Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe.Joseph Kakunda
ameiagiza mikoa na Halmashauri zote Nchini kuhakikisha kuwa zinaunda Kamati za
kushughulikia mahitaji ya watu wenye Ulemavu katika kila Halmashauri, Kata na
Vijiji, kabla ya June 30, 2018.
Mhe. Kakunda ametoa agizo hilo wakati wa Maadhimisho
ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu Duniani, yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa
Halmashauri ya mji Bariadi Mkoani Simiyu.
Amesema Serikali imetenga shilingi milioni 50
kuliwezesha Baraza la wenye Ulemavu Kitaifa kufanya kazi zake kwa mujibu wa
Sheria ikiwa ni pamoja na kuhakikisha Kamati zinaundwa hadi ngazi ya vijiji,
ili kufanikisha azma hiyo, amesema
lazima ziundwe kamati za kushughulikia wenye ulemavu katika kila Halmashauri,
Kata na Vijiji, ambapo ameipongeza mikoa ya Simiyu,, Tabora na Mbeya kwa
kukamilisha zoezi hili.
“Naipongeza mikoa ya Simiyu, Tabora na Mbeya kwa
kuanzisha kamati hizo katika Halmashauri zao
zote, naagiza Kamati hizo ziundwe katika mikoa yote na katika
Halmashauri zote nchini, wale ambao bado hawajakamilisha wakamilishe; tunataka
kuona ifikapo tarehe 30 Juni 2018 mikoa yote iwe na kamati hizo” amesisitiza
Kakunda.
Mhe.Kakunda pia ameziagiza Halmashauri zote Nchini
kuwapa Kipaumbele Wajasiriamali wenye Ulemavu katika utoaji wa Mikopo
inayotokana na asilimia 10 ya Mapato ya ndani ili waweze kujipatia mitaji ya
kuendeshea shughuli zao mbalimbali za ujasiriamali na kujikwamua kiuchumi.
Ameongeza kuwa Serikali imeandaa utaratibu wa Bima
ya Afya kwa watu wote wakiwemo wenye ulemavu ambao ujumuisha upatikanaji wa
huduma tengamavu na vifaa saidizi na itaendelea kuagiza na kutoa vifaa hivyo kwa
watu wenye ulemavu.
Aidha, amesema Serikali itahakikisha miundombinu
inakuwa rafiki na fikivu kwa wenye ulemavu, itaangalia namna bora ya
upatikanaji wa ajira kwao, itawahimiza
wamiliki wa vyombo vya habari kutumia wakalimani wa lugha ya alama, kuendelea kuchukua
hatua kadi dhidi ya wanaofanya ukatili kwa wenye ualbino, italifanyia kazi
suala la ukosefu wa Ofisi kwa ajili ya SHIVYAWATA kwa kuangalia uwezekano wa
kushirikisha Halmashauri kutenga Ofisi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa SHIVYAWATA Bi.Ummy
Nderininanga akiwasilisha risala ya watu wenye Ulemavu, ametoa mapendekezo
kadhaa kwa Serikali na kuomba yafanyiwe kazi ikiwa ni pamoja na watu wenye
ulemavu kupatiwa bima za afya,upatikanaji wa ofisi za SHIVYAWATA, kuongezwa kwa nafasi za ajira kwa watu wenye
ulemavu, kutoa mikopo kwa watu wenye ulemavu,kuongeza ulinzi kwa watu wenye
ualbino na wanafunzi wa elimu ya juu wenye ulemavu kupewa ruzuku badala ya
mikopo, ambayo yote yalitolewa ufafanuzi na Viongozi wa Serikali.
Naye Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anyeshughulikia
wenye Ulemavu, Mhe.Stella Ikupa amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau
mbalimbali imeanza kutoa kipaumbele na kujumuisha watu wenye ulemavu katika
mpango wa ukuzaji ujuzi unaoendeshwa na Ofisi ya Waziri Mkuu na pia imeanza kujadili kuona ni jinsi gani mikopo ya elimu
ya Juu itatolewa kama ruzuku kwa watu wenye ulemavu.
Akiwasilisha salamu za Mkoa kwa niaba ya Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
Mhe.Festo Kiswaga amesema Mkoa wa Simiyu umeweka utaratibu maalum wa kuwatambua
watu wenye ulemavu kuanzia ngazi za vijiji na kubainisha kuwa hadi kufikia
mwaka 2017 jumla ya watu 6305 wenye ulemavu mbalimbali wametambuliwa.
Maadhimisho ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu Duniani,
yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya mji Bariadi Mkoani Simiyu,
Kauli Mbiu isemayo , yenye Kauli Mbiu isemayo “BADILIKA TUNAPOELEKEA JAMII
ENDELEVU NA IMARA KWA WOTE” na
ni mara ya kwanza kufanyika Mkoani Simiyu.
Baadhi
ya watu wenye Ulemavu wakiwa katika Maandamano katika Uwanja wa Halmashauri ya
Mji Bariadi wakati wa Maadhimisho ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu Duniani , yalifanyika
Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya mji Bariadi Mkoani Simiyu.
