa kukabiliana na changamoto zinazotokana na mabadiliko ya tabia
nchi mkoani SIMIYU kwa awamu ya kwanza, ambao
utakuwa suluhisho la kudumu la tatizo la maji mkoani humo
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Maji na
Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe wakati akifungua kikao cha wadau wa
mabadiliko ya tabia nchi kilichofanyika Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Waziri Kamwelwe amesema moja ya shughuli
muhimu na kubwa katika utekelezaji wa Mradi wa kukabiliana na
changamoto zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchi, ni ufikishaji wa huduma ya Maji ya Ziwa
Victoria katika Mji wa Bariadi , Busega na Itilima kwa awamu ya kwanza na
baadaye katika Wilaya ya Meatu na Maswa.
Ameongeza kuwa upatikanaji wa maji
katika Mkoa wa Simiyu uko chini ikilinganishwa na wastani wa Kitaifa na kwa
kutambua hali hii, Serikali kwa
kushirikiana na wadau wa maendeleo ilibuni mradi huu, ili kupata suluhisho la kudumu la tatizo la maji kwa wananchi na mifugo
ambayo ni moja ya shughuli za kiuchumi za wananchi wa Mkoa wa Simiyu.
Aidha, Waziri Kamwelwe amesema lengo la
mradi huu ni kuboresha Afya na kuongeza uzalishaji ili kuinua hali ya
maisha kwa wananchi walioathirika na mabadiliko ya tabia nchi, ambapo amebainisha
kuwa katika kufikia lengo shughuli mbalimbali zitatekelezwa katika nyanja za
maji safi na usafi wa mazingira, kilimo endelevu na ufugaji.
Waziri pia amebainisha kuwa kutakuwa na ujenzi
wa mabwawa ya kilimo cha umwagiliaji endelevu na maji ya mifugo, ujenzi wa
mabwawa ya kutibu maji taka pamoja na vyoo vya mfano katika Shule na Vituo vya Afya.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu
Anthony Mtaka ameishukuru Serikali kwa kutekeleza mradi huo ambao utawasaidia
wananchi wa mkoa huo na utakuwa chachu katika Ujenzi wa Viwanda mkoani humo kwa
kuwezesha upatikanaji wa maji ya uhakika.
“Wananchi wa Mkoa wa Simiyu wote
wanausubiri sana mradi huu wa maji ya Ziwa Victoria; pia Mkoa wetu unaenda
kwenye uwekezaji wa viwanda vikubwa na changamoto tuliyonayo ni suala la
upatikanaji wa maji ya uhakika, utekelezaji wa mradi huu utatusaidia sana
katika viwanda” amesema Mtaka.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji na
Umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo amesema kuwa Simiyu ni Miongoni mwa Mikoa yenye
kiwango cha chini cha upatikanaji wa huduma ya maji ambayo Serikali imetoa kiupaumbele
cha kuipa fedha kutoka katika Fedha za Mfuko wa Maji ili kutekeleza miradi ya
maji itakayoibuliwa na kuwasilisha maandiko yake wizarani.
Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa
Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini amewahimiza Wataalam wa Halmashauri kwa kushirikiana
na Mkoa kuandaa maandiko ya kuibua miradi ya Maji itakayowasilishwa wizara ya
maji, kwa lengo la kuomba fedha za kutekeleza miradi hiyo ili kuongeza na kuboresha
upatikanaji wa huduma za maji mkoani humo.
Mradi wa kukabiliana na
changamoto zinazotokana na mabadiliko ya tabianchi Mkoani SIMIYU ambao
zabuni yake imepangwa kutangazwa Januari 2018; utatekelezwa kwa awamu mbili awamu
ya kwanza utaanza na Mji wa Bariadi, Busega na Itilima pamoja na vijiji 278
vilivyopo pembezoni mwa bomba kuu umbali wa Kilomita 12 kila upande, baadaye maeneo mengine ya Wilaya za Maswa na
Meatu.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi .Isack
Kamwelwe akifungua kikao cha Wadau wa
Mradi wa kukabiliana na changamoto
zitokanazo na Mabadiliko ya Tabianchi (hawapo
pichani) unaotekelezwa katika Mkoa wa Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi kwa
lengo la kujadili mikakati ya utekelezaji wa mradi huo
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na Wadau wa Mradi wa kukabiliana na changamoto zitokanazo na Mabadiliko ya Tabianchi (hawapo pichani) unaotekelezwa
Mkoani humo, katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili
mikakati ya utekelezaji wa mradi huo.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo akizungumza na Wadau wa Mradi wa kukabiliana na changamoto zitokanazo na Mabadiliko
ya Tabianchi (hawapo pichani) unaotekelezwa Mkoani Simiyu kwenye kikao kilichofanyika Mjini Bariadi kwa
lengo la kujadili mikakati ya utekelezaji wa mradi huo.