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Joseph Kakunda akizungumza na watu wenye
uLemavu na wananchi wa Bariadi Mkoani Simiyu(hawapo pichani), wakati wa Maadhimisho
ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu Duniani, yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa
Halmashauri ya mji Bariadi Mkoani Simiyu.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe.Stella Ikupa akizungumza na watu wenye
uLemavu na wananchi wa Bariadi Mkoani Simiyu(hawapo pichani), wakati wa Maadhimisho
ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu Duniani, yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa
Halmashauri ya mji Bariadi Mkoani Simiyu
Mwenyekiti
wa Shirikisho la Vyama vya Walemavu Tanzania(SHIVYAWATA), Bi. Ummy Nderininanga
akizungumza na watu wenye ulemavu na wananchi wa Bariadi Mkoani Simiyu (hawapo
pichani), Maadhimisho ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu Duniani, yaliyofanyika katika
Uwanja wa Halmashauri ya mji Bariadi Mkoani Simiyu.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Anthony Mtaka akitoa ufafanuzi juu ya masuala
mbalimbali kwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe.Joseph Kakunda(kulia)
na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Walemavu, Mhe.Stella
Ikupa(katikati) walipofika Ofisini kwake kabla ya Maadhimisho ya Kimataifa ya
Watu wenye Ulemavu Duniani, yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya mji
Bariadi Mkoani humo.
Katibu
Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini akiwasilisha taarifa ya Mkoa kwa
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe.Joseph Kakunda(hayupo pichani) na
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Walemavu, Mhe.Stella
Ikupa(kulia) walipofika Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa huo,kabla ya Maadhimisho ya Kimataifa
ya Watu wenye Ulemavu Duniani , yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya
mji Bariadi Mkoani humo.
Katibu
Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini (kushoto) akiwaongoza Naibu Waziri
Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe.Joseph Kakunda(kulia) na Naibu Waziri Ofisi ya
Waziri Mkuu anayeshughulikia Walemavu, Mhe.Stella Ikupa(katikati) kwenda
Wagonjwa waliopata Ajali na kulazwa katika Hospitali Teule ya Mkoa huo, kabla
ya Maadhimisho ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu Duniani, yaliyofanyika Kitaifa katika
Uwanja wa Halmashauri ya mji Bariadi Mkoani humo.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe.Joseph Kakunda(hayupo pichani) na
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Walemavu, Mhe.Stella
Ikupa(kushoto)akimjulia hali mmoja wa Wagonjwa waliopata Ajali na kulazwa
katika Hospitali Teule ya Mkoa huo, kabla ya Maadhimisho ya Kimataifa ya Watu
wenye Ulemavu Duniani, yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya mji
Bariadi Mkoani humo
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe.Joseph Kakunda na Naibu Waziri Ofisi ya
Waziri Mkuu anayeshughulikia Walemavu, Mhe.Stella Ikupa(kushoto) wakizungumza
baada ya kuona bidhaa zinazotengenezwa na walemavu, wakati wa Maadhimisho ya Kimataifa
ya Watu wenye Ulemavu Duniani, yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya
mji Bariadi Mkoani Simiyu.
Mkuu
wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga akiwasilisha Salamu za Mkoa kwa niaba
ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka, wakati wa Maadhimisho ya Kimataifa
ya Watu wenye Ulemavu Duniani, yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya
mji Bariadi Mkoani Simiyu.
Mmoja
wa watu wenye Ulemavu, Bw.Athumani Rubandame aliyepata ulemavu kutokana na
ajali za barabarani akitoa ushuhuda juu ya namna ajali za barabarani zinavyochangia
ulemavu, Maadhimisho ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu Duniani, yaliyofanyika Kitaifa
katika Uwanja wa Halmashauri ya mji Bariadi Mkoani Simiyu.
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe.Joseph Kakunda na Naibu Waziri Ofisi ya
Waziri Mkuu anayeshughulikia Walemavu, Mhe.Stella Ikupa wakipata maelezo kutoka
kwa Viongozi wa watu wenye Ualbino, Maadhimisho ya Kimataifa ya Watu wenye
Ulemavu Duniani, yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya mji Bariadi
Mkoani Simiyu.
Baadhi
ya Viongozi na Watu wenye Ulemavu wakimsikiliza Mgeni Rasmi katika, Maadhimisho
ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu Duniani, yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Simiyu, Naibu
Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe.Joseph Kakunda(hayupo pichani).
Katibu
Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini(katikati) akiteta jambo na Mkuu wa
Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga, Mhe.Festo Kiswaga(kulia), katika Maadhimisho
ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu Duniani, yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa
Halmashauri ya mji Bariadi Mkoani Simiyu. (kushoto) Katibu wa SHIVYAWATA
Ndg.Felician Mkude.
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe.Joseph Kakunda(wa pili kushoto) akicheza
pamoja na watu wenye ulemavu na baadhi
ya viongozi , baada ya kumaliza shughuli za Maadhimisho ya Kimataifa ya Watu
wenye Ulemavu Duniani , yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya mji
Bariadi Mkoani Simiyu.
Baadhi
ya Viongozi na Watu wenye Ulemavu wakimsikiliza Mgeni Rasmi Maadhimisho ya Kimataifa
ya Watu wenye Ulemavu Duniani, ambayo yamefanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri
ya mji Bariadi Mkoani Simiyu.Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe.Joseph
Kakunda(hayupo pichani).
Baadhi
ya wananchi wa Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu wakimsikiliza Mgeni Rasmi katika
Maadhimisho ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu Duniani, yaliyofanyika Kitaifa katika
Uwanja wa Halmashauri ya mji Bariadi Mkoani Simiyu, Naibu Waziri Ofisi ya Rais
TAMISEMI, Mhe.Joseph Kakunda(hayupo pichani).
0 comments:
Post a Comment