Katibu
Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini akichangia hoja katika kikao cha Wadau wa
Mradi wa kukabiliana na changamoto zitokanazo
na Mabadiliko ya Tabianchi, unaotekelezwa Mkoani humo kilichofanyika Mjini
Bariadi kwa lengo la kujadili mikakati ya utekelezaji wa mradi huo.
Mkuu
wa Wilaya ya Meatu, Mhe.Dkt.Joseph Chilongani akichangia hoja katika kikao cha
Wadau wa Mradi wa kukabiliana na
changamoto zitokanazo na Mabadiliko ya Tabianchi , unaotekelezwa Mkoani Simiyu,
kilichofanyika Mjini Bariadi kwa lengo
la kujadili mikakati ya utekelezaji wa mradi huo.
Mbunge
wa Jimbo la Maswa Magharibi Mhe.Mashimba Ndaki akichangia hoja katika kikao cha
Wadau wa Mradi wa kukabiliana na
changamoto zitokanazo na Mabadiliko ya Tabianchi , unaotekelezwa Mkoani humo kilichofanyika
Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili mikakati ya utekelezaji wa mradi huo.
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Mji Bariadi, Mhe.Robert Lweyo akichangia hoja katika kikao cha
Wadau wa Mradi wa kukabiliana na
changamoto zitokanazo na Mabadiliko ya Tabianchi ( baadhi hawapo pichani) unaotekelezwa
Mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini hapo kwa lengo la kujadili mikakati ya
utekelezaji wa mradi huo.
PICHA
H:-Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, Ndg.Mariano
Mwanyigu akichangia hoja katika kikao cha Wadau wa Mradi wa kukabiliana na changamoto zitokanazo na Mabadiliko ya Tabianchi (baadhi hawapo
pichani) unaotekelezwa Mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi kwa lengo la
kujadili mikakati ya utekelezaji wa mradi huo.
Mwakilishi
wa Tume ya Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi, Bi.Pili Msati akichangia hoja
katika kikao cha Wadau wa Mradi wa
kukabiliana na changamoto zitokanazo na Mabadiliko ya Tabianchi (hawapo
pichani) unaotekelezwa Mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi kwa lengo la
kujadili mikakati ya utekelezaji wa mradi huo.
Katibu
Mwenezi wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe.Jeremia Shigala akichangia hoja katika kikao
cha Wadau wa Mradi wa kukabiliana na
changamoto zitokanazo na Mabadiliko ya Tabianchi unaotekelezwa
Mkoani humo kilichofanyika Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili mikakati ya
utekelezaji wa mradi huo.
Baadhi ya wadau wa Mradi wa kukabiliana na changamoto zitokanazo
na Mabadiliko ya Tabianchi unaotekelezwa
Mkoani Simiyu akifuatilia masuala mbalimbali yalikuwa yakijadiliwa katika kikao
kilichofanyika mjini Bariadi kwa lengo la kujadili mikakati ya utekelezaji wa
mradi huo
Baadhi ya wadau wa Mradi wa kukabiliana na changamoto zitokanazo
na Mabadiliko ya Tabianchi unaotekelezwa
Mkoani Simiyu akifuatilia masuala mbalimbali yalikuwa yakijadiliwa katika kikao
kilichofanyika mjini Bariadi kwa lengo la kujadili mikakati ya utekelezaji wa
mradi huo.
Mkuu
wa Wilaya ya Busega, Mhe.Tano Mwera akichangia hoja katika kikao cha Wadau wa
Mradi wa kukabiliana na changamoto zitokanazo
na Mabadiliko ya Tabianchi unaotekelezwa Mkoani humo kilichofanyika Mjini
Bariadi kwa lengo la kujadili mikakati ya utekelezaji wa mradi huo.
Waziri
wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe(katikati) akiwa katika picha ya
pamoja na viongozi wa Mkoa wa Simiyu na wadau wa Mradi wa kukabiliana na
changamoto zitokanazo na Mabadiliko ya Tabianchi unaotekelezwa Mkoani humo mara baada ya
ufunguzi wa kikao cha wadau hao kilichofanyika Mjini Bariadi.
Waziri
wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe(katikati) akiwa katika picha ya
pamoja na viongozi wa Mkoa wa Simiyu na wadau wa Mradi wa kukabiliana na
changamoto zitokanazo na Mabadiliko ya Tabianchi unaotekelezwa Mkoani humo mara baada ya
ufunguzi wa kikao cha wadau hao kilichofanyika Mjini Bariadi.
Waziri
wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe(kulia) na KATIBU Mkuu wa Wizara
hiyo, Profesa Kitila Mkumbo wakisaini vitabu vya wageni katika Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, baada ya kuwasili mkoani hapo kwa ajili ya kushiriki kikao cha Wadau wa Mradi wa kukabiliana na changamoto zitokanazo na Mabadiliko ya Tabianchi unaotekelezwa Mkoani
humo, kilichofanyika Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili mikakati ya utekelezaji
wa mradi huo.
0 comments:
Post a Comment